STD VII SAYANSI NECTA ONLINE SELF TESTS(2005-2018)
STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2023 Try This  |  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

05 SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2023

Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote.

3, Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote zinazohitajika katika fomu ya OMR.

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya Namba yako ya Mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.

6. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safe kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB to katika kujibu swali la 1 hadi 40, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.

9. Vifaa vya mawasiliano na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 40)

Katika swali 1 - 40, chagua jibu sahihi kisha weka kivuli katika herufi ya jibu hit() katika fomu ya kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Ni ogani ipi katika mwili inaathirika zaidi kutokana na unywaji wa pombe kupita kiasi?

  1. Ini
  2. Figo
  3. Mapafu
  4. Moyo
  5. Ubongo


2. Takamwili zipi hutolewa na mapafu wakati wa kupumua?

  1. Maji na oksijeni
  2. Kabonidaioksaidi na maji
  3. Maji na chumvi
  4. Urea na maji
  5. Kabonidayoksaidi na oksijeni


3. Ikiwa umealikwa kuwaelimisha wanakuui kuhusu ugonjwa wa vidonda vya tumbo, je, utawashauri kuepuka aina zipi za vyakula pindi wanapopatwa na ugonjwa huo?

  1. Vyakula vyenye sukari
  2. Vyakula vyenye joto
  3. Vyakula vya baridi
  4. Vyakula vilivyo na chumvi
  5. Vyakula vyenye asidi


4. Nini umuhimu wa seli hai nyeupe ndani ya mwili wa binadamu?

  1. Kulinda mwili kutokana na vimelea vya magonjwa
  2. Kugandisha damu katika jeraha jipya
  3. Kusafirisha gesi ya oksijeni kutoka kwenye moyo
  4. Kurekebisha joto la mwilini
  5. Kuzuia vijidudu kuingia mwilini


5. Sikio la kati lina vifupa vitatu vilivyoungana kwa mfuatano ambavyo hupokea mitetemo ya mawimbi ya sauti na kupitisha kwenda sikio la ndani. Je, upi ni mpangilio sahihi wa vifupa hivyo vitatu?

  1. Fuame, nyundo, kikuku
  2. Kikuku, fuame, nyundo
  3. Kikuku, nyundo, fuame
  4. Nyundo, fuame, kikuku
  5. Nyundo, kikuku, fuame


6. Katika ukuaji wa mimea, mizizi hukua kuelekea ardhini. Ni kwa nini mizizi ya mimea hukua kwa mtindo huo?

  1. Kufuata hewa na maji
  2. Kufuata maji na mwanga
  3. Kufuata mwanga na madini
  4. Kufuata maji na madini
  5. Kufuata joto la wastani na hewa


7. Umeombwa umsaidie mdogo wako wa kike kazi ya kubainisha viumbe hai na visivyo hai. Utachagua kundi lipi kuwakilisha viumbe hai?

  1. Mti, gogo la mti, kipepeo na chura
  2. Maji, mmea wa mhindi, samaki na chura
  3. Kipepeo, chura, maji na mti
  4. Samaki, mjusi, mti na kipepeo
  5. Maji, nyuki, nyasi na nzi


8. Mwalimu aliwafundisha wanafunzi wake kuwa udongo tifutifu ni bora zaidi kwa kilimo kuliko aina nyingine ya udongo. Ni sifa ipi inayoufanya udongo huo kuwa bora zaidi kuliko aina nyingine?

  1. Una mabonge makubwa yanayozuia maji kupita
  2. Una kichanga, mfinyanzi na maozo ya viumbe hai
  3. Huruhusu maji kupita kwa urahisi zaidi
  4. Hupitisha maji kwa taratibu sana
  5. Hukauka haraka kuliko mchanga


9. Baba yetu alitufundisha kulima kwa kubadilisha mazao kati ya jamii ya nafaka na mikunde. Unafikiri kufanya hivyo kuna faida gani?

  1. Huongeza kaboni
  2. Hurahisisha ukuaji wa mimea
  3. Hurutubisha ardhi
  4. Huzuia mmomonyoko wa udongo
  5. Huzuia magonjwa


10. Ukiandika neno SHULE kwenye karatasi nyeupe na kuliweka mbele ya kioo bapa, ni taswira ipi itaonekana katika kioo hicho?



11. Moto umekuwa ukitumika kupasha joto miili yetu wakati wa baridi. Ni kwa njia gani joto hilo huufikia mwili?

  1. Mzunguko
  2. Mnururisho
  3. Msafara
  4. Mpitisho
  5. Mvukizo


12. Endapo umepewa nafasi ya kuishauri serikali kuhusu aina ya nishati itakayosaidia kuhifadhi mazingira, utashauri kutumika kwa aina gani ya nishati?

  1. Fueli
  2. Makaa ya mawe
  3. Mafuta ya dizeli
  4. Kuni
  5. Jua


13. Fundi simu aliangusha skrubu za simu kwenye mchanga alipokuwa akipuliza uchafu uliokuwa umejaa kwenye simu. Utamshauri atumie kifaa gani kuzipata skrubu kwa muda mfupi zaidi?

  1. Hadubini
  2. Sindano
  3. Sumaku
  4. Mfagio
  5. Kurunzi


14. Ni badiliko gani hutokea wakati wa kupika ugali kwa kutumia unga wa mahindi?

  1. Kiumbo
  2. Kimazingira
  3. Kikemikali
  4. Kimaada
  5. Kiyabisi


15. Ni kwa njia gani harufu huweza kusambaa kutoka ndani ya nyumba kwenda nje?

  1. Osimosisi
  2. Fotosinthesisi
  3. Respiresheni
  4. Foto-osmosisi
  5. Difyusheni


16 Sifa za badiliko la kikemikali ni tofauti na sifa za badiliko la kiumbo. Ni sifa ipi inaonesha badiliko la kikemikali?

  1. Hakuna kitu kipya kinachotokea baada ya badiliko
  2. Hakuna tofauti kati ya uzani wa awali na ule wa baada ya badiliko
  3. Joto jingi hutumika au kutolewa wakati wa badiliko
  4. Tabia ya kitu kinachotokea baada ya badiliko inafanana na kitu cha awali
  5. Kitu cha awali kinaweza kurudia kwa urahisi half yake


17. Kapira aliweka maji na mafuta ya taa kwenye chombo kimoja. Mafuta ya taa yalielea juu ya maji. Je, ni sababu ipi ilifanya mafuta ya taa kuelea juu ya maji?

  1. Densiti ya mafuta ya taa ni ndogo kuliko densiti ya maji
  2. Kanielezi ya mafuta ya taa ni kubwa kuliko kanielezi ya maji
  3. Kani uvutano kwa maji ni kubwa kuliko kani uvutano kwa mafuta ya taa
  4. Tungamo la maji ni dogo zaidi kuliko tungamo la mafuta ya taa
  5. Tungamo la maji ni kubwa zaidi kuliko tungamo la mafuta ya taa


18. Ni maada ipi ina kani ya mvutano kubwa zaidi kati ya molekyuli?

  1. Chuma
  2. Mbao
  3. Hewa
  4. Mvuke
  5. Maziwa


19. Mawasiliano ni muhimu katika jamii ili kupashana habari. Kifaa kipi kinatumika kama njia ya mawasiliano ya asili?




20. Mwalimu wa TEHAMA aliwapa wanafunzi wa Darasa la Saba zoezi la kuchapa barua kwenye tarakilishi. Programu gani itatumiwa na wanafunzi hao kuchapa barua?

  1. Jedwali
  2. Tumizi
  3. Chapishi
  4. Endeshi
  5. Andishi


21. Picha ipi inaonesha kisakuzi cha Safari?



22. Wazazi wako wamenunua simu ya mkononi kwa ajili ya mawasiliano ya kifamilia. Utafuata hatua zipi wakati wa kutumia simu ili kuwajulisha kuhusu dharura inayoweza kujitokeza?

  1. Wasiliana → andika namba ya simu →bonyeza kitufe cha kupiga simu
  2. Andika namba ya simu → wasiliana → bonyeza kitufe cha kupiga simu
  3. Andika namba ya simu → bonyeza kitufe cha kupiga simu → wasiliana
  4. Piga simu → andika namba ya simu → bonyeza kitufe cha kukata simu
  5. Andika namba ya simu → bonyeza kitufe cha kukata simu →wasiliana


23. Kuna umuhimu gani wa kuzima tarakilishi baada ya kuitumia?

  1. Kuhifadhi taarifa kwa muda mrefu
  2. Kuiwezesha kufanya kazi kwa kasi kubwa zaidi
  3. Kuiwezesha kudumu kwa muda mrefu na kufanya kazi sawa sawa
  4. Kuhakikisha kuwa hakuna virusi wanaoweza kuishambulia
  5. Kuzuia watumiaji wasiohusika


24. Toroli ni mashine rahisi inayotumika kubeba mizigo toka sehemu moja kwenda nyingine. Upi ni mpangilio sahihi wa sehemu za nyenzo katika toroli?

