FORM TWO KISWAHILI NECTA 2014

2014 - KISWAHILI

UFAHAMU

Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Sasa hivi kuna Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Lakini kuendelea kuwepo kwa Jumuiya yoyote iliyo imara na isiyotetereka si suala dogo hata kidogo. Ni suala linalohitaji uendeshaji na usimamizi ulio makini katika namna zote. Kwa sasa Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Hata hivyo, kumekuwepo na vuguvugu la kutaka kuanzisha Shirikisho la nchi zinazounda Jumuiya hiyo. Watu mbalimbali wamekuwa na mawazo tofauti juu ya wazo hilo.

Baadhi ya watu wana maoni kwamba wazo la kutaka kuanzishwa kwa shirikisho la nchi hizi ni wazo zuri na linalofaa likichukuliwa kwa hadhari inayostahili. Hii ni kwa sababu kila moja kati ya nchi za Jumuiya hiyo ina matatizo yake ya ndani ya nchi. Si jambo la busara hata kidogo kuupuza ukweli kwamba matatizo ya ndani ya nchi hizi yanaweza kuziathiri vibaya jitihada za kuanzisha shirikisho hilo. Kwa hiyo litakuwa jambo la busara sana kama kila nchi itaanza kwanza kushughulikia matatizo yake ya ndani kabla haijafikiria kujitumbukiza katika shirikisho hilo.

Wengine wana mawazo tofauti na mawazo hayo. Wao wanadai kwamba hakuna haja kusubiri nchi zikamaliza matatizo yake ya ndani ya nchi kwa sababu pengine haitawezekana kufikia wakati ambao nchi zote hizo zitakuwa zimeyashughulikia matatizo yote ya ndani ya nchi. Kila uchao kuna matatizo mengine yanayozuka. La msingi ni kuhakikisha kwamba jitihada za kuanzisha shirikisho zinaendelea bila kurudi nyuma huku ikikumbukwa kuwa kilicho kizuri hakikosi ila.

Vyovyote itakavyokuwa, ni muhimu kuzingatia kwamba kila upande una hoja zake, ambazo si vema kuzipuuza. Kuna haja ya kuzingatia hoja zote ili kuona ni lipi litiwe maanani na lipi lipuuzwe katika kila upande. Tusichague upande mmoja tu na kutupilia mbali hoja zote za upande mwingine. Kwa kuangalia pande zote mbili, na kwa kuzingatia kuwa umoja ni nguvu tutafaidika zaidi kimawazo.

MASWALI

(a)      Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano.........

(b)     Kuna pande mbili za mawazo zinazopingana kuhusu uanzishwaji wa shirikisho.

Pande hizo ni zipi?

(c)      Onesha matatizo yaliyomo kwa kila upande.

(d)     Eleza maana ya maneno na misemo ifuatayo kama ilivyotumika katika kifungu cha habari ulichosoma:

(i) Shirikisho.........

(ii) Hadhari .........

(iii) Jitihada ........

(iv)Kizuri hakikosi ila .................

(v) Umoja ni nguvu . ............

(e)     Kwa kifupi toa maoni yako kuhusu pande zote mbili.

(f)      Fupisha aya ya pili na ya tatu kwa maneno yasiyozidi 40.

View Ans


SEHEMU B

UTUMIZI WA LUGHA NA USAHIHI WA MAANDISHI

2. (a) Kwa kauli zifuatazo, andikaKWELI kwa kauli iliyo sahihi au SIO KWELI kwa kauli isiyo sahihi.

(i) Kigezo cha ubora wa kazi ya fasihi Sio uwiano wa fani na maudhui.

(ii) Barua rasmi lazima iwe na anwani moja.

(iii) Kipi, gani, wangapi, nani, yupi, mingapi, nini, na mangapi ni vivumishi na viwakilishi viulizi,

(iv)Katika lugha, kunyumbua neno ni kuongeza viambishi katika kiini ili kupata maneno mengine ..

(v)Ngonjera hazina muundo wa mashairi ya kimapokeo.

(b)     Andika tungo zifuatazo kwa usahihi:

(i) Toya ni mwizi. Ameniiba fedha zangu.

(ii)Ninachukua nafasi hii kuwapongeza kwa kumaliza kidato cha pili.

(iii)Sikuwa najua kuwa Mwalimu wa Kiswahili anaitwa Kingunge.

(iv)Nikifika Uingereza nitakupelekea barua.

 (v) Katika ajali hiyo watu kumi waliuawa.

(c) Andika rejesta ya kila sentensi zifuatazo kulingana na muktadha wake:

(i) Ndiyo Afande! Nitawapeleka sasa hivi.

(ii) Tumia moja kutwa mara tatu.

(iii) Kituo kinachofuata ni Kibaha. Nani anashuka?

