SURA YA PILI

UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA MATUKIO YA KIHISTORIA

Msamiati

  • Diski- chombo cha kieletroniki kinachotumika kuhifadhi taarifa mbalimbali
  • Makumbusho- jingo au eneo maalum linalohifadhi vitu mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu
  • Nyaraka- kumbukumbu inayotunzwa kwa maandishi
  • Teknolojia-Tasnifu- maarifa ya sayansi yaliyowekwa katika matumizi ya vitu kama vile zana au mitambo
  • Tasnifu- Maandiko ya kitaaluma yanayotokana na kufanya tafiti
  • Tovuti- ahali katika mtandao penye ukurasa mmoja au zaidi zinazoweza kutoa taarifa kuhusu jambo maalum kwenye mtandao
  • Wavuti- mtandao wa komyuta wa mawasiliano wenye taarifa mbalimbali za kimataifa

Dhana ya kumbukumbu za matukio ya kihistoria

Kumbukumbu za matukio ya kihistoria ni taarifa za matukio yaliyotokea na kuhifadhiwa na jamii inayohusika kwa nyakati tofauti. Kumbukumbu hizo z;naweza kuwa za familia, mtaa, shule, kata, tarafa, wilaya, mkoa au taifa. Ili tukio liwe la kihistoria, lazima liwe na sifa za kipekee. Kwa mfano tukio lazima liwe:

  • Muhimu katika jamii nzima;
  • Linaonesha utofauti wa kipekee Iikilinganishwa na matukio mengine ya kawaida;
  • Lina faida za kisiasa, kijamii au kiuchumi kwa binadamu; na;
  • Lina athari za wazi na kubwa katika jamii (mfano vita, vifo vya watu wengi, au tetemeko kubwa lenye madhara).

Kupanga kumbukumbu za matukio ya kihistoria

Kumbukumbu za matukio ya kihistoria zinaweza kupangwa kv.a kutumia njia mbalimbali. Kwa mfano, zinaweza kupangwakwa kuonesha:

(a) Sehemu tukio lilipotokea. kwa mfano, tukio la Tanganyika kupata uhuru lilitokea nchini Tanganyika mkoani Dar-es-Salaam katika Uwanja wa Uhuru;

(b) Kipindi au wakati lilipotokea. Kama vile kwa kutaja:

  • Siku: tarehe, mwezi na mwaka: mfano, Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9, mwezi wa 12, mwaka 1961;
  • Muongo: kipindi cha miaka kumi;
  • Karne: kipindi cha miaka mia moja;
  • Milenia: kipindi cha miaka elfu moja;

(c) Mtiririko wa nyakati; matukio ya kihistoria yaiiyopangwa kwa mtiririko wa nyakati hupangwa kutoka tukio la mwanzo kwenda tukio la mwisho. Mfano wa matukio ya kihistoria yaliyopangwa kwa mtiririko wa nyakati umeoneshwa katika jedwali namba 1.

Umuhimu wa kupanga matukio ya kihistoria kwa kufuata mtiririko

  • Upangaji wa matukio ya kihistoria kwa kufuata mtiririko husaidia kuhusianisha matukio ya kihistoria.
  • Pia husaidia kutumia taarifa za awali katika kutatua changamoto za wakati uliopo.
  • Vile vile husaidia kutambua matukio muhimu ya kihistoria katika vipindi tofauti na namna yanavyochangia kuleta au kudidimiza maendeleo ya jamii inayohusika.

Soma habari ifuatayo kuhusu sehemu ya historia ya Baba wa Taifa la Tanzania kisha jibu maswali yanayofuata

Baba wa Taifa Ia Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alizaliwa mwaka 1922, katika kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma, mkoani Mara. Alikuwa ni mmoja kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila Ia Wazanaki. Alipokuwa mtoto,Mwalimu Nyerere alichunga mifugo ya baba yake. Akiwa na umri wa miaka 12, alijiunga katika Shule ya Msingi Mwisenge iliyopo Musoma rnjini umbali wa kilomita 30 kutoka nyumbani kwake Butiama. Mwalimu Nyerere alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda kusomea ualimu kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.

Aliporudi Tanzania alifundisha Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Maria (St. Mary's), iliyokuwa mkoani Tabora. Siku hizi shule hii inajulikana kama Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora. Mwaka 1949, alipata ufadhili wa masomo kwenda kusoma Shahada ya Uzamili ya Historia na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti nchini Uingereza. Mwalimu alikuwa Mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza.