  1. Jitihada huwa kati ya egemeo na gurudumu
  2. Mzigo huwa kati ya jitihada na egemeo
  3. Jitihada huwa kati ya egemeo na mzigo
  4. Egemeo huwa kati ya jitihada na mzigo
  5. Egemeo huwa kati ya mzigo na gurudumu


25. Mwalimu aliwaelekeza wanafunzi wa Darasa la Saba kutumia silinda kipimio yenye ujazo wa sm1000 katika kupima ujazo wa maji badala ya kutumia kikombe. Je kwa nini aliwaelekeza kutumia kifaa hicho?

  1. Ili kujaza maji kwa urahisi
  2. Ili kuzuia maji yasipotee
  3. Ili kutoa matokeo sahihi
  4. Ili kuokoa muda
  5. Ili kuonesha maji yanayopimwa


26. Mkasi una kiasi cha mwendo dhahiri cha 16 na manufaa ya kimakanika ya 8. Tafuta ufanisi wa mkasi huo.

  1. 200%
  2. 50%
  3. 128%
  4. 100%
  5. 150%


27. Mfanyabiashara alihifadhi samaki kwenye kikapu lakini baada ya siku tano vote walioza. Je, ungepewa nafasi ya kumshauri namna nzuri ya kuhifadhi samaki kwa muda mrefu, ungeshauri aweke wapi?

  1. Kwenye nailoni
  2. Kwenye maji
  3. Kwenye ndoo
  4. Sehemu ya wazi
  5. Kwenye jokofu


28. Ni seti ipi inawakilisha vipimio rasmi vinavyotumika kupima vitu?

  1. Rula, futi kamba na ndoo
  2. Rula, ndoo na jagi
  3.  Rula, futi kamba na jagi
  4. Futi kamba, ndoo na mzani wa mawe
  5. Rula, futi kamba na mzani wa mawe


29.Kifaa gani cha umeme kinatengenezwa kwa kutumia waya mwembamba ambao unaweza kuyeyuka iwapo mkondo wa umeme utazidi katika sakiti?

  1. Fyuzi
  2. Waya wa ethi
  3. Saketibreka
  4. Swichi
  5. Plagi


30. Mwanafunzi wa Darasa la Saba alipata jeraha. Ingawa jeraha lilifungwa kwa kutumia bandeji, damu iliendelea kutoka kwa muda. Ni kwa nini damu iliendelea kutoka?

  1. Damu yake ilikuwa na plazima iliyozidi
  2. Damu yake ilikuwa na upungufu wa sell nyeupe
  3. Damu yake ilikuwa na upungufu wa plazima
  4. Damu yake ilikuwa na chembe sahani zilizozidi
  5. Damu yake ilikuwa na upungufu wa chembe sahani


31. Upi ni ugonjwa wa kurithi kati ya magonjwa yafuatayo?

  1. Hemofilia
  2. Pumu
  3. Saratani
  4. Dondakoo
  5. Pepopunda


32. Vyakula kama siagi, karanga, korosho na alizeti hupatikana katika kundi lipi?

  1. Protini
  2. Vitamini
  3. Madini
  4. Mafuta
  5. Wanga


33. Ikiwa utapewa kazi ya kupendekeza njia bora inayoweza kutumika kuondoa mabaki ya plastiki kwenye mazingira, utapendekeza njia ipi?

  1. Kukusanya na kuchoma moto
  2. kufukia aridhini
  3. Kutupa kwenye shimo la taka
  4. kurejeleza
  5. Kuuza kwa wenye uhitaji


34. Kijana alifanya ngono zembe na kuugua magonjwa atakuwa aliugua magonjwa yapi?

  1. Kisonono, saratani, trikomonasi
  2. Kaswende, trikomonasi, kuhara
  3. Kisukari, klamidia, kichocho
  4. Kisonono, fangasi, klamidia
  5. Kaswende, trikomonasi na kichocho


35. Mtoto alianza kuharisha na kutapika baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu. Je ni dutu gani ilipungua kwa haraka zaidi mwilini?

  1. Maji
  2. Chakula
  3. Chumvi
  4. Damu
  5. Virutubisho


36. Wabeba mizigo sokoni hutumia nguvu nyingi katika kufanya kazi hiyo. Je ni chakula gani wanastahili kula kwa wingi kutokana na kazi wanayofanya?

  1. Wanga
  2. Mafuta
  3. Madini
  4. Vitamini
  5. Protini


37. Umepewa nafasi ya kutoa ushauri wa kitaalamu kwa vijana wanaoishi na VVU/UKIMWI kuboresha afya zao. Ni ushauri gani utawapatia?

  1. Kula mlo kamili na kuzingatia kanuni za afya
  2. Kufanya mazoezi na kutumia ARV
  3. Kupumzika vya kutosha na kula vizuri
  4. Kuzingatia usafi na kufanya mazoezi
  5. Kufanya ibada na kupumzika


38. Kwa nini kina mama wanashauriwa kuwanyonyesha watoto wao wadogo angalau kwa miaka miwili?

  1. Maziwa huwafanya watoto wale
  2. Maziwa yanawafanya watoto walale
  3. Maziwa yana virutubisho vyote
  4. Watoto wanapenda maziwa
  5. Watoto wasiponyonyeshwa hulia


39. Katika jamii zetu, kuna makundi mbalimbali ya watu ambayo yamepangwa kutokana na mahitaji maalumu ya kundi husika. Ni kundi lipi linahitaji huduma maalumu za afya?

  1. Watoto, wajawazito, wazee na wagonjwa
  2. Watoto, vijana, askari na walimu
  3. Watoto, wajawazito, walimu na madaktari
  4. Walimu, wazee, wagonjwa na vijana
  5. Wagonjwa, vijana, wajawazito na wazee


40. Asha aliambiwa aandae mlo kamili. Ni kundi lipi la vyakula atatumia kuandaa mlo huo?

  1. Mahindi, samaki, papai, karanga na maji
  2. Viazi, mayai, embe, karanga na maharage
  3. Ndizi, samaki, maharage, maji na wali
  4. Mchele, nyama, papai, chungwa na maji
  5. Mtama, maziwa, tango, embe na chungwa


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2022 Try This  |  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 

05 SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2022

Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote zinazohitajika katika fomu ya OMR.

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya namba yako ya mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.

6. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio sail kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB to katika kujibu swali la 1 hadi 40, na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.

9. Vifaa vya mawasiliano na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 40)

Katika swali 1 - 40, chagua jibu sahihi kisha weka kivuli katika herufi ya jibu bilo katika fomu ya kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Mfumo wa mzunguko wa damu wa binadamu umeundwa na sehemu tatu. Sehemu hizo ni zipi? 

  1. Damu, moyo na mishipa ya damu.
  2. Plazima, damu na mishipa ya damu.
  3. Chembe sahani, moyo na sell nyekundu.
  4. Tishu, moyo na sell nyeupe.
  5. Plazima, tishu na chembe sahani.


2. Dereva wa lori alipata ajali iiiyosababisha mwili wake kushindwa kuwa katika msawazo. Je, ni sehemu gani ya sikio lake iliathirika?

  1. Nyundo 
  2. Vifereji nusu duara 
  3. Fuawe
  4. Kikuku 
  5. Miatus


3. Bwana chapombe aiipewa jina hilo kutokana na unywaji wa pombe uliokithiri. Ni ogani gani ina weza kuathirika kutokana na tabia hiyo?

  1. lni 
  2. Figo 
  3. Mapafu
  4. Moyo 
  5. Ubongo


4. Nini kitatokea endapo mwanaume atapata ajali na korodani zake kuathirika kabisa?

  1. Gamete ume hazitaweza kuingia katika uke.
  2. Gamete ume hazitaweza kuzalishwa.
  3. Gamete ume hazitasafirishwa kwenda kwenye uretha.
  4. Gamete ume na mkojo hautaweza kuzalishwa.
  5. Gamete ume zitazalishwa na kufa.


