KISWAHILI FORM FOUR REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

Namba Ya Mtahiniwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

OFISI YA RAIS TAWALA - TAMISEMI TAHOSSA ROMBO DISTRICT EXAMINATION SYNDICATE

MTIHANI WA UTAMIRIFU KIDATO CHA NNE

021 KISWAHILI

MUDA : SAA 3:00 Agusti, 2024

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una sehemu tatu ambazo ni A, B na C yenye jumla ya maswali kumi na moja (11)
  2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A na B, na maswali mawili(2) kutoka sehemu C ambapo swali la kumi (10) ni lazima.
  3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu
  4. Zingatia matumizi sahihi ya alama za uandishi na lugha fasaha

SEHEMU A (Alama16)

1. Katika swali la i-x, chagua herufi ya jibu sahihi kutoka katika mapendekezo uliyopewa. Andika jibu kwa herufi kubwa

i Amina huimba nyimbo katika utaratibu wa kupandisha na kushusha sauti yake. Uimbaji huo humvutia kila anayemsikiliza. Je utaratibu huu kiisimu hujulikana kama?

  1. Mkazo
  2. Kiimbo
  3. Lafudhi
  4. Kitomeo

ii “Walilima, wakapanda”. Je hii ni aina gani ya sentensi?

  1. Sahili
  2. Ambatano
  3. Shurutia
  4. Changamano

iii Jumla ya silabi zinazounda mshororo huitwaje?

  1. Vina
  2. Bahari
  3. Mizani
  4. Muwala

iv “Nimekufia mtoto mzuri”. Huu ni mtindo gani wa lugha?

  1. Simo
  2. Methali
  3. Msemo
  4. Rejesta

v “Shangazi yupo shambani kwake” kifungu hiki cha maneno kipo katika ngeli ipi?

  1. I – ZI
  2. YU – A – WA
  3. PA – MU – KU
  4. KI – VI

vi Ifuatayo ni moja ya sifa ya mhakiki wa kazi ya Fasihi.

  1. Awe anamfahamu mwandishi kwa undani.
  2. Awe amesoma kazi nyingi za fasihi.
  3. Hapaswi kumpa mwandishi ari ya kuendelea na uandishi.
  4. Awe zao la jamii iliyoandikwa

vii Mtoto alikuwa mwizi. Neno alikuwa ni

  1. T
  2.  t
  3. Ts
  4. U

viii Musa alifurahi alipopata maswali yote ya Kiswahili. Neno lililopigiwa mstari ni aina gani ya neno?

  1. Nomino
  2. Kielezi
  3. Kitenzi
  4. Kishazi tegemezi kielezi

ix Mzizi wa neno kula

  1. –l-
  2.  kul-
  3. kula
  4.  –lax

Mama hupenda kusimulia hadithi kuhusu vita vya majimaji. Je hizi nia aina gani za hadithi?

  1. Tarihi
  2.  Ngoma
  3. Vigano
  4. Visasili

2. Oanisha maelezo ya kifungu A na maelezo ya kifungu B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia

KIFUNGU A KIFUNGU B
  1. Ni moja ya vigezo vya uandishi wa tangazo rasmi
  2. Ni sifa ya matangazo yasiyo rasmi
  3. Ni mojawapo wa vigezo vya uadishi wa insha.
  4. huandikwa kwa mtiririko wa mawazo yaliyo katika mpangilio wa aya.
  5. ni mojawapo ya sifa za uandishi wa matangazo.
  6. Nilipofika nyumbani nilimkuta hayupo
  1. Hutolewa kiholela bila kupitia mamlaka zinazohusika.
  2.  Insha
  3. Mstari habari
  4. Tangazo
  5. Liwe fupi na la kueleweka.
  6.  Huratibiwa na kuhaririwa kabla ya kufikia umma.
  7. Sanaa
  8. Kutozingatia matamshi sahihi
  9. Kutozingatia mantiki
  10. Uzembe wa mtamkaji

SEHEMU B (Alama 54)

3. a) Nini maana ya Lugha?

b) Kila siku baba na mama wamekuwa wakigombana. Hali hii husababishwa na mama kushindwa kutumia lugha vizuri. Wewe kama mtoto msomi katika familia eleza mambo manne yatakayomsaidia mama kutumia lugha vizuri.

4. i) Tunga sentensi kubainisha matumizi yafuatayo ya mofimu “KI”

  1. Masharti
  2. Kitendo kuendelea kwa muda
  3. Kitenzi kishirikishi
  4. Upatanisho wa kisarufi
  5. Udogoishi

ii) Kwa kila sentensi onesha kiima na kiarifu kwa kutenga na kistari na kuandika “K” kwa kiima na “A” kwa kiarifu.

  1.  Mwanasiasa alikuwa anahutubia wanakijiji wote leo.
  2. Mbuzi wangu mkubwa amekula majani yote.
  3. Ng’ombe wetu amekunywa maji machafu mno.
  4. Walifika Asubuhi walimu wetu.

5. (a) Eleza sababu nne za kujitokeza kwa rejesta katika jamii

(b) Salome ni mwanafunzi wa kidato cha nne anayetegemea kutembelea maeneo mbalimbali katika kijiji chake. Toa mfano mmoja wa lugha atakayotumia katika Mazingira yafuatayo:-

  1. Sokoni
  2. Kanisani
  3. Michezoni
  4. Mtaani
  5. Bungeni

6. (a) Andika semi yenye maana sawa na semi zifuatazo

  1. Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza
  2. Mfa maji haishi kutapatapa
  3. Atekaye maji mtoni hatukani mamba
  4. Hakuna masika yasiyokuwa na mbu

(b) Utohoaji ni moja ya njia ya uundaji wa maneno kwa kila tungo ifuatayo taja lugha ambavyo neno au tungo hiyo imetoholewa

  1. Leso
  2.  Divai
  3. Bendera
  4. Bibo
  5.  Ngeli.

7. Kwa kumia kigezo cha upatanisho wa kisarufi tunga sentensi mbili zenye o-rejeshi. Tumia ngeli zifuatazo:

  1. Ngeli ya pili
  2. Ngeli ya tano
  3.  Ngeli ya tatu

8. Andika insha yenye maneno yasiyozidi 250 inayohusu “Siku ambayo hutaisahau

SEHEMU C (ALAMA 30)

Jibu maswali mawili tu kutoka sehemu hii.Swali la kumi(10) ni la lazima.

9. “Uchaguzi wa majina ya vitabu husaidia kuibua dhamira za mwandishi” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila tamthiliya kati ya tamthiliya mbili ulizosoma.

10. Msanii ametumia taswira katika kazi ili kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa. Thibitisha hoja hii kwa kutumia diwani mbili ulizosoma. Toa hoja tatu katika kila diwani.

11. “ Mafanikio ya mwanajamii huletwa na mwanajamii mwenyewe.” Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kutoka katika riwaya katiya mbili ulizosoma.

ORODHA YA VITABU

USHAIRI

  • Wasakatonge M.S.Khatibu
  • Malenga wapya .. ...TAKILUKI
  • Mashairi ya Chekacheka T.A. Mvungi

RIWAYA

  • Takadini ..Ben J. Hanson
  • Watoto wa Mama N’tiliye ..E. Mbogo
  • Joka la Mdimu A.J. Safari

TAMTHILIYA

  • Orodha Steve Reynords
  • Ngoswe penzi kitovu cha uzembe ...E. Semzaba
  • Kilio Chetu .Medical Aid Foundation

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 226  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 226  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA — MKOA WA PWANI 

MTIHANI WA UTAMILIFU WILAYA KEDATO CHA NNE

 KISWAHILI 

Msimbo 021

MUDA: SAA 3 : 00 MWAKA, 2024

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) to kutoka sehemu C.
  3. Vifaa vya mawasiliano haviruhusiwi katika chumba cha mtihani.
  4. Majibu yote yaandikwe ndani ya kijitabu chako cha kujibia kwa wino wa buluu na mweusi.
  5. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  6. Kumbuka kuandika namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kitabu chako clia kujibia.

SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswall yote kutoka sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele (i)-(x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karalasi yako ya kujibia

(i) Mwalimu aliwaagiza wanafunzi wawili wajibizane mbele ya wenzao darasani Ni kipera kipi cha ushairi kinawakilisha walichofanya wanafunzi hao?

  1. Ngonjera 
  2. Majigambo 
  3. Kichekesho
  4. Igizo 
  5. Ushairi

(ii) Ukiwa kama mhudumu wa hotelini utatumia kamusi gani kuloa huduma kwa wageni wa aina tatu wanaoongea lugha tofauti tofauti?

  1. Kamusi wahidiya 
  2. Kamusi mahuluti 
  3. Kamusi thaniya
  4. Kamusi ya kiingereza 
  5. Kamusi ya Kiswahili sanifu

(iii) Ally na Nasma wametokea katika sehemu mbili tofauti na kila mtu anatumia lugha yake. Je, ni lugha gani ya mseto inayozuka pindi wawili hao wakutanapo?

  1. Lugha ya vizalia 
  2. Pijini 
  3. Kibantu
  4. Kiswahili 
  5. Kiunguja

iv. Ni jukumu lipi Ia kisarufi linalotekelezwa na neno lililopigiwa mstari katika maneno "wakutanapo hugombana"

  1. Hutumika kurejelea mtendwa 
  2. Hutumika kurejelea njeo
  3. Hutumika kama kiunganishi 
  4. Hutumika kurejelea mtenda
  5. Hutumika kurejelea mahali

v. Ipi kati ya sentensi zifuatazo ina kishazi tegemezi kivumishi

  1. Angelisoma kwa bidii angelifaulu mtihani
  2. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa mtiifu sana
  3. Dokta Kim anasoma alichofundishwa darasani
  4. Simba inacheza uwanjani
  5. Mbuzi aliyechinjwa jana ameliwa leo asubuhi

vi. Taasisi ya taaluma ya Kiswahili (TATAKI) ni moja ya asasi zilizofanyiwa maboresho kutoka kwenye asasi kongwe ambayo ni

  1. TAKILUKI 
  2.  UKUTA 
  3. TUKI
  4. CHAWAKAMA 
  5. BAKITA

vii. "Chajio na Waviji" ni maneno yaliyopatikana kwa njia gani ya uundaji wa maneno?

  1. Uambishaji mwanzoni 
  2. Uambatanishaji 
  3.  Kutohoa
  4. Uhulutishaji E. Ufupishaji

viii. Wazazi wako wamekuita katika kikao cha familia iii kujadili mambo mbalimbali ya familia yenu. Je, ni nani kati ya hawa ana jukumu la kuandika kumbukumbu ya kikao kilichofanyika, 

  1. Mwenyekili 
  2. Mtunza fedha 
  3.  Katibu
  4. Mjumbe 
  5. Mtu nza muda

ix. "Kiti cha mfalme kinaheshimiwa" katika sentensi hii neno lililopigiwa mstari ni aina gani ya neno katika uanishaji wa maneno.

  1. Kiunganishi 
  2. Kihusishi 
  3.  Kihisishi
  4. Kiigizi 
  5. Kivumishi cha A- unganifu

x. Fungu Ia sauti zinazotokeza katikati au mwishoni mwa kila mstari wa shairi hujulikana

  1. Kituo 
  2. Vina 
  3. Mizani
  4. Silabi 
  5. Mstari

2. Oanisha maana ya dhana zilizopo katika Orodha A kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi katika orodha B, kisha andika herufi husika katika karatasi yako ya kujibia

ORODHA A

ORODHA B

  1. Kuteuliwa kwa Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano
  2. Kutangazwa kwa Kiswahili kuwa lugha ya taifa '
  3. Kuundwa kwa Baraza la Kiswahili Taifa
  4. Mwalimu J.K.Nyerere alihutubia bunge kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza
  5. Kuundwa kwa "The inter-territorial Swahili language committee"
  6. Ufisadi,Ari mpya,Ujasiriamali ni misamiati iliyojitokeza
  1. 1970
  2. 1930
  3. 2005 - 2015
  4. 1961
  5. 1947
  6. 1967
  7. 1964
  8. 1962

SEHEMU B (Mama 54)

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii

3 (a) Mama yake Dorah alimuuliza inwanao .kwaihni =eel] mtihani wa muhula huu "Dorah alijibu "Si unajua Yule ticha ni nomaa yaani anapendelea kinoma nami ananichunia" Kutokana na taanfa hiyo taja mambo matano ya msingi ambayo Dorah alipaswa kuzingatia kabla ya kuzungumza na mama yake

(b) Watumiaji wengi wa lugha ya Kiswahili hufanya makosa katika utumizi wa lugha aidha kwa kujua au kutokujua. Wewe kama mtaalamu wa Kiswahili bainisha makosa manne ya kisarufi yanayofanywa na watumiaji wa lugha ya Kiswahili kwa mifano dhahiri

4 (a) Unda maneno mapya mawili kutoka katika kila neno kati ya maneno haya

  1. Imla
  2. Samaki
  3. Kila
  4. Fau

(b) Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii, iii msamiati ukue sharti maneno mapya yaundwe. Je, maneno yafuatayo yamepatikana kwa njia gani?

  1. CHAKA
  2. Papai
  3. Ndizi mkono wa tembo
  4. Kigoda.
  5. Mwenyekiti

5. Konzo anaamini kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu, lakini Kilatu anaamini upo uhusiano kali ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu. Ukiwa kama mbobezi wa lugha ya Kiswahili tumia hoja sita zenye mifano kuondoa utata huo

6. Wewe ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia, umealikwa katika mahafali ya kidato cha nne kama mgeni rasmi katika shule ya sekondari Mpeponi. Toa hotuba kwa wanafunzi, Walimu na Wananchi waliohuhudhuria hafla hiyo.

7 Kwa kutumia Tamthiliya ya KILIO CHETU fafanua madhara yatokanayo endapo vijana wakikosa elimu ya kijinsia.hoja sita (6).

8. Soma kifungu cha habari kifuatacho ,kisha jibu maswali yanayoluala.

Kijiji cha Songambele kilikuwa na watu wengi walioishi kwa kushinkiana. Watu wa kijiji hicho walifanya kazi kwa pamoja na ushirikiano. Ardhi ya Songambele ilikuwa kubwa na yenye ruluba lakini chakula kilikuwa haba kutokana na ukame. Ukosefu wa mvua kwa muda mrefu ulisababisha vijito na visima vidogodogo kukauka. Watu wa kijiti cha Songambele waliishi kwa tabu na mifugo yao ilidhoofu.

Katika kijiti cha Songambele kulikuwa na Mzee mmoja aliyejulikana kwa jina Ia Kichwa Matata. Mzee Kichwa Matata alikuwa na hekima na busara nyingi na hakupendezwa na hali ya kijiji cha Songambele. Siku moja aliwaita wanakijiji wote wa kijiti cha Songambele alitaka awaeleze mawazo yake.

Wanakijiji walikusanyika, Mzee Kichwa Matata alisimama akawaambia "Ndugu zangu nina neno la kuwaambia".Watu wote walinyamaza ili wamsikilize, Akamuita mtoto mmoja apite mbele yao akampa kijiti kimoja akamwambia "vunja" mtoto akakivuja kijiti kite kwa urahisi Mzee Kichwa Matata akampa vijiti kumi vilivyofungwa pamoja ili avivunje mtoto akashindwa kuvunja. Akamuita Mzee Kichwa Maji avivunje nae akashindwa Vijana kadhaa wahopdai kuwa na nguvu sana wakajaribu mmoja mmoja kuvunja vile vijiti kumi kwa pamoja nao wakashindwa

Mzee Kichwa Matata akasimama akawaambia mfano huu wa vijiti unatuhusu sisi, Mtoto ameweza kuvunja kijili kimoja kwa urahisi lakini ameshindwa kuvunja vijiti vingi. Vijana hao pamoja na Mzee Kichwa Maji ni mfano wa ukame. Ni rahisi kwa ukame kumshinda mtu mmoja mmoja kama ilivyokuwa rahisi kwa mtoto mmoja kuvunja kite kijiti kimoja, lakini ukame hauwezi kuwashinda watu wengi wanaoshirikiana kwa pamoja.

Baada ya mfano huo, Mzee Kichwa Matata aliwasisitiza watu wa Songambele kushirikiana kama siafu kwa kuwa siafu ni viumbe wadogo lakini wanaweza kumshambulia na hata kumuua adui yao. Maelezo yake yaliwapendeza sana wanakijiji wa Songambele.

Siku ile watu wa Songambele walianza kuweka mikakati ya kukabiliana na tatizo Ia ukame kijijini humo. Walikubaliana kuchimba kisima cha kijiji, kila mtu alitoa kitu alichoweza ili kufanikisha zoezi hilo. Watu wa kijiji cha Songambele walifanya kazi usiku na mchana kukamilisha malengo yao. Baada ya muda kisima kilikamilika na maji ya kutosha yalipatikana

Watu wa Songambele walifurahi sana kupata maji kwa ajili ya mahitaji yao na mifugo.

Maswati

  1. Pendekeza kichwa cha habari uliyosoma.
  2. Kijiji cha Songambele kilikubwa na tatizo gani?
  3. Wananchi wa Songambele walifanya nini iii kuondokana na tatizo lililowakumba katika kijiji chao?
  4. Eleza maana ya methali isemayo "Umoja ni nguvu,utengano ni udhaifu".
  5. Fupisha habari uliyoisoma kwa maneno 50 tu.

SEHEMU C (Alama 30)
Jibu maswali mawili (2) tu kutoka sehemu hii,swali la 9 ni Ia lazima.

ORODHA YA VITABU

MASHAIRI

  • Wasakatonge - M.S. Khatibu
  • Malenga wapya - Takiluki
  • Mashairi ya Cheka Cheka T.A.Mvungi

RIWAYA

  • Takadin i- Ben J. Hanson
  • Watoto wa mama Ntiliye - E. Mbogo
  • Joka la mdimu - A.J. Safari

ORODHA

  • Orodha - Steve Reynolds
  • Ngoswe penzi kitovu cha uzembe - Semzaba
  • Kilio chetu - Medical Aid foundation

9. Washairi ni wataalamu waliobobea katika utumizi wa fani, kwa kutumia diwani mbili ulizosoma thibitisha dai hili kwa kutoa hoja latu za muundo kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizozisoma.

10. Ugonjwa wa UKIMWI bado ni lishio kwa jamii ya Tanzania na dunia kwa ujumla Hali hayo imepelekea wanafasihi watumie kalamu zao kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa huo Tumia tamthiliya ya KILIO CHETU ukionesha mambo yaliyopelekea maambukizi kwa jam na tumia tamthiliya ya ORODHA ukionesha namna ya kuepuka maambukizi hayo

11. Adui yeyote hukwamisha maendeleo katika jamii, Fafanua jinsi waandishi wa riwaya mbili ulizosoma walivyojitahidi kupambana na maadui hao Hoja latu kwa kola riwaya

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 216  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 216  


TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA — TAMISEMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI

MTIHANI WA UTAMILIFU WILAYA KEDATO CHA NNE

CODE: 021 KISWAHILI 

MUDA: SAA 3 MACHI, 2024

Maelekezo 

1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11) 

2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C 

3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30). 

4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali 

5. Simu za mkononi na vitu visivyoruhusiwa HAVITAKIWI katika chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 16) 

Jibu maswali yote katika sehemu hii. 

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi ya kujibia.

(i) Yafuatayo ni madai ya kiisimu kwamba, Kiswahili ni Kibantu isipokuwa:- 

  1. Mwishilizo wa vitenzi 
  2. Msamiati
  3. Muundo wa sentensi
  4. Upatanisho wa kisarufi  
  5. Utenzi wa fumo Lyongo

(ii) Maneno ya Kiswahili huundwa kwa njia mbalimbali. Je neno kukua limeundwa kwa njia gani? 

  1. Utohoaji
  2. Kufananisha sauti 
  3. Uambatanishaji wa maneno
  4. Kufananisha umbile
  5. Kazi ya kitu

(iii) Leta wali kuku, wapi chai, ukizingua nitakuharibia, demu wake mkali kinyama. Ni rejesta za aina gani? 

  1. Rejesta za shuleni na kanisani
  2. Rejesta za jeshini na msikitini 
  3. Rejesta za hotelini na mtaani
  4. Rejesta za hospitalini na sokoni
  5. Rejesta za sokoni na barabarani

(iv) Sifa mojawapo ya ngeli ya YXA-WA ni zipi? 

  1. Inahusu nomino zote zenye kuanzia na A na kuishiwa AW 
  2. Inahusu nomino zote zenye uwezo wa kidhahania 
  3. Inahusu nomino zote zenye uwezo wa kujongea kutoka sehemu moja na nyingine 
  4. Inahusu nomino zenye kutaja mahali 
  5. Inahusu nomino zote zinazohesabika

(v) Mashairi ni mpangilio mzuri wenye ruwaza mahususi ya silabi, lugha ya kato na kutumia sana tamathali za semi. Ni aina gani ya shairi ambalo halifuati urari wa vina na mizani? 

  1. Utao 
  2. Ukwapi
  3. Mwandamizi 
  4. Mapingiti  
  5. Tendi 

(vi) Chukulia kuwa unataka kujifunza jinsi ambavyo vitamkwa vya lugha ya Kiswahili vinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha ya Kiswahili. Je ni utanzu gani wa sarufi utashughulika nao iii kuupata uelewa wa mambo hayo? 

  1. Fonolojia
  2. Mofolojia 
  3. Sintaksia 
  4. Semantiki
  5. Pragmati 

(vii) Ni sehemu gani ya sentensi ambayo hujazwa na kikundi nomino katika kiarifu? 

  1. Ngeli za majina
  2. Kikundo nomino 
  3. Shamirisho 
  4. Prediketa
  5. Chagizo 

(viii) Maneno yapi kati ya yafuatayo yanatokana na fugha ya Kireno? 

  1. Leso, meza, bendera
  2. Doti, dobi, leso
  3. Bakuli, pesa, bendera 
  4. Meza, Leso, dobi
  5. Beseni, meza, leso

(ix) Katika kipindi cha harakati za kudai uhuru, lugha ya Kiswahili ilipata kukua na kuenea kwa kasi, kwa kaama ya kuongezeka kwa misamiati na kukua kimatumizi, katika kipindi hicho maneno yafuatayo yaliibuka;- 

  1. Uhuru na Urnoja, uhuru na kazi
  2. Baba Kabwela, unyonyaji 
  3. Kupe, baba kabwela, uhuru na kazi
  4. Uhuru na umoja, unyonyaji kupe
  5. Kupe, umoja na kazi, baba kabwela

(x) Kucheza kwake kunafurahisha. Neno lililopigiwa mstari ni aina gani ya neno? 

  1. Kitenzi
  2. Kivumishi 
  3. Kiwakilishi 
  4. Kihisishi
  5. Nomino

2. Oanisha maana ya dhana zilizopo katika Orodha B kwa kuoanisha na maneno husika katika Orodha A kisha andika jibu sahihi.

ORODHA A

ORODHA B

(i) Wawe

(ii) Nyiso

(iii) Kongozi

(iv) Kimai

(v) Tendi

(vi) Tenzi

  1. Nyimbo za jandoni na Unyagoni
  2. Nyimbo zinazohusu shughuli za baharini
  3. Nyimbo ndefu za kimasimulizi au za mawaidha
  4. Nyimbo ndefu za masimulizi juu ya matendo ya mashujaa
  5. Nyimbo za kwenye shughuli za kilimo
  6. Nyimbo za kuaga mwaka kwa waswahili
  7. Nyimbo za msibani
  8. Nyimbo za kubembelezea watoto
  9. Nyimbo za kuwaaga walimu

SEHEMU B (Alama 54)

3. Mwalimu wa kidato cha nne aliwaambia wanafunzi wake waunde maneno mapya. Bainisha njia tisa walizotumia kuunda maneno hayo na kwa kila njia toa mfano mmoja.

