MADA YA PILI

MATUKIO YA KIHISTORIA

Msamiati

  • Hamasa- msukumo wa ndani wa kufanya jambo
  • Hitilafu- Kasoro katika utendaji
  • Kunena- kusema jambo
  • Kurekodi-kuchukua au kuandika taarifa kwa kalamu kwenye karatasi aukwa njia ya kielekroniki ili kuisoma au kujitambulisha baadaye
  • Maktaba-nyumba au chumba ambacho hutumika kuhifadhi na kusomea machapisho au vitabu
  • Simulizi-hadithi za matukio halisi au za kubuni zinazohusu hali halisi ya Maisha
  • Ukoo- Muungano wa familia nyingi zenye asili moja

Katika sura hii, utajifunza matukio yaliyotokea katika familia yako na shuleni. Pia, utajifunza njia za kupata taarifa za matukio. Vilevile, utajifunza vifaa vinavyotumika kuchukua taarifa za matukio. Mwisho, utajifunza njia za kutunza taarifa za matukio ya kihistoria.

Matukio ya kihistoria katika jamii

  • Matukio ya kihistoria hutokea kila siku katika maisha. Matukio haya ni kama vile siku ya uhuru na siku ya kifo cha Baba wa Taifa.
  • Pia, siku yako ya kuzaliwa na hata siku ya kuanza shule ni miongoni mwa matukio ya kihistoria.

Soma habarHfuatayo, kisha jibu maswali.

Mwalimu wetu wa somo la Maarifa ya Jamii alimwalika mgeni. Mgeni huyo alikuwa anaitwa mzee Kahonda. Mzee Kahonda alikuja kuelezea juu ya matukio yaliyowahi kutokea katika familia yake. Tulijiandaa kumuuliza maswali iii tuweze kuelewa vizuri alichokusudia kutusimulia. Mgeni alikaribishwa na mwalimu darasani iii azungumze nasi. Mazungumzo yalikuwa hivi:

Mzee Kahonda:Hamjambo wanafunzi?

Wanafunzi: Hatujambo, shikamoo mzee Kahonda.

Mzee Kahonda:Marahaba! Mnaendeleaje na masomo?

Wanafunzi: Tunaendelea vizuri.

Mzee Kahonda: Nimealikwa na mwalimu wenu kuja kuelezea matukio yaliyowahi kutokea katika familia yangu. Ninaamini mtajifunza mengi, hivyo nisikilizeni kwa makini. Muwe huru kuuliza maswali. Miaka kumi iliyopita katika familia yangu, palitokea moto mkubwa. Moto huo uliunguza nyumba na vitu vyote vilivyokuwa ndani. Vitu kama vyakula, nguo, madaftari na sare za shule za watoto na wajukuu zangu viliungua. Wanafamilia walilia na kuumia sana.

(Mzee Kahonda alipomaliza kusimulia alituruhusu tumuulize
maswali. Mwanafunzi wa kwanza kuuliza swali alikuwa Halima.)


Halima:

Mzee Kahonda: Katembu:

Mzee Kahonda:

Machupa:

Mzee Kahonda:

Katunda:

Mzee Kahonda: Runia:

Mzee Kahonda:

Kagoma:

Mzee Kahonda:

(Akasimama na kuuliza). Chanzo cha moto kilikuwa ni nini?

Ilikuwa hitilafu ya umeme.

Baada ya tukio hilo, hall ilikuwaje?

Hall haikuwa nzuri kwani vitu vyote viliteketea kwa moto. Lakini ndugu na majirani walitusaidia chakula na kutuchangia fedha. Fedha zilitumika kununulia vifaa vya kujengea nyumba yetu upya. Kwa sasa tunaendelea na maisha kama hapo awali.

Pole sana mzee wetu.

Asante sana. Mbali na tukio la moto, yapo matukio mengine yaliyotokea katika familia yangu.

Ni yapi hayo?

Mwaka juzi tulikuwa na sherehe za mavuno. Mlisherehekea mavuno ya nini?