5. Chunguza Kielelezo Namba 1 kinachoonesha kasoro katika jicho kisha jibu swali linalofuata.

Kielelezo Na. 1

Je ni kasoro ipi inarekebishwa na lenzi mbinuko?

  1. (i)
  2. (ii)
  3. (iii)
  4. (i) na (ii)
  5. (ii) na (iii)


6. Kwa nini seli za mmea zina uwezo wa kujitengenezea chakula chake zenyewe wakati seli za mnyama haziwezi?

  1. Seli ya mmea ina saitoplazirmi. 
  2. Seli ya mmea ina maitokondria.
  3. Seli ya mmea ina stomata. 
  4. Seli ya mmea ina chloroplasti.
  5. Seli ya mmea ina nyukliasi.


7. Unapojaza hewa kwenye puto ukubwa wake huongezeka na hewa ikizidi hupasuka. Ongezeko la ukubwa wa puto lina maana gani kisayansi?

  1. Hewa huchukua nafasi. 
  2. Hewa ni nzito kuliko puto.
  3. Hewa ina chembechembe ndogo. 
  4. Puto ni laini sana.
  5. Puto linavutika.


8. Iii wanyama waweze kuishi wanahitaji chakula kutoka kwenye mimea na vitu vingine kutoka katika mazingira. Je, ni vitu gani vingine wanahitaji tofauti na chakula?

  1. Mwanga na joto. 
  2. Maji na upepo.
  3. Hewa na virutubisho. 
  4. Mwanga na upepo.
  5. Maji na hewa.


9. Moja kati ya atomu iliyoko kwenye mbolea zilizo nyingi hupatikana hewani kama gesi. Je atomu hiyo ni ipi?

  1. Agoni 
  2. Oksijeni 
  3. Haidrojeni
  4. Naitrojeni 
  5. Kabonidayoksaidi


10. Uendeshaji wa mitambo ya viwanda kwa kutumia nishati itokanayo na makaa ya mawe una athari gani9

  1. Husababisha uchafuzi wa angahewa.
  2. Huharibu mitambo ya viwanda.
  3. Hutoa nishati ndogo sana.
  4. Huzalisha hewa ya nitrojeni.
  5. Nishati yake ina ukinzani mkubwa.


11. Endapo itatokea vifaa vyote vya umeme ikiwemo runinga, radio na taa za shuleni kwenu vimezitna ghafla, je, ni hatua gani ya kwanza utachukuwa ill kutatua tatizo?

  1. Kubadilisha fyuzi za vifaa hivyo.
  2. Kukagua mfumo wa umeme.
  3. Kubadilisha fyuzi za plagi.
  4. Kubadilisha fyuzi za kikata umeme.
  5. Kurekebisha swichi kuu.


12. Mwindaji alilazimika kuwasha moto kwa kutumia miwani yake yenye lenzi mbinuko ill aweze kuchoma nyama. Ni tabia gani ya mwanga ilioneshwa na miwani hiyo ya mwindaji?

  1. Kusharabiwa kwa mwanga. 
  2. Kukusanya kwa mwanga.
  3. Kutawanya kwa mwanga. 
  4. Kuakisiwa kwa mwanga.
  5. Kupinda kwa mwanga.


13. Nyumba ya Bwana Matata ina vyumba vitatu na vyote.vinatumia umeme unaotoka kwenye njia kuu moja. Utatambuaje kama nyumba hiyo inatumia sakiti sambamba?

  1. Glopu ya chumba cha kwanza ikiondolewa, glopu 2a. chumba cha pill na cha tatu zitazima.
  2. Glopu ya chumba cha kwanza ikiondolewa, glopu.zaichumba cha pill na cha tatu zitaendelea kuwaka.
  3. Glopu ya chumba cha pill ikiondolewa, glopu ya cha tatu itazima.
  4. Glopu ya chumba cha tatu ikiondolewa, glopu ya 'cliumba cha pill itazima na ya chumba cha kwanza itaendelea kuwaka.
  5. Glopu ya chumba cha pill ikiondolewa, glopu ya chumba cha kwanza itazima.


14. Mtoto alikuwa akicheza nje mbali na jikoni, alihisi harufu nzuri ya chakula alichokuwa anapika dada yake. Ni kwa njia gani harufu hii ilimfikia mtoto?

  1. Difyusheni
  2. Respiresheni
  3. Osmosisi
  4. Molekyuli
  5. Uyeyushaji


15. Mada huonesha badiliko la kiumbo au kikemikali. Ipi ni mifano ya badiliko la kikemikali? 

  1. Chuma kupata kutu, kuchacha kwa maziwa na kuungua kwa mkaa.
  2. Kuchacha kwa maziwa, kuoka mkate na kuyeyusha sukari kwenye mail.
  3. Kupika chakula, kuoka mkate na kuchanganya chumvi na maji.
  4. Maji kuwa barafu, kuchacha kwa maziwa na kuungua kwa mkaa.
  5. Kuyeyusha sukari kwenye maji, kuungua kwa mkaa na kuoka mkate.


16. Mwalimu wa TEHAMA aliwapa wanafunzi zoezi la kuingiza data kwenye mkekakazi. Je ni sell gani itaruhusu kuchapa data inayotakiwa?

  1. Sell ya kwanza. 
  2. Sell amilifu. 
  3. Sanduku sell.
  4. Safumlalo sell. 
  5. Safuwima sell.


17. Ndugu Hamza anataka kununua antena kwa ajili ya kupokea mawimbi mbalimbali ya runinga na redio. Je utamshauri anunue aina gani ya antena?

  1. Kitanzi 
  2. Yagi-Uda 
  3. Honi
  4. Kipenyo 
  5. Akisi


18. Mwalimu aliwapa wanafunzi zoezi la kubainisha aina za vitumi kwenye tarakilishi. Je kifaa kipi ni mfano wa vitumi ingizi?

  1. Monita 
  2. Printa 
  3. Kibodi
  4. Kipaza sauti
  5. Kichakato kikuu


19. Madilu anahitaji mashine ya kieletroniki yenye uwezo wa kupokea, kuchakata, kuhifadhi na kutoa taarifa za mauzo katika duka lake. Je utamshauri anunue mashine gani?

  1. Runinga 
  2. Tarakilishi 
  3. Kisimbuzi
  4. Kadi kumbukizi 
  5. Sumakuumeme


20. Kifaa kipi cha mawasiliano hupokea mawimbi ya sumakuumeme na kuyabadili kuwa sauti na picha?

  1. Antena 
  2. Runinga 
  3. Redio
  4. Simu 
  5. Kisimbuzi


21. Mwalimu wa soma la Sayansi aliagiza wanafunzi wote wa Darasa la Tatu kuleta rula kwa ajili ya kufanya vipimo. Ni kipimo gani alitaka wanafunzi wafanye?

  1. Ujazo
  2. Urefu
  3. Tungamo
  4. Uzito
  5. Muda


22. Kwa kufuata mpangilio wa sehemu za wenzo, upi ni mpangilio sahihi unaowakilisha mashine daraja la kwanza?

  1. Jitihada inapatikana katikati ya egemeo na gurudumu.
  2. Mzigo unapatikana katikati ya jitihada na egemeo.
  3. Jitihada inapatikana katikati ya egemeo na mzigo.
  4. Egemeo linapatikana katikati ya jitihada na mzigo.
  5. Mzigo unapatikana katikati ya egemeo na msawazo.


23. lkiwa jumla ya kazi iliyofanywa na mwanafunzi aliyevuta sanduku kwa umbali Oa mita 20 ni Jouli 240. Je ni kani ya kiasi gani ilitumika katika Nyutoni?

  1. 4,800 
  2. 120 
  3. 12
  4. 48
  5. 480


24. Mwalimu wa Sayansi alitumia betri yenye volti 2 na kikinza chenye ohm 0.2 kuunganisha sakiti ya umeme. Je alipata kiasi gani cha mkondo wa umeme katika sakiti?

  1. 0.01 A 
  2. 0.1A 
  3. 10A
  4. 0.4A 
  5. 40A


25. Dereva wa basi alitumia kioo cha pembeni kuona taswira ya gari lililokuwa nyuma yake. Ni aina gani ya kioo alichotumia?

  1. Kioo mbonyeo 
  2. Kioo bapa
  3. Kioo cha kisasa 
  4. Kioo mbinuko
  5. Kioo cha kawaida


26. Gesivunde inajumuisha mchanganyiko wa gesi mbalimbali. Je, ni gesi ipi iko kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko zingine?