4. (a) Sentensi za Kiswahili hujipambanua kwa sifa zake. Taja nne (4) 

(b) Changanua sentensi ifuatayo kwa mkabala wa kimuundo

(i) Watu wote walimsikiliza Rais (Kwa njia ya matawi)

5. Tofauti za kimatamshi kwenye baadhi ya maneno katika lugha yenye asili moja ni jambo halikwepeki katika lugha yoyote ile duniani na ipo hata katika lugha yetu ya Kiswahili, je tofauti hizi husababishwa na mambo gani? Toa hoja nne (04) Je hizi tofauti zina umuhimu gani katika lugha ya kiswahii? Toa hoja zako tano (5)

6. Ukuaji na Ueneaji wa lugha ya Kiswahili umepitia vipindi tofauti. Fafanua kwa mifano mambo manne (04) yaliyosaidia kukua na kuenea kwa Kiswahili kipindi cha Waingereza. 

7. (a) Utata katika mawasiliano huweza kusababishwa na mambo mengi. Taja sababu tano zinazosababisha utata katika lugha. 

(b) "Tabibu mzuri ni yule anayejua njia za kutibu ugonjwa" Kwa kutumia msemo huu, onesha njia nne zinazoweza kuondoa utata katika lugha. 

8. (a) Umeanzishwa mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa mpunga katika cha Itunundu kilichopo wilayani Iringa, wewe kama Mratibu wa mradi huo, andika barua ya kuomba kuagiziwa zana za kilimo kwa meneja wa kiwanda cha zana za kilimo kijulikanacho kama kilimo kwanza, chenye anuani S. L. P 3000 Dar es Salaam, jina lako liwe Chungu Tamu wa S. L.P. 400 IRINGA. 

(b) Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yafuatayo; 

1. Wa ubani Rawaziri, na kandoro kadharika, 

Lumbano la kishairi, gazetini kuliweka, 

Nami nimejikusuri, maoni kuyatamka, 

Ua si ruwaza njema, tuzo ya mtu kupewa. 

2. Kutunzwa watu wa enzi, kwa ua sijaridhika, 

Siyo ZAWAD1 azizi, hasa inaheshimika, 

Bado hamjamaizi, kwa tunzo inosifika, 

Ua si ruwaza njema, tuzo ya mtu kupewa.

3. Ua kupewa harusi, nikaha inapofika, 

Na siku ya taanusi, kwa bibi kuheshimika, 

Lakini ua ni tusi, kwa dume kalipachika, 

Ua si ruwaza njema, tuzo ya mtu kupewa.

4. Ua hupambwa maiti, jeneza likapambika, 

Harufu kila wakati, haiba kuongezeka, 

Na wengine hawataki, uchuru watatamka 

Ua si ruwaza njema, tuzo ya mtu kupewa.

MASWALI 

(i) Andika kituo cha shairi hili. 

(ii) Andika kina bahari cha shairi hili. 

(iii) Je, shairi hili limetumia mtindo gani? Toa sababu moja. 

(iv) Je, shairi hili limetumia muundo gini? Toa sababu moja.

SEHEMU C (Maksi 30) 

Jibu maswali mawili tu (2) kutoka katika sehemu hii swali la 9 ni la lazima. 

9. Onesha matumizi ya taswira yalivyo na mchango mkubwa katika kutoa ujumbe kwa jamii. Ukitumia mashairi mawili uliyosoma.

10. "Matatizo ya. Mwanajamii huletwa na mwanajamii mwenyewe" Thibitisha usemi huu kwa kutoa hoja tutu kwa kila riwaya kati ya mbili ulizosoma.

11. Eleza namna wahusika .wafuatao walivyo chukizo kwa jamii FURAHA, ECKO na PADRE JAMES kutoka katika tamthiliya ya ORODHA na CHAUSIKU, JOTI na SUZI kutoka katika tamthiliya ya KILIO CHETU.

ORODHA YA VITABU

RIWAYA

  • TAKADINI - Ben J. Hanson
  • WATOTO WA MAMA NTILIE  - E. Mbogo
  • OKA LA MDIMU -  A. J. Safari

TAMTHILIYA

  • ORODHA - Steve Reynolds - 
  • NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE - E. Semzaba 
  • KILIO CHETU - Medical Aid Foundation

USHAIRI

  • MASHAIRI YA CHEKACHEKA - T. A Mvungi 
  • MALENGA WAPYA - TAKILUKI 
  • WASAKATONGE - Mohamed S. Khatibu

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 210  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 210  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA - MKOA WA SONGWE, HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

MTIHANI KABLA YA MTIHANI WA UTAMILIFU

021 KISWAHILI

MUDA: SAA 3 MACHI, 2024

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11)
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C. Swali la kumi (10) ni la lazima.
  3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B ina alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30)
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali
  5. Simu za mkononi na vitu vingine haviruhusiwi kwenye chumba cha mtihani
  6. Andika namba yako ya mtihani kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia

SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Katika kipengele (i) –(x), chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kijitabu chako cha kujibia.

(i) Maneno yapi kati ya haya yafuatayo yameundwa kwa njia ya ufananisho

  1. Takataka,chepechepe,sawasawa 
  2. Mtutu,kengele,cherehani 
  3. Kengele,teketeke,kiwiliwili 
  4. UKUTA,UKIMWI,CKD 
  5. Shati,gauni,meza

(ii) Zipi ni tanzu kuu za lugha ?

  1. Sarufi na fasihi 
  2.  Irabu na Konsonanti 
  3. Fasihi na Konsonanti 
  4. Sarufi na Irabu
  5. Mazungumzo na maandishi

(iii) Ngeli ipi inazungumzia majina ambayo hayabadiliki umbo katika umoja na wingi

  1. KI-VI 
  2. U-I 
  3. I-ZI 
  4. LI-YA 
  5. U

(iv) “Kiti cha mfalme kinaheshimiwa”katika sentesi hii neno lililopigiwa mstari ni aina gani ya neno katika uainishaji wa maneno?

  1. Kivumishi 
  2. Kiunganishi 
  3. Kitenzi 
  4. Kihusishi 
  5. Kielezi

(v) Kiarifu huu na jozi ipi kati ya zifuatazo?

  1. T,SH,CH,Ts,T,P 
  2. W,N,CH,Ts,T 
  3. CH,SH,W,T 
  4. CH,T,W,KN 
  5. N,T,SH,CH.

(vi) Miongoni mwa changamoto zilizoathiri ukuaji na ueneaji wa Kiswahili wakati wa utawala wa Mwingereza ni…

  1. Kiswahikili kutumika kama lugha ya taifa
  2. Kiswahili kuchukuliwa kama lugha duni
  3. Kiswahili kutumika kwenye vyombo vya habari
  4. Kiswahili kutumika kama lugha ya mawasiliano
  5. Kiswahili kutumika katika shughuli za kibiashara

(vii) Tarihi ni moja wapo katika vipera vya hadithi ambavyo hueleza kuhusu …

  1.  Asili ya vitu kama vile milima,mito 
  2. Kuonya kuhusu maisha ya watu
  3. Kueleza matukio ya kihistoria 
  4. Makosa na uovu wa watu na kueleza maadili yanayofaa
  5. Masimulizi yenye kuchekesha na kukejeli

(viii) Nitungo gani ambayo haigawanyiki katika sehemu ya kiima na kiarifu

  1. Sentensi 
  2. Kishazi 
  3. Kirai 
  4. Kiarifu 
  5. Mofimu

(ix) Jina jingine la mashairi ya kisasa huitwa …

  1. Ukwapi 
  2. Utao 
  3. Mapingiti 
  4. Tarbia 
  5. Inkisari

(x) Herufi za lugha zilipangwa kwa utaratibu maalumu…

  1. Kidahizo 
  2. Silabi 
  3. Vitomeo 
  4. Abjadi 
  5. Neno

2. Chagua kifungu cha maneno kutoka Orodha B kinachotoa maelezo sahihi ya neno katika Orodha A.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Miviga
  2. Muwala
  3. Vigano
  4. Nahau
  5. Ngonjera
  6. Tenzi
  1. Tungo zenye mpangilio wa silabi zinazolingana kila mstari
  2. Kauli fupifupi zenye lugha ya picha
  3. Kauli za maonyo zenye maana iliyofichika
  4. Ufananisho wa habari kutoka ubeti hadi ubeti
  5. Aina ya maigizo ambayo wahusika wake hutumia lugha ya ushairi
  6. Sherehe zinazofanywa na jamii katika vipindi mbalimbali
  7. Hadithi fupi zinazoeleza uovu wa watu kwa kusudi la kuadilisha

SEHEMU B: (Alama 54)

 Jibu maswali yote katika sehemu hii 

3. (a) Taja njia zilizotumika kuunda msamiati ufuatao katika lugha ya Kisawahili

(i) msomi ii. Mwananchi iii. Kizunguzungu iv. Ukimwi v. hela

(b) Kwa kutumia mifano taja njia nne zinazotumika kuunda misimu

4. Katika kila sentensi onesha kiima na kiarifu kwa kutenga na mstari kisha andika K kwa kiima na A kwa kiarifu

  1. mama amelala sakafuni
  2. asha si mkorofi
  3. mwanafunzi aliefaulu amepewa zawadi
  4. yule kijana aliyekuja hapa juzi jioni amefaulu
  5. watoto wote ni watundu

5. (a) Wewe kama mwanafunzi bora wa fasihi waambie wazazi kwa kifupi sana madhara manne yatakayotokana na ukosefu wa elimu ya kijinsia. Tumia tamthilia ya KILIO CHETU

(b) Tambulisha kazi nne za viambishi na kisha toa mfano mmoja kwa kila kazi

6. Kwa kutumia mifano fafanua dhana zifuatazo kama zinazotumika katika fasihi

(i). Tashibiha (ii). Takriri (iii). Sitiari (iv). Tashhisi (v). Mubalagha

7. Ukuaji na ueneaji wa lugha ya Kiswahili umepitia vipindi vingi tofauti. Fafanua kwa mifano mambo manne yaliyosaidia kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili baada ya uhuru

8. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yafuatayo.

Kijiji cha Kivumbi kilikuwa na watu wengi walioishi kwa kushirikiana. Watu wa kijiji hicho walifanya kazi kwa umoja na ushirikiano. Ardhi ya kivumbi ilikuwa kubwa na yenye rutuba lakini chakula kilikuwa haba kutokana na ukame. Ukosefu wa mvua kwa muda mrefu ulisababisha vijito na visima vidogodogo kukauka. Watu wa kijiji cha kivumbi waliishi kwa tabu na mifugo yao ilidhoofu.

Katika kijiji cha kivumbi kulikuwa na mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la Ndumbwi. Mzee Ndumbwi alikuwa na hekima na busara nyingi na hakupendezwa na hali ya kijiji cha kivumbi. Siku moja aliwaita wagtu wote wa kijiji cha kivumbi aliwataka awaambie mawazo yake.

Watu walipokusanyika mzee Ndumbwi alisimama akawaambia “ndugu zangiu nina neno la kuwambia” watu wote wakanyamaza ili wamsikilize. Akamuita mtoto mmoja apite mbele yao akampa kijiti kimoja akamwambia “Vunja” mtoto akakivunja kijiti kile kwa urahisi. Mzee Ndumbwi akampa vijiti kumi vilivyofungwa pamoja ili avivunje mtoto akashindwa kuvunja. Akamuita mzee Kole avivunje nae akashindwa. Vijana kadhaa waliojidai kuwa na nguvu sana wakajaribu mmoja mmoja kuvunja vile vijiti kumi kwa pamoja nao wakashindwa.

Mzee Ndumbwi akasimama akawaambia mfano huu wa vijiti unatuhusu sisi. Mtoto ameweza kuvunja kijiti kimoja kwa urahisi lakini ameshindwa kuvunja vijiti vingi. Vijana hawa pamoja na mzee Kole ni mfano wa ukame. Ni rahisi kwa ukame kumshinda mti mmoaj mmoja kama ilivokuwa rahisi kwa mtoto mmoja kuvunja kile kijiti kimoja, lakini ukame hauwezi kuwashinda watu wengi wanaoshirikiana kwa pamoja.

Baada ya mfano huo, Mzee Ndumbwi aliwasisitiza watu wa kivumbi kushirikiana kama siafu kwa kuwa siafu ni viumbe wadogo lakini wanaweza kumshambulia hata kumuua adui yao. Maelezo yake yaliwapendeza sana wanakijiji.

Siku ile watu wa kivumbi walianza kuweka mikakati ya kukabiliana na tatizo la ukame kijiji humo. Walipatana kiuchimba kisima cha kijiji kila mtu alitoa kitu alichoweza ili kufanikisha zoezi hilo. Watu wa kijiji cha kivumbi walifanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha malengo yao. Baada ya muda kisima kilikamilika maji yakutosha yakapatikana. Watu wa kivumbi walifurahi sana kupata maji kwa ajili ya mahitaji yao na mifugo.

Maswali

  1. Pendekeza kichwa cha habari uliyosoma
  2. Kijiji cha kivumbi kilikumbwa na tatizo gani
  3. Wananchi wa kivumbi walifanya nini ili kuondokana na tatizo lililowakumba katika kijiji chao
  4. Eleza maana ya methali isemayo “ Umojana ni nguvu, utengano ni udhaifu”
  5. Umepata mafunzo gani kutokana na kisa hiki?

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali (2) mawili kutoka sehemu hii, swali la kumi (10) ni la lazima

 ORODHA YA VITABU

USHAIRI

  • Wasakatonge - M. S. Khatibu (DUP)
  • Malenga wapya - TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi ya ChekaCheka – T. A. Mvungi

RIWAYA

  • Takadini – Ben J. Hanson (MBS)
  • Watoto wa mama Ntilie - E. Mbogo (H.P)
  • Joka la Mdimu – A. J. Safari (H.P)

TAMTHILIYA

  • Orodha - Steve Reynolds (MA)
  • Ngoswe Penzi Kitovu Cha uzembe - E. Semzaba (ESC)
  • Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

9. Fasihi ni chuo cha kufundisha maisha ya jamii husika. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma.

10. Washairi ni wataalamu wazuri na waliobobea katika kutumia jazanda zinazotoa ujumbe kwa jamii.Tumia jazanda tatu kwa kila Diwani mbili ulizosoma.

11.Ustadi wa msanii hudhihirishwa na fani.Dhihirisha kauli hii kwa kutumia vipengele vitatu vya lugha kwa kutumia Tamthiliya ulizosoma.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 209  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 209  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OR TAMISEMI) HALMASHAURI YA WILAYA YA RUFIJI

MTIHANI WA AWALI KABLA YA MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA NNE – 2024

021 KISWAHILI

MUDA: SAA 3:00 Ijumaa15 Machi, 2024 Mchana

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali 11.
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B, na maswali mawili (2) kutoka sehemu C. Swali la 11 ni la lazima.
  3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali
  4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  5. Andika Namba yako ya mtihani kwa usahihi katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia

SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kijitabu chako cha kujibia.

i. Babu yetu alitusimulia hadithi inayoeleza sababu zilizomfanya chura awe na ngozi yenye mabakamabaka, ni aina gani ya hadithi Babu aliyosimulia?

A.Vigano B.Visasili C. Tarihi D. Soga E. Ngano.

ii. Bainisha sentensi yenye muundo wa kiwakilishi + kirai kivumishi + kitenzi kikuu + chagizo

  1. Sisi sote tulicheza vizuri sana 
  2. Wale wote wanapenda muziki
  3. Mimi na yeye hatuelewani hata kidogo 
  4. Mwalimu wetu anafundisha vizuri
  5. Sokoni kuna watu wengi.

iii. Ni seti ya maneno inayodhihirisha maneno yaliyoundwa kutokana na Uhulutishaji

  1. Moro, Dar, na Prof 
  2. Ikulu, kitivo na kigoda 
  3. Tawi, kupe na Rais
  4. Nyamafu, chajio na jotoridi 
  5. Barabara, kizunguzungu na kiwiliwili.

iv. Dhima kuu ya mnyambuliko katika lugha ya Kiswahili ni:

  1. Kuficha jambo kwa wasiohusika 
  2. Kuzalisha maneno mapya
  3. Kupatanisha maneno 
  4. Kuunda mizizi ya maneno 
  5. Kuongeza ukali wa maneno.

v. Mwalimu wa Kiswahili aliwafundisha wanafunzi wake vipengele vya maudhui, Unadhani alibainisha vipengele vipi kati ya vifuatavyo?

  1. Mandhari, wahusika, migogoro, dhamira na lugha
  2. Mandhari, lugha, wahusika, muundo na mtindo
  3. Dhamira, ujumbe, migogoro, falsafa na mtazamo
  4. Mtindo, muundo, migogoro, falsafa na lugha
  5. Lugha, dhamira, ujumbe, muundo na mtindo

vi. Ni tamathali ipi ya semi inayohusu ulinganishaji wa vitu tofauti bila ya kutumia maneno ya ulinganishaji au viunganishi?

A. Tabaini B.Mubalagha C.Tashibiha D.Sitiari E. Tashihisi

vii. Mambo gani muhimu ya kuzingatia katika kuteua maneno na miundo ya tungo wakati wa kuzungumza?

  1. Mada, Muktadha, na Mazungumzo ya ana kwa ana
  2. Mada, Mazungumzo na uhusiano wa wazungumzaji
  3. Mada, Mzungumzaji na Muktadha wa wazungumzaji
  4. Mada, Mzungumzaji na Uhusiano wa wazungumzaji
  5. Mada, Muktadha na Uhusiano wa wazungumzaji.

viii. Ipi maana sahihi ya nahau isemayo “ kukaza buti”

  1. Kuongeza juhudi 
  2. Kufunga buti vizuri 
  3. Kupunguza juhudi
  4. Kumkasirikia mtu 
  5. Kuweka sawa buti.

ix. Ubantu wa lugha ya Kiswahili hudhihirika katika vipengele vifuatavyo isipokuwa?

  1. Ngeli za majina 
  2. Tungo za Kiswahili 
  3. Vitenzi
  4. Lugha chotara 
  5. Msamiati wa msingi.

x. Hali ya kuunda nomino kutokana na aina nyengine za maneno huitwa?

A. Utohoaji B. Unominishaji C. Kirai nomino D. Unyambuaji E.Kitenzi jina

2. Oanisha maana ya istilahi zilizopo katika Orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.

Orodha A Orodha B

i. Ni uwekaji wa nomimo mbalimbali za Kiswahili katika makundi yake yanayohusiana

ii. Ni utamkaji wa maneno unaozingatia kanuni za sarufi ya lugha

iii. Ni maneno yanayoonesha uhusiano kati ya neno na neno au kifungu cha maneno na kifungu kingine

iv. Ni vitenzi vinavyoonesha hali ya kuwepo au kutokuwepo kwa kitu, hali au jambo

v. Ni namna ya mtu ya kutamka maneno ambayo humtambulisha mahali anapotokea

vi. Ni njia ya uundaji wa maneno kwa kuchukua vijisehemu vya maneno na kuunda neno jipya

  1. Akronimia
  2. Vitenzi vishirikishi
  3. Lafudhi
  4. Matamshi
  5. Kikundi nomino
  6. Vihusishi
  7. Uhulutishaji
  8. Vitenzi vikuu
  9. Ngeli za nomino
  10. Mkazo
  11. Vihisishi

SEHEMU B (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. (a) Umeshiriki katika mdahalo unaohusu tungo za kiswahili, kwa kuzingatia maana ya sentensi wabainishie washiriki wa mdahalo huo sifa mbili (2) kuu za sentensi.

(b) Kwa kutumia uelewa ulioupata katika somo la Kiswahili, ainisha sentensi (i) – (iv) kisha bainisha muundo wa kila sentensi.

  1. Ugonjwa wa Ukimwi hautibiki wala hauna kinga
  2. Shule zote zilifungwa ulipoingia ugonjwa wa mlipuko
  3. Ajali haina kinga
  4. Ungenisalimia ningekuitikia.

4. Baadhi ya watumiaji wa lugha hufanya makosa ambayo hupelekea kutokea utata katika tungo za Kiswahili. Wewe ukiwa mtaalamu wa Kiswahili, eleza maana ya utata kisha bainisha mambo manne (4) ya kuzingatia ili kuondosha au kupunguza utata katika mawasiliano.

5. (a) Eleza kwa ufupi tofauti kati ya dhana ya ukuaji na ueneaji wa lugha.

(b) Ukiwa mwanafunzi wa kidato cha nne uliyepata maarifa ya Somo la Kiswahili, waelimishe wanafunzi wa kidato cha tatu kwa kuwabainishia changamoto nne (4) zilizoathiri ukuaji na ueneaji wa Kiswahili katika utawala wa Waingereza.

6. Kwa kutumia hoja nne (4) kutoka katika Riwaya ya TAKADINI iliyoandikwa na Ben J. Hanson, fafanua madhara yanayotokana na jamii kushikilia mila na desturi potofu zilizopitwa na wakati.

7. Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata.

Halizuki somo bora, kuliko makosa yetu,
Kosa halina sogora, hulitenda kila mtu,
Zingatia kwa imara, kukosa tabia kwetu.

Kosa likija mapema, kuongoka si vigumu,
Hutengeza mambo vema., utakayo yakatimu,
Hapana kurudi nyuma, na kulegeza hatamu.

Kosa hukuza fikra, na mnyama kuwa mtu,
Kisha huamsha mara, bidii na ari zetu,
Ria zetu hudorora, mpaka tukose kitu,

Kila kiumbe lazima, kosa lake kufahamu,
Ya kuwa ni sura njema, asome aihitimu,
Ndipo awapo mzima, fahamu kuwa timamu.

Makosa yakitukera, ndipo tuzukapo watu,
Na uwezo na busara, kutafuta cheo chetu,
Tukapigana kwa ghera, ushindi ukawa wetu.

Njoo mapema lawama, mwili ungali mgumu,
Usije nina kilema, nimetokwa na fahamu,
Njoo ningali mzima, sijakuwa mahamumu

Makosa yana tijara, kwa kutanabahi mtu,
Kwamba ndipo ishara, ya kupigania utu,
Mpaka tutie fora, katika matendo yetu.

Kosa kitu cha daima, asiyekosa karimu,
Aliyeumba wanyama, na ndege na wanadamu,
Wenye maungo kuuma, na wa uvundo wa damu.

Makosa sikuyabera, silika ya kila mtu,
Tena yana hasara, ilo nzito kwa watu,
Walakini ni tohara, bora ya Maisha yetu.

Hapa mwisho wa kilima, na shairi limetimu,
Likiwa refu si jema, halitakuwa na tamu,
Wazee wetu husoma, tungo ni ladha na hamu.

MASWALI

(a) Eleza maana ya maneno yaliyokolezwa wino kama yalivyotumika katika shairi ulilosoma

(b) Andika kichwa cha shairi hili kisichopungua maneno matano (5)

(c) Taja aina ya tamathali ya semi iliyotumika katika ubeti wa tisa (9)

(d) Bainisha aina ya kituo kilichotumiwa na msanii katika shairi hili.

(e) Eleza mambo mawili (2) yanayomfanya mshairi aamini kuwa hapana somo bora kuliko makosa yetu.

8. Wewe ukiwa kama katibu wa kamati ya ujenzi katika shule yako, andika barua ya kuagiza vifaa vya ujenzi kwa mzabuni aliyepo katika Wilaya yako kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa madarasa unaotarajiwa kuanza hivi karibuni, jina lako liwe MUSA MATATA.

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka katika sehemu hii

ORODHA YA VITABU

USHAIRI

  • Wasakatonge - M.S Khatibu (DUP)
  • Malenga wapya - TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi ya chekacheka - T.A .Mvungi (EP & D.LTD)

RIWAYA

  • Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
  • Watoto wa Mama N’tilie - E.Mbogo (H.P)
  • Joka la Mdimu - A.J.Safari (H.P)

TAMTHILIYA

  • Orodha - Steve Reynold (M.A)
  • Kilio chetu - Medical Aids Foundation (TPH)
  • Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Senzaba (E.C)

9. “Ujenzi wa taswira ni nyenzo muhimu inayotumiwa na washairi ili kufikisha ujumbe kwa jamii” Thibitisha kauli hii kwa kutumia diwani mbili (2) ulizosoma kwa kutoa hoja tatu (3) kutoka katika
kila Diwani.

10. “Waandishi wa riwaya hutumia mbinu mbalimbali katika kuzijenga kazi zao ili kuzifanya ziwe na mvuto” Thibitisha kauli hii kwa kutumia mbinu tatu (3) kutoka katika kila riwaya kati ya Riwaya
mbili (2) ulizosoma.