(iv) Okwi alimpiga chenga Jaja, hatimaye akaipatia Simba goli.

(v)  Ndege nyingi zilikuwa zikitua na kupaa

View Ans


SEHEMU C

SARUFI

3.Andika aina ya neno lililokolezwa wino katika sentensi zifuatazo:

Sentensi ya kwanza ni mfano.

(i)Mtoto mchanga ameumia ... ... ... Neno mchanga ni Kivumishi

(ii)Yamenunuliwa Maembe matamu 

(iii) Nitakwendashuleni 

(iv) Nani amefika? 

(v) Ameondoka leo .. 

(vi)Kumbe! Sikujua asali ni dawa .

(b) Bainisha mzizi wa asili kwa kila neno katika maneno yafuatayo. Neno la kwanza ni mfano.

(i) Ningelipenda - Mzizi wa asili ni -pend— (ii) Anawafundisha .....

(iii)Muuguzi ...............

(iv)Wanywaji . ..........

(v)Muongozaji . ..............

(vi)Tutafaulu .............

(vii)Mabadiliko . ..........

(viii)Mtamrekebisha . ..............

(ix)Ulikula ..........

(x)Walikimbia . .................

(xi)Kilipambika ..........................

(c) Andika kazi moja ya viambishi awali katika kila neno lililokolezwa wino:

(i) Juma na John vvamebadilishana magari.

(ii)Mbona mlichelewa kufika shuleni jana?

(iii) Mwalimu aliyefika ni huyu hapa.

(iv) Leo sijala chochote.

(v) Mimi nitashinda mtihani huu.

SEHEMU D

FASIHI SIMULIZI

View Ans


4.Eleza kwa kifupi maana ya dhana zifuatazo:

(i) Maigizo 

(ii) Semi ......... 

(iii) Tarihi .

(iv) Majigambo ..........

(v) Mizani . . . . . . . ..

(b) Jaza nafasi iliyoachwa wazi kukamilisha methali zifuatazo:

(i)Hamadi kibindoni ... ... ...

(ii).. ......yasiyokuwa ncha.

(iii)......... si mwisho wa uhunzi.

(iv)Mwenye shibe .............

(v)......... embe tunda la msimu.

(c) Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata:

Kweli kito mahabubu, Muweza mjaze kweli,

Kweli siriya ajabu, huwapa watufadhili,

Kweli chimbo la dhahabu, linahimili kweli,

Kweliyajambo hekima, na mifanoya akili.

Kweli nguvuya imani, moyoni muwe na kweli,

Kweli kitu cha thamani, fahariyetu ni kweli,

Kweli itupe makini, tutoe majibu kweli,

Kweli kwa mtu ni tija, woga huvunjwa na kweli.

Kweli huniadabisha, utu huletwa na kweli,

Kweli hunielimisha,jinsiya kuwa kamili,

Kweli hunipa maisha,ya mwangaza wa kandili,

 Kweli haina kiwango, manufaa yake kweli.

Kweli katika baraza, maongeziyawe kweli, 

Kweli au hupendeza,zamaza kujibu swali, 

Kweli itakuongoza, uweze kufanya kweli,

Kweli huwa mfaulu, katika pambono kali.

Kweli leo iwe pambo, upambile kweli kweli,

Kweli ikujaze mambo,yoteyaliyoya kweli,

Kweli ikupe kiimbo, chenye majibu ya kweli,

Kweli tatua mafumbo, uwemahiri wa kweli.

Kweli hapa kaditama, ni mimi mtunzi kweli, Kweli ikujaze mema, ufaulu kweli kweli, Kweli itakupa chema, Kidato cha tatu kweli, Kweli mhimili wako, pokea kwa dhati kweli.

MASWALI

(i) Mtunzi wa shairi hili anatoa ujumbe gani?

(ii)Katika ubeti wa pili mshairi anasisitiza jambo gani?

(iii)Bainisha kina bahari katika shairi ulilosoma.

(iv) Mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi ulilosoma huitwaje? Toa sababu moja. (v) Mshairi ana maana gani anaposema," Kweli mhimili wako, pokea kwa dhati kweli."

(vi) Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi ulilosoma.

  •   Mahabubu
  •    Fahari            
  •    Kandili
  •    Zama
  •     Mahiri
View Ans


SEHEMU E

UANDISHI WA INSHA/UTUNGAJI

5. Umeteuliwa kuwakilisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Katola. Andika barua kwa Mkuu wa shule yako kuomba ruhusa ya kuhudhuria semina ya mafunzo maalumu ya kujifunza Kompyuta kwa njia ya mtandao itakayofanyika huko Nairobi katika Shule ya Sekondari Kamenyu kuanzia tarehe 30/11/2014. Jina lako liwe Teule Nywila, S.L.P 1020. Rukwa. Barua yako ipitie kwa Mwalimu wako wa darasa.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256