  1. Haidrojeni salfaidi 
  2. Kabonidayoksaidi
  3. Methani 
  4. Amonia
  5. Haidrojeni


27. Mwili wa mtu mwenye kisukari hushindwa kuzalisha insulin. Ni kiungo kipi cha mtu huyo huwa na tatizo?

  1. Ini 
  2. Kongosho 
  3. Ubongo
  4. Figo
  5. Mfuko wa nyongo


28. Ni mgonjwa yupi yupo hatarini zaidi kuambukizwa VVU/ UKIMWI

  1. Mwenye kuuguwa kaswende na malaria.
  2. Mwenye kuuguwa kipindupindu na kichocho.
  3. Mwenye kuuguwa kisonono na fangasi.
  4. Mwenye kuuguwa trikomonasi na kifua kikuu.
  5. Mwenye kuuguwa klamidia na pumu.


29. Mgonjwa alikwenda hospitalini ambapo daktari aligundua kuwa kinga yake ya mwili iko chini. Unafikiri daktari alimpa ushauri gani mgonjwa huyo?

  1. Kula mlo kamili na kufanya mazoezi.
  2. Kukaa katika mazingira safi na kula kwa wingi wanga. 
  3. Kunywa maji ya kutosha na kupumzika kidogo.
  4. Kufanya mazoezi ya kutosha na kupumzika kidogo, 
  5. Kutumia virutubisho na kula kwa wingi wanga.


30. Sababu inayotofautisha magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza ni kwamba magonjwa ya kuambukiza:

  1. huathiri viungo vyote vya mwili.
  2. husababisha homy kali.
  3. huenea kwa haraka sana.
  4. huenezwa kwa njia ya hewa.
  5. hutibika kwa chanjo.


31. Daktari alimshauriwa Amina kula vyakula vyenye wanga. Ni kundi gani la vyakula linawakilisha vyakula hivyo?

  1. Mchele, viazi, mtama na samaki.
  2. Mahindi, maharage, karanga na mtama. 
  3. Ngano, ndizi, nyama na muhogo.
  4. Viazi, miwa, mahindi na ngano. 
  5. Mchele, viazi, siagi na korosho.


32. Katika jamii zetu kuna mtazamo usio sahihi ambapo wagonjwa wa kifua kikuu huchukuliwa kuwa wana VVU/UKIMWI. Unafikiri ni kwa nini mtazamo huo sio sahihi?

  1. Dalili za UKIMWI hazihusiani na kifua kikuu.
  2. Ukiwa na UKIMWI una kifua kikuu.
  3. UK1MW1 hutambuliwa kwa kupima.
  4. Kifua kikuu hutibika lakini UKIMWI hautibiki.
  5. UKIMWI husababisha kifua kikuu.


33. Mandevu ni mwanafunzi anayevaa nguo chafu na haogi. Kutokana na tabia hizo, ni ugonjwa gani anaweza kupata?

  1. Surua
  2. Mafua
  3. Kifua kikuu
  4. Ugonjwa wa vipele
  5. Tetekuwanga


34. Watoto wanahitaji vyakula vinavyotumika kujenga na kukuza mwili. Ni kundi lipi linawakilisha vyakula hivyo?

  1. Wali, maharage, samaki, madini, spinachi na embe.
  2. Maji na madini, wall, samaki, spinachi na mapapai. 
  3. Ugali, maharage, maziwa, mkatc na chungwa.
  4. Nyama, samaki, mayai, maziwa na maharage. 
  5. Wali, uyoga, madini, nyama, spinachi na chungwa.


35. Ni kundi lipi la vifaa ambavyo tunatumia katika maisha yetu ya kila siku lakini likitumika vibaya linaweza kuchangia kusambaa na kuongezeka kwa maambukizi ya VVU?

  1. Wembe, pini na mkasi
  2. Wembc, pini na kichongeo.
  3. Wembe, pini na chanuo.
  4. Kisu, kichongeo na chanuo.
  5. Wembe, pini na chanuo.


36. Bwana Mambo alipata vidonda vya koo, maumivu ya kichwa na kutokwa damu puani, masikioni na mdomoni. Unafikiri Bwana Mambo alikuwa na ugonjwa gani?

  1. Malaria 
  2. Hama ya uti wa mgongo
  3. Ebola 
  4. Covid 19
  5. Kipindupindu


37. Utatumia mfano gani kama unataka kumwelekeza mwenzako kuhusu badiliko la kiumbo?

  1. Kuchachusha maziwa 
  2. Chuma kupata kutu
  3. Kuunguza kipande cha karatasi 
  4. Kuyeyusha barafu
  5. Kupika chakula


38. Upi ni mpangilio sahihi wa hall za maada kulingana na kani ya mvutano ya molekuli kuanzia ndogo hadi kumbwa?

  1. yabisi, gesi, kimiminika. 
  2. kimiminika, yabisi, gesi.
  3. gesi, kimiminika, yabisi. 
  4. yabisi, kimiminika, gesi.
  5. kimiminika, gesi, yabisi.


39. Mwanafunzi wa Darasa la Saba alipewa kimiminika alichotakiwa kukitambua. Alidondoshea matone machache kwenye karatasi nyekundu ya litimasi ambayo ilibadilika rangi na kuwa ya bluu. Je, kimiminika hicho kilikuwa na nini?

  1. Tindikali 
  2. Nyongo 
  3. Vinega
  4. Sukari 
  5. Karboneti


40. Misumari mitano iliwekwa katika makopo matano tofauti. Ni jaribio lipi litaonesha matokeo chanya ya chuma kupata kutu?

  1. Lenye msumari uliopakwa kilainishi.
  2. Lenye msumari na lililofunikwa baada ya maji kuchemshwa.
  3. Lenye msumari uliopakwa mafuta ya kupikia.
  4. Lenye msumari, unyevunyevu na lililoachwa wazi.
  5. Lenye msumari, maji yaliyochemshwa na yenye mafuta.


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2021 Try This  |  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI

05 SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2021

Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote zinazohitajika katika fomu ya OMR.

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya namba yako ya mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.

6. Weka kivuli kwenye herufi ya jibu sahihi kwa swali la 1 hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya HB tu katika kujibu swali la 1 hadi 40, na kalamu ya Wino wa bluu au mweusi kujibu swali la 41 hadi 45.

9. Vifaa vya mawasiliano na Vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 40)

Katika swali 1 - 40, chaguajibu sahihi kisha weka kivuli katika herufi yajibu hilo katika fomu maalum ya kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Mfumo wa utoaji takamwili katika mwili wa binadamu umeundwa na ogani kuu nne. Ogani ipi inahusika na utoaji wa kabonidayoksaidi na maji katika hali ya mvuke? 

  1. Mapafu 
  2. Figo 
  3. Ini 
  4. Pua 
  5. Ngozi


2. Mzee alionekana akiyumbayumba barabarani baada ya kunywa pombe nyingi. Je, ni sehemu gani ya sikio iliathiriwa na pombe?

  1. Kikuku. 
  2. Ngoma ya sikio. 
  3. Vifereji nusuduara. 
  4. Koklea. 
  5. Neva za akustika.


3. Baadhi ya watu wana matatizo ya kutoona vizuri wakati wa usiku. Matatizo haya yanasabishwa na ukosefu wa vitamini ipi?

  1. A
  2. B1
  3. B2
  4. D
  5. C


4. Mama alikuwa akihisi kizunguzungu na mwili kuishiwa nguvu. Baada ya daktari kumfanyia uchunguzi alibaini kuwa ana upungufu wa damu. Je, utamshauri ale vyakula vya aina gani?

  1. Vyakula vyenye sukari ya kutosha. 
  2. Vyakula vyenye madini ya ayani.
  3. Vyakula vyenye mafuta ya kutosha. 
  4. Vyakula vya wanga pekee. 
  5. Vyakula visivyo na chumvi.


5. Rafiki yako anashindwa kuona vizuri mpira uliowekwa karibu naye. Je, utamshauri atumie aina gani ya miwani?

  1. Lenzi mbinuko 
  2. Lenzi mbonyeo 
  3. Lenzi mbili 
  4. Lenzi kubwa 
  5. Lenzi ndogo


6. Kaka yangu alijikata kwenye kidole wakati alipokuwa anamenya viazi vitamu. Alifunga jeraha kwa kutumia bandeji, lakini damu iliendelea kutoka kwa muda mrefu. Je, damu ya kaka yangu ilikuwa na upungufu gani?