11. “Elimu ni nguzo muhimu sana kwa vijana na hata wazee, na jamii yeyote inapokosa elimu huweza kusababisha madhara makubwa katika familia na jamii kwa ujumla” Thibitisha kauli hii kwa kutumia Tamthiliya mbili (2) ulizosoma kwa kutoa hoja tatu (3) kutoka katika kila Tamthiliya.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 204  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 204  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA

MTIHANI WA PAMOJA WA WILAYA KIDATO CHA NNE

021 KISWAHILI

Muda: Saa 3:00 Jumanne 19/03/2024 Mchana

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B ina alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45).
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5. Simu za mkonomi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi utakayojibia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua jibu sahihi kutoka katika maswali yafuatayo kisha andika herufi ya jibu sahihi katika sehemu ya kujibia.

(i) “Mtoto anacheza mpira polepole sana” sentensi hii imeundwa na vipashio gani?

  1. N+T+Sh+Ch 
  2. N+T+Sh+Sh+Ch
  3. N+T+Ch+Sh 
  4. N+TS+T+Ch+Sh
  5. Silabi, Neno, Kirai na Sentensi.N+T+Sh+Ch+Sh

(ii) Ni methali ipi kati ya hizi zifuatazo yenye maana sawa sawa na methali “Ndo! Ndo! Ndo! si chururu”

  1. Pole pole ndio mwendo 
  2. Mwenda pole hajikwai
  3. Simba mwenda pole ndio mla nyama 
  4. Haba na haba hujaza kibaba
  5. Bandu bandu humaliza gogo

(iii) Mang’winda amekuwa mtoro sana. Neno lililopigiwa mstari limetumika kama aina gani ya neno?

  1. Kitenzi kikuu 
  2. Kiunganishi 
  3. Nomino
  4. Kitenzi kisaidizi 
  5. Kitenzi kishirikishi

(iv) Ni hali ya viambishi vya maneno ndani ya tungo kukubaliana na kushikamana ili kuletamaanailiyokusudiwa.

  1. Tungo 
  2. Sentensi 
  3. Lugha
  4. Upatanisho wa kisarufi 
  5. Lugha ya mazungumzo

(v) Ni upi mpangilio sahihi wa mjengo wa Tungo?

  1. Kirai, Neno, Sentensi na Kishazi 
  2. Neno, Kirai, Kishazina Sentensi
  3. Kishazi, Kirai, Sentensi na Neno 
  4. Kishazi, Kirai, Sentensi na Neno
  5. Sentensi, Neno. Kishazi na Kirai

(vi) Bainisha tabia ya umbo lililopigiwa mstari katika kitezi ib-w-a

  1. Kaulitendeka
  2. kauli tendea
  3. Kauli tendeana 
  4. Kauli tendwa
  5. Kauli tendesha

(vii) Ipi ni fasili sahihi kuhusu “Vina “miongoni mwa fasili zifuatazo?

  1. Msitari wa mwisho wa shairi unaobadilika ubeti mmoja hadi mwingine.
  2. Mistari wa mwisho wa ubeti wa ushairi wenye kujirudia kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
  3. Idadi ya silabi zinazopatikana katika mstari wa ubeti wa ushairi
  4. Silabi za kati na mwisho za mstari wa ubeti wa shairi zenye mlio unaofanana.
  5. Kifungu cha maneno kinachobeba wazo kuu mojawapo la ushairi

(viii) “Serikali imeweka mikakati kabambe ili kupunguza umaskini” Nenoilikatikasentensihiiniaina ganiyaneno?

  1. Kivumishi 
  2. Kiwakilishi
  3. Kihisishi 
  4. Kielezi
  5. Kiunganishi

(ix) ……………. Ni kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana. Maana hiyo yaweza kuwa ya kisarufi au kileksika;

  1. Isimu 
  2. Shina 
  3. Mzizi
  4. Kiimbo 
  5. Mofimu


(x) Kiti cha mfalme kinaheshimiwa. Katikasentensihiinenolililopigiwamstariniainaganiyaneno katika uainishajiwamaneno?

  1. Kiunganishi
  2. Kihusishi 
  3. Kivumishi
  4. Kiigizi 
  5. Nomino

2. Oanisha maelezo yaliyo katika orodha A ambayo ni aina ya tungo na orodha B ambazo ni aina za maneno yanayo unda tungo hizo kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

Orodha A Orodha B

(i) Mizungu

(ii) Sanaa za ghibu

(iii) Kituo bahari

(iv) Tanakalisauti

(v) Masalalee! Tumekwisha

  1. Anamatopea. Mfano chururu si ndo! Ndo! Ndo!
  2. Ni mstari katika ubeti wa shairi
  3. Mstari wa mwisho wa kila ubeti na hujirudia rudia kwa kila ubeti wa shairi
  4. Miti yote nitakwea, mtarawanda utanishinda
  5. Uzuri unaogusa hisia kama: nyimbo, mziki, ushairi n.k
  6. Ni hadithi zinazoelezea watu wa kale
  7. Ni uzuri unaojitokeza kwenye umbo linaloonekana
  8. Ni mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti
  9. H+T
  10. U+T

SEHEMU B (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Chunguza kwa makini nomino zifuatazo. Kisha kwa kuzingatia aina za nomino, tenganisha nomio hizo katika makundi yake: mbuzi, Ashura, usingizi, kijiko, Januari, jeshi, matatizo, Zanzibar, kamati, Mungu.

4. Taja dhima tano za viambishi awali kwa mifano.

5. Eleza kazi za viambishi vilivyopigiwa mstari

(a) alitukimbia (b) nitakibeba (c) kitoto (d) ukila (e) kilianguka

6. Sentensi zifuatazo zina makosa, zichunguze kwa makini kisha uziandike kwa usahihi

(a) Ninyi wote mmechelewa
(b) Wanafunzi waliyosoma wamefaulu
(c) Ngombe zake zimeuzwa
(d) Walimu wamewakilisha michango yao

7. Si kila mtu anaweza kuwa mhakiki bora. Thibitisha kauli hii kwa hoja 6 (sita).

8. Badilisha simu ifuatayo ya maandishi kuwa barua

HALIMA SAIDI SLP 50 LIWALE NITAKUJA KWAKO MWEZI HUU AMINA

SEHEMU C ( Alama 45)

Chagua maswali matatu kutoka sehemu hii.

9. FasihiSimulizindiofasihi ya awali iliyoanza wakati binadamu alipoanza kutumia lugha. Mara kwa mara inapowasilishwa kwa hadhira huchukua sifa muhimu kadhaa ambazo sio rahisi kuziona katika fasihi Andishi. Thibitisha ukweli huu kwa hoja tano (5).

10. “Kero zinazo jitokeza katika maisha husababisha migogoro katika jamii” jadili kwa kuonesha kero zilizojitokeza katika riwaya mbili ulizosoma jinsi zilivyosababish amigogoro.

11. Kwa kutumia diwanimbiliulizosoma, elezajinsitaswiratatu kutoka katika kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwa jamii.

12. Ugonjwa wa UKIMWI ndio dhamira pekee iliyo jadiliwa na waandishi wengi, jadili kauli hii kwa kutumia tamthilia mbili ulizozisoma.

ORODHA YA VITABU TEULE KWA SWALI LA 10 – 12

TAMTHILIYA

  • Orodha - Steve Raynolds (MA)
  • Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
  • KilioChetu - Medical Aid Foundation

RIWAYA

  • Takadini -Ben J hanson
  • Watoto wa Mama ntilie -Emmanuel mbogo
  • Joka la mdimu -Abdalah J. Safar

USHAIRI

  • Mashairi ya cheka cheka -T. Mvungi
  • Malenga wapya -TAKILUKI (DUP)
  • Wasakatonge -Mohamed Seif Khatibu

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 203  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 203  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

HALMASHAURI YA WILAYA YA GAIRO 

MTIHANI WA KUJIPIMA KABLA YA MTIHANI WA

UTAMILIFU KIDATO CHA NNE

021 KISWAHILI

MUDA SAA 3:00 MCHANA 19/03/ 2024

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na zenye julma ya maswali kumi na mbili(11)
  2. Jibu maswali yote katika sehemu na na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
  3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu alama hamsini nne(54) na sehemu C
    ina alama (30)
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5. Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

 SEHEHU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kijitabu chako cha kujibia.

(i) Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo HAINA maana Zaidi ya moja?

  1. Kaka amefua nguo
  2. Nipe sahani ya kulia
  3. Suedi amenunua mbuzi
  4. Eva amenunua kanga
  5. Joni amempigia mpira

(ii) Kiimbo hutafsiriwaje katika mazungumzo?

  1. Kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti
  2. Kuzungumza na kuongea kwa sauti
  3. Kuzungumza kwa kupandisha mawimbi ya sauti
  4. Kuzungumza kwa kushusha mawimbi ya sauti
  5. Kuzungumza na kushuka kwa mawimbi ya sauti

(iii) Mkisi ameenda Dodoma. Neno Dodoma limetumika kama aina gani ya neno?

  1. Kielezi
  2. Nomino
  3. Kivumishi
  4. Kiwakilishi
  5. kihisishi

(iv) “Changa bia” nahau hii katika lugha ya Kiswahili ina maana ipi?

  1. Kuepuka matatizo kwa ujanja
  2. Fika mwisho
  3. Kula kwa ushirika
  4. Chombo kipo hatarini
  5. Kumaliza kikao

(v) Mawazo makuu ya mtunzi wa kazi za fasihi humfikia mlengwa kwa njia ipi kati ya hizi zifuatazo?

  1. Fani
  2. Maudhui
  3. Dhamira
  4. Falsafa
  5. Migogoro

(vi) Ipi ni tofauti ya msingi kati ya mashairi na ngonjera?

  1. Mpangilio wa vina na mizani
  2. Idadi ya mizani na mishororo
  3. Majibizano baina ya watu wawili au Zaidi
  4. Mpangilio maalumu wa silabi na lugha ya mkato
  5. Mapigo ya kimuziki na ridhimu

(vii) Jambo gani muhimu huzingatiwa na mtunzi wa insha ya hoja?

  1. Lugha yenye ukinzani
  2. Lugha ya kisanaa
  3. Lugha isiyo na mvuto
  4. Lugha ya kufikirisha
  5. Lugha inayosifia

(viii) Uwasilishaji wa kazi za fasihi unatofautiana kati ya mtunzi mmoja na mwingine huitwaje?

  1. Muundo
  2. Mtindo
  3. Maudhui
  4. Falsafa
  5. Fani

(ix) Unyambulishaji katika lugha ya Kiswahili huhusisha upachikaji wa viambishi___

  1. Kabla ya mzizi
  2. Katikati ya mzizi
  3. Baada ya mzizi
  4. Kabla na baada ya mzizi
  5. Kabla, katikati na baada ya mzizi

(x) Ili kuepuka utata katika tungo, ni muhimu 

  1. Kuepuka matumizi ya maneno yenye maana Zaidi ya moja
  2. Kutumia nahau
  3. Kutumia aina zote za maneno katika tungo
  4. Kutumia alama za uandishi
  5. Kutumia mofu ya kauli ya kutendea

2. Oanisha dhana za nyimbo zilizopo katika ORODHA A na aina ya nyimbo katika ORODHA B Kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijedwali hapo chini.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Huimbwa jandoni
  2. Huimbwa wakati wa kilimo
  3. Huimbwa wakati wa shughuli za baharini.
  4. Huimbwa wakati wa kuuaga mwaka.
  5. Huimbwa katika michezo ya watoto.
  6. Huimbwa katika msiba.
  1. Kongozi.
  2. Tenzi.
  3. Kimai
  4. Wawe.
  5. Nyimbo za Watoto
  6. Nyiso.
  7. Mbolezi.

SEHEMU B. (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. (a) Eleza dhima za mofimu “li” kama ilivyotumika katika sentensi zifuaatazo:-

  1. Shamba letu li kubwa sana.
  2. Walichelewa kurudi.
  3. Tunalifuatilia
  4. Limeharibika
  5. Shikilia

(b) Andika sentensi zifuatazo katika hali ya ukanushi.

  1. Ameshiba sana
  2. Watoto wengi wanaogelea
  3. Mvua ilinyesha kwa wingi sana
  4. Kijana anakula chakula kingi sana

4. (a) Utata katika mawasiliano husababishwa na mambo mengi.Taja sababu Tano (5) zinazosababisha Utata katika lugha.

(b)  "Tabibu mzuri ni yule anayejua njia za kutibu ugonjwa"ukitumia msemo huu onesha njia nne (4) zinazoweza kuondoa Utata katika lugha.

5. "Mwalimu wa kidato Cha nne aliwaambia wanafunzi wake waunde maneno mapya."Bainisha njia Tisa (9) walizozitumia kuunda maneno hayo na Kwa Kila njia toa mfano mmoja.

6. Malimusi na Wasakatonge walikuwa wanajadili kuhusu tenzi na mashairi , Malimusi anasema tenzi na mashairi zote ni tungo za kishairi hivyo zinafanana lakini Wasakatonge alikinzana na Malimusi kwa hoja kuntu. Jadili upande wa Wasakatonge kwa hoja sita (6) huku ukitolea mifano hoja zako.

7. Asasi mbalimbali zilizoanzishwa kabla na baada ya Uhuru,mfano UKUTA (1959) na TATAKI(2009) Kwa lengo la kukuza na kuendeleza kiswahili.Onesha changamoto SITA sinazozikumba asasi hizo katika ukuzaji wa kiswahili.

8. Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali yafuatayo.

Ndugu wazazi,kumbe safari yenu inahusu harusi ya Zaituni? Mkuu wa shule aliwauliza wazazi “ndiyo” wazazi walijibu kwa Pamoja bila aibu. “inategemewa kufungwa lini”? mkuu aliendelea kuhoji. Harusi hii ilikuwa ifanyike wakati zaituni anapofika kidato cha nne,lakini zainabu huyu ametufanyia uhuni na vituko visivyoelezeka . nasi sasa tunachukiwa na Kijiji kizima na kudharauliwa na kila mtu.

Hii imetuudhi sana, tumetungiwa nyimbo na kufanyiwa kila shutuma. Hatuna raha; hivyo tumeonelea bora tuje kukuomba umfukuze shule ili kiburi kimwishe.

Nasi tupo tayari kukulipa kiasi chochote cha fedha ukitimiza haja yetu hii, “mzee Abdallah alieleza”. Muda wote mkuu wa shule alikuwa akimtazama mzee kwa chata sana.Kisha akauliza swali la kuchochea Zaidi, “zaituni ana kiburi kumbe”

Mama Zaituni hakutaka hilo limpite himahima akatoa maelezo yake. “Mama wewe, zaituni usimuone hivi”. Zaituni mwanangu hataki kufuata utamaduni wetu wa kuolewa. Zaituni ati achague mchumba mwenyewe, ati mahari haioni kama ni kitu cha msingi. Kiburi hicho kinatokana na elimu mliyompa. Mtoto sasa ameharibika. Anafanya apendavyo, elimu gani isiyojali adabu, wala utii?” mama zaituni alimaliza huku jasho na machozi yanamtoka.

Hapa mkuu wa shule aliona kwanza awaelimishe kabla hajawatolea kauli ya mwisho. Alikwishatambua kwamba wazazi wa zaituni walikuwa wameachwa nyuma na wakati. Kila upya wa mawazo waliuita kiburi.

MASWALI

  1. Wazazi wa Zaituni walikwenda shuleni kufanya nini?
  2. Wazazi walisema kuwa Zaituni amefanya kosa gani?
  3. Eleza mgogoro mkuu uliopo kati ya Zaituni na wazazi wake.
  4. Fupisha Habari hiyo kwa maneno yasiyopungua hamsini( 50) na yasiyozidi sitini(60).


SEHEMU C. (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka katika sehemu hii, Swali la kumi ni lalazima.

ORODHA YA VITABU 

USHAIRI

  • Wasatonge – M. S Khatibu (DUP)
  • Malenga wapya - TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi ya chekacheka - T. A. Mvungi (EP& D. LTD)

RIWAYA

  • Takadini - Ben. J. Hanson (MBS)
  • WAtoto wa mama N’tilie - E. Mbogo(H.P)
  • Joka la mdimu - A. J. Safari (H.P)

TAMTHILIYA

  • Orodha - Steve Reynolds (M)
  • Ngoswe penzi kitovu cha uzembe - E. Semzaba(ESC)
  • Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

9. Msanii yeyote wa kazi ya fasihi anafananishwa na mwavuli kwa jamii yake, kwa kuwa anatumia macho yake kuona maovu yaliyomo katika jamii na hutumia kalamu yake kuishauri na kuikinga jamii yake isipatwe na mabaya. Thibitisha kauli hii kwa kudadavua maovu yaliyoibuliwa na waandishi wa riwaya mbili ulizosoma. Hoja tatu kwa kila riwaya.

10. Waandishi wengi wa fasihi hupenda kutumia jazanda mbalimbali katika kuelimisha jamii katika maswala kadha wa kadha.Hivyo tumia jazanda mbalimbali kutoka diwani mbili ulizosoma kuonesha walivyosaidia kuelimisha jamii.Toa hoja tati(3)wa Kila kitabu.

11. "Uibushaji WA migongano katika tamthiliya ni nyenzo muhimu katika ufanikishaji wa tamthiliya "Kwa kutumia vitabu viwili(2)kati yavile ulivyosoma,Jadili kauli hii Kwa kutoka hoja tati (3) Kwa Kila kitabu.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 202  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 202  

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA UTIMILIFU KIDATO CHA NNE KANDA

(MIKOA YA MBEYA, SONGWE, NJOMBE, RUKWA & KATAVI)

021 KISWAHILI

MUDA SAA 3 MWAKA 2023

MAELEKEZO:

  1. Karatasi hii ina sehemu A,B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11)
  2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A na B na chagua maswali mawili (2) tu kutoka sehemu C. Swali la 11 ni la lazima.
  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
  4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa kwenye mtihani havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  5. Kumbuka kuandika Namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia.

SEHEMU A: (alama 16)

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika sehemu hii. Andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu hako cha kujibia.

i. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?

  1. Kiunganishi 
  2. Kivumishi 
  3. Kihisishi 
  4. Kiwakilishi 
  5. Kielezi [     ] 

ii. Njia ipi ya kuhifadhi fasihi simulizi imetokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia?

  1. Njia ya kichwa 
  2. Njia ya maandishi 
  3. Njia ya simu
  4. Njia ya kanda za Sinema na Video 
  5. Njia ya magazeti.[     ] 

iii. Zifuatazo ni dhana sahihi za mswahili isipokuwa:-___________

  1. Mtu mwenye maadili mema 
  2. Mzaliwa wa pwani
  3. Mtu yeyote anayezungumza Kiswahili 
  4. Mtu mwenye asili ya kiafrika
  5. Mtu yeyote mjanja, azungumzaye sana pia muongo.[     ] 

iv. Joshua ni mwanafunzi wa kidato cha nne alialikwa kwenye sherehe ya matambiko na alipata nafasi ya kuongea ili kuwaelimisha jamii kuhusiana na athari za matambiko na alitoa athari moja ambayo ni,__________

  1. Hukuza na kudumaza ubunifu 
  2. Sherehe husababisha ugomvi, chuki na uhasama
  3. Hujenga dhana potofu katika jamii 
  4. Husaidia kukuza uongo na uwoga
  5. Huongeza hasira kwa mizimu [     ] 

v. Wafanyabiashara kutoka Rukwa na Iringa walikutana kwa lengo la kufanya biashara, lakini kati yao ilizuka lugha ambayo ilirahisisha mawasiliano katika biashara zao. Kwa kutumia maarifa ya somo la Kiswahili lipi ni jina la lugha hiyo kati ya majinayafuatayo?_______

  1. Lugha ya vizalia 
  2. Pijini
  3. Kibantu 
  4. Kiswahili 
  5. Kunguja [     ] 

vi. Oi na Mari waliafikiana kuwa “watamfitinia” mwalimu wao kwa mkuu wa shule yao. Je azimio hilo la Oi na Mari lipo katika kauli ipi kati ya zifuatazo?

  1. Kutenda 
  2. Kutendana 
  3. Kutendea 
  4. Kutendeana 
  5. Kutendewa  [     ] 

vii. Asia aliandika habari kuhusu nchi ya Tanzania, katika habari hiyo alizingatia mpangilio mzuri na unaoeleweka kwa wasomaji wa habari yake, Je kwa uelewa wako alichokizingatia Asia kinajulikana kama nini?

  1. Mantiki 
  2. Insha 
  3. Wazo 
  4. Ayaaa 
  5. Kistari  [     ] 

viii. Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi Fulani ya kifasihi?________

  1. Muundo wa kazi husika 
  2. Wahusika wa kazi husika 
  3. Jina la kazihusika
  4. Jina la mtunzi wa kazi husika 
  5. Mtindo wa kazi husika  [     ] 

ix. Bainisha sentensi ambatano zenye muundo wa sentensi changamano mbili kati ya sentensi zifuatazo______ 

  1. Gari lililomteka tumeliona na dereva aliyetekwa ameonekana
  2. Mtoto aliyeumia jana amelazwa na mtoto mwingine hajitambui
  3. Mpe haki yake yote iliyopotea ili naye akupe haki yako yote
  4. Baba anayetaka kujenga nyumba anaumwa lakini mama hataki kabisa kumuuguza
  5. Uchaguzi uliofanyika juzi umezaa matunda  [     ] 

x. Dhima kuu ya rejesta katika lugha ni ipi?____________

  1. Kurahisisha mawasiliano katika shughuli maalum 
  2. Kuunda mzizi wa neno
  3. Kupatanisha maneno 
  4. Kuunganisha maneno mawili tofauti
  5. Kutambulisha aina za maneno  [     ] 

2. Oanisha maelezo ya dhana yaliyo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika Orodha B. kisha andika herufi husika katika karatasi ya majibu.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Huonesha maana katika mazingira maalumu.
  2. Kanda
  3. Maigizo mafupi yaliyojaa ucheshi na mzaha
  4. Wingi wa shule
  5. Huunganisha maneno mawili yenye hadhi tofauti
  6. Shamirisho
  1. Vichekesho
  2. Shule
  3. Ni kipashio cha kiarifu
  4. Kiunganishi
  5. Mashule
  6. Neno tata
  7. Miviga
  8. Kihusishi
  9. Rejesta

SEHEMU B: (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. (a) Bainisha mzizi wa asili wa kila neno katika maneno yafuatayo:

i. Mkimbizi 

ii. Mlaji

iii. Muumbaji 

iv. Nisingelipenda 

v. Waligawana

(b) Upatanisho wa kisarufi ni kigezo kimojawapo kati ya vigezo vya kuunda ngeli za nomimo. Thibitisha dai hili kwa kutunga sentesi mbili katika kila ngeli kwenye ngeli zifuatazo:-

i. Ngeli ya pili ii. Ngeli ya tatu iii. Ngeli ya nne iv. Ngeli ya tano

4. (a) Fafanua maana ya misimu kama inavyofasiriwa katika lugha ya Kiswahili

(b) Misimu ina sifa nyingi katika lugha ya Kiswahili. Taja sifa tano za misimu katika lugha.

5. (a) Tofautisha dhana ya kukua na kuenea kwa lugha ya kiswahili.

(b) Ukuaji na ueneaji wa lugha ya Kiswahili, umepitia vipindi vingi tofauti, fafanua kwa mifano mambo sita (6) yaliyosaidia kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili baada ya uhuru.

6. (a) Nini maana ya semi?

(b) Semi zina vipera vyake. Fafanua vipera vitano na kutoa mfano mmoja kwa kila kipera.

7. Soma simu ifuatayo kwa makini, kisha jibu swali linalofuata chini yake;

image

Kutoka katika simu hiyo hapo juu, jifanye unasoma shule ya sekondari Makolo SLP 13 Njombe, Andika barua kwa mkuu wa shule kupitia kwa mwalimu wa darasa kuomba ruhusa ya siku nane (8).

8. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata chini yake:

Maimuna alikuwa ni binti mwenye miaka sita alipokuwa anaanza kusoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Minjingu. Alikuwa na tabia, sura na umbo zuri. Pia alikuwa na uwezo mkubwa darasani na ndoto ya kusoma mpaka chuo kikuu na kuishi maisha mazuri baadaye. Kutokana na tabia yake na uwezo wake mzuri darasani, walimu walimpenda sana na kumtia moyo mara kwa mara katika masomo yake.

Tabia ya Maimuna ilianza kubadilika siku hadi siku alipofikia darasa la sita baada ya kufikisha umri wa kuvunja ungo. Kwani alizidi kunawiri na umbo lake likazidi kuonekana vizuri. Mabadiliko hayo yalitokana na yeye kujiingiza katika suala la mapenzi ambapo alikuwa akifuatwa na wavulana wengi kwa sababu ya umbile lake la kuvutia.

Baada ya kuhitimu elimu ya msingi, Maimuana alijiunga na elimu ya sekondari na hapo ndipo suala la mapenzi kwake lilizidi kupamba moto zaidi mpaka kufikia hatua ya kutojali kitu chochote duniani. Yeyote yule ambaye angejitokeza kumueleza habari za mapenzi hakuweza kukataa. Kutokana na tabia hiyo watu walimfananisha na daladala ambayo hupandwa na kila mtu, nguo ambayo huvaliwa na kila mtu na dampo ambapo kila uchafu hutupwa. Tabia yake iliendelela mpaka chuo kikuu ambapo ilifika hatua ya kutoa mimba hovyohovyo bila kuwaza njia njia zitumikazo kuzuia. kukimbilia hospitalini kupima afya yake na daktari alibaini ana ugonjwa wa UKIMWI pia alikuwa amepoteza uwezo wa kubeba mimba.

Hatimaye Maimuna alihitimu masomo yake na kupata mchumba na ndoa ikafanyika. Siku ya ndoa hiyo halaiki ya watu walihudhuria kwenye sherehe. Baada ya miezi mitano Maimuna alipata homa kali na Maskini! Maimuna alisikitika sana alipopata habari hizo na mwisho daktari alimshauri ameze dawa, ale matunda, afanye mazoezi, apumzishe mwili wake, aishi kwa matumaini na kumrudia Muumba wake. Maswali:

i. Pendekeza kichwa kinachofaa kutokana na habari uliyosoma.

ii. Eleza maana ya maneno yaliyokolezwa wino kama yalivyotumika kwenye habari.

iii. Daktari alimshauri nini Maimuna baada ya kupima afya yake? (Hoja mbili)

iv. Ni sababu ipi iliyopelekea tabia ya Maimuna kubadilika?

SEHEMU C : (Alama 30)

Jibu maswali mawili katika sehemu hii, swali la kumi na moja (11) ni la lazima.

ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 10-11

TAMTHILIYA:

  • KILIO CHETU – MEDICAL AID FOUNDATION
  • NGOSWE – PENZI KITOVU CHA UZEMBE – E. SEMZABA
  • ORODHA – STEVE REYNOLDS

RIWAYA

  • JOKA LA MDIMU – A. SAFARI
  • TAKADINI – BEN J. HANSON
  • WATOTO WA MAMANTILIE – E. MBOGO
  • DIWANI
  • MALENGA WAPYA – TAKILUKI

USHAIRI

  • MASHAIRI YA CHEKACHEKA – THEOBALD MVUNGI 
  • WASAKATONGE – MOHAMED KHATIB

9. Msanii yeyote wa kazi ya fasihi anafananishwa na mwamvuli kwa jamii yake, kwakuwa anatumia macho yake kuona maovu yaliyomo katika jamii na hutumia kalamu yake kuishauri na kuikinga jamii yake isipatwe na mabaya. Thibitisha kauli hii kwa kudadavua maovu yaliyoibuliwa na waandishi wa riwaya mbili ulizosoma. Hoja tatu kwa kila riwaya.

10. Kutokukubaliana miongoni mwa wanajamii kumekuwa chanzo cha mivutano mbalimbali kati yao na kupelekea kukosekana kwa amani, utulivu na utengamano katika jamii. Onesha ukweli wa kauli hii kwa kufafanua mivutano iliyoibuliwa na waandishi wa tamthiliya mbili ulizosoma kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu.

11. Ubora wa mashairi haubebwi na maudhui yake tu bali kwa kiasi kikubwa huchagizwa na lugha itumikayo katika kazi hizo. Jadili kauli hii ukieleza jinsi waandishi walivyotumia jazanda kuboresha na kupamba kazi zao. Hoja tatu kwa kila diwani.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 178  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 178  

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA TABORA

 MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA, KIDATO CIA NNE

021 KISWAHILI

(Kwa Watahiniwa Walioko na Wasioko Shuleni)

Muda: Saa 3 Jumanne, Mel 9, 2023, Mchana.

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jurnla ya maswali 11.
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili kutoka sehemu C. Swali la 11 ni lazima.
  3. Sehemu A na B ina Alama 70 na sehemu C ina Alama 30.
  4. Andika kwa kutumia kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  5. Vifaa vya mawasiliano na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Zingatia maelekezo ya kila sehemu ya swali.
  7. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEIIEMU A: (ALAMA 16)

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele Cha (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu Cha kujibia ulichopewa.

(i) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza hisia za mtenda au mtendwa

  1. Kiunganishi
  2. Kivuinishi
  3. Kihisishi
  4. Kielezi
  5. Kiswaltili

(ii) Kategoria ya kisarufi inayowakilisha wakati katika kitenzi.

  1. Leksimu
  2. Kiambishi
  3. Shina
  4. Mtenda/mtendwa
  5. Njeo

(iii) Sarah alipozunguniza kwa mara ya kwanza kwenye mkutano walimgundua kuwa ametoka mkoa wa Mara, Kitu gani kilimfanya agundulike?

  1. Kushuka na kupanda kwa sauti yake
  2. Mkazo wa sauti yake
  3. Uongeaji wa taratibu
  4. Umbo lake namba nane
  5. Lafudhi yake

(iv) Kifungu cha maneno ambacho hujibu maswali ya ziada kuhusu tendo katika sentensi huitwa?

  1. Kiingizi
  2. Kirai nomino
  3. Tungo
  4. Kirai kielezi
  5. Kikundi kivumishi

(v) Dhana mojawapo kati ya hizi huwa na dhima ya kuokoa muda

  1. Ufahamu
  2. Fasihi
  3. Lugha fasaha
  4. Masimulizi
  5. Hadithi

(vi) Ipi ni tofauti ya msingi kati ya Mashairi na Ngonjera?

  1. Mpangilio wa vina na mizani
  2. ldadi ya mizani na mshororo
  3. Majibizano baina ya watu wawili au zaidi
  4. Mpangilio maalumu wa silabi na lugha ya mkato
  5. Mapigo ya kimuziki na ridhimu

(vii) Ni muundo upi wa ushairi wa fasihi unaundwa na mistariimishororo mitano?

  1. Sabilia
  2. Takhmisa
  3. Tathmisa
  4. Tathlita
  5. Tashibiha

viii. Neno mama lina mofimu ngapi?

  1. Nne
  2. Mbili
  3. Tatu
  4. Moja
  5. Tano

ix. Kanuni za kipekee katika utunzi wa kazi za fasihi andishi ambazo hutofautisha utunzi mmoja wa fasihi andishi na utunzi ni Nvingine usio wa kifasihi hujulikana kama:

  1. Mtindo
  2. Muundo
  3. Wahusika 
  4. Matumizi ya lugha 
  5. Tungo

x. Mtangazaji wa televisheni huhakikisha watazamaji wanapata habari sahihi kwa wakati. Katika fasihi kazi hiyo hufanywa na nani kati ya hawa wafuato? 

  1. Wasikilizaji
  2. Hadhira
  3. Fanani
  4. Wasomaji 
  5. Wazungumzaji

2. Oanisha maana ya dhana zilizopo katika orodha A na dhana husika katika orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Kongozi
  2. Kimai
  3. Wawe
  4. Nyiso
  5. Mbolezi
  6. Bembea
  1. Huimbwa jandoni
  2. Huimbwa wakati wa kilimo
  3. Huimbwa wakati wa shughuli za baharini
  4. Huimbwa wakati wa kuaga mwaka
  5. Huimbwa katika michezo ya watoto
  6. Huimbwa katika msiba
  7. Huimbwa ili kubembeleza watoto
  8. Huirnbwa ili kusifia Taifa

SEHEMU B; (ALAMA 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. 

  1. Unaelewa nini kuhusu dhana ya misimu?
  2. Onesha vyanzo viwili vya misimu
  3. Misimu huweza kuundwa kwa njia tofauti tofauti. Eleza njia zilizotumika kuunda misimu ifuatayo
  1. Demu
  2. Kumzimikia
  3. DISCO
  4. Ferouz ni twiga
  5. Mataputapu

4. Batuli alitaka kuhifadhi methali na vitendawili kwa njia ya kichwa tu kwa ajili ya kizazi kijacho. Lakina Kibuyu alimkataza asifanye hivyo badala yake atumie njia nyingine

  1. Toa hoja nne (4) kama sababu ya katazo hilo
  2. Taja njia tano (5) sahihi ambazo unahisi Kibuyu angemshawishi batuli atumie.

5. Ukiwa kama Mtendaji wa Kata ya Chemchem andaa hotuba utakayoisoma mbele ya
viongozi wa chini yako kuhusu ufanikishaji wa ujenzi wa madarasa katika kata yako.

6. Eleza kinagaubaga tofauti zilizopo kati ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo;

  1. Uwasilishaji
  2. Uhifadhi
  3. Mabadiliko

7. Upatanisho wa kisarufi ni kigezo kimojawapo kati ya vigezo vya kuunda ngeli za nomino. Thibitisha dai hilo kwa kutunga sentensi ukitumia ngeli zifuatazo:-

  1. U -I
  2. U -ZI
  3. KI - VI
  4. LI -YA
  5. U - YA
  6. U — WA

8. Soma kifungu habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

"Ndugu wazazi, kumbe safari yenu inahusu harusi ya Maria ?".Mkuu wa shule aliwauliza wazazi."Ndiyo," wazazi walijibu kwa Pamoja bila aibu."inategemewa kufugwa lini ."Mkuu aliendelea kuhoji. Harusi hii ilikuwa ifanyike wakati Maria anapofika kidato cha nne, Lakini Maria huyu ametufanyia uhuni na vituko visivyoelezeka. Nasi sasa tunachukiwa kijiji kizima na kudharauliwa na kila mtu.Hii imetuudhi sana, tumetungiwa nyimbo na kufanyiwa kila shutuma. Hatuna raha ;hivyo tumeonelea bora tuje kukuomba umfukuze shule ili kiburi kimwishie .Nasi tupo tayari kukulipa kiasi chochote cha fedha ukitimiza haja yetu hii,"Mzee Abdallah alieleza." Muda wote mkuu wa shule alikuwa akimtazama Mzee kwa chati sana .Kisha akauliza swali la kuchochea zaidi: Maria ana kiburi kumbe?"

Mama Maria hakutaka hilo limpite ,hima hima akatoa maelezo yake ."Mama wewe ,Maria usimuone hivi. Maria mwanangu hataki kufuata utamaduni wetu wa kuolewa. Maria ati achague mchumba mwenyewe, ati mahari haiyoni kama ni kitu cha msingi. Kiburi hicho kinatokana na elimu mliyompa.

Mtoto sasa ameharibika .Anafanya apendavyo elimu gani isiyojali adabu.wala utii?" Mama Maria alimaliza huku jasho na machozi yanamtoka".

Hapa mkuu wa shule aliona kwanza awaelimishe kabla hajawatolea kauli ya  mwisho.Alikwishatambua kwamba wazazi wa Maria walikuwa wameachwa nyuma na wakati .Kila upya wa mawazo waliuita kiburi.

Maswali

  1. Bainisha dhima nne (04) zilizotokana na habari uliyosoma.
  2. Fupisha habari hiyo kwa maneno yasiyopungua 70 na kuzidi 80.

SEHEMU C: (ALAMA 30)

Jibu maswali mawili kutoka katika sehemu hii, swali la 11 ni lazima

ORODHA YA VITABU.

USHAIRI. 

  • Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP).
  • Malenga wapya -TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi ya Chekacheka - T.A.Mvungi(EP&D.LTD)

RIWAYA. 

  • Takadini -Ben J.Hanson (MBS)
  • Watoto wa Mama N'tilie - E.Mbogo(HP)
  • Joka la Mdimu - A.J.SaiTari (HP)

TAMTHILIYA

  • Orodha - Steve Reynolds(MA)
  • Ngoswe Penzi Kitovu Cha uzembe - E. Semzaba (ESC)
  • Kilio chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

9. Fasihi ya Kiswahili imemuweka mwanamke katika hadhi tofauti tofauti. Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila riwaya.

10. Chanzo cha matatizo mengi ya jamii nyingi huletwa na kusababiskwa na mwanajamii mwenyewe. Thibitisha dai hili kwa kutumia tamthilia mbili ulizozisoma. Toa hoja tatu kwa kila tamthilia.

11. Eleza kwa mifano madhubuti sababu tano (05) za uamuzi wa kuendelea kutumia Kiswahili katika mawasiliano mara tu baada ya uhuru.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 152  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 152  

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA LINDI

MTIHANI WA DHIHAKA

KISWAHILI

KIDATO CHA NNE

021

 MUDA: 3:00                                                                                            MEI  2023

MAELEKEZO:

  1.                Mtihani huu una sehemu A, B, na C wenye jumla ya maswali 11.
  2.                Jibu maswali yote sehemu A, B na maswali mawili kutoka sehemu C, ambapo swali la 9 ni la lazima.
  3.                Andika namba ya mtihani katika kila kurasa za karatasi yako ya kujibia.
  4.                Zingatia maelekezo ya kila swali na kila sehemu.

SEHEMU A :( ALAMA 16)

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele(i) hadi(x), kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.

  1. Mtunzi wa kazi ya fasihi kipindi anataka kuteua wahusika alikuwa anatafakari ni kwa vipi atateua wahusika wa kazi yake,msaidie mtunzi huyo ili aweze kubaini ni seti ipi inawakilisha kikamilifu wahusika wa fasihi simulizi?

)vitu,mahali,wanyama,binadamu,fanani na maleba.

B)Hadhira,wanyama,maleba,binadamu na fanani.

C)Hadhira,binadamu,wanayama,vitu  na fanani.

D) Fanani,vitu,mahali,binadamu,maleba na wanyama.

 

  1. Baba alinunua viatu vizuri.  Vizuri vyote viliwekwa kabatini. Dada alivipanga vizuri. Katika mfuatano wa sentensi hizo neno VIZURI limetumika kama.
  1.               Kiwakilishi,kivumishi na kielezi.
  2.               Kivumishi ,kielezi na kiwakilishi.
  3.               Kiwakilishi,kitenzi na kielezi.
  4.              Kivumishi, kiwakilishi na kielezi.

 

  1. Bibi yangu binti zilipendwa huwa anatusimulia hadithi kila ifikapo usiku ijapokuwa hakuwahi kwenda shule, je unafikiri bibi  yangu anatumia njia ipi ya uhifadhi wa kazi ya fasihi simulizi?

A)Maandishi.

B) Kichwa.

C).Mikanda ya video.

D)Kinasa sauti.

 

  1. Uchanganuzi wa sentensi kwa mkabala wa kimuundo hujikita katika……
  1.               A Kiima na kiarifu
  2.               Kirai nomino na kivumishi
  3.               Kirai kitenzi na kishazi tegemezi kielezi
  4.              Kirai nomino na kirai kitenzi.

v.Kumbilamoto na Mchapakazi walikuwa wakibishana kuhusu miundo ya kiima na 

kiarifu.Mchapakazi alitaja miundo ya kiima kuwa ni N ,W ,V , na  KTG(BV).Je unadhani 

Kumbilamoto alitaja miundo ipi ya kiarifu.

  1.               T, Ts+ T,  t+ Sh, Sh, Ch.
  2.               W+ N+  T+ V+ Sh.
  3.               Ch + Sh , T+Ts.
  4.              T  ,T+Ts ,N +  KTg.

Vi.Katika ufundishaji wa muundo wa mashairi mwalimu alielezea kuhusu uwepo wa idadi ya 

mistari katika beti .Je unafikiri mwalimu alipofundisha shairi lenye idadi ya mistari mitano 

kwa kila ubeti alitaja jina gani?

  1.               Tarbia.
  2.               Tathilitha.
  3.               Takhimisa.
  4.              Sudusia.

Vii. “Mtangazaji wa televisheni kuhakikisha watazamaji wanapata habari  sahihi na kwa 

wakati” katika fasihi ,kazi hiyo hufanywa na nani kati ya hawa wafuatao?

  1.               Wazungumzaji
  2.               Hadhira
  3.               Fanani
  4.              Wasomaji.

viii.  Maneno yapi kati ya haya yafuatayo yameundwa kwa njia ya uambatanishaji?

  1.               Mwanahewa, kizunguzungu ,mwimbaji.
  2.               . Shamrashamra, televisheni,  kataupepo.
  3.               . Kifaurongo,  kisimbuzi, miundombinu.
  4.              .Mbwamwitu, mitishamba,  Afisaelimu.

 

ix.  Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana zaidi ya moja.

  1.               .Kaka amefua nguo.
  2.               Nipe sahani ya kulia.
  3.               Suedi amenunua mbuzi.
  4.              . Eva amenunua kanga.

 

 

x.   Kiswahili kilianza kutumika kama lugha ya mawasiliano na kufanywa kuwa lugha ya Taifa nchini 

Tanganyika wakati gani?

  1.               Enzi ya utawala wa waingereza.
  2.               .Enzi ya utawala wa wajerumani.
  3.               . Enzi ya utawala wa waarabu.
  4.              . Baada ya kupata uhuru.

 

2. Oanisha Maelezo yaliyopo katika Orodha A na dhana zilizopo katika Orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi.

ORODHA “A”

ORODHA  “B”

i .Imani na mawazo ya mwandishi kuhusu uhusiano wa watu katika jamii

  1.               Muwala

ii. Hali ya mwandishi kutetea mawazo yake bila kutetereka

  1.               Itikadi

iii.  Uwiano wa mambo katika kazi ya fasihi

  1.                Msimamo

iv. Namna mwandishi anavyoyaona mambo kwa upana na kusimamia imani yake katika maisha

  1.              Mtindo

v. Utofautisha mwandishi mmoja na mwingine

E . Tenzi

Vi .Tungo ndefu za kishairi zenye usimulizi wa visa na matukio.

        F.    Mtazamo

 

  1.              Muundo

 

  1.              Ngonjera

 

  1.                  Falsafa

 

SEHEMU B. (ALAMA 54)

3.    a)  Eleza maana ya kielezi huku ukitolea  mfano mmoja.

b) Kwa kutumia mifano kwa kila hoja fafanua dhima nne za vielezi 

katika lugha ya Kiswahili.

4. Kipindi Mwalimu anafundisha  alimwambia Nguvukazi “njoo uchukue kibao” ,              

Nguvukazi akabaki anashangaa afanye maamuzi ya kuchukua kibao kipi?.Toa 

utata kwa kuelezea  maana tano za  neno tata hilo na kila neno toa mfano

 mmoja mmoja.

5.Bainisha maneno yenye makosa katika sentensi zifuatazo kisha andika sentensi hizo kwa usahihi.

  1.               Mwanafunzi ayejitambua hawapendagi mzaha katika masomo.
  2.               Shule yetu ina vifaa vya samani.
  3.               Mti uliokuwa karibu na bustani ya maua umedondoka.
  4.              Mzee Kiza amedhuru mbuga za wanyama.

6.Malimusi na Wasakatonge walikuwa wanajadili kuhusu tenzi na mashairi ,

Malimusi anasema tenzi na mashairi zote ni tungo za kishairi  hivyo zinafanana 

,lakini Wasakatonge alikinzana na Malimusi kwa hoja kuntu .jadili upande wa 

Wasakatonge kwa hoja nne huku ukitolea mifano hoja zako.

7. Vyombo vya habari vilikuwa na mchango gani katika kukuza na kueneza lugha ya 

Kiswahili kuanzia miaka ya 1961 hadi sasa?. bainisha  hoja nne kwa mifano kuntu.

8.Unataka kuwa kiranja mkuu katika shule ya sekondari Kazamoyo S.L.P 10

iliyopo  Morogoro ,mwandikie barua mwalimu wako wa nidhamu kumwelezea 

hitaji hilo katika shule yako.

SEHEMU C  (ALAMA 30)

Jibu maswali mawili kutoka sehemu hii swali la ni la LAZIMA

9.”Watunzi wa kazi ya fasihi huwa na dhima anuwai kwa jamii zao kupitia kazi zao 

za fasihi wanazotunga”Thibitisha dai hili kwa kutumia tamthiliya mbili 

ulizosoma kwa kutoa hoja tatu kutoka kila kitabu.

10. Lugha ni mhimili  katika kazi yoyote ya fasihi,Watunzi hutumia lugha kiufundi ili 

kufikisha ujumbe kwa jamii husika .Kwa kutumia Jazanda au taswira tatu kutoka 

katika  diwani mbili ulizosoma  na uonyeshe namna zinavyofikisha ujumbe kwa 

jamii.

11.”Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo au mambo hayapo sawa” Kauli hii inaweza kuwiana na waandishi wa riwaya juu ya jamii inayowazunguka, kwa kutoa hoja tatu kutoka kila riwaya katika riwaya mbili ulizosoma ,Jadili kwa nini wasanii hao hulia?.

ORODHA YA VITABU TEULE

USHAIRI  

Wasakatonge …………………………………………………….  M.S Khatib (Dup)

Malenga Wapya…………………………………………………. Takiluki (Dup)

Mashairi Ya Chekacheka……………………………..…..T.A Mvungi (Ep &D.Ltd)

RIWAYA

Takadini………………………………………………………..Ben J. Hanson (Mbs)

Watoto Wa Mama N’tilie ………………………………………….E. Mbogo   (H.P)

Joka La Mdimu…………………..………………………………….A.J Safari (H.P)

TAMTHILIYA

Orodha…………………………………………………………..Steve Reynolds (Ma)

Ngoswe Penzi Kitovu Cha Uzembe…………………………...…….E.Semzaba (Esc)

Kilio Chetu ……………………………………………Medical Aid Foundation (Tph)  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 142  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 142  


IMG_20230509_084505NEMBO

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYAYA MVOMERO

 

MTIHANI WA UTIMILIFU KIDATO CHA PILI 

 

021                                               KISWAHILI

MUDA: MASAA 3:00                                                                   MEI 2023

 

Maelekezo

 

  1.                Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).

 

  1.                Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2)kutoka sehemu C.

 

  1.                Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30).

 

  1.                Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.

 

  1.                Simu za mkononi na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.

 

  1.                Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

 


SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1.                Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi yako ya kujibia.
  1.               Upi kati ya ushahidi ufuatao ni ushahidi wa kiisimu kuwa Kiswahili ni kibantu.
  1.               Ugunduzi wa Malcon Guthrie
  2.               Mnyumbuliko wa vitenzi na viwakilishi
  3.               Ugunduzi wa Dkt. Livingstone
  4.              Ugunduzi wa Ali – Idris
  5.                Historia ya Kilwa

 

  1.             Zifuatazo ni sifa muhimu za mofimu, isipokuwa
  1.               Maana ya mofimu humilikiwa na kufasiriwa katika ubongo wa mzungumzaji.
  2.               Maana ya mofimu inaweza kuwa ya kisarufi au ya kileksika.
  3.               Maana ya kimsingi ya neno hubebwa na leksimu ya neno linalohusika.
  4.              Mofimu huru ina uwezo wa kusimama pekee.
  5.                Mofimu ikiongezwa katika neno hupanua maana na ikiondolewa huathiri maana.
  1.           Ni hali ya kuunda nomino kutoka kwa kategoria nyingine za maneno.
  1.               Uambishaji                                    B.  Uhulutishaji

C.  Unominishaji                                 D.  Utohozi 

E.  Uambatishaji

  1.           Ipi ni sifa ya vishazi tegemezi isiyoathiri maana ya sentensi?
  1.               Hutambuliwa kwa O – rejeshi.
  2.               Hufuatwa au kutanguliwa na kishazi huru.
  3.               Huweza kufutwa katika sentensi.
  4.              Kuwa na kitenzi kikuu ndani yake.
  5.                Kuwa kikubwa kuliko kishazi huru.
  1.             Ni aina gani ya nyimbo ambazo zinahusu malezi hasa ya jando na unyago?
  1.               Bembelezi                                        B.  Nyiso

C.   Kimai                                              D.  Wawe

E.   Hodia

  1.           Ni seti ipi kati ya zifuatazo inahusisha muundo sahihi wa kumbukumbu za mkutano
  1.               Kichwa cha kumbukumbu, Mahudhurio, Ajenda, Kufungua mkutano na Kufunga mkutano.
  2.               Kichwa cha kumbukumbu, Utangulizi, Mwanzo, Mahudhurio, Ajenda na Kufunga mkutano.
  3.               Mahudhurio, Ajenda, Kichwa cha kumbukumbu, Kufunga mkutano na Kufungua Ajenda.
  4.              Kichwa, Utangulizi, Kiini, Ajenda na Hitimisho.
  5.                Salaam, Shukurani, Ajenda, Kufungua mkutanonaKufungamkutano.

