MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

URAIA NA MAADILI A TANO

DEMOKRASIA

 

Chagua jibu sahihi

  1. Wajibu mojawapo wa rais wa Tanzania ni:
  1. Kujitangaza kwenye vyombo vya habari ili watu wote wakufahamu
  2. Kutumia mali za umma kadri unavyoweza
  3. Kulinda, kudumisha na kuhifadhi uhuru, mamlaka na umoja wa taifa
Choose Answer


  1. Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina sura ngapi?
  1. 9
  2. 10
  3. 11
Choose Answer


  1. Kazi ya vyama vya siasa nchini ni Pamoja na:
  1. Kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo
  2. Kuitisha mikutano ya hadhara na kuhamasisha maandamano ya uvunjifu wa amani nchini
  3. Kuomba kura kwa wananchi wakati wa uchaguzi tu
Choose Answer


  1. Kuwa na uhuru wa kutoa maoni ni moja ya nguzo za:
  1. Kutii sheria
  2. Uwajibikaji
  3. Demokrasia
Choose Answer


  1. Mgawanyo wa madaraka husaidia:
  1. Kuepusha kuingiliana katika kutekeleza majukumu
  2. Kupunguza kazi na kupinga unyonyaji
  3. Mtu mwenye madaraka kunyenyekewa
Choose Answer


  1. Wanachama wa vyama tofauti vya siasa wanapokosoana na kushindana kwa misingi ya haki, ukweli na amani, hali hii tunaweza kuiita:
  1. Utulivu na kisiasa
  2. Uvumilivu wa kisiasa
  3. Changamoto za kisiasa
Choose Answer


  1. Mtu anapata uraia wa Tanzania kwa kuzaliwa, kurithi na:
  1. Kuwatembelea wazazi wanaoishi Tanzania
  2. Kutumia kitambulisho cha mpiga kura
  3. Kujiandikisha
Choose Answer


  1. Sifa mojawapo ya mtu anayeomba uraia wa Tanzania:
  1. Aukubali uraia wanchi alikotoka kwa maandishi
  2. Sio lazima kutangaza kwenye vyombo vya habari
  3. Awe hajawahi kukutwa na kosa lolote la jinai toka aingie nchini
Choose Answer


 

Andika KWELI au SI KWELI katika sentensi hizi:

  1. Misingi ya demokrasia inazingatia haki za binadamu ………..
  2. View Answer


  3. Utawala wa demokrasia unatambulika kwa kutii sheria za nchi pekee………
  4. View Answer


  5. Katika mfumo wa kidemokrasia wananchi ni wapokeaji tu,hawawajibiki kwa lolote………..
  6. View Answer


  7. Wanawake hawana haki sawa na wanaume katika mfumo wa demokrasia…………..
  8. View Answer


  9. Kazi mojawapo ya vyama vya upinzani hapa nchini ni kukosoa utendaji wa serikali ya chama cha utawala……….
  10. View Answer


  11. Uvumilivu wa kisiasa kwa vyama vyote hudumisha amani…………..
  12. View Answer


  13. Mikutano ya vyama vya siasa ikivurugwa na wanachama wa vyama vingine inaonesha ukomavu wa kisiasa………….

 

View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256