Baada ya kurejea kutoka masomorti, Mwalimu Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Francis (St. Francis) ambayo siku hizi inaitwa Shute ya Sekondary Pugu. Mwaka 1953 Mwalimu Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA). Mwaka 1954, alikibadilisha chama cha TAA na kuwa chama cha siasa cha kupigania uhuru wa Tanganyika. Chama hiki kiliitwa Tanganyika African National Union (TANU).

Mwalimu Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 baada ya kuteuliwa na serikali ya kikoloni. Mnamb mwaka 1960 alichaguliwa kuwa Waziri Kiongozi wa serikali ya madaraka. Aidha, tarehe 9 Disemba mwaka 1961, Tanganyika ilipata uhuru wake na Mwalimu Nyerere alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika huru. Mwalimu Julius K. Nyerere alikuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika kuanzia mwaka 19q mwaka mwaka1964, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuunganisha Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume ni viongozi muhimu katika kufanikisha muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 mwezi Aprili mwaka 1964. Muungano huo ulisababisha kuundwa kwa Taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. llipofika mwaka 1977, Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) kiliungana na Chama cha African Shiraz Party, (ASP) na kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM). Mwalimu Nyerere aliendelea kuwa mwenyekiti wa CCM.

Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 alipong'atuka madarakani na kumwachia nafarais wa awamu ya pili, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi. Hata hivyo aliendelea kuiongoza CCM kama mwenyekiti hadi mwaka 1990. Baada ya lsustaafu kazi ya ukuu wa nchi, Mwalimu Nyerere alikaa muda mwingi Butiama alikozariwa akiishi kama mkulima wa kawaida.

Mwaligiu Nyerere alianza kuumwa mwezi Agosti mwaka 1999. Alipata matibabu katika hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza hadi alipofariki dunia tarehe 14 mwezi wa 10 mwaka1999. Kutokana na utumishi na uongozi wake uliotukuka, Mwalimu Nyerere anatambulika kama Baba wa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maswali

  1. Chora jedwali lenye safu tatu. Safu ya kwanza ioneshe namba; ya pili tukio a ya tatu mwaka. Tumia matini uliyosoma hapo juu kujaza historia,4a Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwenye jedw0- hilo ukianzia mwanzo hadi mwisho wa matukio ya historia yake.
  2. Hayati Mwalimu Nyerere alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, akiwa na umri wa miaka mingapi?
  3. Hayati Mwalimu Nyerere aliongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama rais kwa muds wa miaka mingapi?

Utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria

  • Utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria ni njia ya kuhifadhi taarifa za matukio yaliyowahi kutokea katika jamii au taifa kwa lengo la kurithisha matukio hayo kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
  • Njia za utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria
  • Kuna njia mbalimbali zinazotumika kutunza kumbukumbu muhimu za matukio ya kihistoria katika jamii, Njia ya kwanza ni utunzaji wa kumbukumbu za kihistoria kwa njia ya masimuiizi ya mdomo.
  • Njia ya pill ni kutunza vielelezo vya kumbukumbu za matukio ya kihistoria kupitia masalia ya kihistoria. Njia ya tatu ni kutunza kumbukumbu za matukio ya kihistoria katika majengo ya makumbusho, Njia ya nne ni kutunza taarifa za kumbukumbu za matukio ya kihistoria kwa njia ya maandishi.-
  • Maandishi hayo huweza kuhifadhiwa kama nyaraka, vitabu, magazeti au majarida, Njia ya tano ni lie ya kutunza taarifa kwa kutumia nakala lain' zinazotunzwa kwenye diski za kusikiliza na zile za kusikiliza na kuona.
  • Kwa ujumla, maendeieo ya sayansi na teknoiojia husababisha maendeieo ya njia za utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria, Kwa mfano, maendeieo hayo yamesababisha matumizi ya wavuti, tovuti na diski katika uhlfadhi wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria, Sehemu inayofuata inaonesha njia hizi za utunzaji wa kumbukumbu kwa undani zaidi,

Utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria unaofanywa na binadamu kwa njia ya masimulizi ya mdomo