 

  1.         Moja kati ya vifuatavyo si kigezo kinachotumika katika kuchunguza na kuhakiki mtindo wa mtunzi wa kazi ya fasihi;
  1.               Motifu na dhamira zinazokaririwa katika kazi za watunzi
  2.               Uteuzi wa msamiati wa mtunzi na usawiri wa wahusika
  3.               Uteuzi na matumizi ya tamathali za semi
  4.              Itikadi na utamaduni wa mtunzi
  5.                Motifu na matumizi ya tamathali za semi
  1.       Jozi ipi kati ya jozi zifuatazo inatambulisha utanzu wa sanaa ya maonesho?
  1.               Ngano, tambiko, ngoma, utani.
  2.               Ngonjera, majigambo, miviga, vichekesho.
  3.               Nyimbo, maghani, mafumbo, lakabu.
  4.              Visakale, visasili, soga, vitendawili.
  5.                Methali, utani, misemo, vichekesho.
  1.           Mambo yanayounda mandhari katika kazi ya fasihi ni pamoja na
  1.               Utaratibu wa maisha, muundo na muda au wakati wa tukio kutokea.
  2.               Uhusiano wa wahusika, taswira na Maumbile
  3.               Mpangilio wa vitu mahali fulani na tabia
  4.              Maumbile, wakati wa tukio kutokea na utaratibu wa maisha.
  5.                Muda na urari wa mizani
  1.              Ipi ni sababu mojawapo ya kutumia lugha kulingana na muktadha?
  1.               Kuzuka kwa matukio mbalimbali.
  2.               Kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
  3.               Kumudu shughuli inayofanyika.
  4.              Kupamba mazungumzo.
  5.                Kuwezesha mawasiliano.
  1.                Oanisha dhana zilizopo Fungu A na mifano yake iliyopo Fungu B; kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

 

Orodha A

Orodha B

(i)  Mzizi

 

(ii) Mofu huru

 

(iii)Kiambishi awali

 

(iv) Kiambishi cha kauli

 

(v) Kiambishi tamati

 

(vi) Hali ya mazoea

 

A. mtu

 

B. ha-

 

C. cham-

 

D. -chok - 

 

E. -an - 

 

F.  -ji.

 

G.  u-

 

H. sasa.

 

 

 

SEHEMU B: (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1.                (a) Kwa kurejelea ngeli ya mahali, andika sentensi mbili (2) ukionyesha matumizi ya

      kila moja ya viambishi vyake.

 

(b) Tunga sentensi yenye viambishi vifuatavyo vya sarufi 

  1.               Kikanushi cha ngeli ya A – WA
  2.             Kikanushi cha wakati uliopita

 

  1.                (a) Waingereza wamechangia kukua na kuenea Kiswahili kutokana na juhudi zao hasa kupitia kamati ya lugha waliyounda. Thibitisha kauli hii kwa hoja nne?

      (b) Kwa hoja nne (4) eleza umuhimu wa lahaja katika lugha ya kiswahili.

 

  1.                Taja aina za sentensi zifuatazo, kisha toa sababu za kimsingi za uainishaji huo.
  1.               Mwanafunzi alikuwa darasani.
  2.             Mtoto huyu anapendeza sana ila anaringa.
  3.           Mwizi aliyekamatwa jana Madale kwa Digulu amefikishwa mahakamani.
  4.           Akija tutaondoka.
  1.                Methali hutawaliwa na vipengele mbalimbali vya lugha, onesha vipengele vya lugha vinavyotumika katika utunzi wa methali zifuatazo:
  1.               Kibuzi na kibuzi hununa jahazi.
  2.             Akili ni mali
  3.           Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani
  4.           Baniani mbaya kiatu chake dawa
  5.             Avumae baharini papa, kumbe wengine wapo
  1.                Wewe ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Ndanda kwenye siku ya teknolojia duniani umepewa fursa ya kuwasilisha mada ya uandishi wa Baruapepe. Waelekeze wanafunzi wenzako kuandika baruapepe kwa kufuata taratibu zake.

 

  1.                Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata: -

 

Jina langu Athumani, Mzaliwa Tanganyika,

Tanganyika si mgeni, hakuna wa kuniteka,

Wa kuniteka pembeni, damu yangu kukauka,

Pokea ukikumbuka, fedha zinafedhehesha.

 

Tumekwisha kuwajuwa, pesa walizofutika,

Futika ulizopewa, tumia bila mashaka,

Mashaka utaletewa, mto huu ukivuka,

Pokea ukikumbuka, fedha zinafedhehesha.

 

MASWALI

  1.                Mtunzi wa shairi anazungumzia nini?
  2.               Taja dhamira moja inayopatikana ubeti wa pili.
  3.                Bainisha kituo alichotumia mshairi katika shairi hili.
  4.               Bainisha mtindo uliotumika katika shairi.
  5.                Pendekezwa kichwa cha shairi.

 

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka katika sehemu hii. Swali la kumi (10) ni la lazima.

 

  1.                “Mawazo ya wasanii wa ushairi huzingatia maendeleo ya jamii kwa malengo ya kuikosoa na kuihamasisha ijikwamue” Thibitisha kauli hii kutoka diwani mbili (2) ulizosoma.
  2.           “Waandishi wa kazi za fasihi hutumia mandhari mbalimbali ili kuibua dhamira walizokusudia kwa jamii” Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.
  3.           “Uibushaji wa migongano katika tamthiliya ni nyenzo muhimu katika ufanikishaji wa tamthiliya” kwa kutumia vitabu viwili kati ya vile ulivyosoma. Jadili kauli hiyo hapo juu.

 

 

ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 10 – 11

 

USHAIRI  

Wasakatonge                                                             -       M.s Khatibu (Dup) 

Malenga Wapya                                                        -       TAKILUKI (Dup) 

Mashairi ya Chekacheka                                         -       T. A Mvungi (Ep & DLTD) 

 

RIWAYA  

Takadini                                                                    -       Ben   Hanson(MBS)

 Watoto wa Mama n’tilie                                          -       E. Mbogo (H.P) 

Joka la Mdimu                                                         -       A. J Safari (H.P) 

 

TAMTHILIYA  

Orodha                                                                      -       Steve Raynolds (MA) 

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe                          -       E. semzaba (ESC) 

Kilio Chetu                                                                -       Medical Aid Foundation (TPH)

 

 

 



FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 131  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 131  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SEREKALI ZA MITAA. 
 MKOA WA KILIMANJARO. 
 MTIHAN1 WA UTAMIRIFU WA KIDATO CHA NNE MKOA.

MSIMBO: 021 KISWAHILI

MUDA :SAA 3 MEI 2023

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A,B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C. Swali la 11 ni la lazima.
  3. Sehemu A ina alama kumi na sita( 16), sehemu B alama hamsini nan ne (54) na sehemu C ina alama thelethini (30)
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia

 SEHEMU A. (Alama 16)

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i)-(x), kisha andika here] ya jibu hilo kwenye karatasi ya kujibia.

(i). Neno maji limeundwa kutokana na njia ipi kati kati ya hizi zifuatazo?

  1. Ufananisho
  2. Utohoaji
  3. Unasibu
  4. Uambatanishaji
  5. Uhulutishaji.

ii). Kikundi cha maneno kinachoonesha jambo lililotendwa na mtenda katika sentensi hujulikanaje?

  1. Chagizo
  2. Kitenzi
  3. Kivumishi
  4. Shamirisho
  5. Nomino

iii). Viambishi vya O - rejeshi vya nomino "gari" ni ya vifuatavyo?

  1. O/ YO
  2. YE/
  3. LO/YO
  4. O/ZO
  5. PO/YO

iv)Ni maelezo maalumu yanayotolewa kwenye hadhara ya watu.

  1. Risala
  2. Kumbukumbu za mkutano
  3. Hotuba
  4. Ajenda
  5. Insha

v) Ingawa zipo njia mbalimbali za uundaji wa maneno mapya, Ni njia ipi inayotumika kuunda neno jipya kwa kubadili kategoria ya neno?.

  1. Kuambisha maneno
  2. Kubadili kundi au sifa ya neno
  3. Kuhulutisha maneno
  4. Urudufishaji
  5. Kuhamisha maana ya neno

vi).Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha nne, unaweza kusema kiimbo hufasiliwaje katika mazungumzo ya lugha ya Kiswahili?

  1. Kuzungumza na kuongea kwa sauti
  2. Kuzungumza kwa kupandisha mawimbi ya sauti .
  3. Kuzungumza kwa kushusha mawimbi ya sauti
  4. Kuzungumza na kushuka kwa mawimbi ya sauti
  5. Kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti

vii) Aina za maneno hufafanua kuhusu mambo mbalimbali .Onesha aina ya neno ambalo hufafanua zaidi kuhusu tendo au kivumishi kati ya haya yafuatayo?

  1. Kitenzi
  2. Kihusishi
  3. Kielezi
  4. Kiunganishi
  5. Kiwakilishi

viii) Kuna ngeli tisa za nomino za Kiswahili, katika ngeli hizo kila nomino huwekwa katika ngeli yake.Neno Ngamia lipo katika ngeli ipi kati ya hizi?

  1. I-ZI
  2. YU-A-WA
  3. KI-VI
  4. LI-YA
  5. U-ZI

ix) Mwalimu wa Kiswahili aliwafundisha Wanafunzi wake aina mbili za mofimu na mifano yake.Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha nne, onesha ni neno lipi kati ya haya yafuatayo hufanya kazi ya mofimu huru?.

  1. Uji
  2. Uzuri
  3. Uchache
  4. Ufa
  5. Mtoto

x) Sentensi zote za Kiswahili huundwa kwa miundo mbalimbali.Ni sentensi ipi kati ya zifuatazo yenye muundo wa kiwakilishi+kirai kivumishi+kitenzi kikuu+kirai nomino?

  1. Sisi sote tulicheza vizuri sana
  2. Mimi na yeye hatuelewani hata kidogo
  3. Wao hawataki tuimbe nyimbo zetu
  4. Wale wote wanapeda muziki
  5. Nyinyi nyote tunawapenda sana

2.Oanisha maelezo ya Orodha A na maneno katika Orodha B,kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

ORODHA A  ORODHA B

i Kupangilia visa na matukio katika maandishi kwa lengo la kuburudisha,kuelimisha na kuakisi hall halisi ya jamii.

ii. Masimulizi ya kubuni yanayosawiri tukio,tabia na migogoro katika katika maisha

iii. Mchezo wa kuigiza unaoandikwa ill utendwe jukwaani

iv. Mambo ya kubuni yenye mawanda mapana,lugha ya kinathari, mchangamano wa visa ,dhamira na wahusika kadhaa

v. Mambo ambayo msanii wa kazi ya fasihi anayawasilisha katika jamii yake.

vi. Ni tamathali ya semi ambayo mtu huulizwa swali ambalo tayari ana jibu lake

  1. Tashtiti
  2. Migogoro
  3. Maudhui
  4. Riwaya
  5. Masimulizi
  6. Visa
  7. Hadithi
  8. Utungaji
  9. Tamthiliya

SEHEMU B (Alarm 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Wewe ni mwanaisimu mbobezi wa lugha ya Kiswahili.Tumia utalaamu wako kutoa elimu juu ya kazi za mofimu tegemezi zilizokolezwa wino kwenye maneno yafuatayo:

  1. Hatutasaidiana
  2. Kitoto
  3. Akija
  4. Nilikunywa
  5. Hakumtaka
  6. Ninalima

4. Usanaa wa fasihi hujitokeza katika vipengele mbalimbali muhimu.Kwa kutoa maana ya sanaa, taja vipengele vinne vinavyoonesha usanaa wa fasihi.

5. Wapo baadhi ya wanazuoni wa somo la Kiswahili wanaodai kuwa Kamusi ya Kiswahili haina tija. Ukiwa kama mwanafunzi wa Kidato cha Nne. toa hoja sita kukanusha dai hili.

6. Ingawa Kiswahili kimepata kukua na kuenea sana hata kabla ya kupata uhuru wa Tanganyika.Unafikiri ni sababu zipi zilizosaidia kuenea kwa Kiswahili kuanzia mwaka 1961.Toa hoja sita na mifano kwa kila jibu lako.

7. Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali yafuatayo.

-Ndugu wazazi, kumbe safari yenu inahusu harusi ya Zaituni ?".Mkuu wa shule aliwauliza wazazi."Ndiyo," wazazi walijibu kwa Pamoja bila aibu."inategemewa kufugwa lini ."Mkuu aliendelea kuhoji. Harusi hii ilikuwa ifanyike wakati Zaituni anapofika kidato cha nne, Lakini Zaituni huyu ametufanyia uhuni na vituko visivyoelezeka. Nasi sasa tunachukiwa kijiji kizima na kudharauliwa na kila mtu.Hii imetuudhi sana, tumetungiwa nyimbo na kufanyiwa kila shutuma. Hatuna raha ;hivyo tumeonelea bora tuje kukuomba umfukuze shule ili kiburi kimwishie .Nasi tupo tayari kukulipa kiasi chochote cha fedha ukitimiza haja yetu hii,"Mzee Abdallah alieleza." Muda wote mkuu wa shule alikuwa akimtazama Mzee kwa chati sana .Kisha akauliza swali la kuchochea zaidi: Zaituni ana kiburi kumbe?"

Mama Zaituni hakutaka hilo limpite ,hima hima akatoa maelezo yake ."Mama wewe ,Zaituni usimuone hivi. Zaituni mwanangu hataki kufuata utamaduni wetu wa kuolewa. Zaituni ati achague mchumba mwenyewe, ati mahari haiyoni kama ni kitu cha msingi. Kiburi hicho kinatokana na elimu mliyompa.

Mtoto sasa ameharibika .Anafanya apendavyo elimu gani isiyojali adabu.wala utii?" Mama Zaituni alimaliza huku jasho na machozi yanamtoka".

Hapa mkuu wa shule aliona kwanza awaelimishe kabla hajawatolea kauli ya  mwisho.Alikwishatambua kwamba wazazi wa Zaituni walikuwa wameachwa nyuma na wakati .Kila upya wa mawazo waliuita kiburi.

Maswali.

  1. Wazazi wa Zaituni walikwenda shuleni kufanya nini ?
  2. Wazazi walisema kuwa Zaituni amefanya kosa gani.
  3. Eleza mgogoro mkuu uliopo kati ya Zaituni na wazazi wake.
  4. Fupisha habari hiyo kwa maneno yasiyopungua 50 na yasiyozidi 60.

8. Wewe ni daktari katika hospitali ya Rufaa ya Bugando unayehusika na kitengo cha magonjwa ya Watoto, umealikwa katika cha Nyakato kwenda kuzungumza na
wanakijiji juu ya swala la utapia mlo . Andika risala utakayoitoa kwa Mkuu wa wilaya ya Nyamagana kuwahimiza wanakinikuwapa Watoto mlo kamili.

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka katika sehemu hii. Swali la kumi na moja (11) ni la lazima.

ORODHA YA VITABU.

USHAIRI. 

  • Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP).
  • Malenga wapya -TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi ya Chekacheka - T.A.Mvungi(EP&D.LTD)

RIWAYA. 

  • Takadini -Ben J.Hanson (MBS)
  • Watoto wa Mama N'tilie - E.Mbogo(HP)
  • Joka la Mdimu - A.J.SaiTari (HP)

TAMTHILIYA

  • Orodha - Steve Reynolds(MA)
  • Ngoswe Penzi Kitovu Cha uzembe - E. Semzaba (ESC)
  • Kilio chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

9. -Kumekuwa na mgogoro mkuwa sana kati ya wazazi na vijana jambo ambalo limepelekea vijana wengi kushindwa kuishi na wazazi wao ili hall wakiwa katika umri mdogo na kupelekea vijana hao kukumbwa na changamoto mbalimbali katika maisha yao ya ukuaji na hatimaye kushindwa kutimiza ndoto zoa".Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma toa hoja tatu (3) kwa kila tamthiliya kwa kuonesha chanzo cha migogoro hiyo na namna ya kuitatuta.

10. "Mienendo ya wahusika ni muhimu katika ujenzi wa dhamira za mwandishi wa kazi ya fasihi". Thibitisha kauli hii ukionesha jinsi mienendo ya wahusika ilivyofanikisha kuibua dhamira .Toa hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.

11. "Mshairi ni kama taa imulikayo gizani ili kufichua kilichojificha ".Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka kila diwani kati ya mbili ulizosoma.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 120  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 120  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA PWANI 

MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA NNE

KISWAHILI

(Kwa Watahiniwa walioko na wasiokuwa shuleni)

Muda: Saa 3 Mwaka 2023

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na Moja (11).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B, na maswali mawili (02) kutoka sehemu C, swali la tisa (9) ni la lazima.
  3. SehemuA ina alama kumi na sita (16), sehemu B ina alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30).
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1 . Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) — (x), kisha andika herufi ya jibu hilo ltwenye kijjtabu chako cha kujibia.

Mwalimu Flora Komba aliwasisitiza wanafunzi katika somo la Kiswahili kuwa lugha hutengwa katika mafungu mawili, maana ya msingi na maana ya ziada. Je, maana ya ziada hushughulikiwa na tawi lipi la sarufi?

  1. Fonolojia 
  2. Mofolojia 
  3. Sintaksia
  4. Semantikia 
  5. Sarufi

(ii) Fag, big na Antisosho ni mojawapo ya njia itumikayo kuunda misimu ikiwemo:-

  1. A. Kutumia tanakali sauti 
  2. B. Njia ya kubadili maana ya msingi
  3. C. Kutohoa kutoka katika lugha za kigeni
  4. D. Njia ya kubadili kutoka lugha ya kibantu kwenda lugha ya kiswahili
  5. Njia ya uradidi.

(iii) Duka letu limejaa Vitu kedekede. Neno lililopigiwa msitari ni aina gani ya neno?

  1. Kiwakilishi 
  2. Kivumishi 
  3. Kihisishi
  4. Kiunganishi 
  5. Kielezi

(iv) Kuna vyombo mbalimbali vya kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania ikiwemo taasisi ya kiswahili na lugha za kigeni Zanzibar (TAKILUKI). Je, taasisi hii iliundwa mwaka gani?

  1. 1964 
  2. 1965 
  3. 1967 
  4. 1972 
  5. 979

(v) Katika kazi ya fasihi kuna wahusika ambao hawabadiliki na kupewa majina ambayo hufanya msomaji aelewe tabia na matendo yao. Je wahusika hao huitwaje?

  1. Wahusika duara 
  2. Wahusika wakuu 
  3. Wahusika bapa sugu 
  4. Wahusika shinda
  5. Wahusika wajenzi

(vi) VVanafunzi wa kidato cha nne katika Shute ya Sekondari Saja wanatarajia kufanya rnahafali ya 9 ifikapo mwezi Oktoba 2023 tangu kuanzishwa kwa Shule hiyo, umeteuliwa kuwa katibu wa vikao vya mahafali hiyo. Ni jambo gani kati ya haya yafuatayo si la kuzingatia wakati wa uandishi wa kumbukumbu? 

  1. Jina na saini ya mwenyekiti wa kikao 
  2. Ajenda 
  3. Mahudhurio 
  4. Umri wa katibu 
  5. Kichwa cha kumbukumbu. 

(vii) Bi Upendo Batista ana mwezi mmoja tu tangu awasili nchini Tanzania akitokea Jiji la Liverpool nchini Uingereza na ameanza kujifunza lugha ya Kiswahili. Mwalimu wake amemuagiza akanunue kamusi Mahuluti. Mfafanulie aina hiyo ya kamusi

  1. Ni kamusi yenye lugha nne 
  2. Ni kamusi yenye lugha Tatu
  3. Ni kamusi yenye lugha mbili na kuendelea 
  4. Ni kamusi yenye lugha Moja tu
  5. Ni kamusi yenye lugha mbili

(viii) Mwalimu Okollah amewapa wanafunzi wake kazi ya darasani ya kutunga hadithi, mwisho wa hiyo hæv fithi isomeke "Asiyesikia la mkuu huvunjika guu" Je, hiki ni imagekipera gani cha inacnthi?

  1. Ngano
  2. Visasili
  3. Soga 
  4. Tarihi 
  5. Vigano

(ix) Matumiaji wa lugha kjswahili anapotamka baadhi ya silabi kwenye neno huongeza nguvu kutamka kuzidi nyingine, hali hiyo huitwa?

  1. Kiimbo
  2. Mkazo
  3. Lafudhi 
  4. Fonimu 
  5. Umbo sauti

(x) Ukiwaa kama mtaalamu wa lugha ya kiswahili hususani katika mada ya mjengo wa Tungo, unafikiri ni awanini kiwakilishi na kihisishi havijapewa hadhi ya vikundi au virai badala yake hutokea katika kirai nomino (KN) na Sio katika aina nyingine ya virai?

  1. Kwa kuwa vimeshajitosheleza
  2. Kwa sababu kiwakilishi na kihisishi hutokea upande wa kiima 
  3. Kwa kuwa aina nyingine za virai hutokea upande wa kiarifu 
  4. Kiwakilishi na kihisishi ni aina ndogo za maneno.
  5. Kwasababu kihisishi kimewekwa katika Hali ya mshangao.

2. Oanisha maana ya dhana ya vifungu vya maneno vilivyo katika ORODHA A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika ORODHA B, Kisha andika herufi husika katika kijitabu chako cha kujibia.

ORODHA A

ORODHA B

(i) Kula kichwa

(ii) Aya ndogo yenye kidahizo na taarifa zake zote zinazohitajika.

(iii)Maana yake ni aina au mgawanyo. 

(iv) Bahasha-baghsha 

(v) Ameaga dunia.

(vi) Mtiririko mzuri wa mawazo kutoka ubeti mmoja hadi ubeti mwingine ambao hukamilisha maana ya shairi zima.

  1. Usimulizi
  2. Dhihaka
  3. Rejesta 
  4. Kidahizo
  5. Kiarabu 
  6. Ngeli
  7. Kitomeo
  8. Muwala
  9. Ishara
  10. Tafsida

SEHEMU B (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. (a) Kumekuwa na mabishano ya wanafunzi juu ya matumizi ya kiambishi "Kwa”wengi wao husadifu kuwa hakuna matumizi yoyote ya kiambishi hiko. Ukiwa mtaalamu wa kiswahili, waoneshe kwa mifano dhima tano (05) za kiambishi "Kwa”.

(b) Kwa kutoa mifano thabiti, fafanua majukumu manne (04) ya mnyumbuliko katika lugha ya kiswahili.

4. Mmepewa kazi na mwalimu wa kiswahili kuhusu dhana ya kiarifu. Ukiwa kama mmoja wao uliyeshiriki mjadala, fafanua vipashio sita (06) vya kiarifu (Kila kimoja thibitisha kwa mfano bayana).

5. Kiswahili ni lugha adhimu ambapo imekua kwa kasi sana na hadi sasa kutumika na mataifa mbalimbali. Kwa kutumia hoja sita (06) zenye mashiko, elezea mchango wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza na kueneza Kiswahili kimataifa (nje ya mipaka ya Tanzania)

6. Diwani wa kata yenu ya Serengeti ameandaa harambee kwaajili ya kuchangia ujenzi wa Mabweni. Kwa niaba ya kamati ya maandalizi, andaa kadi ya mwaliko kuwaalika wadau wa Elimu. Harambee itafanyika ukumbi wa Kiluvya Hall Kisarawe Pwani tarehe 1/8/2023. Jina lako liwe Soma Ule wa S.L.P 3012 Kisarawe.