  1. Seli hai nyeupe 
  2. Chembe sahani 
  3. Plazima 
  4. Madini 
  5. Seli hai nyekundu


7. Wakulima walielimishwa na mtaalam wa kilimo kuacha kutumia njia za kilimo zinazosababisha mmonyoko wa udongo. Je, ni njia ipi hawapaswi kuitumia wakulima hao?

  1. Kupanda miti shambani. 
  2. Kulima kwa matuta. 
  3. Kulima kwa kufuata kontua. 
  4. Kulima kwa kufuata ngazi. 
  5. Kusafisha shamba kwa kutumia moto.


8. Ni kundi lipi linawakilisha wanyama wenye uti wa mgongo?

  1. Nyoka, Punda, Konokono na Fisi.
  2. Mjusi, Kipepeo, Pundamilia na Simba.
  3. Mamba, Swala, Tembo nå Panzi.
  4. Swala, Mamba, Kiboko na Twiga.
  5. Konokono, Kaa, Tembo na Pundamilia.


9. Mdogo wako alistaajabu kuiona alama ya fuvu la kichwa kwenye nguzo za umeme na kwenye makopo ya dawa za chooni. Alama hiyo kwenye sehemu hizo huashiria nini? 

  1. Sumu au hatari 
  2. Inashika moto 
  3. Inamomonyoa na kuunguza 
  4. Inalipuka 
  5. Inakereketa


10. Wanafunzi wa Darasa la Tano walifanya jaribio la kutengeneza sakiti rahisi kwa kutumia selikavu, waya na balbu. Je, ni kundi lipi lilifanikiwa kuwasha balbu?



A
B
C
D
E


ll. Mwanafunzi alishuhudia jengo la Shule likibomoka kwa kupigwa na radi. Unapendekeza nini kifanyike kwenye majengo ili tatizo kama hili lisitokee katika majengo mengine?

  1. Yajengwe kwa mawe. 
  2. Yajengwe kwa ukuta mnene. 
  3. Yawe na ukuta wa kuzuia radi. 
  4. Yafungwe waya wa ethi. 
  5. Yafungwe kikinga radi.


12. Mfanyakazi wa kiwanda cha nondo ameingiwa na chembechembe za chuma machoni na anahitaji msaada. Je, utafanya nini ili kumsadia?

  1. Kumuosha uso wake kwa maji safi na sabuni.
  2. Kutumia sumaku itakayonasa chembechembe hizo.
  3. Kutumia pamba ya masikioni kuziondoa chembechembe hizo.
  4. Kutumia kitambaa safi kufuta ndani ya jicho.
  5. Kumwinamisha chini ili chembechembe hizo zidondoke.


13. John alitazama maji yaliyotulia akaona sura yake. Kitendo hicho kinaonesha tabia gani ya mwanga?

  1. Kusafiri 
  2. Kupinda 
  3. Kupenya 
  4. Kuakisiwa
  5. Kusharabiwa 


14. Sababu ipi inaifanya gesivunde kuwa nzuri kuliko kuni kama chanzo cha nishati? 

  1. Ilaitoi moshi wakati wa kutumia. 
  2. Inatoa gesi ya oksijeni.
  3. Inatoa gesi ya kabonidayoksaidi. 
  4. Haina gharama katika uzalishaji. 
  5. Inatumika kwa kiasi kidogo.


15. Mmea hufyonza molekyuli za maji toka kwenye udongo kupitia kwenye mizizi kwenda sehemu mbalimbali. Ni njia ipi ambayo mmea hutumia kufyonza maji?

  1. Osimosisi 
  2. Difyusheni 
  3. Usambazaji 
  4. Uenezi 
  5. Kunyonya


16. Ni tendo lipi litasababisha kutokea kwa maada mpya?

  1. Kuyeyuka kwa sukari kwenye maji. 
  2. Kuchacha kwa maziwa.
  3. Kubadilika kwa maji kuwa mvuke. 
  4. Kuongeza chumvi kwenye chakula. 
  5. Kuchemsha mchanganyiko wa nta na maji.


17. Rafiki yako amekuomba umsaidie kufungua Program jedwali. Je ni hatua zipi utazifuata?

  1. Bofya menu ya start → Microsoft office →Programu jedwali. 
  2. Bofya menu ya start→Microsoft word → Programu jedwali. 
  3. Bofya menu ya start → program jedwali → Microsoft office.
  4. Bofya menu ya start →Y programu jedwali → Microsoft word. 
  5. Bofya menu ya start → Microsoft office → Microsoft word.


18. Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Makuti anataka kubadilisha mfumo wa kutunza kumbukumbu kutoka kwenye mfumo wa daftari la mahudhurio kwenda kwenye mfumo wa kielektroniki. Utamshauri kutumia mashine gani?

  1. Runinga 
  2. Tarakilishi 
  3. Kisimbuzi 
  4. Kashamfumo 
  5. Ruta


19. Mwalimu wa somo la Sayansi na Teknolojia alitaka uwe na barua pepe ya gmail. Je hatua ipi ni ya kwanza kufuata ili kupata barua pepe?

  1. Kutembelea anwani ya tovuti "www.gmail.com".
  2. Kujaza taarifa zote zinazotakiwa katika fomu ya gmail.
  3. Kujaza namba ya simu na terehe ya kuzaliwa katika fomu ya gmail.
  4. Kuchagua aina ya anwani unayotaka kutumia katika gmail.
  5. Kutembelea tovuti ya "www.yahoo.com" na kuandika nywila kwa usahihi.


20. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa redio nyingi katika kijiji cha Magunga zinatumia antena aina ya kitanzi kidogo. Je, wanapata hasara gani kutokana na matumizi ya antena za aina hiyo? 

  1. Husababisha uharibifu wa redio.
  2. Husababisha upotevu wa nishati ya umeme. 
  3. Husababisha uharibifu wa spika.
  4. Zinahitaji gharama kubwa ya matengenezo. 
  5. Zina mwingiliano wa mawimbi.


21. Kwa nini inashauriwa kuzima tarakilishi kwa kufuata hatua sahihi?

  1. Kuilinda dhidi ya kukatika kwa umeme kusikotarajiwa.
  2. Kuepuka kudondoka chini.
  3. Kupunguza joto lililozalishwa ndani ya tarakilishi.
  4. Kuilinda dhidi ya virusi vya tarakilishi.
  5. Kuepuka kupoteza taarifa ambazo hazijahifadhiwa.


22. Mwalimu wa somo la Kiswahili aliwatumia wazazi matokeo ya wanafunzi kwa kutumia barua pepe lakini hawakuyapata matokeo hayo. Je, ni jambo gani muhimu ambalo Mwalimu hakulizingatia wakati wa kutuma barua pepe?

  1. Kuandika anwani ya barua pepe ya mpokeaji kwa usahihi.
  2. Kuandika kichwa cha ujumbe.
  3. Kuandika anwani ya barua pepe ya mtumaji kwa usahihi.
  4. Kufunga akaunti yake baada ya kutumia.
  5. Kuruhusu kisakuzi kukumbuka nywila yake.


23. Mashine tata zimeundwa kwa kutumia mashine rahisi mbili au zaidi. Je, muundo huo una umuhimu gani?

  1. Kuongeza ufanisi. 
  2. B Kuongeza mvutano. 
  3. C Kuongeza msuguano. 
  4. D Kuongeza mwendo. 
  5. E Kupunguza msuguano.


24. Wenzo ina sehemu kuu tatu ambazo zimepangwa kwa mtiririko maalumu. Mpangilio upi unawakilisha nyenzo daraja la tatu?

  1. Jitihada, mzigo na egemeo. 
  2. Egemeo, jitihada na mzigo. 
  3. Egemeo, mzigo na jitihada 
  4. Mzigo, egemeo na jitihada. 
  5. Jitihada, egemeo na mzigo.


25. Ni kanuni ipi inatoa uhusiano uliopo kati ya manufaa ya kimakanika, mzigo na jitihada katika mfumo wa roda?

A.
B.
C.
D.
E.


26. Wanafunzi wa Darasa la Nne waliagizwa kuja na mashine tata ili waitumie kujifunza schemu za mashine Iuzo. .Ie, walileta Vlfaa gani? 

  1. Batskeli, cherehani na mizani.
  2. Kitasa, baiskeli na nyundo.
  3. Kitasa, cherehani na baiskeli.
  4. Cherehani, baiskcli na kifungua chupa. 
  5. Mizani, kitasa na baiskeli.


27. ipi ni kizito cha ukinzani katika umeme?