  • Hapo zamani, kabla ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ya kuweka taarifa kwenye maandishi, taarifa za matukio muhimu katika jamii zilitunzwa na binadamu kwa njia ya masimulizi ya 'mdomo.
  • Aidha, watu kuona au kusimuliwa habari kama za vita, silaha, utamaduni, siasa na uongozi walitunza habari zile katika vichwa vyao.
  • Habari hizi zilipohitajika, watu hawa walitafutwa iii waweze kutoa taarifa hizo kwa njia ya masimulizi. Katika jamii za kitanzania, taarifa kama za uchumi, siasa, na majanga vita, njaa au mafuriko zilitunzwa na kurithishwa kwa vizazi vipya kwa njia ya masimulizi ya mdomo.
  • Kwa mfano, ili kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu, mwanafamilia anapozaliwa katika baadhi ya makabila alihusishwa na tukio la kipindi cha kuzaliwa kwake.
  • Wengine walipewa jinzi la tukio husika. Baadhi ya watu walipewa majina yaliyomaanisha furaha, baa la ukame, njaa, vita au mafuriko ili kuhifadhi kumbukumbu ya hali ya kipindi alichozaliwa.
  • Taarifa zilizohifadhiwa hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya masimulizi ya mdomo.
  • Masimulizi yanaweza kufanywa kwa njia ya hadithi, ngonjera, majigambo, vitendawili au nyimbo.
  • Pamoja na ujio wa njia nyingine za utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria, njia hii bado inatumika hadi sasa. Utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria kupitia binadamu una faida na changamoto zake.

Faida za utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria unaofanywa na binadamu kupitia masimulizi ya mdomo

Zifuatazo ni faida za kutumia masimulizi ya mdomo katika uhifadhi wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria.

Husaidia kupata habari za kale kwa haraka.Habari zilizohifadhiwa kupitia kumbukumbu za binadamu hupatikana kwa haraka ukilinganisha na vyanzo vingine vya taarifa. Chanzo hiki hutoa taarifa kwa njia ya masimulizi ya mdomo. Hakuna ujuzi wa ziada unaohitajika zaidi ya kusikiliza.

Hujenga na kutunza kumbukumbu za kale.Masimulizi ya mdomo, husaidia Hujenga na kutunza kumbukumbu miongoni mwa jamii. Hii hutokana na namna ambavyo masimulizi haya yanavyotumia mitindo mbalimbali kama vile misemo, hadithi, methali na nahau.

Huendeleza utamaduni wa jamii.Masimulizi ya matukio ya kihistoria, husaidia kutambua mila na desturi za kale. Watu wenye umri mkubwa huwaelezea wale wenye umri mdogo matukio ya kale na utamaduni wao katika jamii inayohusika. Kizazi kilichosimuliwa habari hizo, pia husimulia kizazi kingine. Hivyo, matukio na utamaduni uliotokea zamani hujulikana pia kwa kizazi ambacho hakikuwepo wakati wa tukio. Hivyo basi, masimulizi ya mdomo kama chanzo cha taarifa za kihistoria ni kichocheo kikubwa cha kuendeleza utamaduni wa jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Huburudisha jamii.Masimulizi ya matukio ya zamani ni chanzo cha burudani kwa jamii. Wazee wa zamani wanaposimulia matukio ya kihistoria, hutumia mitindo mbalimbali ambayo haichoshi kusikiliza, hivyo huburudisha na kuvutia kusikiliza. Masimulizi haya huambatana na nyimbo, misemo, methali na utani, hivyo hutoa burudani kwa wasikilizaji. Kwa mfano, "Asiyesikia la mkuu huvunjika guu", hii ni methali inayomaanisha mtu asiyesikiliza nasaha za wakubwa zake ataharibikiwa siku za usoni kwa kukosa maarifa aliyopewa hapo awali.

Husaidia kujenga maadili na kurekebisha tabia.Kupitia masimulizi ya mdomo tunapata mafundisho ya mila, desturi, dini, siasa na uchumi. Hivyo, masimulizi huelimisha kwa kutoa mwongozo kwa jamii kuhusu namna nzuri ya kuishi. Ustadi unaotumika kusimulia habari za kihistoria umekuwa ni chanzo cha kutoa maadili kwa jamii. Vipengele vya simulizi kama methali, nyimbo, mafumbo, nahau na misemo kutoka kizazi kimoja hadi kingine, vimekuwa vikihimiza mafundisho ya namna nzuri ya kuishi katika jamii.

Huhitaji kujua kusoma kupata taarifa za matukio ya kihistoria.Njia ya kuhifadhi taarifa kupitia masimulizi ya mdomo haihitaji ujuzi wa kusoma wala kuandika. Hiki ni chanzo kizuri kwa wale wasiojua kusoma na kuandika na hata kwa wale wasioona. Hivyo, chanzo hiki huweza kuwafikia watu wengi zaidi kuliko vyanzo vingine.

