SURA YA PILI
KUJIVUNIA SHULE NA KUIPENDA NCHI YETU
Msamiati
- Dola- chombo chenye mamlaka ya kuendesha utawala au siasa ya nchi
- Dukuduku- machungu, wasiwasi au mfundo unaomsonga mtu moyoni
- Dumisha- kuendeleza jambo
- Katika- jumla ya kanuni taratibu au sheria ambazo huwezesha serikali itawale au chama au kampuni iendeshe shughuli zake
- Maslahi- manufaa au faida aipatayo mtu baada ya kufanya kazi, biashara au kumaliza tendo lolote
- Mhimili- nguzo, kitu kinachozui kingine kisianguke
- Minajili- kwa ajili ya
- Thamini- kukipa kitu hadhi
Katika sura ya kwanza, ulijifunza matendo yenye kuonesha upendo kwa watu wenye mahitaji maalumu, kuheshimu jinsi na kuvaa mavazi yenye staha. Katika sura hii, utajifunza mambo yanayoiletea shule sifa nzuri. Pia, utajifunza umuhimu wa kuenzi tunu za taifa letu ambazo ni tamaduni, mila na desturi zetu. Vilevile, utajifunza alama za utambulisho wa taifa letu pamoja na sikukuu za kitaifa.
Kuipenda na kujivunia shule yetu
- Hebu jiulize, je, unaipenda shule yako?
- Je, unajivunia shule yako?
- Unajivunia vitu gani katika shule yako?
- Sifa nzuri za shule zinajumuisha tabia njema za wanafunzi na walimu, majengo safi na mazingira yanayovutia.
- Hivyo, sifa nzuri ya shule inatokana na shule kuwa na mazingira yanayotunzwa kwa kupandwa miti ya vivuli, miti ya matunda pamoja na maua.
- Vilevile, sifa nzuri ya shule huchangiwa na wanafunzi kuwa nadhifu kwa kutunza sare zao na vifaa wanavyotumia katika mchakato wa kujifunza.
- Wanashirikiana kutunza rasilimali na samani za shule kama vile majengo, madawati, viti, vitabu na madaftari yao.
- Hali kadhalika, wanafunzi wanajituma na kuwajibika ipasavyo bila kusukumwa na mtu mwingine.
- Uwepo wa mambo yote haya husababisha ufaulu mzuri na kujenga sifa nzuri ya shule.
- Sifa mbaya za shule zinajumuisha tabia zilizopo shuleni ambazo hazikubaliki miongoni mwa jamii inayoizunguka. Sifa mbaya ya shule inachangiwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na uchakavu wa miundombinu na mazingira machafu.
- Pia, kuna vitendo vya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wanafunzi, kama vile kutovaa sare ya shule kikamilifu, kushindwa kufua sare zao na kuchana madaftari na vitabu. Vilevile, baadhi ya wanafunzi wana tabia ya utoro, uvivu na kuchelewa kufika shuleni.
- Hali hii huchangia sofa ya shule kuwa mbaya. Aidha, matendo ya baadhi ya walimu kuonesha tabia za uvunjifu wa taratibu na sheria za kazi.
- Mfano wa vitendo hivyo ni ugomvi baina ya walimu, walimu na wanafunzi, walimu kutotumia lugha yenye staha wawapo mazingira ya shule au katika jamii. Mambo yote haya yanaweza kusababisha shule kuwa na sifa mbaya.
Chunguza picha zifuatazo, kisha jibu maswali yanayofuata.
2 | |
Kielelezo namba 1: Utunzaji wa mazingira shuleni
Alama za taifa
Ulipokuwa darasa la nne ulijifunza matendo ya kuipenda nchi yetu kama vile kuonesha heshima kwa wimbo wa taifa na bendera ya taifa, pamoja na kuthamini fedha ya Tanzania. Katika sura hii, utajifunza kwa undani zaidi matumizi ya alama hizi za taifa. Aidha, utajifunza matumizi ya bendera ya taifa, wimbo wa taifa, mnyama wa taifa (twiga), nembo ya taifa, fedha ya taifa, bendera ya rais, mwenge wa uhuru, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ramani ya Tanzania.
Nembo ya Taifa
Matumizi ya alama za taifa
Je, ulishajiuliza umuhimu wa alama za taifa? Alama hizi hutumika wakati fulani, kwenye mazingira fulani na kwa lengo fulani. Hebu tuyabaini matumizi ya alama za taifa Ia Tanzania.
Bendera ya taifa
- Bendera ya taifa inaitambulisha nchi ya Tanzania miongoni mwa mataifa
mengine. Bendera yetu ya taifa hupepea katika nchi zote ambako Tanzania imefungua ofisi za ubalozi. - Pia, viongozi na baadhi ya Watanzania wanaposafiri nje ya nchi kwa lengo la kuiwakilisha Tanzania, hubeba bendera yetu ya taifa.