  1. Volti 
  2. Ohm 
  3. Voltimita 
  4. Ampia 
  5. Amita


28. Ni seti ipi ina vitu vyenye asidi?

  1. Chungwa na majivu. 
  2. Limao na majivu. 
  3. Majivu na magadi. 
  4. Chungwa na limao. 
  5. Chungwa na magadi.


29, Nguo za aina moja zenye rangi nyeupe, nyekundu, nyeusi, njano na kijani zilizotengenezwa na malighafl ya aina moja zilifuliwa kisha kuanikwa sehemu yenye mwanga wa jua. Je, ni nguo ya rangi gani itak'uwa ya kwanza kukauka?

  1. Nyeupe 
  2. Nyekundu 
  3. Nyeusi 
  4. Njano 
  5. Kijani


30. Nguo za rafiki yako zilishika moto uliosababishwa na mlipuko wa mafuta. Je, unapaswa kufanya nini ili kuzima moto huo?

  1. Kumtoa nguo zote. 
  2. Kumfunika na kitambaa cha baridi. 
  3. Kumwagia maji. 
  4. Kumfunika blanketi Zito. 
  5. Kumpeleka hospitali.


31. Mwindaji aliumwa na nyoka mguuni. Je, ni msaada gani wa awali alitakiwa kupewa?

  1. Kumlaza chali huku miguu ikiwa juu.
  2. Kumpeleka hospitali.
  3. Kumsugua kwa majivu na chumvi.
  4. Kumfunga sehemu ya juu ya alipoumwa. 
  5. Kumsafisha kwa maji safl na sabuni.


32. Babu yako ana matatizo ya kutoona mbali. Utamshauri atumie vyakula gani ili vimsaidie katika tatizo lake?

  1. Ndizi, machungwa na karanga.
  2. Wali, nanasi na nyama.
  3. Embe, karoti na mboga za majani.
  4. Karoti, mihogo na maharagwe. 
  5. Mkate, ndizi na mihogo.


33. Wanafunzi walikatazwa kutupa chupa topu za plastiki baada ya kunywa maji katika viwanja wya shule ili kuzuia uchafuzi wa mazingira. Je unashauri njia gani itum?ke ili chupa hizo zis?cndclee kuchafua mazingira?

  1. Kuzichoma moto 
  2. Kuzirudisha kiwandani 
  3. Kuzikatakata vipande na kuzitupa 
  4. kuzifukia kwenye shimo 
  5. kuzitunza stoo


34. Kaka NIkuu aliuaongoza wanafunzi wa Darasa la Tatu kusaf?sha mazingira ya shule ili kuangamiza mazalia ya mbu. Ni shughuli zipi muhimu walizifanya?

  1. Kufyeka na kufukia madimbwi 
  2. Kufagia na kupanda miti 
  3. Kupanda maua na kufiyeka
  4. Kutoa buibui na kudeki 
  5. Kufukia mashimo yaliyojaa na kuchimba mapya


35. ?pi kati ya zifuatazo haihusiani na kanuni za kiafya ambazo kila mmoja anatakiwa azifuate ili awe na afya bora?

  1. Kula lishe bora 
  2. Kusaf?sha mazingira 
  3. Kutumia maji safi na salama 
  4. Kufahamu michezo mbalimbali 
  5. Kupumzika na kulala


36. Ni magonjwa yapi yanayotokana na kurithi kasoro katika vinasaba kutoka kizazi kimoja kuenda kingine?

  1. Kifafa na kichocho 
  2. Selimundu na hemophilia 
  3. Ualibino na homa ya ini 
  4. Pumu na kifua kikuu 
  5. Hemofilia na kisonono


37. Watu wanaofanya kazi ngumu za kubeba mizigo wanastahili kula aina gani ya chakula kwa uingi?

  1. Vitamini 
  2. Mafuta 
  3. Madini 
  4. Wanga 
  5. Protini


38. Nifumo wa mmeng'enyo wa chakula katika mwili wa binadamu unaundwa na sehemu mbalimbali. Ni sehemu gani inayofyonza maji na madini?

  1. Utumbo mpana 
  2. Utumbo mwembamba 
  3. Tumbo 
  4. Nifuko wa nyongo
  5. Umio


39. Densiti ya mbao ni kilogramu 20 kwa meta za ujazo. Ikiwa mbao zina ujazo wa meta 90, tafuta tungamo la mbao.

  1. kg 110.0 
  2. kg 0.222 
  3. kg 4.5 
  4. kg 1800 
  5. kg 180.0


40 Nyambizi ni aina ya meli inayoweza kuzama au kuelea ndani maji. Kama nyambizi ipo ndani ya maji na inatakiwa ielee, ni nini kinatakiwa kufanyika?

  1. Maji kutolewa na hewa kujazwa kwenye matangi.
  2. Maji kulolewa na kuacha matangi yakiwa lupu bila heua.
  3. Kuongeza kanielezi kwenye matang? kua kutumia ugiligili mucpesi.
  4. Hewa kutolewa kwenye matangi ili kupunguza uzito.
  5. Kusawazisha kanielezi na kani ya uvulano kwenye nyambizi.


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2020 Try This  |  

JAMUHUR1 YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA 

MTIHANI WA KUMALIZA ELMU YA MSINGI

05 SAYANSI

Muda: Saa 1: 30 Mwaka: 2020

Maelekezo

l . Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali arobaini na tano (45).

2. Jibu maswali yote katika kila sehemu.

3. Soma maelekezo yote yaliyoko katika fomu maalum ya kujibia (OMR).

4. Jaza taarifa zote zinazohitajika katika fomu ya OMR na katika kurasa zenye swali Ia 41 hadi 45 kwenye karatasi ya maswali.

5. Weka kivuli katika kila tarakimu ya namba yako ya mtihani kwenye nafasi husika katika fomu ya OMR.

6. Weka kivuli kwenye herufi yajibu sahihi kwa swali Ia I hadi 40 katika fomu yako ya kujibia uliyopewa. Kwa mfano, kama jibu sahihi ni A weka kivuli kama ifuatavyo:

image

7. Ukigundua kuwa herufi uliyowekea kivuli si jibu sahihi, futa kivuli hicho kwa umakini kwa kutumia kifutio safi kabla ya kuweka kivuli katika herufi mpya.

8. Tumia penseli ya kwa swali Ia I hadi Ia 40 na kalamu ya wino wa bluu au mweusi kwa swali Ia 41 hadi Ia 45.

9. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi ndani ya chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 40)

Katika swali la 1- 40. chagua jibu sahihi kisha weka kivuli katika herufi ya jibu hilo katika fomu maalum ya kujibia (OMR) uliyopewa.

1. Sifa zipi zinahusu mimea pamoja na wanyama

  1. Respiresheni, mjongeo na fotosinthesisi.
  2. Respiresheni, uzaaji na ukuaji.
  3. Ukuaji, uzaaji na fotosinthesisi.
  4. Mjongeo, uzaaji na transipiresheni.
  5. Ukuaji, respiresheni na fotosinthesisi.


2. Kwa nini shamba la maharage halihitaji mbolea ya naitreti? 

  1. Maharage yanaweza kubadili naitrojeni kuwa naitreti.
  2. Maharage yanaweza kubadili ammonia kuwa nitreti.
  3. Maharage yanaweza kubadili naitrojeni kuwa ammonia. 
  4. Maharage yanaweza kubadili nitreti kuwa naitrojeni.
  5. Maharage yanaweza kubadili ammonia kuwa naitrojeni.


3. Nini faida ya wadudu?

  1. Kusafirisha maua.
  2. Kula maua.
  3. Kukuza maua.
  4. Kuchavusha maua.
  5. Kupukutisha maua.


4. Nini lengo la uzazi wa mpango katika familia?

  1. Kupunguza kuenea kwa magonjwa.
  2. Kuacha nafasi kati ya uzazi mmoja na mwingine.
  3. Kupunguza idadi ya watoto.
  4. Kupunguza idadi ya watoto wa kupeleka kliniki. 
  5. Kuwezesha watoto kupata huduma muhimu.


5. Kwa nini inashauriwa kutovuta sigara? 

  1. Kuepuka saratani ya kifua na damu.
  2. Kuepuka saratani ya damu na ini.
  3. Kuepuka saratani ya mapafu na kifua.
  4. Kuepuka saratani ya ngozi na kifua. 
  5. Kuepuka saratani ya ini na mapafu.