Huwakilisha uhalisia wa tukio.Mara nyingi simulizi za mdomo hutolewa na shuhuda wa tukio. Pia, masimulizi ya mdomo hueridana na hisia namna tukio lilivyotokea. Kwa hiyo wasikilizaji wanaosimuliwa visa vya kihistoria huelewa vizuri zaidi ukilinganishadia vyanzo vingine.

Changamoto za utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria unaofanywa na binadamu kupitia masimulizi ya mdomo

Zipo changamoto mbalimbali zinazotokana na utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria kupitia masimulizi ya mdomo. Zifuatazo ni baadhi ya changamoto hizo:

Upendeleo na ubinafsi.Wakati mwingine masimulizi ya mdomo huathiriwa na upendeleo au ubinafsi wa mtoa masimulizi. Uhalisia wa masimulizi ya mdomo unaweza usiaminike endapo msimuliaji atakuwa na rhaslahi na taarifa anazozisimulia. Mfano, msimuliaji anaweza kusema jamii yake ilishinda vita dhidi ya jamii nyingine tofauti na uhalisia;

Usahaulifu na uwezekeno wa upotoshaji.Iwapo muda wa tukio utakuwa mrefu sana, upo uwezekano wa mtunzaji wa kumbukumbu inayohusika kusahau maudhui kadhaa ya taarifa inayohusika. Pia, msimuliaji anaweza akaongeza taarifa zisizohitajika au kusimulia taarifa za uongo. Kwa sababu taarifa hizi hupatikana kwa njia ya masimulizi kutoka kizazi kimoja hadi kingine, upo uwezekano wa kupotosha taarifa kutoka kwa msimuliaji mmoja na mwingine. Hii ni kwa sababu mtu husimulia wengine alichosikia, alichoelewa na anachokumbuka kutoka kwa msimuliaji wa awali;

Kupotea kwa taarifa.Upo uwezekano wa taarifa muhimu za kihistoria kupotea kama wale wote wenye taarifa hizo watapoteza maisha kutokana na ufupi wa umri wa kuishi wa binadamu. Pia, endapo wale wenye taarifa muhimu za kihistoria wataugua magonjwa ya kupoteza kumbukumbu, matukio ya kihistoria waliyohifadhi yanaweza kusahaulika kabisa;

Utegemezi wa uwezo wa mtu binafsi.Uhifadhi wa matukio ya kumbukumbu za kihistoria hutegemea uwezo wa msikilizaji kusikia, kuelewa na kuchambua kwa usahihi yale allyosimuliwa. Hivyo, kiwango kimojawapo kati ya usikivu, uelewa na kumbukumbu kikiwa ni cha chini njia ya masimulizi ya mdomo huathirika kwa kiasi kikubwa. Hii inaweza kupoteza kabisa taarifa za kumbukumbu inayohusika;

Inaakisi utamaduni wa eneo linalohusika. Masimulizi ya mdomo yana uhusiano na.utamaduni wa msimuliaji, hivyo, masimulizi haya hueleweka vizuri kwa watu wenye utamaduni unaofanana mfano lugha. Kama msikilizaji anatoka kwenye utamaduni tofauti na wa mtoa masimulizi haya, ni vigumu kuelewa visa vinavyosimuliwa; na Ugumu wa kutaja nyakati halisi mfano tarehe au mwaka. Njia hii ina changamoto ya kuelezea muda halisi tukio lilipotokea, hasa msimuliaji anapotoa masimulizi yanayohusiana na mila na desturi za kale.

Namna ya kukabiliana na changamoto za utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria unaofanywa na binadamu kupitia masimulizi ya mdomo

Mbinu zifuatazo zinaweza kutumika kupunguza changamoto zake. Mbinu hizo ni kama vile:

  • Kuhoji mtu zaidi ya mmoja katika taarifa hiyo hiyo;
  • Kutumia vyanzo vingine vya taarifa hiyo hiyo iii kuhakiki uhalisia wa tukio; na
  • Kupata taarifa muhimu za utamaduni wa msimuliaji.

Utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria kupitia sehemu zenye masalia ya kale

  • Hizi ni sehemu zenye uthibitisho wa habari za kale kama mabaki ya mifupa ya wanyama au binadamu, zana zilizotumika na binadamu wa kale, michoro ya zamani, tamaduni za kale, makazi na shughuli mbalimbali za uchumi.
  • kumbukumbu za namna hii zimehifadhiwa sehemu zenye mabaki hayo. Hivyo, sehemu zenye masalia ya kihistoria hutunzwa iii kulinda kumbukumbuku hizo zisiharibiwe au kupotea.
  • Mfano wa baadhi ya sehemu zenye masalia ya kale katika nchi ya Tanzania ni hizi zifuatazo.