- Bendera ya taifa hutambulisha pia vyombo vya usafiri vinavyosajiliwa Tanzania.
- Vyombo hivyo ni meli, ndege, magari na pikipiki. Vilevile, bendera ya taifa hutambulisha ofisi au taasisi za serikali kama vile shule, ofisi ya serikali ya kijiji, kata, wilaya na mkoa, majengo ya mahakama na ofisi za wizara mbalimbali.
Bendera ya Taifa
- Pia, bendera ya taifa hutumika kuonesha majonzi pale inapotokea msiba au janga Ia kitaifa. Mifano ya majonzi hayo ni kama vile kifo cha baba wa taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ajali ya MV Bukoba iliyotokea tarehe 21 mwezi wa 5 mwaka 1996 na Kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 mwezi wa 9 mwaka 2018 katika Ziwa Viktoria ambapo meli na kivuko hicho vilizama na kusababisha vifo vya watu wengi. Katika maombolezo ya matukio kama hayo bendera ya taifa hupepea nusu mlingoti.
Wimbo wa taifa
- Kwa kiasi kikubwa matumizi ya wimbo wa taifa yanafanana na yale ya bendera ya taifa. Wimbo wa taifa huimbwa wakati viongozi wa nchi wanapotembelea nchi nyingine.
- Pia, huimbwa wakati vikundi vya utamaduni na michezo wanapocheza michezo ya kimataifa ndani na nje ya nchi.
- Pia, wimbo wa taifa huimbwa kabla ya tangazo Ia msiba wa kiongozi mkuu wa nchi, kama vile rais, makamu wa rais na waziri mkuu. Hali kadhalika, kabla ya rais kufanya uzinduzi wa jambo muhimu linalogusa maslahi mapana ya taifa, huimbwa wimbo wa taifa.
- Mfano wa matukio hayo ni uzinduzi wa meli mpya au ndege mpya. Aidha, wimbo wa taifa huimbwa katika taasisi mbalimbali kama vile, shuleni na katika vikosi vya majeshi yetu ili kukuza uzalendo.
- Vilevile, wimbo wa taifa huimbwa katika matukio muhimu ya kitaifa, kama vile sikukuu za kitaifa na hafla zinazohusisha viongozi wakuu wa serikali.
Mnyama wa taifa
- Je, unamfahamu mnyama wa taifa? Anaitwa nani ? Na ulimwona wapi? Mnyama wa taifa Ia Tanzania anaitwa twiga.
- Mnyama huyu hutumika kama alama kificho katika fedha ya noti ya Tanzania. Pia, hutumika pamoja na alama ya bendera ya taifa kutambulisha ndege inayomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile, alama ya twiga hutumika kama kielelezo cha utajiri wa maliasili iliyopo Tanzania.
Twiga mnyama wa Taifa
Nembo ya taifa to Tanzania
- Je, umewahi kuiona nembo ya taifa? Ina vitu gani? Uliiona wapi? Nembo ya taifa ina jumla ya alama 13 ambazo ni: mwanamke na mwanaume, mwenge wa uhuru, pembe za ndovu, mlima Kilimanjaro, mawimbi ya bahari, bendera ya taifa, mkuki, mazao ya pamba na karafuu, jembe na shoka, ukanda wenye maneno uhuru na umoja, rangi ya njano na nyekundu.
- Nembo ya taifa inatumika kuonesha umiliki wa mali na nyaraka za Serikali ya Tanzania. Alama hiyo huonekana katika vitabu na machapisho mbalimbali ya serikali, Kati za kusafiria nje ya nchi na mavazi ya viongozi wa juu wa kijeshi.
- Pia, hutumika katika mawasiliano rasmi ya kiserikali kama vile barua za kiserikali na matamko ya kiserikali. Nembo ya taifa la Tanzania hutumika pia kama muhuri wa rais.
Fedha ya Tanzania
Alama nyingine ya kitaifa ni fedha ya Tanzania. Fedha ya Tanzania inaitwa shilingi. Fedha hutumika kwa namna mbili. Hutumika kuitambulisha Tanzania kama nchi huru. Pia, hutumika kuthamanisha vitu na mali. Fedha ya Tanzania iko katika sura mbili: noti na sarafu.
Noti za Tanzania
Bendera ya Rais
- Alama hii hutumika kutambulisha mamlaka rasmi ya rais katika shughuli rasmi ambazo rais anahudhuria ndani au nje ya nchi.
- Vilevile, hutumika katika chombo cha usafiri anachokitumia rais.
Bendera ya Rais
Mwenge wa uhuru
- Mwenge wa uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro siku ambayo Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9 mwezi wa 12 mwaka 1961.
- Mwenge huu wa uhuru hutumika kukumbuka na kuitambulisha Tanzania kama nchi huru.
- Hutumika pia kuonesha mshikamano wa kitaifa. Mwenge wa uhuru hutumika katika matukio ya kuzindua baadhi ya miradi ya maendeleo nchini pindi unapokimbizwa kwenye maeneo husika.