Familia za ukoo wangu huwa na utaratibu wa kusherehekea pale tunapomaliza kuvuna mazao. Mwaka juzi tulivuna magunia mia moja ya mpunga. wanafamilia walifanya sherehe iliyoambatana na kuimba nyimbo na kucheza ngoma za asili.

Ahaa! Sherehe hizi huwa na faida gani kwa wanafamilia?

Sherehe hizi huleta umoja, ushirikiano
na mshikamano kwa wanafamilia. Pia,


huongeza hamasa ya kushiriki kufanya kazi kwa msimu ujao wa kilimo. Vilevile, hujenga na kudumisha utamaduni wa familia yetu.

Wanafunzi, yapo matukio mengi yaliyotokea katika familia yangu. Nikipata muda nitakuja tena kuwasimulia. Asanteni kwa kunisikiliza.

Wanafunzi: (Wote kwa pamoja walipiga makofi kwakumshangilia mzee Kahonda).

Mwalimu: Mgeni wetu tunakushukuru kwa kuja.

Wanafunzi, bila shaka mmeelewa matukio yaliyowahi kutokea katika familia kupitia masimulizi ya mgeni wetu. Je, mmefurahia simulizi za mzee Kahonda?

Wanafunzi: Ndiyo, tumefurahi sana mwalimu.

Halima: Mwalimu, tunaomba umwalike tena mgeni

wetu siku nyingine.

Mwalimu: Sawa Halima, nitafanya hivyo.

Kuna matukio mengine mengi yanayotokea katika familia nyingi za kitanzania. Baadhi ya matukio hayo ni kama vile sherehe za mavuno na harusi. Matukio mengine ni mashindano ya ngoma za kiutamaduni na misiba ya wanandugu. Familia nyingine hukumbwa na matukio ya nyumba kuvamiwa na majambazi au wizi wa mifugo. Vilevile, baadhi ya familia husherehekea siku zao za kuzaliwa. Familia nyingine huwafanyia sherehe za harusi vijana wao wanapooa au kuolewa. Kila familia huwa na matukio tofauti na familia nyingine. Tofauti hii hutegemea aina ya tukio na wakati tukio linapotokea. Matukio mengine katika familia hufurahisha na mengine huhuzunisha. Mfano wa tukio Ia kufurahisha ni harusi na mfano wa tukio Ia kuhuzunisha ni msiba.

Jibu Maswali yafuatayo;

  • Unajifunza nini kutoka kwa masimlizi ya mzee Kahonda
  • Taja matukio mawili yaliyosimuliwa na mzee kahonda
  • Je, unakumbuka matukio yaliowahi

HFLLD

Matukio ya kihistoria katika Shule ya Msingi Kibeho

Katika Kulp cha Kitufe kuna shule ya msingi iitwayo Kibeho. Shule ya Msingi Kibeho ilianzishwa mwaka 2008. Shule hii ilijengwa kwa nguvu za wananchi. Wananchi walijenga shule ili kupunguza umbali mrefu waliokuwa wakitembea watoto waokwenda shuleni. Shule ya Msingi Kibeho ilifahamika sana kwa kuwa na wanafunzi wenye nidhamu. Pia, shule hii ilijaliwa kuwa na wanafunzi wenye vipaji vya michezo mbalimbali.

Katika miaka michache iliyopita Shule ya Msingi Kibeho ilikuwa maarufu sana. Umaarufu huu ulitokana na matukio mbalimbali yaliyowahi kutokea katika shule hiyo.

Jedwali lifuatalo Iinaonesha matukio yaliyowahi kutokea shuleni Kibeho.

Hadi sasa yapo matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea katika shule ya Kibeho. Mwaka huu shule imeletewa mwalimu mkuu mwingine aitwaye Kayelo Mapupa. Mwalimu huyu amedhamiria kuendeleza taaluma, michezo na nidhamu ya shule hiyo. Kweli Shule ya Msingi Kibeho imekuwa na mafanikio makubwa.

