MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

SAYANSI DARASA LA NNE

VIRUSI VYA UKIMWI NA UKIMWI

Chagua Jibu Sahihi

1. VVU ni kifupi cha . . . . . .

  1. Virusi Vinavyozaliana
  2. Virusi Vya Ukimwi
  3. Via Vya Uzazi
  4. Viungo Vya UKIMWI
Choose Answer



2. Mwathirika wa VVU/UKIMWI anaweza kuthibitishwa kwanjia ipi?

  1. Kupima damu yake hospitali ni
  2. Kumtazama uso wake
  3. Kuangalia tabia yake
  4. Kupima uzito wake
Choose Answer


3.UKIMWI husambazwa kwa kupitia:

  1. kusalimiana kwa kushikana mikono na mgonjwa wa UKIMWI
  2. kulala chumba kimoja na mgonjwa wa UKIMWI
  3. kuongea na mwathirika wa UKIMWI
  4. kuwekewa damu
  5. kuosha nguo za mwathirika wa UKIMWI.
Choose Answer


4. Ili kuepuka kupata maambukizi mapya ya UKIMWI tunashauriwa:

  1. kumeza dawa na kufanya mazoezi
  2. kuwa mwaminifu na kuepuka ngono zembe
  3. kuepuka kushirikiana na waathirika
  4. kuepuka kula pamoja na kubadilishana nguo na waathirika
  5. kupata chanjo ya UKIMWI na Kifua Kikuu.
Choose Answer


5.Lipi kati ya yafuatayo linapaswa kuzingatiwa kabla ya kumhudumia mgonjwa wa UKIMWI?

  1. Vaa nguo safi
  2. Nawa kwa sabuni
  3. Vaa glovu
  4. Sali
  5. Mruhusu apumzike
Choose Answer


6. Ni hoja ipi kati ya zifuatazo iko sahihi kuhusu VVU na UKIMWI?

  1. Kuwa na VVU ni sawa na kuwa na UKIMWI
  2. Chanzo cha VVU na UKIMWI ni magonjwa ya zinaa.
  3. Ni rahisi kujikinga na UKIMWI kuliko VVU.
  4. Ukiepuka maambukizi ya VVU pia umeepuka UKIMWI.
  5. Mtu mwenye VVU hana chembe nyeupe za damu.
Choose Answer


7. Virusi Vya Ukimwi hushambulia aina gani ya chembe hai katika damu?

  1. chembe sahani
  2. chembe hai nyeupe
  3. Chembe hai nyekundu
  4. Hemoglobini
  5. Plazima
Choose Answer



8. Kipi kati ya vifuatavyo ni maarufu kwa kuchangia maambukizi ya VVU katika jamii?

  1. Uchangiaji wa sindano, miswaki, damu na ngono zembe.
  2. Kanda za video, nyimbo, muziki na maigizo.
  3. Televisheni, magazeti na vipeperushi kuhusu VVU.
  4. Kondomu, wataalamu wa afya, semina na taasisi za UKIMWI.
  5. Tohara kwa wanaume na wanawake.
Choose Answer



9.Ipi kati ya zifuatazo siyo dalili ya UKIMWI?

  1. Kuvimba kwa matezi
  2. Kupoteza uzito
  3. Kuharisha kusikokoma
  4. Kikohozi cha muda mrefu kisicho cha kawaida.
  5. Kutoa jasho kusiko kwa kawaida wakati wa usiku.
Choose Answer



10. Njia sahihi ya kumtambua mtu mwenye virusi vya UKIMWI ni:

  1. Kupima kifua kikuu.
  2. Kupima mwenendo wa joto la mwili.
  3. Kuangalia kama amekonda kwa mda mfupi.
  4. Kuangalia kama ana vidonda mdomoni na usoni.
  5. Kupima kiwango cha kinga kwenye damu.
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256