MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

URAIA NA MAADILI A TANO

KUJIJALI NA KUWAJALI WENGINE

 

Chagua jibu sahihi

  1. Kujijali na kuwajali wenzako kunasaidia mwanafunzi:
  1. Kufanya mambo yanayokubalika katika jamii
  2. Kuogopwa
  3. Kutenda uovu
  4. Kuwa mkorofi
Choose Answer


  1. Kugombana na wenzako mara kwa mara unapokuwa shuleni au nyumbani ni tabia:
  1. Isiyokubalika
  2. Inayoonesha kujali wenzako
  3. Ya upendo
  4. Ya unyenyekevu au kishujaa
Choose Answer


  1. Matendo yafuatayo yanakuza uhusiano na watu wengine:
  1. Kushirikiana, kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu, kuheshimiana na kujiunga katika vikundi vya kusaidiana
  2. Kuonesha upendo, kuheshimiana, ugomvi na unafiki
  3. Kuwasaidia watu wenye mahitaji, kusema uongo, kushirikiana na kuheshimiana
  4. Kuwasaidia watu wote na kuwafanyia unafiki
Choose Answer


  1. Moja ya faida za kujiunga na klabu za masomo shuleni ni:
  1. Kukuza uelewa na uongo
  2. Kukuza uelewa na kujiamini
  3. Kushindana kwa majibizano ya ujeuri
  4. Kuwa maarufu na kuvunja haki za binadamu
Choose Answer


  1. Ni njia mojawapo ya kutomsaidia mwanafunzi mwenye matatizo:
  1. Kumshika mkono
  2. Kumkumbatia
  3. Kumshauri namna ya kutatua tatizo
  4. Kumtenga
Choose Answer


  1. Namna bora ya kushirikiana na majirani zako unapokuwa nyumbani:
  1. Kuwakimbia wanapokuwa na shida
  2. Kutowapokea mizigo
  3. Kujumuika nao katika matukio ya shida na raha
  4. Kuwakwepa pale wanapoomba msaada
Choose Answer


  1. Unaposhuhudia vitendo vya ukatili uwapo shuleni unatoa taarifa:
  1. Mahakamani
  2. Polisi
  3. Kwa mwalimu wa ushauri nasaha
  4. Kwa mwenyekiti wa mtaa tu
Choose Answer


  1. Ni madhara ya vitendo vya kikatili katika familia:
  1. Vifo na kushirikiana
  2. Kuvuna mazao mengi
  3. Kuwafundisha na kuwapiga
  4. Kusambaratika kwa familia
Choose Answer


  1. Umuhimu wa kushiriki shughuli za kifamilia kwa wanafunzi:
  1. Kutopata ajira
  2. Kumjengea mwanafunzi ari ya kujitegemea
  3. Kutopenda kula chakula anachopika
  4. Kutowahi kufika nyumbani baada ya kutoka shuleni na matembezini
Choose Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256