7. Mwandishi wa diwani ya Chekacheka ndugu Theobald A. Mvungi amemchora mwanamke katika namna tofauti tofauti. Eleza kwa ufupi hoja nne (04).

8. Soma shairi lifuatalo, Kisha jibu maswali yanayofuata

(i) Busara haitokua, kuanza pasi salamu,

Salamu nasalimia, wakubwa na wa makamu, 

Halaiki naongea, naiongelea simu,

Ni sawa na kunywa sumu, kutumia simu shule.

(ii) Kweli zina umuhimu, si kidogo maishani,

Wasiliana si ngumu, ila sio mashuleni,

Kunielewa ni ngumu, lakini sikilizeni,

Ni sawa na kunywa sumu, kutumia simu shule.

(iii) Madhara nawatajia, ya hayo yenu masimu,

Uelewa kuzuia, akifundisha mwalimu,

Dunia kufatilia, masomo huwa magumu,

Ni sawa na kunywa sumu, kutumia simu shule.

(iv) Busara kuzizuia, kutumia hizi simu,

Darasani zatutoa, kwa ubize wa magemu,

Maana tungepotea, na kuja kujilaumu,

Ni sawa na kunywa sumu, kutumia simu shule.

MASWALI

(a) Pendekeza kichwa cha shairi kinachofaa, kisichozidi maneno matatu 

(b) Taja madhara mawili ya simu za mkononi yaliyotajwa na mshairi.

(c) Onesha maneno mawili ya kigeni yaliyotumiwa na mshairi katika shairi lake. 

(d) Bainisha maana ya maneno yaliyokolezwa wino na kupigiwa msitari.

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (02) kutoka katika sehemu hii. Swali la tisa (9) ni la lazima.

ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 9 - 11

USHAIRI

  • Wasakatonge - M.S. Khatib (DUP)
  • Malenga Wapya - TAKIRUKI (DUP) 
  • Mashairi ya Chekacheka - T. A. Mvungi (EPRD. LTD)

RIWAYA

  • Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
  • Watoto wa Mama N'tilie - E. Mbogo
  • Joka la Mdimu - A. J. Safari (HP)

TAMTHILIYA

  • Orodha. - Steve Reynolds (M.A)
  • Ngoswe Penzi kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
  • Kilio Chetu. - M. A. Foundation (TPH)

9. Mshairi mzuri ni yule anayeitazama jamii yake na kusisitiza suala zima la Ukombozi kila penye dhuluma, uonevu na ukandamizaji. Wewe ukiwa kamamwanafasihi na mhakiki wa kazi za fasihi, fafanua aina tofauti tofauti za Ukombozi na ni kwa jinsi gani washairi wetu wameonesha hali hiyo, kwa kurejea diwani mbili ulizosoma kwa hoja tatu (03) kila diwani.

10. Wapo baadhi ya wanaume hukimbia familia zao kwa kupenda au kutokupenda, hali hii humfanya mwanamke (Mama) apambane peke yake juu ya kulea familia hiyo iliyokimbiwa na Baba. Ukiwa kama mwanajamii, elezea mchango hasi wa mwanaume ambao ni kikwazo cha maendeleo ya mwanamke, kwa kurejea katika riwaya mbili ulizosoma kwa kutoa hoja tatu (03) kwa kila riwaya.

11. Uzuri wa nyumba sio mlango, ingia ndani ujionee. Uteuzi wa jina la kitabuhuweza kuakisi au kutoakisi yaliyomo kitabuni. Kubali au kataa dai hili kwa kutoa hoja tatu (03) kwa kila kitabu katika tamthiliya mbili ulizosoma.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 109  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 109  

Namba ya Mtahiniwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA 

image

MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA NNE 

021 KISWAHILI

Muda: Saa 3:00 Aprili, 2023

MAELEKEZO 

  1. 1. Karatasi hii ina sehemu A, B, na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
  2. 2. Jibu maswali yote kutoka Sehemu A na B na maswali mawili kutoka Sehemu C. Swali la 11 ni la lazima.
  3. 3. Sehemu A ina alama 16, Sehemu B alama 54 na Sehemu C alama 30.
  4. 4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali.
  5. 5. Vitu visivyoruhusiwa katika vyumba vya mtihani kamwe visiingie.
  6. 6. Andika namba ya upimaji katika kila ukurasa.

 SEHEMU A (ALAMA 16)

Jibu maswali yote katika Sehemu hii.

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

(i) Bainisha tabia ya umbo lililopigiwa mstari katika kitenzi “ibwa.”

  1. Kauli ya kutendeka 
  2. Kauli ya kutendea
  3. Kauli ya kutendeana
  4. Kauli ya kutendwa
  5. Kauli ya kutendewa

(ii) Bainisha jozi sahihi ya vipera vya Sanaa za Maonesho:

  1. Muziki, fasihi, ususi, uhunzi na utarizi
  2. Tarihi, ngano, visasili, soga na hadithi.
  3. Ngonjera, miviga, ngoma, tambiko na majigambo
  4. Maigizo, viechekesho, majigambo, lakabu na maghani
  5. Michezo ya watoto, utani, ngonjera, mizungu na muziki

(iii) Neon “beberu” limeundwa kwa njia ipi kati ya hizi zifuatazo za uundaji wa maneno?

  1. Kutumia fasili sisisi
  2. Kuangalia athari za kitu
  3. Kuhamisha maana ya neno
  4. Kuangalia kazi ya kitu
  5. Kuangalia sauti, sura na tabia

(iv) “Mtangazaji wa televisheni huhakikisha watazamaji wanapata habari sahihi kwa wakati.” Katika fasihi, kazi hiyo hufanywa na nani kati ya hawa wafuatao?

  1. Wasikilizaji
  2. Hadhira
  3. Fanani
  4. Wasomaji
  5. Wazungumzaji

(v) Mende anapenda uchafu. Neno lililopigiwa mstari lipo katika ngeli ipi?

  1. KI – VI
  2. U – I
  3. A – WA/YU – A – WA
  4. KU
  5. LI – YA

(vi) Mofimu –me- katika sentensi “Rosa amenitaarifu leo asubuhi” ni:

  1. Kiambishi awali kikanushi
  2. Kiambishi awali cha njeo
  3. Kiambishi awali cha urejeshi
  4. Kiambishi awali cha nafsi ya tatu
  5. Kiambishi tamati cha kutendesha

(vii) Mzee Jimbi na Kifaruhande ni miongoni mwa wahusika katika Tamthiliya ya . . . . . . . . . .

  1. Kilio Chetu
  2. Takadini
  3. Orodha
  4. Ngoswa – Penzi Kitovu cha Uzembe
  5. Joka la Mdimu

(viii) Ashirafu na Hamisi wakati wanaandika barua rasmi walisahau kujumuisha hatua inayofuata baada ya kipengele cha mwisho wa barua. Ni hatua ipi iliyokuwa imesahaulika ? 

  1. Jina la Mwandishi
  2. Cheo cha Mwandishi
  3. Salamu za maagano 
  4. Saini ya Mwandishi
  5. Anuani ya Mwandikiwa

(ix) Tamathali ya semi inayotumika kufananisha vitu bila kiunganishi huitwa _________.

  1. Tashibiha
  2. Tashihisi
  3. Sitiari
  4. Tashititi
  5. Taniaba

(x) "Kutwa mara tatu”. Dhima ya muundo wa mazungumzo haya ni ipi?

  1. Kupunguza ukali wa mazungumzo
  2. Kufupisha urefu wa mazungumzo
  3. Kupamba lugha ya mazungumzo
  4. Kuonesha msisitizo
  5. Kukidhi haja ya mazungumzo

2. Oanisha maana za tamathali za semi zilizopo katika Orodha A na tamathali husika kutoka Orodha B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.

ORODHA A 

ORODHA B

(i) Ushangaaji wa jambo fulani, aghalabu huambatana na alama ya mshangao.

(ii) Upangiliaji wa maneno katika namna ya kupingana ili kusisitiza mawazo fulani.

(iii)Ulinganishaji wa vitu viwili au zaidi vyenye sifa tofauti kwa kutumia viunganishi.

(iv)Uhuishwaji w akitu kisichobinadamu kupewa uwezo wa kutenda kama binadamu.

(v) Urudiaji wa meneno ili kuonesha msisitizo wa jambo.

(vi)Huuliza swali hali jibu linafahamika wazi.

  1. Tashbiha
  2. Takriri
  3. Sitiari
  4. Tabaini
  5. Tashihisi
  6. Nidaa
  7. Tashititi
  8. Tanakalisauti
  9. Balagha

SEHEMU B (ALAMA 54)

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii

3. Kwa kutumia mifano, taja vipashio sita vya kiima.

4. Kwa kutumia hoja tatu (3), eleza faida za kutumia lugha fasaha na hoja tatu (3) hasara za kutumia lugha isiyo fasaha.

5. Andika rejesta tatu (3) zinazotumika katika miktadha ifuatayo:

  1. Bungeni
  2. Michezoni
  3. Shuleni
  4. Mtaani
  5. Kwenye nyumba za ibada
  6. Gulioni/mnadani

6. (a) Eleza kirefu cha neno BAKITA.

(b) Eleza kazi nne (4) za BAKITA.

7. Kwa kutumia mifano kuntu kutoka katika tamthiliya ya Kilio Chetu na Orodha, eleza kwa kifupi namna Mwanamke alivyochorwa katika sura tofauti tofauti. (Hoja tatu (3) kutoka kila tamthiliya.)

8. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata:

1. Enyi vijana sikiliza, nawapa wangu wosia,

Nataka kuwaeleza, ushauri ulo mwema, 

Hakika nawapongeza, hapa mlipofikia, 

Hongereni, hongereni, Hongereni kuhitimu.

2. Ni mbali mlipofikia, kamwe msijebweteka, 

Matashi yenu kufikia, huo ni mwanzo sikia, 

Usije kuvitupia, vitabuvyo kwenye taka, 

Hongereni, hongereni,  Hongereni kuhitimu.

3. Shuleni mmejifunza, kusoma kwa uhakika, 

Kwa umakini mkajifunza, Kiswahili bila kuchoka, 

Lugha mkajifunza, bila hata kubweteka, 

Hongereni, hongereni, Hongereni kuhitimu.

MASWALI

(a) Andika kichwa cha shairi hili kwa maneno yasiyozidi manne.

(b) Neno “bweteka” lina maana gani kadiri ya lilivyotumika katika shairi hili?

(c) Mwandishi ametumia muundo gani?

(d) Taja tamathali mojawapo ya semi iliyotumika katika beti zote za shairi na mfano wa tamathali hiyo.

(e) Taja idadi ya mizani zilizopo katika mstari wa kwanza wa ubeti wa pili.

SEHEMU C (ALAMA 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka sehemu hii. Swali la 11 ni la lazima.

9. Fasihi simulizi ni ndizi ambazo huweza kubebwa katika vifungashio vya rangi tofauti. Eleza vifungashio vinne (4) na uelezee changamoto moja kwa kila kifungashio.

10. Mshairi hutumia taswira mbalimbali katika kufikisha ujumbe katika jamii. Dhihirisha dai hilo kwa kutumia diwani mbili ulizosoma. (Hoja tatu kwa kila diwani.)

11. Watanzania wa leo hawahitaji sio tu kiongozi bora bali mwenye uthubutu katika kupambania mahitaji yao. Kwa kutumia riwaya mbili ulizosoma, jadili mambo ambayo kiongozi anapaswa kuyakemea katika jamii.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 104  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 104  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA TANGA

MTIIIANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA NNE 

(Kwa wanafunzi waliopo na wasiokuwepo shuleni) 

MSIMBO: 021 KISWAHILI

MUDA: SAA 3 MEI, 2023

MAELEKEZO 

  1. Karatasi hii ina schcmu A,B na C zenye jutnla ya maswali kumi na moja(1 1).
  2. Jibu maswali yotc katika sehemu A na B na maswali mawili kutoka schcmu C na swali la kumi na moja ni la lazima.
  3. Sehemu A ina alama 16 na sehemu B ina alama 54 na sehemu C ina alama 30.
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehcmu ya kila swali
  5. Simu za mkononi na vitu visivyotakiwa haviruhusiwi katika chumba cha mtihani
  6. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu cha kujibia.

SEHEMU A (ALAMA 16)

Jibu maswali yote

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i)-(x) kisha andika herufi ya jibu hilo

i. Mzee Jimbi aliwasimulia wajukuu zake chanzo cha nyoka kutambaa na jongoo kuwa na miguu mingi.Unahisi ni kipera gani cha hadithi Mzee Jimbi alikitumia? 

  1. Vigano 
  2. Soga 
  3. Visasili
  4. Tarihi
  5. Ngano 

ii. Mama Mazoea alimnunulia mwanawe zawadi ya kamusi ya Kiswahili sanifu ya TUKI iliyichapishwa mwaka 1981 baada ya mwanawe kufaulu mtihani wg kidato cha nne ambapo alifaulu mchepuo wa HKL.Je Mama Mazoea alimnunulia mwanawc aina gani ya kamusi? 

  1. Kamusi mahuluti 
  2. KamuSi wahidiya 
  3. Kamusi Thama 
  4. Kamusi za scmi 
  5. Kamusi za visawe. 

iii. Ombeni alijinasibu mbele ya rafiki yake "wakati wa likizo napenda kwenda Dar Es salaam" lakini rafiki yake alimjibu , " mimi napendaga kwenda jiji la kizota" je katika kauli ya rafiki yake Ombeni ni kosa gani amelifanya 

  1. Upatanisho wa kisarufi 
  2. Kosa la kimantiki 
  3. Hakuna jiji la Kizota 
  4. Kosa la kimatamshi 
  5. Kosa la kuongeza viambishi 

iv. Juma alikuwa akitaniana na Mathayo "Juma akamwambia Mathayo ni mnene kama pipa" na Mathayo akamwambia Juma ni mwembamba mithili ya sindano.Je Juma na Mathayo wametumia tamathali gani za semi? 

  1. Tashbiha 
  2. Tanakali sauti 
  3. Sitiari 
  4. Tafsida
  5. Tahaini

v. Mzee Kifaruhande anauguza mgonjwa  nyumbani kwake.je neno lililopigiwa mstari Tina jumla ya silabi ngapi?

  1. Nne
  2. Tano
  3. tatu
  4. Mbili
  5. Sita

vi. Amani ni jambo la muhimu sana ndani ya Taifa letu" Tumeshuhudia kwenye nchi za wenzetu maiti zikizagaa kila mahali kwasababu ya vita, je neno maiti linapatikana katika ngeli gani?

  1. U-I
  2. LI-YA
  3. A- WA
  4. I -Zl
  5. KU.

vii. Tu tayari kufanya mtihani wa Taifa 2023.Je sentensi hii ipo katika nafsi ya ngapi?

  1. Nafsi ya pili
  2. Nafsi ya kwanza
  3. Nafsi ya tatu
  4. Nafsi ya nne
  5. Nafsi ya tano

viii. Kija alimsihi shangazi Yembe awasaidie kulipa ada ya Maisara iii aendelee na masomo yakc.Shangazi aliwapa kisogo. Kauli iliyopigiwa mstari ina maana: 

  1. Alikubaliana nao
  2. Aliwasikiliza
  3. Aliwaramba kisogo
  4. Aliwapuuza
  5. Aliwaitikia

ix. Juma alifurahi alipopata maswali yote ya Kiswahili.Neno lililopigiwa mstari ni;

  1. Notnino
  2. Kielezi
  3. Kitenzi
  4. Kishazi tegemezi kivumishi
  5. Kishazi tegemezi kielezi

x. Hamsini,laki,kasri na fikiri ni miongoni mwa maneno yanayothibitisha kuwa asili ya Kiswahili ni;

  1. Krioli
  2. Kibantu
  3. Kiarabu
  4. Pijini
  5. Chotara

2. Oanisha mifano ya tamathali za semi zilizopo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya mfano husika katika orodha B,kisha andika herufi husika katika karatasi yako ya kujibia.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Tulimlilia Nyerere hadi tukajaza bahari ya machozi
  2. Viatu vya Mwajuma vilionekana vikicheka
  3. Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambaragc Nyerere alifariki dunia 1999
  4. Mlikaa, mkasubiri, mkachoka
  5. Dada alitumbukia majini chubwi!!
  6. Aliimba wimbo wake vizuri lakini . . . . . . . 
  1. Tafsida
  2. Mubalagha
  3. Tabaini
  4. Tashihisi
  5. Mdokezo
  6. Mjalizo
  7. Onomatopeia
  8.  Takriri
  9. Taniaba

SEHEI1U B (ALAMA 54)

Jibu maswali yote

3.. Uainishaji wa sentensi huzingatia vipashio vilivyopo katika scntensi husika.Tunga sentensi moja kwa kila kipashio katika vipashio vifutavyo

  1. Kishazi hum kimoja
  2. Kishazi tegemezii kimoja na kishazi huru kimoja
  3. Vishazi tegemezi viwili na kishazi hum kimoja
  4. Kishazi tegemezi kimoja na vishazi hum viwili
  5. Vishazi tegemezi viwili na vishazi hum viwili.

4. a. Nini maana ya kiarifu?

b. Kwa kutumia mifano bainisha vipashio vinne vinavyounda kiarifu.

5. Zipo nadharia mbalimbali zinazoelezea chimbuko la Kiswahili lakini ipo nadharia inayokubalika kutokana na kuwa na ushahidi wa kisayansi na kihistoria.Kwa kutumia mifano hai toa hoja nne za kisayansi kubainisha nadharia hiyo.

6. Kwa kutumia mifano ya lugha ya Kiswahili taja sababu nne za utata katika mawasiliano.

7. Soma kifungu cha habari, kisha jibu maswali yanayofuata.

Mwanadamu ni kiumbe anayehitaji kuwa na rafiki iii aweze kuondoa ukiwa kwa kumletea faraja. Kwa kawaida marafiki hufahamiana, huzoeana na kuchangamkiana katika maongezi. Mandhari ya aina yoyote unaweza kupata marafiki yaani nyumbani, shuleni, kanisani, kazini na hata kisimani.

Kutokana na ukweli kuwa ushauri wa marafiki huwa na nguvu na ni rahisi kwa marafiki kuambukizana tabia, seuze hayo rafiki anaweza kukusababishia simanzi .na si kukuletea furaha. Kwa hiyo ni muhimu kuchunguza kwanza tabia za mtu unaetaka kuwa rafiki yake. Ni hen kukosa rafiki kuliko kuwa na rafiki mlevi, mwongo, mwizi, mvivu au mwenye tabia mbaya nyinginezo. Rai yangu kwako, rafiki wa kukufaa ni yule mwenye adabu njema, busara, hekima na mwaminifu na pia mwenye utayari wa kukutakia mafanikio mema katika maisha yako.

Wahenga walisema akufaayc kwa dhiki ndiye rafiki. Ni ukweli usiopingika mtu anaycweza kukusaidia kwa dunia ya sasa ni yule mwenye kujua thamani ya mtu na si vinginevyo.

Maswali

  1. Andika kichwa cha habari kinachoendana na habari uliyosoma.
  2. Taja sehemu unazowcza kupata marafiki (sehemu tatu).
  3. Toa maana ya maneno yaliyopigiwa mstari kama yalivyotumika katika habari.
  4. Eleza faida ya kuwa na rafiki.

8. Soma kwa makini mazungumzo ya simu kati ya SIKITU na MGENI kisha andika kadi ya mwaliko

SIKITU : Halloo.Habari za jioni.

MGENI: Nzuri. Nani mwenzangu?

SIKITU : Sikitu hapa.Nimekupigia kukujuza kuwa ile harusi ya kaka Bahati itakuwa siku ya Jumamosi ya tarehe 6/7/2023 kuanzia saa 10 jioni.

MGENI : Heh mbona mapema hivyo?

SIKITU: Ndivyo walivyopanga.Ndoa itafungwa kanisa la pentacosta

Miembeni.Kisha shcrchc itafanyika Nyumbani Mabibo mtaa wa Samora ilivyo unakaribishwa.

MGENI: Asante.Nitumie kadi yangu.

SEHEMU C: (ALAMA 30)

Jibu maswali mawili(2) tu.Swali la 9 ni lazima

9. Waandishi wa tamthiliya mara nyingi hutumiamandhari ya mjini au kijijini kufikisha ujumbe fulani kwa jamii.Je ni mambo gani yanayokushawishi kugundua kuwa mandhari iliyotumika ni mjini au kijijini? Toa sababu tatu(3) kwa kila tamthiliya kati ya tamthiliya mbili ulizosoma.

10. Ni kwa namna gani waandishi wa kazi za riwaya wanavyotumia kipengele cha migogoro kuwasilisha dhamira zao.Toa hoja tatu kutoka katika kila riwaya.

11. Washairi ni walimu wazuri sana wa jamii yetu.Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja tatu(3) kutoka katika Diwani mbili ulizosoma.

ORODHA YA VITABU

USHAIRI

  • Wasaka Tonge - M.S Khatibu (DUP)
  • Malenga Wapya- TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi ya Chekecheka- T.A Mvungi (EP LTD)

RIWAYA

  • Takadini- Ben. J. Hanson (MBS)
  • Watoto wa Mama Ntilie- E. Mbogo (H.P)
  • Joka la Mdimu- A.J.Safari (H.P)

TAMTHILIYA

  • Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe- E. Semzaba (ESC)
  • Kilio Chetu- Medical Aid Foundation (TPH)
  • Orodha- Steve Raynolds (MA)


FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 99  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 99  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA DAR ES SALAAM NA IRINGA

MTIHANI WA PAMOJA WA UTAMILIFU KIDATO CHA NNE - 2022, KISWAHILI

MSIMBO: 021

MUDA: MASAA 3:00

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una sehemu A, B, na C zenye jumla ya maswali (12) kumi na mbili
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B ina alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45)
  4. Zingatla maelekezo ya kila sehemu na kila swali
  5. Simu za mkononi na vitu vingine visivyoruhusiwa havitakiwi kwenye chumba cha mtihani
  6. Andika namba yako ya mtihani kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia

SEHEMU A: (Alama 15)

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia

(i) Vijana wanauza maembe uwanjani. Neno Maembe katika sentensi hii limesimama kama:- 

  1. Chagizo
  2. Kielezi
  3. Shamirisho
  4. Kiwakilishi

(ii) _________________ ni aina ya sentensi ambayo huundwa kwa kishazi tegemezi kimoja au zaidi na kishazi huru kimoja au zaidi

  1. Shurutia
  2. Ambatano
  3. Sahili
  4. Changamano

(iii) Ipi kati ya zifuatazo siyo dhima ya viambishi?

  1. Hudokeza nafsi
  2. Hudokeza wakati/njeo
  3. Hudokeza nomino
  4. Hudokeza mzizi wa neno

(iv) Katika lugha a kiswahili kuna aina ngapi za viwakilishi?

  1. 9 (tisa)
  2. 6 (sita)
  3. 4 (nne) 
  4. 5 (tano)

(v) Umbo -tu- katika neno "watakapotupambanisha" hutambulisha__________

  1. wakati uliopita
  2. O-rejeshi watenda
  3. Kiambishi awali cha mashart
  4. Urejeshi watendwa

(vi) Ni kauli inayotumia maneno ya kawaida lakini hutoa maana tofauti kabisa na ilivyokwenye maneno yale?

  1. Mafumbo
  2. Nahau
  3. Misemo
  4. Semi

(vii) Vipi kati ya vifuatavyo ni vipera vya hadithi?