- Vilevile, mwenge wa uhuru hutumika kuhamasisha na kudumisha uzalendo kwa Watanzania.
- Wakati wa kukimbiza mwenge wa uhuru, kuna wimbo maalumu unaoimbwa iii kuwakumbusha Watanzania jukumu lao la kuulinda uhuru wao.
- Mbio za mwenge hufanyika mara moja kila mwaka kuzunguka nchi nzima.
Rais Samia Akiwasha Mwenge wa Taifa
Hebu imba, kisha tafakari maudhui ya wimbo huu wa "Kuwasha mwenge."
K inuz ih rrnus e
"Sisi tumekwisha kuwasha Mwenge,
Tumekwisha kuwasha Mwenge, Na kuuweka juu ya mlima, Mlima Kilimanjaro.
Kuwasha Mwenge, Kuwasha Mwenge, Na kuuweka Kilimanjaro.
Umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini,
Pale ambapo hakuna matumaini, Upendo mahali ambapo pang chuki,
Na heshima ambapo pamejaa dharau."
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Katiba ni sheria, kanuni na taratibu zinazotumika kuendesha shughuli za nchi, chama au kikundi cha watu wenye malengo yanayofanana.
- Tanzania tunatumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonesha muundo, madaraka na majukumu ya serikali.
- Katiba huonesha pia haki na wajibu wa raia wa Tanzania.
- Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni alama mojawapo miongoni mwa alama zinazolitambulisha taifa letu.
- Katiba hutumika kuhifadhi na kulinda sheria zote zinazotungwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Inaeleza bayana mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili mikuu mitatu ya dola ambayo ni serikali, bunge na mahakama.
- Katiba hutumika wakati viongozi wanapoapishwa baada ya kuteuliwa na kuchaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi.
- Wanaapishwa na katiba ili kuitetea na kuilinda katiba hiyo. Vilevile, katiba hueleza bayana madaraka na mipaka ya viongozi iii kuepusha migogoro na matumizi mabaya ya madaraka.
- Aidha, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huhifadhi sheria zinazotetea maslahi na haki za binadamu.
Katiba ya Tanzania
Ramani ya Tanzania
- Alama hii hutumika kutambulisha na kuonesha mipaka ya nchi yetu na nchi nyingine zilizo jirani yetu. Upande wa mashariki,Tanzania inapakana na Bahari ya Hindi, upande wa magharibi inapakana na nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Rwanda. Upande wa kaskazini Tanzania imepakana na nchi za Kenya na Uganda. Upande wa kusini inapakana na nchi za Malawi, Msumbiji na Zambia.
Sikukuu za kitaifa
Je, unazifahamu sikukuu gani za kitaifa? Kama mwanafunzi umewahi
kushiriki sikukuu gani za kitaifa? Sikukuu za kitaifa ni zile siku ambazo
zinaadhimishwa kitaifa kila mwaka, iii kukumbuka matukio muhimu ya
kitaifa. Ifuatayo ni orodha ya sikukuu zinazoadhimishwa kitaifa nchini Tanzania:
Jedwali namba 2: Sikukuu za Kitaifa
Pia, kuna sikukuu nyingine za dini ya Wakristo kama vile Krismas, Ijumaa Kuu, Pasaka na Jumatatu ya Pasaka. Vilevile, kuna sikukuu za Waislamu, mfano Eid - El Fitri, Eid - El Haji na Maulid.
Umuhimu wa sikukuu za kitaifa
- Sikukuu za kitaifa hutumika kuenzi matukio ya kitaifa na kudumisha ujumbe ulio katika matukio hayo.
- Sikukuu za kitaifa, hutoa fursa kwa viongozi kueleza mafanikio na changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi.
- Wakati wa maadhimisho ya sikukuu hizo, viongozi hutumia nafasi hizo kuchanganua na kufafanua mambo ya kitaifa na kutafakari mwelekeo wa nchi. Pia, hutoa elimu mbalimbali kwa wananchi kuhusu mambo yanayohusu maendeleo ya nchi yao.
- Kwa mfano, wakati wa sherehe za wakulima ambazo huadhimishwa tarehe 8 mwezi wa 8 kila mwaka, viongozi wetu wa kitaifa huwahamasisha wakulima kutembelea maonesho mbalimbali yatakayo wasaidia wakulima kupata mbinu na njia za kisasa za kuboresha kilimo na ufugaji.
- Vilevile, sikukuu hizi huwasaidia wananchi kupata fursa ya kuwasiliana na viongozi wao. Aidha, kwa kupitia sikukuu hizi wananchi hupata fursa ya kusherehekea mafanikio na kutafakari changamoto mbalimbali.
- Mfano, katika sikukuu ya Mei Mosi wafanyakazi hutoa dukuduku zao kuhusu changamoto zinazowakabili.