Olduvai Gorge (Arusha):

  • Bonde la Olduvai ni sehemu maarufu Tanzania na duniani kutokana na kuwa chimbuko la binadamu wa kale. Sehemu hii ni muhimu kwa kumbukumbuku za kihistoria kutokana na ugunduzi wa masalia ya fuvu la binadamu wa kale zaidi duniani.
  • Ugunduzi huu ulifanywa na wataalamu wa Akiolojia ambao ni Dkt Louis Leakey na mkewe Dkt Mary Leakey mwaka 1959 katika bonde la Olduvai, mkoani Arusha.
  • Akiolojia ni sayansi ya kuchimba chini ya ardhi ill kupata masalia ya viumbe na utamaduni wa zamani uliofukiwa ardhini.

Engaruka (Arusha):

  • Hii ni sehemu ya kumbukumbu za kihistoria na ipo eneo la kaskazini mwa Tanzania, mkoa wa Arusha, katika wilaya ya Ngorongoro.
  • Eneo hili ni maarufu kwa kuwa na mabaki masalia ya mifumo ya kilimo cha umwagiliaji iliyotumika na watu wa kale katika eneo hilo.

Amboni (Tanga):

  • Ni eneo la kihistoria linalopalikana kflomita 8 kaskazini mwa Jiji la Tanga katika barabara ya kuelekea Horo - Mombasa nchini Kenya
  • Sehemu hii ni maarufu kwa kumbukumbu ya urithi wa istoria ya Tanzania kwa kuwa na mapango makubwa yenye maumbo mbalimbali.
  • Mapango haya yenye asili ya chokaa yameundwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Mapango ya Amboni yamehifadhiwa kwa kuwa ni urithi na kumbukumbu ya taifa.

ISimila (Iringa):

  • Ni eneo la kumbukumbu za kihistoria linalopatikana katika mkoa wa lringa. Eneo hill lipo umbali wa kilomita 20 kutoka Iringa mjini. Hili ni eneo lenye masalia ya zana za mawe za mwanzo zilizotumika na wakazi wa eneo hill.
  • Sehemu hii ni muhimu kwani imetunza kumbukumbu za masalia ya zana za mawe za kale.

KiIwa Kisiwani (Lindi):

Hili ni eneo la kumbukumbu za kihistoria lililopo katika mkoa wa Lindi. Eneo hill ni muhimu kwa kumbukumbu za kihistoria kwa sababu lina mabaki ya majengo ya kale yaliyojengwa na Waarabu ikiwemo misikiti. Utamaduni wa Waarabu unajionesha kwenye ujenzi wa nyumba.

Kaole na Mji Mkongwe wa Bagamoyo (Pwani):

  • Mkoa wa Pwani una maeneo makubwa mawili yenye masalia ya kihistoria ambayo ni Kaole na Mji Mkongwe wa Bagamoyo. Kaole ni eneo lililopo katika mji wa Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
  • Hili ni eneo lenye kumbukumbu nyingi za kihistoria. Kumbukumbu hizo ni za mabaki ya masalia ya majengo ya misikiti na vito vya thamani vilivyoletwa na kutumiwa na wafanyabiashara kutoka Mashariki ya Mbali.
  • Kaole palikuwa ni kituo kikubwa cha Pwani ya bahari ya Hindi kwa Tanganyika kabla na wakati wa ukoloni. Wageni kutoka Asia na nchi za Kiarabu kama Oman na Guba ya Uajemi walifika maeneo ya Kaole, Bagamoyo kwa sababu ya biashara.
  • Inasadikika kuwa, masalia ya majengo na vito vya thamani katika eneo is Kaole vilitumika katika karne ya 13.
  • Mji ,Mkongwe wa Bagamoyo ni miongoni mwa vilivyokuwa vituo vikubwa vya biashara ya utumwa.
  • Watumwa waliochukuliwa maeneo mbalimbali nchini walifikishwa eneo hill kabla hawajasafirishwa na majahazi kupelekwa Zanzibar, Uarabuni na kwingineko.
  • Kutokana na Bagamoyo kuwa soko kuu la watumwa, eneo hill lina kumbukumbu za masalia ya majengo yaliyotumiwa kwa ajili ya biashara ya utumwa.
  • Eneo hili pia lina kumbukumbu za kanisa la kwanza la Kikatcliki Tang6nyika. Awali Wamisionari walikaa katika eneo hill na kujenga makanisa. Aidha, yapo makaburi ya wageni waliopatwa na umauti wakiwa Bagamoyo.
  • Zipo Iola kumbukumbu za utawala wa Kijerumani. Vitu vyote hivi vimehifadhiwa kwa ajili ya kumbukumbu za vizazi vijavyo.