6. Jamii inawezaje kujikinga dhidi ya malaria? 

  1. Kwa kutumia vyandarua vyenye dawa.
  2. Kwa kumeza vidonge vya malaria.
  3. Kwa kufua chandarua.
  4. Kwa kuua plasmodiamu.
  5. Kwa kuzuia na kuua bakteria.


7. Kwa nini inashauriwa kuchemsha maji ya kunywa?

  1. Ili kuyafanya yawe safi. 
  2. Ili kuyafanya yawe meupe. 
  3. Ili kuyafanya yawe salama. 
  4. Ili kuyafanya yawe ya moto. 
  5. Ili kuyafanya yawe matamu.


8. Nini umuhimu wa gesi ya kabonidioksaidi kwa mimea?

  1. Hutumika katika kufanyika kwa maua.
  2. Hutumika katika uchavushaji.
  3. Hutumika katika respiresheni.
  4. Hutumika katika kufanyika kwa matunda. 
  5. Hutumika katika usanisi wa chakula.


9. Ni sifa ipi ya wanyama katika kundi la amfibia inawatofautisha na ndege? 

  1. Kuwa na damu moto. 
  2. Mifupa mifupi. 
  3. Kutaga mayai. 
  4. Kuishi majini. 
  5. Kuishi nchi kavu.


10. Ipi ni jozi ya magonjwa ya kurithi?

  1. Malaria na trakoma.
  2. Saratani na tetekuwanga.
  3. Selimundu na hemofilia.
  4. Trakoma na surua.
  5. Pepopunda na UKIMWI.


I l . Nini mahitaji muhimu kwa uhai?

  1. Maji, chakula na hewa.
  2. Vitamini, maji na hewa. image
  3. Protini, wanga na madini.
  4. Maji, hewa na matunda.
  5. Hewa, mavazi na mwanga.


12. Sehemu ipi ya uzazi kwa mwanamke inafanya kazi sawa na mrija wa manii kwa mwanaume?

  1. Ovari 
  2. Uterusi 
  3. Seviksi 
  4. Mrija wa Falopia 
  5. Uke


13. Kwa nini maziwa ya mama ni umuhimu kwa mtoto?

  1. Yana jotoridi sawa na jotoridi la mama.
  2. Yana virutubisho na viini vya kinga ya asili.
  3. Yana jotoridi sawa na maziwa yaliyochemshwa.
  4. Hayana viini vya kuambukiza magonjwa. 
  5. Yanapatikana muda wowote yakihitajika.


14. Ipi ni kazi ya mifupa?

  1. Kulinda misuli.
  2. Kutengeneza chembehai za damu.
  3. Kutengeneza chumvi.
  4. Kulinda mfumo wa damu. 
  5. Kulinda ngozi.


15. Vyanzo vikuu vya protini ni vipi'?

  1. Maziwa, nyama na mayai.
  2. Maziwa, samaki na mboga mboga.
  3. Maziwa, samaki na matunda.
  4. Maziwa, nyama na karoti.
  5. Maziwa, samaki na mahindi.


16. Ipi kati ya zifuatazo Sio kazi ya mate mdomoni?

  1. Kumeng'enya protini.
  2. Kumeng'enya wanga.
  3. Kulowesha chakula.
  4. Kulainisha chakula. 
  5. Kuwezesha umezaji wa chakula


17. Nini chanzo cha ugonjwa wa kisukari?

  1. Ukosefu wa homoni ya thairoidi.
  2. Ukosefu wa homoni ya adrenali.
  3. Hitilafu katika tezi ya thairoidi.
  4. Hitilafu katika tezi ya pituitari.
  5. Hitilafu katika tezi ya kongosho.


18. Ipi ni kazi ya ukutaseli katika mmea?

  1. Kutofautisha sehemu za chembehai ya mmea.
  2. Kufanya chembehai ya mmea kuwa Iaini.
  3. Kuunda umbo la chembehai ya mmea.
  4. Kuzuia maji yasitoke kwenye mmea. 
  5. Kuwezesha mmea kusanisi chakula.


19. Popo yuko katika kundi gani la wanyama?

  1. Mamalia 
  2. Reptilia 
  3. Ndege
  4. Bundi 
  5. Amfibia


20. Ni ushauri upi haumfai mwathirika wa UKIMWI

  1. Kutumia dawa kama ilivyoelekezwa na daktari.
  2. Kuwa na wapenzi wasio na UKIMWI.
  3. Kujikubali na kuelimisha wengine.
  4. Kuishi kwa matumaini na kujijali.
  5. Kula mlo kamili na kupima afya mara kwa mara.


21. Ni njia gani itumike ili kupunguza maambukizi ya VVU

  1. Kutenga maeneo maalum ya kuishi watu wenye VVU.
  2. Kutokuchangia chakula na watu wenye VVU.
  3. Kula mlo kamili na kunywa maji salama.
  4. Kubadili tabia na kuacha ngono zisizo salama. 
  5. Kufanya mazoezi ya viungo.


22. Vitu vifuatavyo vinaweza kupitisha joto isipokuwa

  1. waya 
  2. Hewa 
  3. Plastiki 
  4. Msumari 
  5. Maji


23. Katika nyenzo daraja la kwanza egemeo huwa sehemu gani?

  1. Nyuma ya jitihada. 
  2. Pembeni mwa mzigo.
  3. Mbele ya jitihada. 
  4. Sawa na gurudumu. 
  5. Katikati ya mzigo na jitihada.


24. Kwa nini mashine ni muhimu katika maisha ya kila siku?

  1. Hutumika kuongeza nguvu. 
  2. Hutumika kurahisisha kazi.
  3. Hutumika kubeba mizigo. 
  4. Hutumika kuimarisha misuli. 
  5. Hupunguza maumivu ya viungo.


25. ?pi kati ya vitu vifuatavyo ni mashine rahisi?

  1. Uwenzo
  2. Winchi 
  3. Baiskeli
  4. Gari 
  5. Pikipiki


26. Unawezaje kutofautisha sumaku na aina nyingine za maada? 

  1. Sumaku ina nguvu zaidi ikilinganishwa na maada nyingine.
  2. Sumaku ina uwezo wa kunasa vitu vya chuma.
  3. Sumaku imeundwa kwa chuma cha pua.
  4. Sumaku ni nzito kuliko maada nyingine. 
  5. Sumaku ina rangi nyeusi.


27. Ikiwa mashine inabeba mzigo wa nyutoni 60 kwa jitihada ya nyutoni 75, nini manufaa ya kimakanika?

  1. 450 
  2. 4500 
  3. 8
  4. 0.8 
  5. 1.25


28. Kifaa kipi hutumika kupima mkondo wa umeme?

  1. Kikinza 
  2. Swichi 
  3. Amita
  4. Voltimita 
  5. Testa


29. Hafizi alipotumbukiza kipande cha chuma kwenye kopo liliyojaa maji, kiasi cha sm 100 za maji kilimwagika. Maelezo yapi ni sahihi kuhusu tendo hili la kisayansi? 

  1. Kiasi cha maji yaliyomwagika ni sawa na kilichobaki katika ndoo.
  2. Ujazo wa jiwe ni sawa na ujazo wa maji yaliyomwagika.
  3. Maji yaliyomwagika ni mazito kuliko jiwe.
  4. Jiwe ni zito kuliko maji yaliyomwagika.
  5. Maji yaliyomwagika na jiwe vina uzito sawa.


30. Ni kwa namna gani mtu anayetokwa na damu puani huhudumiwa?

  1. Kwa kulazwa chini kifudifudi.
  2. Kwa kuwekewa kitambaa nyuma ya kichwa.
  3. Kwa kuwekewa kitambaa chenye maji ya vuguvugu usoni.
  4. Kwa kuwekewa kipande cha pamba sikioni. 
  5. Kwa kuminywa pua kwa dakika chache.


31. Nini kifanyike ili kumsaidia mwanafunzi anayetapika?

  1. Kumpa maji yenye chumvi na sukari.
  2. Kumlaza na kuita muuguzi ili apate tiba.
  3. Kumpumzisha kivulini.
  4. Kumpa chakula laini. 
  5. Kuita wazazi wake.


32. ?pi ni hatua ya mwisho katika ufanyaji wa jaribio la kisayansi?

