STD VII SAYANSI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2010

SAYANSI 2010

 SEHEMU A

Chagua jibu sahihi na kuandika herufi inayohusika mbele ya namba ya kilo swali katika karatasi ya kujibia.

1. Ipi kati ya zifuatazo si faida ya michezo kwa afya zetu?

  1. Husaidia kujenga misuli
  2. Huzuia mwili kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara
  3. Husababisha shinikizo la damu
  4. Huleta burudani
  5. Hudumisha afya ya mwili
Chagua Jibu


2. Maji yaliyochanganywa na sukari na chumvi ni huduma ya kwanza kwa mtu. anayesumbuliwa na

  1. Malaria na kuumwa kichwa
  2. Kuhara na kutapika 
  3. Uti wa mgongo na homa ya matumbo
  4. Kifua kikuu na mafua 
  5. Kuvunjika mguu au mkono
Chagua Jibu


3. Moja ya magonjwa yafuatayo si ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya zinaa

  1. UKIMWI 
  2. Trikomona
  3. Kaswende 
  4. Klamedia
  5. Trakoma
Chagua Jibu


4. Ni vitamin ipi kati ya zifuatazo hutengenezwa mwilini kwa kuwepo mwanga wa jua? 

  1. Vitamini A            
  2. Vitamini B
  3. Vitamini C 
  4. Vitamini D
  5. Vitamini E
Chagua Jibu


5. Chanjo ina manufaa gani kwa binadamu?

  1. Hupunguza maumivu 
  2. Huponyesha maradhi
  3. Huzuia magonjwa 
  4. Hurudisha vitamin na madini mwilini
  5. Hurudisha seli chakavu mwilini
Chagua Jibu


6. Ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na bacteria gani?

  1. Wote walioko hewani 
  2. Basili
  3. Plasimodiamu 
  4. Fungi 
  5. Amiha
Chagua Jibu


7. Viwanda havipaswi kujengwa karibu na makazi ya watu kwasababu

  1. ujenzi wake huchukua eneo kubwa
  2. sehemu kubwa ya taka za viwandani huwa na kemikali ambazo ni sumu
  3. mitambo ya viwandani hutoa sauti kubwa hivyo kuathiri ngoma za masikio
  4. viwanda husababisha watu kuhamahama makazi
  5. wenye viwanda hawaweki mazingira yao katika hall ya usafi
Chagua Jibu


8. Vitendo vifuatavyo huharibu vyanzo vya maji isipokuwa

  1. kukata miti
  2. kuchoma misitu
  3. kulisha wanyama wengi kupita kiasi kwenye vyanzo vya maji
  4. kutupa taka za kemikali katika vyanzo vya maji
  5. kuchota maji ya kupikia toka kwenye vyanzo vya maji
Chagua Jibu



9. Asilimia kubwa ya uso wa dunia imefunikwa kwa maji. Sehemu kubwa ya maji haya hupatikana kwenye

  1. bahari 
  2. Mito 
  3. maziwa 
  4. mabwawa 
  5. madimbwi
Chagua Jibu


10. Mahali palipoinuka panafaa zaidi kujenga choo cha shimo kwasababu

  1. ni rahisi kujenga ukuta
  2. harufu itakuwa mbali na usawa wa ardhi
  3. si rahisi kuharibika upesi
  4. maji yatakuwa mbali na usawa wa choo chenyewe
  5. choo hakitafurika kwa muda mfupi
Chagua Jibu


11. Maji yanayobubujika kutoka ardhini hujulikana kwa jina gani?

  1. Bahari 
  2. Ziwa 
  3. Chemichemi 
  4. Bwawa 
  5. Mto
Chagua Jibu


12. Vitu muhimu katika uotaji wa mbegu ni

  1. udongo, mwanga wa jua na maji
  2. udongo, hewa na maji
  3. joto la kiasi, maji na hewa ya oksijeni
  4. joto la kiasi, udongo na mwanga wa jua
  5. maji, udongo na hewa ya kabonidayoksaidi
Chagua Jibu


13. Kundi la viumbe hai waishio majini na nchi kavu hujulikana kama

  1. Amfibia 
  2. Athropoda 
  3. Samaki 
  4. Ndege 
  5. Mamalia
Chagua Jibu


14. Kati ya viumbe wafuatao ni yupi si mamalia?

  1. Popo 
  2. Nyangumi 
  3. Simba 
  4. Sungura 
  5. Mamba
Chagua Jibu


15. Chunguza Kielelezo Namba 1 kwa makini kisha jibu swali lifuatalo

Kielelezo Na.1

Kiumbe aliyeoneshwa katika kielelezo Namba 1 huishi kwa kutegemea

  1. asali
  2. Nyama
  3. nafaka
  4. vyakula vya majini
  5. maada zilizooza
Chagua Jibu


16. Mmea uliochorwa katika kielelezo Namba 2 una sifa ya kuishi wapi?

Kielelezo Na. 2

  1. Kwenye misitu minene
  2. Majini
  3. Kwenye majani marefu
  4. Jangwani
  5. Milimani
Chagua Jibu


17. Kwanini baadhi ya mimea haipukutishi majani yake wakati wa masika?

  1. kuhifadhi maji yake 
  2. kuruhusu transipiresheni
  3. kuhifadhi chakula chake 
  4. kuhifadhi udongo
  5. kuufanya udongo uwe na rutuba
Chagua Jibu



18, Mchoro katika kielelezo Namba 3 unaonesha picha ya ua

Kielelezo 3

Ni sehemu gani  ya ua huvutia wadudu kuja kulichavua

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
Chagua Jibu


 19. Umeme unaotolewa katika seli kavu, chanzo chake ni nishati gani?

  1. Jua
  2. Kimakanika
  3. Sauti
  4. Sumaku
  5. Kikemikali
Chagua Jibu


20. Kibata alitumia nyutoni 50 kusukuma ukuta kutwa nzima bila mafanikio. Je, lipi sahih: kutokana na tukio hilo?

  1. alitengeneza kazi 
  2. alitumia kani kubwa sana
  3. hakufanya kazi yoyote 
  4. alifanya kazi nzuri
  5. alitumia kani ndogo
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256