STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2012

MAARIFA YA JAMII 2012

SEHEMU A

URAIA

Chaguajibu sahihi kisha andika katika karatasiyakoya kujibia.

1. Mwakilishi wa wananchi katika vikao vya Wilaya vya Serikali za Mitaa ni ....

  1.  Mkuu wa Wilaya.
  2.  Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji.  
  3. Afisa Mtendaji Kata.
  4. Mwenyekiti wa Wilaya wa Chama Tawala.
  5.  Diwani wa Kata.
Chagua Jibu


2. Mojawapo ya majukumu ya Halmashauri ya Wilaya ni kutoa ruzuku kwa .....

  1.  Serikali za Kata. 
  2.  Serikali Kuu. 
  3.  Vyama vya siasa. 
  4.  Serikali za Vijiji.
  5.  Mashirika yasiyo ya kiserikali.
Chagua Jibu


3. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya au Manispaa huteuliwa na .....

  1.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  2. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
  3.  Baraza la Madiwani la Halmashuri au Manispaa husika. 
  4.  Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
  5.  Katibu Mkuu Kiongozi.
Chagua Jibu


4. Katika Bendera ya Taifa rangi ya kijani kibichi inawakilisha ...

  1.   madini           
  2.  maji
  3.  uoto wa asili 
  4.  kilimo 
  5.  ardhi
Chagua Jibu


5. Ni wakati gani Bendera ya Taifa hupeperushwa nusu mlingoti? 

  1. Wakati wa ziara za viongozi wa mataifa mengine. 
  2.  Rais anapotangaza hali ya hatari.
  3.  Linapotokea janga la kitaifa au tukio la huzuni. 
  4.  Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Taifa.
  5.  Rais anapokuwa nje ya nchi.
Chagua Jibu


6.  Uchaguzi wa Rais na Wabunge hapa Tanzania hufanyika kila baada ya

  1.  miaka 10     
  2.  miaka 3        
  3.  miaka 4 
  4.  miaka 5       
  5.  miaka 6. 
Chagua Jibu


7. Haki za binadamu zinapaswa kutolewa kwa watu wote bila kujali .

  1. vyama vya siasa. 
  2.  katiba ya nchi.
  3. haki za makundi maalumu.
  4. umri wa mtu.
  5. rangi, dini, jinsi na kabila.
Chagua Jibu


8. Kazi mojawapo ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni .........

  1.  kupokea na kuhakiki taarifa ya rasilimali na madeni ya viongozi wa umma
  2.  kusuluhisha migogoro baina ya viongozi wa umma
  3.  kufanya utafiti na kuelimisha jamii kuhusu haki za binadamu na utawala bora 
  4. kuchunguza tuhuma zozote dhidi ya Afisa wa serikali anayehusishwa na rushwa
  5.  kuthibitisha uteuzi wa mawaziri.
Chagua Jibu


9.   Ni chombo gani chenye jukumu la kulinda nchi yetu na mipaka yake? 

  1. Jeshi la Polisi Tanzania. 
  2. Jeshi la Magereza la Tanzania.
  3. Jeshi la Kujenga Taifa. 
  4. Jeshi la Wananchi la Tanzani.
  5. Jeshi la Mgambo.
Chagua Jibu


10. Lengo kuu la Polisi jamii ni ......... 

  1. kufundisha raia kazi za Polisi.
  2. kujenga mahusiano ya kirafiki baina ya Polisi na raia.
  3. kuwezesha Maafisa wa Polisi kuishi na raia. 
  4. kuwafanya raia kuwa wakakamavu kama polisi.
  5. kuzuia matumizi ya dawa za kulevya katika jamii.
Chagua Jibu


11. Mila zinazoathiri afya ya uzazi wa kinamama ni pamoja na .........

  1.  mahari na uzazi wa mpango.
  2.  ukeketaji wanawake na uzazi wa mpango.
  3.  ndoa za utotoni na mahari.
  4. ukeketaji wanawake na ndoa za utotoni. 
  5. kunyonyesha watoto kwa muda mrefu.
Chagua Jibu


12.  Mojawapo ya changamoto wanazozipata wajasiriamali ni pamoja na .......

  1.  ukosefu wa leseni za biashara.
  2.  kutokuwepo kwa benki na taasisi za fedha. 
  3. upatikanaji wa masoko ya bidhaa na huduma.
  4.  uwepo wa askari polisi na mgambo wengi maeneo ya mijini.
  5.  kutokuwepo sera ya uwekezaji.
Chagua Jibu


13. Ni chombo gani chenye jukumu la kumchagua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?

  1.  Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa. 
  2.  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 
  3.  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 
  4.  Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.
  5.  Mahakama Kuu ya Kimataifa.
Chagua Jibu


14. Mtumishi wa umma ambaye ni Mbunge kwa mujibu wa nafasi yake katika utumishi wa umma ni ....

  1.  Jaji Mkuu
  2.  Katibu Mkuu Kiongozi
  3.  Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali 
  4.  Msajili wa vyama vya siasa. 
  5.  Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Chagua Jibu


SEHEMU B

HISTORIA

Chagua jibu sahihi uliandike katika karatasi yakoya kujibia.

15. Mabaki ya Zinjanthropus yaligunduliwa ......... 

  1.  Kondoa Irangi.                       
  2.  Kalenga.                               
  3.  Olduvai.
  4.  Isimila.                                               
  5.  Engaruka.
Chagua Jibu


16. Wafanyabiashara wa mwanzo wa kigeni kuja Tanganyika walitoka ......... 

  1.  Amerika.         
  2.  Amerika Kaskazini. 
  3.  Asia
  4.  Ulaya.         
  5.  Amerika Kusini.
Chagua Jibu


17. Mojawapo ya athari ya utawala wa Waingereza katika visiwa vya Unguja ilikuwa ....

  1.  kukomesha biashara ya utumwa. 
  2. kuanzishwa kwa dini ya kikristu.
  3.  kuondoa umaskini.
  4.  kuanzisha kilimo cha karafuu. 
  5. kuanzisha vyama vya siasa.
Chagua Jibu


18. Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi vya siasa katika Tanzania ulifanyika mwaka

  1.  1992 
  2.  1990 
  3. 1961 
  4.  2005 
  5. 1995.
Chagua Jibu


19. Elimu kwa wote (UPE) nchini Tanzania ilianzishwa mwaka ...

  1.  1974 
  2. 1970 
  3.  1972   
  4.  1980
  5.  1977
Chagua Jibu


20. Nchi ya Afrika iliyokuwa inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1980 ni .....

  1.  Zimbabwe. 
  2.  Tanzania. 
  3.  Botswana.
  4.  Ghana.                                                    
  5.  Ethiopia.
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256