Kondoa-Irangi (Dodoma):

  • Hii ni sehemu iliyopo katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma. Sehemu hii ina michoro mbalimbali ya mapangoni iliyochorwa katika miamba.
  • Michoro hii huonesha mazingira ya binadamu aliyoishi na uwindaji wa wanyama waliokuwepo wakati huo.
  • Kielelezo namba I kinaonesha baadhi ya sehemu zenye masalia ya kihistoria nchini Tanzania.

Kielelezo: Baadhi ya sehemu zenye masalia ya kihistoria Tanzania

Faida za kutumia sehemu zenye masalia ya kale kupata taarifa za kihistoria

Zifuatazo ni faida za kutumia sehemu zenye masalia ya kale kama chanzo cha taarifa za kihistoria:

  • Huhifadhi kumbukumbu za kale hivyo kuwafanya wanahistoria kutafsiri tamaduni hizo na kuandika historia ya sehemu husika na watu wake;
  • Huvutia shughuli za utalii;
  • Hutoa ajira;
  • Huingiza fedha za kigeni kupitia utalii;
  • Hutoa taarifa za kihistoria kwa watafiti wa mambo ya kale; na
  • Hulinda utamaduni wa sehemu inayohusika.

Changamoto za kutumia sehemu zenye masalia ya kale kama vyanzo vya taarifa za kihistoria

Changamoto za kutumia sehemu zenye masalia ya kale kama vyanzo vya taarifa za kihistoria ni kama ifuatavyo:

  • Baadhi ya zana na vitu vinavyopatikana katika sehemu hizi ni rahisi kuharibika;
  • Sehemu nyingi hazifikiki kirahisi hivyo ni gharama kutumia njia hii;
  • Uwepo wa wataalamu wachache wanaoweza kutafsiri masalia ham na
  • Ni rahisi sana kuharibiwa na majanga ya asili kama vile tetemeko la ardhi, mafuriko, au kimbunga.

Utunzaji wa kumbukumbu katika majengo ya makumbusho

  • Kumbukumbu za kihistoria pia hutunzwa katika majengo maalumu. Majengo haya huitwa makumbusho.
  • Makumbusho ni sehemu maalumu itunzayo kumbukumbu za nyanja zote' yaani uchumi, siasa, michezo, sayansi na teknolojia. Katika majengo ya makumbusho kuna hifadhi ya kumbukumbu kama vile silaha, zana za kufanyia kazi, vito vya thamani na mabaki ya mifupa ya wanyama na binadamu wa kale.
  • Tanzania imeanzisha majengo ya makumbusho ya Taifa maeneo kadhaa nchini kuwa sehemu ya kuhifadh kumbukumbu za zamani.
  • Makumbusho inaweza kuwa ya kitaifa, taasisi, mkoa, Maya, kijiji au familia. Makumbusho za Taifa ni kama vile Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni iliyopo Mtaa wa Shaaban Robert. Jijini Dar es Salaam; Kujiji cha Makumbusho kilichopo eneo la Kijitonyama Dar es Salaam; Makumbusho ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yaiiyopo Butiama mkoani Mara.
  • Pia, kuna Makumbusho ya Vita vya Majimaji iliyopo Ruvuma; Makumbusho ya Azimio la Arusha na Makumbusho ya Historia za Asiii zote za mkoani Arusha na Makumbusho ya Kalenga mkoani Iringa, lilikohifadhiwa fuvu la Chifu Mkwawa. Kielelezo kinaonesha baadhi ya sehemu zenye makumbusho ya Taifa nchini Tanzania.

