FORM TWO KISWAHILI NECTA 2011

KISWAHILI 2011

SEHEMU A

UFAHAMU

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Miti ina faida nyingi sana kwa binadamu. Miti husitiri nchi kama vile nguo zimsitirivyo mtu. Nchi isiyokuwa na miti ni sawa na mtu ambaye amevuliwa nguo.

Kuongezeka kwa idadi ya watu na kutokuwepo kwa nishati mbadala kama
vile gesi na umeme mijini na vijilini kumesababisha kuwepo kwa matumizi

ya kuni na mkaa katika shughuli za binadamu za kujikimu. Hall hii imesababisha baadhi ya sehemu za nchi yetu kuanza kugeuka jangwa. Matukio ya uhaba wa mvua na upungufu wa maji kwenye mito na mabwawa yamejitokeza miaka ya hivi karibuni.

Viongozi wa nchi yetu waliliona hili mapema ndiyo maana walianzisha

za kuhimiza upandaji miti kwa kupitia vyombo vya habari. Kulikuwa na: "Kata mti, panda mti mmoja, panda miti miwili na hata kukataza kabisa ukataji wa miti. Lakini utekelezaji haujawahi kuwa wa mafanikio kwa asilimia mia moja.

Hata hivyo, ni muhimu kuendelea kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwani kama wasemavyo waswahili: "Usipoziba ufa utajenga ukuta". Ni muhimu ifike mahali mmoja wetu atambue kuwa miti an misitu ni ya taifa.

Binadamu hunufaika na miti kwa njia nyingi. Watu wengine hupikia kuni au mkaa na wengine hujengea miti. Watu wengine hupasua miti mikubwa na kupata mbao ambazo zinatumika kutengeneza kama meza, viti, kabati, madawati, rafu n.k. Mbao zingine hutumika kupaulia nyumba kutengeneza milango na vifaa vingine vya nyumbani.

Pia miti hutupatia matunda mbalimbali ambayo ni matamu na mazuri kwa afya ya mwili kama vile malimao, machungwa, maembe, zambarau n.k. Nyuki pia hutumia maua ya miti kama sehemu ya malighafi ya kutengenezea asali.

Faida nyingine ya miti au misitu ni kurekebisha hali ya hewa. Nchi isiyo na miti ya kutosha haipati mvua za kutosha kwani sehemu zenye misitu ndizo zipatazo mvua nyingi na za kutosha. Tatizo la mgao wa umeme lililoikumba nchi yetu kwa kiasi kikubwa limetokana na uharibifu wa uoto wa asili ikiwemo miti, vichaka, nyasi na mimea mingine. Miti au mimea ikiharibiwa ardhi hukauka, vyanzo vya mito au chemchem hukauka na kina cha maji kwenye mabwawa hupungua.

Miti pia humfaa binadamu kwa kumpatia dawa asili kwenye majani yake, maua, magome au hata mizizi.

Faida tote hizi zinadhihirisha kuwa miti ni rafiki mkubwa wa binadamu ambaye hajatendewa haki kwa kukatwa katwa ovyo na kuchomwa moto. Ikumbukwe kuwa tukiiangamiza miti na sisi tunaangamia.

  1. Andika kichwa cha habari uliyoisoma kwa maneno yasiyozidi
  2. Mwandishi ana maana gani anaposema "usipoziba ufa utajenga ukuta"?
  3. Taja faida za miti au misitu.
  4. Eleza kwa kifupi maana ya maneno yaliyopigiwa mstari kama yalivyotumika kwenye habari uliyosoma.
  5. Fupisha habari uliyoisoma kwa maneno yasiyopungua 50 wala kuzidi 80.
View Ans


SEHEMU B

2. (a) Oanisha .orodha A na orodha B ili kujenga dhana iliyokamilika na sahihi.

Orodha A

(i) Baadhi ya misimu

(ii) Mazingira ya jambo husika.

(iii) Mojawapo ya tanzu za lugha.

(iv) Mtindo wa lugha inayozungumzwa kulingana na muktadha na kusudi maalumu.

(v) Taaluma inayoshughulikia maumbo au mjengo wa maneno katika tungo.

Orodha B

  1. Ambaa, oyaa, mshikaji, misheni, dingi.
  2. Lugha ya mazungumzo
  3. Muktadha
  4. Rejesta
  5. Sarufi maumbo
  6. Silabi
  7. Tanbihi
View Ans


(b) Misimu ina matumizi mengi tofauti. Taja matumizi matano.

View Ans


(c) Tunga sentensi mbil zenye maana tofauti kwa kila neno kati ya maneno yafuatayo:

  1. Kaa
  2. Mbuzi
  3. Tupa
  4. Paa
  5. Kanga
View Ans


3. (a) Eleza dhima ya mofimu zilizopigiwa mstari katika maneno yafuatayo.

  1. Am_ekimbia
  2. Watamkaribisha
  3. Akija
  4. Aliy_efariki
  5. Waliopigana
View Ans


(b) Majina yafuatayo yamo kwenye daftari la wagonjwa Hospitali ya rufaa Buganda. Yapange kwa mfuatano wa kialfabeti. Zena, Yohana, Sakina, Haruna na Amina.

View Ans


(c) Bainisha aina ya maneno yaliyopigiwa mstari kwenye tungo zifuatazo kwa kuandika kifupisho cha aina ya maneno kilicho sahihi.

(T, t, E) V, W, H, U)

  1. Ng'ombe huyu na matata sana.
  2. Kitanda cha ..wanza kushoto ndicho alichotandika.
  3. Macho malegevu.
  4. mchezaji aliyeshika tama hajapata zawadi.
  5. Baba analima kaka amesimama.
View Ans


4. (a) Bainisha vipengele vinavyounda Tani na maudhui katika kazi ya fasihi,

View Ans


(b] Kamilisha mchoro ufuatao wa jedwali la fasihi simulizi kwa kujaza visanduku vilivyoachwa wazi.


View Ans


(c) Taja njia za uhifadhi wa fasihi simulizi na uzipe namba (i) hadi (iv),

ukionesha faida moja na hasara mbili kwa kila njia.

(v) Ni ipi njia ya kisasa?

View Ans


SEHEMU E
UANDISHI WA INSHA/UTUNGA)I

5. Andika mazungumzo au dayalojia kati ya mzazi na mwanawe juu ya rnatokeo ya mtihani wa muhula yasiyoridhisha ukilenga mzazi kutoa ushauri wa jinsi ya kupata ufaulu bora muhula unaofuata.

Mzazi: ...............................................................................

Mtoto: ................................................................................


Mzazi: ...............................................................................

Mtoto: ................................................................................


Mzazi: ...............................................................................

Mtoto: ................................................................................

Mzazi: ...............................................................................

Mtoto: ................................................................................


Mzazi: ...............................................................................

Mtoto: ................................................................................

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256