  1. semi, ngano, nyimbo, misemo
  2. Soga, methali, ngonjera, misemo
  3. Ngano, tarihi, visasili, soga, vigano
  4. Vigano, hadithi, soga, nyimbo

(viii) Yafuatayo ni matawi ya sarufi isipokuwa____

  1. Maumbo
  2. Mtindo
  3. Mantiki
  4. Maana

(ix) Neno "Chakachua" ni neno la msimu ambalo linaweza kuwa mfano wa__

  1. Misimu zagao
  2. Misimu ya kitarafa
  3. Misimu ya pekee
  4. Rejesta ya Ofisini

(x) Ni sehemu katika sentensi inayokaliwa na mtenda wa jambo

  1. Kiarifu
  2. Kishazi huru
  3. Kirai
  4. Kiima

2. Oanisha maana ya dhana zilizo katika orodha A kwa kucha ua herufi ya dhana husika katika orodha B kisha andika herufi husika katika kijitabu chako cha kujibia

Orodha A Orodha B
  1. Ni sehemu inayo kaliwa na mtenda au mtendwa
  2. Ni neno au maneno yanayofafanua namna wakati au mahali kitendo kilichofanyika
  3. Kipashio kidogo cha kimuundo chenye neno moja au zaidi ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu
  4. Tungo inayotawaliwa na kitenzi kinachojitosheleza kimaana
  5. Kipashio kidogo kabisa cha kiisimu chenye maana ya kisarufi na kileksika
  1. Mofimu
  2. Kirai
  3. Fonimu.
  4. Shamirisho
  5. Prediketa
  6. Chagizo
  7. Kiima
  8. Kishazi huru

SEHEMU B: (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Bainisha njia zilizotumika kuunda maneno yafuatayo:-

  1. Pembetatu
  2. Harakaharaka
  3. Batamzinga
  4. Pikipiki

4. Onesha kiima na kiarifu katika tungo zifuatazo:-

a) Mwalimu mfupi atafuta ubao

b) Vijana watakaosoma vizuri watapewa nafasi ya kwanza

c) Mtoto anacheza

d) Kuimba kwake kunafurahisha sana

5. (a) Je, uandishi wa tangazo una umuhimu gani? (toa hoja tatu (3))

(b) Kwa kutumia kielelezo cha picha, Andika tangazo la kuuzwa kwa Gari aina ya Nissan Patrol nyeusi.

6. Hata baada to uhuru, Kiswahili kimekuwa kikikabiliwa na matatizo mbalimbali. Eleza kwa ufupi matatizo manne (4) yanayokikabili katika ukuaji na ueneaji wake nchini.

7. Soma shairi lifuatalo kicha jibu maswali yanayofuata

1. Corona ugonjwa gani, umezua taharuki, 

Chanjo haipatikani, Ulaya hakukaliki,

Tiba haijulikani, Dunia haifurukuti,

Corona ina maafa, kujikinga ni lazima

2. Hofu kubwa imetanda, wakubwa kwa wadogo, 

Mafua, homa kupanda, utaonauki "gugo", 

China mpaka mpanda, Corona haina vigo, 

Corona ina maafa, kujikinga ni lazima.

3. Walakini juu ya yote, mapenzi yameoteshwa,

Karantini kwa wote, makapera wameoa, 

Mabinti wasiopenzini, huu msimu wa ndoa, 

Corona ina maafa, kujikinga ni lazima.

4. Hakika baniani mbaya, kiatu chake dawa,

Wanandoa walishane, penzi bila taabu, 

Nao wapenzi wachanga, wasubiri janga lipite, 

Corona ina maafa, kujikinga ni lazima.

5. Mungu atasaidia, corona itaisha,

Elimu tazingatia, wizara wanakumbushia, 

Tunawe yetu mikono, epuka msongamano, 

Corona ina maafa, kujikinga ni lazima.

MASWALI

  1. Pendekeza kichwa cha habari kisichozidi maneno matatu 
  2. Unafikiri ni kwa nini mshairi anatuasa kuwa Corona ina maafa kujikinga ni lazima? 
  3. Mwandishi ametumia muundo gani katika shairi hili? 
  4. Kutokana na shairi ulilosoma eleza njia tano unazozijua utakazotumia kuepukana na ugonjwa wa corona.

8. Wewe ni mwenyekiti wa mtaa ambao umekumbwa na mafuriko lakini wananchi wako wanakataa kuhamia makazi mapya. Andaa hotuba utakayoitoa kwa wananchi wa mtaa wako ili kuwashawishi kuondoka katika sehemu hiyo. Jina la mtaa ni Kwamachombo na eneo la Makazi Mapya linaitwa Kitivo

SEHEMU C: ( Alama 45)

Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii

9. "Fasihi ni bidhaa adimu inayopaswa kuuzwa na kununuliwa sokoni" Kwa kutumia fasihi simulizi dhihirisha ukweli huu kwa kuzipambanua sifa zake mahususi. (Toa hoja sita (6)).

10. Utamu wa maji ya dafu ni kunywa kwenye kifuu chake, na utamu wa shairi ni lugha. Eleza jinsi waandishi wawili walivyotumia lugha ya picha katika kupamba mashairi yao. (Toa hoja tatu (3) kwa kila diwani)

11. Katika kazi ya fasihi jina Ia kitabu husadifu yaliyomo ndani ya kitabu. Kwa kutumia riwaya mbili ulizosoma, Toa hoja tatu (3) kwa kila riwaya kuthibitisha dai hilo.

12. "Wahusika mbalimbali katika kazi za fasihi huonyesha tabia mbalimbali ambazo nyingine ni mfano wa kuigwa na nyingine hazifai kuigwa katika jamii. Onyesha wahusika ambao tabia zao hazifai kuigwa". Tumia tamthiliya mbili kati ya tatu ulizosoma na utoe hoja tatu kwa kila tamthiliya

ORODHA YA VITABU VYA SWALI LA 10 - 12

USHAIRI

  • Wasakatonge -  MS Khatibu (DUP)
  • Malenga Wapya  - TAKILUKI (DUP)
  • Chekacheka  - T.A. MVUNGI (EP & D. LTD)

RIWAYA

  • Takadini - Ben 3. Hanson (MBS)
  • Watoto wa Mama ntilie - E. Mb000 (H.P)
  • Joka la Mdimu  - A.J. Safari (H.P) 

TAMTHILIYA

  • Orodha -  Steve Reynold (M.A)
  • Ngoswe Penzi Kitovu Cha Uzembe  - E. Semzaba (ESC)
  • Kilio Chetu  - Medical Aid Foundation

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 91  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 91  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA KILIMANJARO

MTIHANI WA UTAMIRIFU KIDATO CHA NNE

MSIMBO 0021 KISWAHILI 

MUDA: 3:00 27/06/2022

MAELEKEZO

l. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenyej umla ya maswali kumi nambili (12)

2. Jibu maswali yote katika sehemuAna B na maswali matatu (3)kutoka sehemu C

3. SehemuA ina alama kumi na tano(15) sehemu B ina alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45)

4. Zingatİa maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali

5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoıuhusiwa havitakiwi katikachumba cha mtihani

6. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi za kujibia

SEHEMU A (ALAMA 15)

1. Chaguaherufi yajibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kishaandikaherufi yajibu hilo katika karatasi ya kujibia.

i. Maneno yapi kati ya yafuatayo yanatokana na lugha za kibantu

  1. Kitambara na bendera
  2. Kitivo na ngeli
  3. Hela na mtu
  4. Godoro na sharubati 

ii. Ni neno lipi linalotoa taarifa kuhusu nomino?

  1. Kitenzi
  2. Kielezi
  3. Kivumishi
  4. Kiunganishi 

iii. Nj ia mojawapo ya kuzuia utata katika lugha ya mazungumzo ni ipi kati ya zifuatazo?

  1. Kuepuka makosa ya kisarufi na kimantiki
  2. Kutumia neno lenye maana zaidi ya moja
  3. Kutumia kiwakilishi kiambata katika neno
  4. Kutumia mofimu sahihi za wakati

iv. Neno lipi kati ya haya ni mofimu huru?

  1. Uji
  2. Uzuri
  3. Uchache
  4. Ufa

v. Ni semi zinazoonesha upinzani wa fikra.

  1. Nahau
  2. Vitendawili
  3. Lakabu
  4. Mizungu

vi. Ni hatua inayofuata baadayakipengele chamwisho wa baruakatika uandishi wa barua rasmi.

  1. Jina la mwandishi
  2. Cheo cha mwandishi
  3. Saini ya mwandishi
  4. Salamu za maagano

vii. Nisifaipi haitofautishi fasihi simulizinafasihi andishi?

  1. Ukubwa
  2. Uhifadhi
  3. Ukuaji
  4. Uwasilishaji

viii. Ni maneno yapi kati ya haya yafuatayo yametokana na njia ya kuambatanisha maneno?

  1. Jenga na toweka
  2. Pango na Pangisha
  3. Pundamilia na mtu mwema
  4. Hela na mtutu 

ix Tarihini mojawapo kati ya viperavyahadithiarnbavyo huelezeakuhusu.

  1. Asili ya vitu kama vile milima, mito, wanyama, n.k
  2. Kuonya kuhusu maisha ya watu
  3. Makosa na uovu wa watu na kueleza maadili yanayofaa.
  4. Kueleza matukio ya kihistoria

x. Moja kati ya zifuatazo Sio tabia ya Vitenzi halisi?

  1. Kuonesha njeo
  2. Kuoneshajina la mtenda
  3. Kuonesha uyakinishi
  4. Kuonesha nafsi

2. Oanishamaananadhanakatika Orodha A kwakuchaguaherufiyadhanahusikakatika Orodha B kasha andika herufi husika

SAFU A

SAFU B

i. Ng'ombe zangu wanatoamaziwa mengi 

ii. Huandikwakwa lugha mbili 

iii. Ni kanuni,sheria na taratibu zinazowabana wazungumzaj iwa lugha wapate kuelewana

iv. Manenoyasiyo sanifuyanayozungumzwanakikundi kidogo cha watu

v. Misemo yapicha ambayo huletamaana iliyofichika.

  1. Misimu
  2. Sarufi
  3. Kamusi za watoto
  4. Tungo tata
  5. Kiarifu
  6. Kamusi mahuluti
  7. Nahau
  8. Methali
  9. Makosa ya upatanisho wa kisarufi
  10. Misemo

SEHEMU B (ALAMA 40)

(Jibu maswali yote katika sehemu hii)

3. Kwakila sentensi onesha kiima na kiarifu kwa kutenga na kistarina kuandika "K" kwa kiimana "A" kwa kiarifu

i. Mwanasiasa alikuwa anahutubia wanakij iji wote leo 

ii. Mbuzi wangu mkubwa amekula majani yote.

iii.Ng'ombe wetu amekunywa maji machafu mno.

iv. Walifika asubuhi walimu wetu.

v. Mwalimu alikuj a kufundisha Kiswahili asubuhi.

4. Tungozifuatazo zinamaanazaidiyamoja. Toamaanambili tukwakilatungo.

A.Nimenunua mbuzi

B. Eda ameshinda shuleni

C. Ukija njoo na nyanya

D.Nyumbani kwao kuna tembo.

5. a) Soma kwa makini sentensi (i) hadi (iv) kasha fafanua kwa pamoja vipengele vinne (4) vinavyodhihirisha uhusiano baina ya Kiswahili na lugha za kibantu kisayansi

i. Mtoto amelala(kiswahili) 

ii. Mwana agonile(kingoni) 

iii. Mwana yogonile(kigogo) 

iv. Omwana yanagile(kihaya)

b) Kwa kutumia mifano na kutoa hoja mbili kwa kila hoja moja, eleza kwa utupl mafanikio ya lughayaKiswahili enzi za waarabu katika.

i) Dini 

ii) Biashara.

6. Kwa kutumia mifano kutoka katika tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe E. Semzaba (ESC). Eleza kwa kifupi madhara manne yanayoweza kutokea katikajamii iwapo zoezi la uhesabuji watu (Sensa) litakumbwa na Uzembe.

7. Fikiria kuwa umekutana na mtu ambaye ameteuliwa kutoa hotuba kwenye mkutano wa kijiji kinachoendekeza mila potofu ya unyanyasaji wa walemavu wa ngozi lakini hajawahi kutoa hotuba tangu azaliwe. Wewe kamamwanafunzi wa kidato cha nne eleza kwa ufupi mambo makuu matano (05) atakayopaswa kuzingatia wakati wa utoaji wa hotuba hiyo ili ujumbe uliokusudiwa uweze kuwafikia walengwa.

8. Soma beti zifuatazo za shairi la kimapokeo, 

Kishajibu maswali yanayofuata.

Tuitafute elimu, vitabu vyote vyasema,

Nikitu lilo muhimu, kwa maisha yako mema

Tuipate na idumu, ijenge yalo hekima. 

Elimu dira sahihi, Ongoza yetu maisha

Elimu kwetu ni mali, uishike ninasema,

Haitaki ukatili,yakutaka uwe mwema, 

Maisha kuyakabili, kuyafanya yawe mema

Elimu dira sahihi, Ongoza yetu maisha

Maswali

a) Bainisha ukwapi na utao wamstari watatu wa ubeti wapili

b) Tajatamathali mbilizasemi kwamifanokutokakatikashairi ulilosoma.

c) Mwandishiwashairi hili anÜungumzianafsi ipi? Thibitishajibulakokwamifanomiwili kutoka katika shairi ulilosoma.

d) Elimu humpatiamtu fedha kwani atalipwa kuendananataalumaaliyonayo lakini kuna watu wana fedha nyingi ila hawana elimu. Kwa muj ibu wa shairi hili unadhani watu hao wanakosa kitu gani cha msingi? Eleza kwa hoja moja.

SEHEMU (Alama 45)

Jibu maswali matatu katika sehemu hii

9. Jifanye umepata baruayamwaliko washereheyasikuyakuzaliwakwarafikiyakoaitwaye Dadakiboga Stella itakayofanyika tarehe 12/08/2022 lakini kwa bahati mbaya Siku tano kablaya sherehe umepata safari ya kikazi kuelekea mkoani Mwanza. Andika barua kumtaarifu rafiki yako Dadakiboga Stella wa sanduku la barua 110 Soweto kuwa hutaweza kuhudhuria sherehe hiyo Jina lako liwe Makoti Msweta, Sanduku la posta 212 Arusha.

ORODHAYAVITABU KWASWALI LA 10-12

USHAIRI

  • Wasakatonge — M.S Khatibu (DUP)
  • Malenga Wapya- TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi - T.A Mvungi (EP &D.LTD)

RIWAYA

  • Takadini - Ben J Hanson (MBS) Watoto Wa -E. Mbogo (HP)
  • Joka La Mdimu —A.J Safari (HP)

TAMTHILIYA

  • Orodha — Steve Reynolds (MA)
  • Ngoswe Penzi Kitovu Cha Uzembe—E Semzaba(ESC)
  • Kilio Chetu — Medical Aid Foundation (TPH)

10. "Mshairi ni mjuzi wa kubuni na kuandaa taaswira itakayo mvuta msomaji katika kazi ya ushairi ” Kwa kutumia diwani mbili kati ya tatu ulizosoma, Elezajinsi mwandishi alivyotumia taaswiratatu kutoka katika kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwaj amii.

1l. Watanzania wa leo wangefaidika sana na tamthiliya kama wangekuwa na utamaduni wakusoma tamthiliya. Thibitisha kauli hii kwa kutumia vitabu viwili kati ya hivyo vilivyotaj wa hapojuu.

12. "Waandishi wa kazi za Fasihi huibua migogoro mbalimbali nakupendekeza masuluhisho ili kuelimisha jamii husika Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa hoj a tatu kutoka katika Riwaya mbili kati ya riwaya tatu ulizosoma.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 35  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 35  

OFSI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MUUNGANO WA WAKUU WA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI(OHONGSS)


MTIHANI WA UTIMILIFU KIDATO CHA NNE 2022

 KISWAHILI 

MASAA : 3 JUNI 2022 

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una sehemu A, B, na C.
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B, na maswali matatu tu katika sehemu C.
  3. Majibu yote yaandikwe kwenye kijitabu cha kujibiwa ulichopewa.
  4. Andika namba yako ya mtihani kwenye kila karatasi ya kijitabu cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua herefi ya jibu sahihi kisha andika jibu lako kwenye kijitabu cha kujibia.

(i) Mhazili ni;

  1. Mwalimu wa chuo kikuu 
  2. Mtu anayerekodi video 
  3. Mtu anayetunza na kuazimisha vitabu maktaba 
  4. Mtu anayeandika kwa mashine kama vile kompyuta na kuhifadhi majalada ya ofisi

(ii) ‘Pigia mstari.’ Msemo huu una maana ya;

  1. Chora mstari chini ya maneno 
  2. Piga kwa mstari 
  3. Hilo ndilo jibu 
  4. Kataa

(iii) Amechomwa na mwiba. Neno lililokolezwa wino ni;

  1. Kihusishi
  2. Kiunganishi  
  3. Kihisishi 
  4. Kivumishi

(iv) Mwanzilishi wa mashairi ya mtindo kujibizana ni;

  1. Shaaban Robert 
  2. Mathias Mnyampala 
  3. Abeid A. Kaluta 
  4. Saadan Kandoro

(v) Neno ‘mbakaji’ limeundwa kwa njia ya;

  1. Mnyumbuliko 
  2. Kufananisha kazi 
  3. Uhulutishaji 
  4. Utohoaji

(vi) Maneno yapi yametokana na mbinu ya ukopaji?

  1. Duka na chujio
  2. Papai na pikipiki  
  3. Namba na kuku 
  4. Kibatari na karoti

(vii) Kipande cha pili katika mshororo wa shairi huitwa;

  1. Utao 
  2. Ukwapi 
  3. Mwandamizi 
  4. Mtawalia

(viii) Utokeaji wa misimu katika jamii hutegemea……………

  1. Uchaguzi wa viongozi
  2. Shughuli itendekayo  
  3. Mabadiliko ya kijamii 
  4. Utani uliopo miongoni mwa wanajamii

(ix) Neno lipi kati ya yafuatayo linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?

  1. Kiunganishi 
  2. Kiwakilishi 
  3. Kihisishi 
  4. Kielezi

(x) Kati ya sababu zifuatazo ni ipi si sahihi kuhusu matumizi ya kamusi?

  1. Kujifunza lugha ya kigeni 
  2. Kubaini kategoria ya neno 
  3. Kusanifisha maneno mapya 
  4. Kujua tahajia za maneno

2. Oanisha maelezo ya kifungu A na maneno katika kifungu B

KIFUNGU A

KIFUNGU B

  1. Sehemu ya kiarifu inayokaliwa na nomino _____________
  2. Neno au mpangilio wa maneno wenye neno kuu moja _________
  3. Sehemu ya kiarifu inayokaliwa na kielezi _________
  4. Huundwa na vitenzi vyenye viambishi vya o-rejeshi _____
  5. “Mwenye duka” ni muundo wa ___________
  6. “Atarudi kesho” ni muundo wa _______
  7. “Mwanafunzi ambaye hakufika jana, asimame” ni mfano wa sentensi ___________
  1. Kirai
  2. Kishazi tegemezi
  3. Kirai kivumishi
  4. Shamirisho
  5. Kirai kitenzi
  6. Kishazi tegemezi kielezi
  7. Chagizo
  8. Kirai kielezi
  9. Kirai nomino
  10. Ambatani
  11. Prediketa
  12. Kiarifu
  13. Changamani

SEHEMU A (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Bainisha mizizi ya maneno yafuatayo:

  1. Anabisha
  2. Nimeibeba
  3. Pamba
  4. Wezesha

4. Eleza miundo minne ya kishazi tegemezi.

5. (a) Bainisha kwa mifano njia nne za uundaji wa misimu.

(b) Eleza mambo manne ya kuzingatia unapofanya mazungumzo.

6. Kiswahili ni kibantu. Thibitisha dai hili kwa kutumia hoja nne.

7. Bainisha taswira mbili kwa kila diwani za Wasakatonge na Malenga Wapya.

8. Chukulia kuwa wewe ni mwalimu Haule Ndomba wa shule ya sekondari Nyika. Mwandikie barua pepe mkuu wako wa shule ukimtaarifu kuwa hutaweza kufika kazini kwa kuwa hujihisi vizuri kiafya.

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu tu katika sehemu hii.

9. Tunga utenzi wenye beti tano kuhusu Sensa ya watu na makazi 2022.

10. Tumia diwani mbili, hoja tatu kwa kila moja, kuonesha ni kwa namna gani waandishi wa kazi za fasihi hutumia kazi zao kuelimisha jamii.

11. Uteuzi mzuri wa wahusika ndio husaidia kuibua dhamira mbalimbali katika kazi za fasihi. Jadili kauli hii kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma. (Hoja 6)

12. Dhihirisha utokeaji wa migogoro katika jamii kwa kutumia riwaya mbili ulizosoma. (Hoja 6)

ORODHA YA VITABU

 USHAIRI

Wasakatonge - M. S. Khatibu (DUP)

Mashairi ya Cheka Cheka - T. Mvungi (DUP)

Malenga Wapya - TUKI

 RIWAYA

Watoto wa Mama N’tilie - E. Mbogo

Joka la Mdimu - A. J. Safari (HP)

Takadini -

 TAMTHILIYA 

Kilio Chetu - Steve Raynolds (MA)

Orodha - Medical Aid Foundation

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - Edwin Semzaba

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 30  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 30  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA UMOJA WA KITAALUMA KANDA YA MIKUMI

MTIHANI WA KIDATO CHA NNE WA  KUJIANDAA NA UTAMILIFU

021  KISWAHILI

(Kwa watahiniwa walioko shule tu

Muda: Saa 3 Alhamisi Machi 18, 2021 

MAELEKEZO:

1. Mtihani huu una sehemu A, B, na C zenye jumla maswali 12.

2. Jibu maswali yote katila sebemu A na B kisha maswali matatu (3) kutoka sebemu C.

3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.

4. Hauruhusiwi kuingia na simu wala nakala yoyote inayohusiana na somo la Kiswahili.

5. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu Chako cha kujibia.

SEHEMU A (ALAMA 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

l. Katika kipengele cha i-x chagua jibu sahihi kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu Chako cha kujibia

i.Sentensi ipi kati ya zifuatazo ina kiambishi cha mtendwa nafsi ya pili umoja?

  1. Wao walituibia madafrari
  2. Wewe umeona taka mbali
  3. Nitakununulia nguo mpya
  4. Nimekiona kilichopotea
  5. Baba anamuonea huruma 

ii.________________ ni mabadiliko ambayo yamesababisha uhitaji wa neno nywila

  1. Uchumi
  2. Sayansi na teknolojia
  3. Utamaduni
  4. Siasa

iii. Zifuatazo ni nomino za kawaida isipokuwa

  1. Bunge
  2. Meza
  3. Shali
  4. Dawati
  5. Mwanajeshi

iv. Sentensi "Waziri wa fedha atawakilisha bajeti ya mwaka wa fedha 2010/2011" ina kosa gani la kisarufi?

  1. Kosa la kimsamiati
  2. Kosa kimuundo
  3. Kosa la kimatamshi
  4. Kosa la kimantiki
  5. Kosa la kimaana

v. Maneno, nahau au sentensi ambatano hutumiwa na wasanii wafasihi ili kutia nguvu katika maana, mtindo na sauti katika maandishi ama kusoma huitwa

  1. Ujumbe
  2. Tamathali za semi
  3. Majigambo
  4. Matumizi ya lugha 
  5. Msisitizo

vi. Vifuatavyo ni vigezo vya kiisimu vinavyothibitisha ubantu wa Kiswahili isipokuwa

  1. Upatanisho wa kisarufi
  2. Msamiati
  3. Muundo wa sentensi
  4. Ushairi wa Kiswahili
  5. Ushahidi wa Malcon Guthrie 

vii. Ni seti ipi haina tawi la sanaa?

  1. Maonesho, ususi, uhunzi, ufumaji, utarizi na uchongaji.
  2. Ususi, uhunzi, ufumaji, utarizi, uchongaji na ufinyanzi.
  3. Fasihi, sarufi, muziki, uchoraji, ngoma, ufinyanzi na ususi,
  4. Fasihi, maonesho, ususi, uhunzi, uchoraji, na utarizi.
  5. Hakuna jibu sahihi.

viii. Zifuatazo ni dhima za uundaji wa maneno mapya katika lugha isipokuwa

  1. Kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambayo huchukua sura mpya karibu kila siku
  2. Kwa ajíli ya kuweza kutafsiri maneno mengi kutoka lugha yako kwenda lugha nyingine, 
  3. Ili kupata msamiati utakaokubalika katika shughuli mahususi kama Vile benki, forodhani.
  4. Kwa ajili ya kuburudisha na kuonya jamii.
  5. IIi kukidhi haja ya mawasiliano.

ix. Viambishi vya 0-rejeshi ya nomino "gari" ni vipi kati ya vi fuatawo?