Kielelezo:Sehemu zenye makumbusho ya Taifa Tanzania

Faida za makumbusho kama sehemu ya kutunza kumbukumbu za matukio ya kihistoria

Zipo faida nyingi za makumbusho kama sehemu ya kutunza kumbukumbu za matukio ya kihistoria. Baadhi ya faida hizo ni;

  • Huhifadhi aina mbalimbali za vitu na zana zilizotumika wakati wa kale, hivyo habari za kihistoria hupatikana kwa uhalisia wake. Mfano, Bari alilotumia Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, wakati Tanganyika ilipopata uhuru, linatunzwa kwenye makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam hadi leo;
  • Kumbukumbu hulindwa vizuri hivyo siyo rahisi kupotea, kuharibika au kuharibiwa;
  • Makumbusho ni kivutio cha utalii wa ndani na nje ya nchi; watu wengi hupenda kutembelea makumbusho ili kujifunza mambo ya kale. Hivyo, makumbusho ni chanzo cha mapato ya fedha za ndani na za kigeni kutokana na watalii kutembelea maeneo hayo;
  • Makumbusho hutoa ajira. Kila makumbusho ina wafanyakazi wanaohakikisha kwamba vitu vyote vilivyohifadhiwa vinatunzwa vizuri na maelezo muhimu kuhusu vitu hivyo, yanatolewa kwa usahihi. Wataalamu hao hupata ajira ya kufanya hivyo;
  • Makumbusho ni chanzo cha burudani na hivyo watu hutembelea na kuona vitu vilivyotunzwa; na
  • Makumbusho hutumika kutunza utamaduni wa sehemu inayohusika.

Changamoto za kutumia makumbusho kutunza kumbukumbu za kihistoria

Zipo changamoto za kutumia makumbusho kutunza kumbukumbu za kihistoria. Baadhi ya changamoto hizo ni;

  • Gharama kubwa inayohitajika kujenga na kutunza makumbusho;
  • Ni vigumu kuazima vifaa kutoka makumbusho hivyo ni lazima kutembelea eneo linalohusika; .
  • Vifaa vingine huharibika kwa urahisi kama taratibu za uhifadhi na utunzaji hazijazingatiwa;
  • Baadhi ya vifaa haviwezi kuhifadhiwa kwenye makumbusho mfano majengo na vifaa vingine vikubwa kama meli; na
  • Kutokana na makumbusho mengine kuwa mbali, sio watu wote wanaoweza kutembelea sehemu hizo na kupata taarifa mubashara.

Utunzaji wa kumbukumbu kwa maandishi

  • Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesababisha mabadiliko kwenye utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria. Ugunduzi wa karatasi pamoja na ujuzi wa kuandika umeyafanya matukio yaliyo mengi ya kihistoria kutunzwa kwa njia ya maandishi na kuhifadhiwa kama nyaraka, machapisho, magazeti na vitabu.
  • Ujio wa maandishi umerahisisha kazi ya upatikanaji wa habari za matukio ya kihistoria kwa njia ya maandishi. Kumbukumbu za matukio mbalimbali ya kihistoria zilizoandikwa kama barua, ramani, picha, magazeti, na kumbukumbu za mikutano huitwa `nyaraka..
  • Nyaraka hizi hutunzwa kwenye taasisi za kutunzia nyaraka za serikali na zisizo za serikali. Taasisi hizo huitwa Ofisi za Kumbukumbu na Nyaraka. Ofisi kubwa ya Taifa hapa Tanzania ipo Dar es Salaam.
  • Zipo ofisi nyingine za serikali za kanda kwenye mikoa ya Dodoma, Mbeya, Arusha na Mwanza. Machapisho mengine kama vitabu, magazeti na tasnifu hutunzwa maktaba.

Faida za utunzaji wa kumbukumbu kwa njia ya maandishi

Kuna faida kadhaa za utunzaji wa kumbukumbu kwa njia ya maandishi. Baadhi ya faida hizo ni:

  • Kumbukumbu za maandishi hudumu kwa muda mrefu;
  • Taarifa zilizoandikwa ni ngumu kupotoshwa zinaposomwa kwani husomwa katika uhalisia wake;
  • Uhifadhi wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria kupitia maandishi huchangia kupunguza mapungufu ya njia ya masimulizi ya mdomo;
  • Uhifadhi wa taarifa za kihistoria kwa kutumia maandishi huieta urahisi wa kupata taarifa hizi kwa watu wengi wanaojua kusoma na kuandika;
  • Ni rahisi kutafsiri kumbukumbu hizo kwenda katika lugha nyingine; na
  • Sio rahisi kubadilisha ujumbe kama ilivyo kwenye taarifa za masimulizi ya mdomo baina ya watu.

