MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

URAIA NA MAADILI A TANO

KUSIMAMIA MAJUKUMU

 

Chagua jibu sahihi

  1. Mtu kuwa na utayari wa kupokea majukumu hufuatana na:
  1. Kujitambua na kuwa na utayari wa kupokea ushauri
  2. Kushindana na wenzako
  3. Kukataa ushauri kutoka kwa mtu yeyote
  4. Kukubali bila pingamizi
Choose Answer


  1. Usimamizi wa majukumu shuleni hufanywa na;
  1. Walimu peke yao
  2. Wanafunzi wenyewe tu
  3. Walimu wakishirikiana na viongozi wa serikali ya wanafunzi
  4. Wazazi
Choose Answer


  1. Viongozi wote wanapaswa kuzingatia:
  1. Maendeleo yao tu
  2. Misingi ya utawala bora
  3. Utawala wa kiimla
  4. Upendeleo
Choose Answer


  1. Utii wa sheria:
  1. Haubagui kiongozi au mwananchi
  2. Bila shuruti hauwezekani
  3. Unasababisha ucheleweshaji wa majukumu
  4. Ni wa kiimla
Choose Answer


  1. Mwalimu mkuu ana majukumu ya:
  1. Kupokea fedha za ada na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi
  2. Kuongoza na kusimamia mambo yote shuleni
  3. Kuadhibu wanafunzi kwa uonevu
  4. Kufundisha walimu wengine
Choose Answer


  1. Sanduku la maoni husaidia:
  1. Kutotunza siri za wanafunzi
  2. Kuwaficha walimu kinachoendelea shuleni
  3. Kuwasilisha maoni kwa siri
  4. Kuwafichua waalifu
Choose Answer


  1. Kiongozi bora ni:
  1. Mtu anayependwa na watu wengi
  2. Mtu anayetawala kwa kufuata haki
  3. Mtu anayechaguliwa kwa kura nyingi
  4. Mtu anayependelea marafiki
Choose Answer


  1. Migogoro shuleni itakwisha endapo:
  1. Wanafunzi wote wakorofi hawatafukuzwa shule
  2. Walimu watashirikiana na baadhi ya wazazi
  3. Shuleni kutakuwa na uwazi na uongozi unaofuata sheria na haki
  4. Watu wote watamtii mkuu wa shule
Choose Answer


  1. Tunapaswa kuwatii viongozi wetu
  1. Kila mara
  2. Wanapofanya mambo mazuri
  3. Wanapotusamehe
  4. Tunapohitaji msaada
Choose Answer


  1. Ipi kati ya hizi ni utovu wa nidhamu?
  1. Kuvaa nguo za nyumbani shuleni
  2. Kuzingatia usafi wa mwili
  3. Kuwahi shuleni
  4. Kutii kengele  shuleni
Choose Answer


 

Katika sentensi zifuatazo andika neno KWELI kwa sentensi iliyo sahihi na neno SI KWELI kwa sentensi isiyo sahihi.

  1. Majukumu ni shughuli ambazo mtu anapaswa kuzitekeleza…………..
  2. View Answer


  3. Usimamizi wa shughuli ni kazi ya kinyapara…………
  4. View Answer


  5. Ili kutimiza majukumu hapana budi kusukumwa na kusimamiwa…………
  6. View Answer


  7. Mwanafunzi mwenye usikivu mzuri yupo tayari kuyatimiza majukumu anayopewa kwa kushurutishwa…………
  8. View Answer


  9. Kupokea ushauri ni kukubali mapungufu na ni njia ya kutaka kujifunza Zaidi……….
  10. View Answer


  11. Utawala bora ni uongozi unaotumia sheria kwa maslahi ya watu wachache…………
  12. View Answer


  13. Utii wa sheria husaidia kufanya mambo yaende kwa mpangilio………..
  14. View Answer


  15. Kutokuwa mtoro ni moja ya mfano wa sheria za shule…………
  16. View Answer


  17. Usafi wa mazingira ya shule ni wajibu wa wanafunzi wachache………
  18. View Answer


  19. Utawala bora huleta amani na kutatua migogoro katika jamii………

 

View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256