  1. O/NO
  2. YE/O
  3. LO/YO
  4. O/ZO 
  5. PO/YO

x.Taja seti iliyosahihi katika mambo yanayounda fasili ya lugha.

  1. Kukidhi haja ya mawasiliano, sauti, nasibu, mama,
  2. Sauti, nasibu, kukubaliwa na jamii, maana, kufurahisha
  3. Sauti, nasibu, maana, kukubaliwa najamii kukidhi haja ya mawasiliano
  4. Sauti, nasibu, maana, kukubaliwa najamii kuelimisha
  5. Sauti, maana, nasibu fonimu kukubaliwa najamii

2. Oanisha maana ya dhana ya vifungu vya maneno vilivyo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika orodha B, kisha andika herufi husika katika kijitabu chako cha kujibia.

ORODHA A

ORODHA B

(i) Simo

(ii) Tungo shurutia 

(iii) Kamusi wahidiya

(iv) Ngeli

(v) Kiambishi cha nafsi ya pili wingi

  1. Tungo yenye maana zaidi ya moja
  2. Mnaimba
  3. Mtoto aliyekuja jana anaumwa
  4. Ni maneno yasiyosanifu yanayotumiwa na kikundi cha watu fulani wenye utamaduni wa aina moja.
  5. KU
  6. Kamusi iliyoandikwa kwa lugha mbili
  7. Neno lenye asili ya kichaga
  8. Kamusi iliyoandikwa kwa lugha moja
  9. Akija atanikuta nyumbani
  10. Wanaimba

SEHEMU B (ALAMA 40)

Jibu maswali yote kutoka schemu hii

3. Kwa mifano dhahiri, unadhani watanzania watakumbwa na matatizo gani endapo watatumia lugha isiyofaha katika mawasiliano yao ya kila siku, Tao hoja nne.

4. Kwa kawaída fasihi simulízi huweza kukumbwa na matatizo katika vipengele vyake vikubwa vinne. Vitaje

5. (a) Nini maana ya Msamiati?

(b) Moja ya tabia ya lugha ni kujizalisha ili kupata msamiati mpya utakaokidhi haja ya mawasiliano. Kwa kifupi, eleza mbinu tano ambazo lugha ya Kiswahili inaweza kuzitumia ili kujizalishia maneno mapya.

6.(a) Toa mfano wa neno linaloonesha dhima ya kiambishi ulichopewa kulingana na maelezo yake na ukipigie mstari.

(i) "Li" - kuonesha urejeshi wa mtendwa

(ii) "Kwa" — kuonesha sababu na kuulizia sababu

(iii) ‘Tu’ kuonesha nafsi

(iv)"Ku" kuonesha wakati uliopita

(b). Kwa maelezo mafupi tofautisha istilahi zifuatazo.

(i) Sarufi na Fasihi

7. Waarabu, Wajerumani na Waingereza kwa nyakati tofauti waliitawala Tanganyika, eleza kwa ufupi mambo matano (5) yaliyofanywa na Waingereza katika kuikuza na kuineza lugha ya kiswahili.

8. Soma shairi lifuatalo kishajibu maswali yatakayofuata

l. Mtu wa fikra njema na kwa watu huacha jina.

Kwa kujua dunia nzima, likawa kubwa hazina

Kwa kujua jambo jema, lisilokuwa na shari,

Na watu wajao nyuma, wakapenda kulisoma.

2. Mvuka nguo chutama, wendapo wajihadhari, Na busara ni kutenda, tendo ambalo ni jema, Viumbe wakalipenda, ukapata na heshima, Tabasuri na hekima, ni muhimu maishani.

3. Maisha daima yenda, utaacha nini nyuma?

Ni roho yenye hekima, usambe ni santuri,

Ambayo huweza sema, maneno kwa kukariri, Hali haina uzima, ufahamu ni tafakuri.

4. Kama akili hunena, tungeshindwa na vinanda,

Vya sauti nzuri sana,visivyoweza kutenda,

Matendo yenye maana, ambayo mtu hutenda,

Fikra ni fani bora, katika fani za watu,

5. Weledi wenye busara, na maarifa ya vitu,

Wafahamu kwa sura, ulimwengu wetu wote,

Hekima na busara ya mtu, hupimwa kwa matendo mema, Ayatendayo yenye utu, na wala si maneno mengi kinywani.

(a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.

(b) Neno jina lina maana gani katika shairi?

(c) Mtu mwenye akili ni mtu wa namna gani?

(d)Eleza maana ya maneno yaliyokolezwa wino kama yalivyotumiwa kwenye shairi hili.

(e) Kwa nini hekima na busara ya mtu humpimwa kwa matendo na siyo maneno?

SEHEMU C (ALAMA 45)

 Jibu maswali matatu (3) tu kutoka schemu hii

9. Andika insha ya hoja isiyopungua maneno mia mbili (200) na isiyozidi maneno mia mbili na hamsini (250) kuhusu madhara ya kuchafua mazingira.

ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 10-12

USHAIRI

  • Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)
  • Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D. LTD)

RIWAYA

  • Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
  • Watoto wa mama N’tilie - E. Mbogo (H.P)
  • Joka la Mdimu - A. J. Safari (H.P)

TAMTHILIYA

  • Orodha - Steve Reymond (MA)
  • Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
  • Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

10. ‘Mshairi siku zote hukemea uonevu katika jamii.’ Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tano kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma

11."Waandishi wa kazi za fasihi ni walimu wa jamii", Wewe kama mwanajamii, eleza namna ulivyonufaíka na ualimu wa waandishi wawili wa riwaya ulizosoma. Toa hoja tatu kila kitabu.

12. Vijana ndio nguvu kazi ya Taifa lakini mara nyingi vijana hao huliangusha taifa kwa kutenda matendo yasíyofaa. Kwa kutumia tamthilíya mbili ulizosoma, fafanua matendo yasiyofaa yanayotendwa na vijana. Toa hoja tatu kila kitabu

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 50  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 50  

Namba ya Mwanafunzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA UTIMIRIFU MKOA WA ARUSHA MEI 2021

KIDATO CHA NNE

KISWAHILI

MAELEKEZO

  • Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12)
  • Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka katika sehemu C.
  • Zingatia maagizo ya kila sehemu ya kila swali
  • Simu ya mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  • Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurabawa kitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (ALAMA 15)

1.Jibu maswali yote Katika sehemu hii,

(i) Ni aina ya wahusika ambao hawabadiliki na wamepewa majina ambayo humfanya msomaji aelewe tabia na matendo yao;

  1. Wahusika wakuu
  2. Wahusika bapa sugu
  3. Wahusika duara
  4. Wahusika bapa vielelezo
  5. Wahusika shinda

(ii) Vishazi tegemezi vimegawanyika katika aina kuu mbili ambazo ni;

  1. Vishazi tegemezi viwakilishi na vielezi
  2. Vishazi tcgemezi vivumishi na viunganishi
  3. Vishazi tegemezi vumishi na vielezi
  4. Vishazi tegcmezi vikuu na visaidizi
  5. Vishazi tegemezi nomino na vihusishi

(iii) Anatoa ufafanuzi juu ya ubantu wa Kiswahili kwa kuelezea wakazi wa mwambao waliojulikana kama "Wazanji" na watawala wao waliojulikana kama "Wakilimi"

  1. Ali-Idris
  2. Al-Masudi
  3. Marco Polo
  4. Ibin Batuta
  5. Fumo Liyongo

(iv) Ni lahaja zinazopatikana Mombasa;-

  1. Kitumbatu, kingazija, kimvita na kingare
  2. Kizwani kintang'ta, kinakunduchi na kibajuni
  3. Kijomvu, kingare, chichifundi, na kimvita
  4. Kitumbatu, kingare, kimvita na chichifundi
  5. Kimvita, chichifundi, kingazija na kijomvu

(v) Mofimu ku iliyopigiwa mstari imebeba dhima gani katika kitenzi sikukukumbuka

  1. Ukanushi wakati uliopita
  2. Ukanushi nafsi ya kwanza umoja
  3. Kauli ya kutendeka
  4. Kiambishi kirejeshi kauli ya kutenda
  5. Kudokeza mtendwa

(vii) Sehemu ya mzizi asilia iliyoambikwa kiambishi "a" mwishoni

  1. Shina
  2. Mzizi huru
  3. Mofu
  4. Kauli
  5. Mofimu huru

(viii) Ni tamathali ya semi ambayo Jina la mtu hutumiwa kwa watu wengine wenye tabia, mienendo, hulka au kazi sawa na mtu huyo

  1. Taniaba
  2. Tabaini
  3. Majazi
  4. Tashtiti
  5. Ritifaa

(ix) Neno SHADARA limepatikana Iwa kutumia njia gani ya uundaji wa maneno?

  1. Kutohoa
  2. Ufupishaji
  3. Miambatano
  4. Uhulutishaji
  5. Kukopa

(x) Chama cha kukuza na kueneza Kiswahili "TAKILUKI" kilianzishwa mwaka

  1. 1964
  2. 1967
  3. 1979
  4. 1972
  5. 1965

(xi) Aina ya hadithi za ngano zenye wahusika wanyama tu hujulikana kama,

  1. Hekaya
  2. Hurafa
  3. Istiara
  4. Soga
  5. Vigano

2. Chagua kifungu cha maneno kutoka orodha B kinachotoa maelezo sahihi ya maneno neno katika orodha A.

ORODHA A

ORADHA B

  1. Kauli
  2. Lakabu
  3. Kitenzi kishirikishi
  4. Bendera
  5. Prediketa
  1. Kireno
  2. Jutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti
  3. Huoncsha hali ya kuwepo au kutokuwa kwa jambo/kitu
  4. Husaidia kitenzi kikuu kukamilisha maana
  5. Uhusiano uliopo kati ya kiima na kitenzi au kiima kitenzi na yambwa
  6. Kihindi
  7. Majina yakupanga ambayo baadhi ya watu hupewa kutokana na sifa zao za kimaumbile au kinasaba
  8. Ni kipcra cha ushairi
  9. Sehemu ya kiarifu ambayo hukaliwa na kitenzi
  10. Kipashio cha kiarifu kinachooncsha mtenda wa jambo

SEHEMU B ( Alama 40)

3. Bainisha aina ya kauli katika vitenzi vilivyopigiwa mstari, huku ukifafanua kiambishi kinachojenga kauli hiyo katika tungo zifuatazo.

(i) Matukio ya ubakaji yanaogofya

Waoga wanafahamika

(iii) Nyumba itajengwa na wazazİ

(iv) Dawa za kienyeji zilimlevya sana

4. Huku ukuota mifano. Fafanua dhima nne za mofimu "M" katika lugha ya Kiswahili.

5. Fafanua kwa hoja nne, mambo yanayothibitisha kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni pwani ya Afrika ya Mashariki,

6. Methali hutawaliwa na vipengele mbalimbali vya lugha, onesha vipengele vya lugha vilivyotumika katika utunzi wa methali zifuatazo.

(i) Kibuzi na kibuzi hununa jahazi

(ii) Akili ni mali

(iii) Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?

(iv) Baniani mbaya kiatu chakc dawa.

(v) Avumayc 'baharini papa, kumbe wengine wapo

7. Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata Mtu wa fikra njema, kwa watu umcacha jina

Chuma chetu imara, Afrika na dunia nzima,

Mikakati imara lojenga, Tanzania nuru kuangaza

Jiwe Ietu limeondoka takuenzi daima

Katika yote dunia, Jinalo lilivema

Misimamo yenye mashiko, ndiyo yako şifa njema 

Nia kubwa kujenga, boma, ndiyo ndoto yako imara

Chuma chetu kimelala, hakika umeacha alama


'Umoja uliujenga, utengano likemea

Uchapakazi ulihimiza, nani alibaki nyuma?

Macndeleo kuyajcnga, Elimu hukuacha nyuma.

Nguzo yetu imeinama, nyoyo zetu zimechutama

Wangu wosia naweka, aloacha kuyaenzi

Uzalendo tuudumishe, Ufisadi tuupinge

Vizazi vijavyo tupate hadilhia, mazuri ya mwamba wetu. 

Takuombea daima, lalc kwa ushindi shujaa.

Maswali

(a) (i) Shairi hili limejegwa kwa kutumia muundo gani?

(ii)Fafanua mambo ya msingi yakuzingatia wakati wa uchambuzi wa muundo katika ushairi (Hoja Nne)

(b) Onesha upekee wa mıvandishi katika shairi hili (Hoja Nne)

(c) Mwandishi ana maana gani anaposema jiwe, mwamba chuma na nguzo?

(d) Andika kichwa cha habari cha shairi hili.

(e) Mwandishi anahimiza nini katika kumuenzi shujaa.

8. Kijiji chenu cha Kiloza kimeanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji. Wewe kama afisa manunuzi, andika barua katika kampuni ya Olotu inayojihusisha na uuzaji pembejeo za kilimo kuangiza bidhaa zitakazotumika katika kuendesha mradi. Jina lako ni Ombeni Mtapewa.

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu kutoka katika sehemu hii.

9. Ni kweli kwamba lugha ya Kiswahili imevuka mipaka na kuenea katika maeneo mbalimbali duniani. Thibitisha ukweli wa dai hili (Hoja - 5)

TAMTHILYA

Orodha - Steve Reynolds (MA)

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe -E. Semzaba (ESC)

Kilio chetu - Medical Aid Foundation

RIWAYA

Takadini - Ben Hnson (MBs)

Mamantilie - Emanuel Mbogo

Joka la mndimu - A. J. Safari (HP)

USHAIRI

Cheka cheka - T. Muungi

Malenga wapya - Takiluki

Wasaka tonge - Mohamed Seif Khatibu

10. Washairi ni wataalamu wazuri na waliobobea katika kutumia jazanda zinazotoa ujumbe kwajamii. Tumia jazanda tatu kwa kila diwani mbili uliyosoma.

11. Lugha ni kipengele cha msingi katika ujenzi wa kazi ya fasihi ambayo husaidia katika kufikisha wazo la msanii kwa jamii. Kwa kutumia riwaya teule mbili (2) ulizozisoma. Jadili jinsi wasanii wa riwaya hizo walivyotumia kipengele cha tamathali za semi hoja Sita (6)

12. Mwandishi ni Mjenzi wa jamii. Thibitisha ukweli wa dai hili kwa kutoa hoja tatu kutoka katikaTamthilia mbili ulizozisoma


FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 27  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 27  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA UTAMILIFU MKOA WA DODOMA 2020

021 KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

MUDA: SAA 3 Alhamisi, 6 Agosti 2020 mchana

Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).

2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A, B na chagua maswali matatu (03) kutoka sehemu C.

3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.

4Andika kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi

5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

6. Andika namba yako ya mtihani katika kila karatasi yako ya kujibia.

SEHEMU A, (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

 1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi yako ya kujibia.

(i) Ni kanuni, sheria na taratibu zipi zinazozingatiwa na wazungumzaji wa lugha fulani?

  1. Mofimu, Neno, Kirai, Kishazi na Sentensi
  2. Herufi, Sauti, Mofimu,Silabi na neno.
  3. Sarufi Maana, Sarufi Miundo, Sarufi Maumbo na Sarufi Matamshi.
  4. Sarufi maana, Mofimu, Neno na Kirai
  5. Silabi, Neno, Kirai na Sentensi.

(ii) ………………. Ni sauti zinazotamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti.

  1. Sauti
  2. Herufi
  3. irabu
  4. Silabi
  5. Konsonanti

(iii) Zipi ni nyenzo za lugha yoyote duniani?

  1. Sarufi na Fasihi 
  2. Irabu na Konsonanti
  3. Sarufi, Irabu na Konsonanti 
  4. Fasihi, Irabu na Konsonanti
  5. Sarufi, Fasihi, Irabu na Konsonanti

(iv) Mpangilio sahihi wa ngeli za kisintaksia ni upi?

  1. YU/A-WA, I-ZI, LI-YA, U-I, KI-VI, U-ZI, U-YA, KU, PA-MU-KU
  2. U-ZI, I-ZI, LI-YA, U-I, KU, YU/A-WA, U-YA, KI-VI, PA-MU-KU
  3. YU/A-WA, I-ZI, LI-YA, U-YA, KI-VI, U-ZI, U-I, KU, PA-MU-KU
  4. YU/A-WA, I-ZI, LI-YA, U-I, KI-VI, U-ZI, U-YA, PA-MU-KU, KU
  5. YU/A-WA, I-ZI, LI-YA, U-I, KI-VI, U-ZI, U-YA, KU, PA-MU-KU

(v) Ni upi mpangilio sahihi wa mjengo wa Tungo?

A Kirai, Neno, Sentensi na Kishazi

B Neno, Kirai, Kishazi na Sentensi

C Kishazi, Kirai, Sentensi na Neno

E Sentensi, Neno. Kishazi na Kirai

(vi) Ni lugha mseto ya muda inayozuka pindi makundi mawili yenye lugha mbili tofauti yakutanapo.

  1. Lugha ya vizalia 
  2. Pijini
  3. Kibantu 
  4. Kiswahili
  5. Kiunguja

(vii) Mambo muhimu yanayopatikana katika maana ya lugha ni kama yafuatayo, isipokuwa;

  1. Ni sauti za nasibu 
  2. Ni mfumo
  3. Lugha hufurahisha na kufundisha 
  4. Lugha inamuhusu binadamu
  5. Lugha ni chombo cha mawasiliano

(viii) Ni sentensi ipi sio sentensi huru?

  1. Juma anacheza mpira
  2. Anaimba vizuri
  3. Mtoto aliyepotea jana amepatikana.
  4. Asha ni mtoto mzuri
  5. Yule alikuwa anataka kucheza mpira.

(ix) ……………. Ni kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana. Maana hiyo yaweza kuwa ya kisarufi au kileksika;

  1. Isimu 
  2. Shina
  3. Mzizi 
  4. Kiimbo
  5. Mofimu

(x) Ni seti ipi inawakilisha kikamilifu wahusika wa fasihi simulizi?

  1. Vitu, mahali, wanyama, binadamu, fanani na maleba.
  2. Hadhira, wanyama, maleba, binadamu na fanani.
  3. Fanani, vitu, mahali, binadamu, maleba na wanyama.
  4. Wanyama, manju, binadamu, vitu, mahali na maleba
  5. Hadhira, binadamu, wanyama, vitu, mahali na fanani.

2. Oanisha maelezo yaliyo katika orodha ‘’A’’ ambayo ni aina ya tungo na orodha ‘’B’’ ambazo ni aina za maneno yanayounda tungo hizo kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

ORODHA “A”

 ORODHA “B”


i. Wale waliamini maneno yangu

ii. Salama alikuwa mwanafunzi wangu

iii. Walikuwa wanataka kwenda kulima

iv. Alikuwa anajisomea darasani polepole

v. Loo! Yule anapenda ugomvi

A. N + t +N +V

B. H + w +T + N

C. W + T + N + V

D. Ts + T + E +E

E. Ts + Ts + Ts + T

F. N + V + t +E

G. N + U+ N+ T

 SEHEMU B (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Tunga sentensi moja kwa kila alama kuonesha matumizi ya alama zifuatazo.

i. Mkato

ii. Mabano

iii. Alama za mtajo

iv. Nukta pacha

4. Andika maana ya methali zifuatazo;

  1. Kikulacho ki nguoni mwako.
  2. Mtaka cha uvunguni sharti ainame.
  3. Mchumia juani hulia kivulini.

5. (a) Tenga kiima na kiarifu katika sentensi zifuatazo. Tumia alama ya mkwaju (/) na kuweka herufi “K” juu ya kiima na herufi “A” juu ya kiarifu.

i. Mdogo wangu anaongea sana

ii. Yule kijana aliyekuja hapa juzi amefariki dunia

iii. Frank ni kijana mpole sana

iv. Mama amelala sakafuni

(b) Changanua sentensi zifuatazo kwa njia ya matawi kwa kutumia mkabala wa kimapokeo

i. Fisi mkubwa ameuawa kichakani jana alfajiri.

ii. Mtoto aliyekuwa anacheza uwanjani amevunjika mguu.

6.(a) Kwa kutumia mifano miwili kwa kila kipengele, fafanua kwa ufupi jinsi vipengele vifuatavyo vinavyoonesha kuwa vitenzi vya Kiswahili na lugha za kibantu vina asili moja.

  1. Mpangilio wa viambishi katika vitenzi
  2. Kiambishi tamati katika vitenzi

b) Eleza kwa ufupi juu ya nadharia zifuatazo kwa jinsi zinavyoelezea asili ya Kiswahili

  1. Kiswahili ni pijini au krioli
  2. Kiswahili ni kiarabu

7. Kwa kutumia mifano, fafanua dhana zifuatazo kama zinavyotumika katika fasihi

  1. Tashibiha
  2. Takriri
  3. Sitiari
  4. Tashihisi
  5. Mubaalagha

8. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali yanayofuata;

Wanangu, toka zamani bara letu la Afrika lilikuwa na mambo yaliyohitilafiana na haya tunayoyaona sasa. Hadithi, vitimbi, na visa vilivyotokea zamani katika bara letu vinatofautiana sana na mabara yoyote mengine. Vyetu ni vitamu na bora kuliko vyote vile vilivyotokea katika mabara hayo.

Miujiza ya mambo yaliyotokea ina mizizi ambayo viini vyake hubenua waziwazi mila na desturi za asili tangu zamani, hivyo, hadithi hizo zina tija ya makumbusho ya daima milele. Kwa hiyo, katika hali yoyote yatupasa kuhifadhi hazina za mila zetu. Mila zetu zidumishwe; kwa mfano watu kuzunguka moto huku kizee kikongwe au ajuza akisimulia hadithi za mambo ya kale liwe ni jambo la kawaida kabisa. Katika dunia ya leo simulizi hizo za ujasiri na uzalendo zimeenea kutoka vizazi hadi vizazi. Mambo mengi yamebadilika kutoka mitindo aina aina, hivyo mabadiliko hayo yasitufanye sisi kusahau simulizi zetu katika mitindo yetu. Ni wajibu utupasao kuendeleza tabia hizi ili tubenue mbinu za masimulizi hata kwa vitabu.

Maswali

  1. Pendekeza kichwa cha habari hii kisichozidi maneno matatu.
  2. Bara la Afrika lina mambo gani mawili mazuri.
  3. Mwandishi anatuhimiza tudumishe mila ipi?
  4. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua 50 na yasiyozidi 60.

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu(3) kutoka katika sehemu hii.

9. Wewe kama afisa Manunuzi wa kiwanda cha mbao cha Mshikamao S. L. P 100 Chamwino, andika barua kwa mfanyabiashara yeyote mashuhuri wilayani kwenu kuhusu agizo la vifaa vifuatavyo; Misumeno 5, gundi ya mbao lita 20, misumari ya nchi sita Kg 25, na kofia ngumu 40. Jina lako liwe Shukrani Kazamoyo.

10. Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma, eleza jinsi taswira tatu kutoka kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwa jamii.

11. “Kazi ya fasihi ina radha kwa sababu inamzungumzia pia mwanamke kwa namna tofautitofauti” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu katika riwaya mbili ulizosoma.

12. Chagua wahusika wawili katika tamthiliya teule mbili ulizosoma na uoneshe ujumbe unaowasilishwa na waandishi kupitia matendo yao.

ORODHA YA VITABU

USHAIRI

Wasakatonge ---------------------------- M. S Khatibu (DUP)

Malenga wapya-------------------------- TAKILUKI (DUPU)

Mashairi ya Chekacheka---------------- T. A. Mvungi (EPdD.LTD)

RIWAYA

Takadini ----------------------------------- Ben J. Hanson (MBS)

Watoto wa Mama Ntilie ----------------- E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu ---------------------------- A. J. Safari ( H.P)

TAMTHILIYA

Orodha ------------------------------------ Steve Reynolds ( M. A)

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe ----- E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu --------------------------------- Medical Aid Foundation (TPH)


FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 11  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 11  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256