Kazi ya kufanya

.

Tembelea ofisi ya mwalimu mkuu na ulizia matukio yaliyowahi kutokea hapo shuleni kwenu. Andika matukio hayo kama ilivyooneshwa kwenye jedwali. Wasimulie wenzako darasani. Usisahau kumshirikisha mwalimu wako.


Njia zinazotumika kupata taarifa a matukio

Soma habari ifuatayo, kisha jibe maswali.

Umejifunza matukio mbalimbali yaliyowahi kutokea katika familia na shuleni. Zipo njia mbalimbali za kupata taarifa za matukio hayo. Tunaweza kutumia simulizi, redio na runinga. Wakati mwingine njia kama magazeti, vitabu na simu hutumika kupata taarifa za matukio.

Baadhi ya taarifa za matukio hupatikana kwa njia ya masimulizi au mitandao. Jamii nyingine huwa na sehemu maalumu za kumbukumbu kama makumbusho. Watu wengine hutembelea maktaba na kusoma vitabu na majarida mbalimbali iii kupata taarifa za matukio. Ukifanya uchunguzi kwa kuuliza watu juu ya jambo fulani unaweza pia kupata taarifa za matukio.

Ni vema kutunza taarifa za matukio yanayotokea katika familia zetu na shuleni. Unaweza kuchukua taarifa za matukio kwa kutumia vifaa kama kalamu na daftari. Vifaa hivi hutumika kuandika taarifa za matukio. Wakati mwingine watu kutumia kamera kupiga picha za matukio mbalimbali.

Ni muhimu kutambua kuwa tukio likitokea, hung budi kuchukua taarifa take na kuzitunza. Hii husaidia kuwa na kumbukumbu za matukio hayo.

Kutunza kumbukumbu za matukio ya masomo

Unatakiwa kutunza kumbukumbu za matukio yanayotokea shuleni. Matukio mengi yanatokea katika jamii na hata shuleni. Matukio haya yanaweza kuwa ya kihistoria au yasiwe ya kihistoria.

Angalia mchoro unaoonesha vifaa vya kutunza kumbukumbu za matukio ya masomo shuleni, kishsa jibu maswali yanayofuata.

Umuhimu wa kutunza kumbukumbu

  • Inatusaidia kukumbuka yaliyotokea zamani
  • Inahifadhi kumbukumbu kwa vizazi vijavyo
  • Inasaidia kurejea yaliyopita
  • Kumbukumbu ni hazina
  • Inasaidia kurekebisha makosa ya zamani

Soma shairi, kisha jibu maswali.

  1. Mbele yenu tokezea, jambo nataka kunena, Ninapenda elezea, kumbukumbu naziona, Zamani yalotokea, hadi sasa twayaona, Kumbukumbu zitunzeni, turejee yalopita.
  2. Kumbukumbu kuzitunza, ni muhimu nawambia, Historia twafifunza, kumbukumbu zatwambia, Habari tukizitunza, hazina kuhifadhia,

Kumbukumbu zitunzeni, turejee yalopita.

  1. Kutotunza kumbukumbu, mambo mengi hupotea, Asotunza kumbukumbu, hukosa la kunenea, Kutotunza kumbukumbu, hasara hututokea, Kumbukumbu zitunzeni, turejee yalopita.
  2. Kuzitunza kumbukumbu, Labia njema jengea, Ukiwa na kumbukumbu, heshima kujiwekea, Jiwekee kumbukumbu, kwa yale yalotokea, Kumbukumbu zitunzeni, turejee yalopita.

Jibu Maswali yafuatayo kutokana na shairi

  1. Ni ujumbe gani umeupata kutoka kwenye shairi ulilosoma?
  2. Ni faida zipi za kutunza kumbukumbu za masomo shuleni zilizotajwa kwenye shairi?
  3. Taja vifaa vine vya kutunza kumbukumbu za matukio nyumbani kwenu?
  4. Nini kitatokea usipotunza kumbukumbu za masomo yako?

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256