Changamoto za utunzaji wa kumbukumbu kwa njia ya maandishi

Zipo changamoto kadhaa za kutumia maandishi kama vyanzo vya kupata taarifa za matukio ya kihistoria. Baadhi ya changamoto hizo ni:

  • Wasio na ujuzi wa kusoma hukosa taarifa walizokuwa wanazihitaji;
  • Uandishi wa kitabu huchukua muda mrefu;
  • Waandishi hasa wa historia, wanaweza kupotosha ukweli wa jambo kutokana na msimamo wao kuhusu jambo analoliandikia. Kwa mfano, historia ya sababu za kutawaliwa kwa Afrika iliyoandikwa na wakoloni na lie ya Waafrika inaweza ikawa tofauti;
  • Taarifa zilizotunzwa katika maandishi ni ngumu kuzifanyia marekebisho iwapo zitakuwa zinapotosha; na
  • Nyaraka zinaweza kuharibiwa na kupoteza kumbukumbu kutokana na majanga ya moto, wizi, mafuriko, tetemeko au kimbunga.

Utunzaji wa matukio ya kihistoria kwa kutumia nakaia laini

  • Aidha, maendeieo hayo ya sayansi na teknolojia yamesababisha taarifa za kumbukumbu za matukio ya kihistoria kutunzwa kwa kutumia nakaia laini. Utunzaji huu hujuiikana kama njia ya kieletroniki ya kutunza matukio. Mifano ya nakaia laini ni wavuti, tovuti na diski.
  • Kwa kutumia njia hii, kumbukumbu kama picha, michoro, mabaki ya zana za kale, maandishi na masimulizi ya mdomo huweza kuwekwa kwenye nakaia laini. Taarifa za matukio ya kihistoria zilizohifadhiwa katika nakaia laini hutunzwa kwa njia ya kusikiliza na kuona.
  • Nakala hizi baadaye hutunzwa kwenye ofisi za kutunza kumbukumbu za taifa, mkoa, wiiaya, kata, Nip au binafsi.

Faida za utunzaji wa kumbukumbu kwa kutumia nakala laini

Kuna faida kadhaa za utunzaji wa kumbukumbu kwa kutumia nakala lain'. Baadhi ya faida hizo ni:

  • Kumbukumbu za kihistoria zilizotunzwa katika nakala laini kama vile sauti, simulizi na picha hupatikana katika uhalisia wake kwa jamii nzima;
  • Nakala laini huhifadhi taarifa nyingi na kubwa za kumbukumbu kwa urahisi kutegemea maendeleo ya teknolojia iliyotumika; na
  • Ni rahisi kusambaza taarifa za kumbukumbu za kihistoria katika eneo kubwa kwa wakati mmoja.
  • Kwa mfano, taarifa zilizohifadhiwa katika nakala laini zinapooneshwa katika luniga ni rahisi watu wengi kuzipata kwa wakati mmoja.

Changamoto a utunzaji wa kumbukumbu kwa kutumia nakala laini

Zipo changamoto kadhaa za kutumia nakala laini kama chanzo cha utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria. Baadhi ya changamoto hizo ni:

  • Nakala hizi zinatakiwa zitunzwe na wataalamu waliobobea kwenye utunzaji wa kumbukumbu kwa kutumia nakala laini. Hii ni pamoja na uchaguzi wa nakala hizo kwa makini;
  • Utunzaji wa nakala hizi unatakiwa uzingatie masharti yanayoambatana na nakala hizo. Kwa mfano, nakala hizi hazitakiwi zitunzwe sehemu zenye vumbi, unyevunyevu, joto kali au baridi kali;
  • Nakala laini zisipotunzwa vizuri huharibika mapema na kupoteza ubora wake; na
  • Ni gharama kutunza kumbukumbu kwa njia hii kwa sababu ya vifaa vingine huhitaji umeme mfano kompyuta

Umuhimu wa kutunza kumbukumbu za matukio ya kihistoria

Kutunza kumbukumbu za matukio ya kihistoria ni jambo muhimu kwa jamii na taifa kwa ujumia. Umuhimu wake ni kama ifuatavyo:

  • Husaidia kuziunganisha jamii na wakati, mahali na matukio yaliyotokea hapo awali;
  • Huhifadhi utamaduni wetu;
  • Huhifadhi kumbukumbu za siasa, uchumi na teknolojia ya jamb inayohusika kutoka kizazi kimoja hadi kingine;
  • Huendeleza uzalendo wa jamb inayohusika kwa kuhifadhi tamaduni zao;
  • Husaidia taifa kutathmini mabadiliko katika maisha ya wananchi wake kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kiteknolojia kutoka enzi za kale; na
  • Husaidia jamii kujifunza kutokana na matukio yaliyopita

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256