  1. Kuweka lengo. 
  2. Kuandika hitimisho. 
  3. Kubainisha njia. 
  4. Kuandaa vifaa. 
  5. Kutoa matokeo.


33. Ni njia gani ya kisayansi inatumika ili kupatajibu sahihi lajaribio?

  1. Kuandaa dodoso. 
  2. Kukusanya taarifa.
  3. Kufanya uchunguzi. 
  4. Kujibu maswali. 
  5. Kufanya majadiliano.


34. Utabiri kuhusu chanzo cha tatizo linalotarajiwa kufanyiwa uchunguzi hujulikana kama

  1. jaribio 
  2. data 
  3. matokeo 
  4. dhanio 
  5. hitimisho


35. Chunguza Kielelezo Namba I kisha jibu swali linalofuata:

Ni kemikali gani itakayokuwa katika bika baada ya asidi yote kuungana na besi?

  1. Maji na asidi. 
  2. Magadi soda. 
  3. Chumvi na besi. 
  4. Sukari na maji. 
  5. Chumvi na maji.


36. Sifa ipi inahusu badiliko la kikemikali?

  1. Rangi ya dutu mpya iliyoundwa ni sawa na ya elementi.
  2. Dutu mpya haiwezi kurudia hali yake ya awali.
  3. Dutu mpya inaweza kuungana na maji kutengeneza asidi.
  4. Hakuna dutu mpya inayoweza kuundwa.
  5. Dutu mpya inaweza kuungana na asidi kutengeneza chumvi.


37. Kwa nini 'moshi' hutokea mdomoni unapopumua wakati wa hali ya baridi?

  1. Joto katika hewa ya nje ni nyevu.
  2. Joto katika hewa ya nje ni dogo.
  3. Hewa ya baridi haina unyevu.
  4. Jotoridi la nje ni chini ya 00C.
  5. Joto katika hewa ya ndani ni nyevu.


38. Ni dutu gani husababisha chuma kupata kutu?

  1. Unyevu na haidrojeni. 
  2. Kaboni na oksijeni. 
  3. Neoni na oksijeni. 
  4. Oksijeni na unyevu. 
  5. Naitrojeni na unyevu.


39. Ni rangi gani hutokea wakati maji ya chokaa yakichanganywa na gesi inayotoka wakati wa upumuaji?

  1. Njano 
  2. Bluu 
  3. Mazisva 
  4. Hudhurungi 
  5. Kijani


40. Mlinganyo upi kati ya ifuatayo umesawazwa?

  1. O2 + 2H2 → 2H2O
  2. O2 + Mg → 2MgO
  3. 2Ca + O2  → CaO
  4. 2Ca + Cl2  → 2CaCl
  5. H2O + O2 + 2H2


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2018 Try This  |  

SAYANSI - 2018

SEHEMU A

Chagua herufi ya jibe sahihi, kisha andika katika karatari ya rnajibu/kujibia.

1. Ipi jozi sahihi kati ya zifuatazo inahusu sehemu za uzazi katika mimea na wanyama?............

  1. Chavua katika mimea na manii katika wanyama
  2. Filamenti katika mimea na fallopian katika wanyama
  3. Tunda katika mimea na korodani katika wanyama
  4. Maua katika mimea na uterasi katika wanyama
  5. Mbegu katika mimea na ovari katika wanyama


2. Ili mimea iweze kuendelea kuishi katika mazingira yake inahitaji:

  1.  hewa na udongo 
  2.  hewa na maji
  3.  udongo na mbolea 
  4.  udongo na maji
  5.  jotoridi na hewa


3. Mpunga kuzaliana kwa kutumia:

  1.  majani 
  2.  mbegu 
  3.  mizizi 
  4.  mashina 
  5.  matawi


4. Kundi lipi linawakilisha wanyama wenye uti wa mgongo?

  1.  Nyoka, nge, buibui na mamba 
  2.  Konokono, nyoka, kenge na samaki
  3.  Kenge, nyoka, bulbul na samaki 
  4.  Konokono, samaki, chura na mamba
  5.  Mjusi, nyoka, kenge na mamba


5. Kiwavi ni hatua mojawapo ya ukuaji wa:

  1.  nyuki 
  2.  rnbungo 
  3.  funza 
  4.  mende 
  5.  kipepeo


6. Zipi kati ya zifuatazo ni sifa za viumbe hal?

  1. Kukua, kupumua, kusanisi chakula, kujongea
  2. Kukua, kupumua, kulala, kujongea
  3. Kukua, kupumua, kujongea na kuzaliana
  4. Kukua, kuona, kujongea na kuzaliana
  5. Kukua, kusanisi chakula, kujongea na kuzaliana


7. Umeme unasababishwa na mtiririko wa:

  1.  elektroni 
  2.  protoni 
  3.  nyutroni 
  4.  chaji 
  5.  atomi


8. Ipi kati ya zifuatazo ni sifa ya kinyonga?............

  1.  Hubadili mlio wa sauti yake 
  2.  Huchagua aina ya chakula
  3.  Hubadili rangi ya mwili 
  4.  Hatoi taka mwili
  5.  Hubadili mwendo


9. Yupi kati ya wafuatao ni mamalia?............

  1.  Konokono 
  2.  Bata 
  3.  Popo 
  4.  Mjusi 
  5.  Chura


10. Ipi kati ya zifuatazo siyo kazi ya mizizi katika mimea?..............

  1.  Kusharabu madini ya chumvi. 
  2.  Kusharabu maji
  3.  kushikilia mmea 
  4.  Kutengeneza chakula cha mmea
  5.  Kutunza chakula cha mmea


11. Gesi ipi hupunguzwa angani na mimea?..................

  1.  Kabondioksaidi 
  2.  Oksijeni 
  3.  Haidrojeni
  4.  Kabonimonoksaidi 
  5.  Naitrojeni


12. Ili maji yawe salama kwa kunywa yanapaswa kifanywa nini?

  1. Kuchemshwa na kufunikwa
  2. Kuchujwa na kuhifadhiwa
  3. kuchemshwa, kuchujwa na kuhifadhiwa
  4. kuwekwa juani kutwa nzima na kupozwa
  5. Kuwekwa kwenye mtungi na kufunikwa


13. Yafuatayo ni mahitaji muhimu kwa uhai na ukuaji wa mimea isipokuwa:

  1.  Mbolea za viwandani 
  2.  Maji
  3.  Hewa ya kabondayoksaidi 
  4.  Mwanga wa jua
  5.  Udongo wenye rutuba


14. Hewa inayohitajika kwa wanyama iii waishi ni:

  1.  Oksijeni 
  2.  Kabondayoksaidi
  3.  Nitrojeni 
  4.  Haidrojeni
  5.  Kabonimonoksaidi


15. Mtu anayekula vyakula vyenye mafuta kwa wingi anaweza kupata:

  1.  beriberi 
  2.  Kifafa
  3. Shinikizo la juu la damu 
  4.  Kisukari
  5.  Shinikizo la chini la damu


16. Ugonjwa unaosababishwa na hitilafu katika chembe hai nyekundu za damu huitwa:

  1.  beriberi 
  2.  selimundu 
  3.  saratani ya damu
  4.  kisukari 
  5.  kifua kikuu


17. Ni gesi ipi hupungua katika chumba kilichofungwa madirisha wakati kina moto wa mkai. 

  1.  Haidrojeni 
  2.  Kabonimonoksaidi
  3.  kabondayoksaidi 
  4.  Oksijeni 
  5.  Natrojeni


18. Ni kitu gani tunaweza kutumia iii tunaweza kuona taswira zetu vizuri?

  1.  Kioo mbinuko 
  2.  Kioo mbonyeo 
  3.  Kioo bapa
  4.  Lenzi mbinuko 
  5.  Lenzi mbonyeo


19. Kwa nini ni muhimu kuosha matunda kabla ya kula?

  1.  Kuondoa sumu 
  2.  Kuondoa vimelea
  3.  Kuondoa utomvu 
  4.  Kuondoa harufu mbaya
  5.  Kuondoa chumvichumvi


20. Sehemu ipi ya mfumo wa umengenyaji chakula inahusika na umengenyaji protini? 

  1.  Mdomo 
  2.  Utumbo mwembamba
  3.  Utumbo mpana 
  4.  Umio 
  5.  Tumbo


21. Magonjwa gani husababishwa na utapiamlo?...............

  1. Unyafuzi, kwashakoo, matege, rovu.
  2. Kiribatumbo, kisukari, kikohozi, kuhara
  3. Unyafuzi, kwashakoo, kupooza, homa ya manjano
  4.  Matege, trakoma, rovu, unyafuzi
  5. Kichocho, malaria, kifua kikuu, matege


22. Ni kitu gani hupotea kwa wingi mtu anapoharisha? . . . . . . . . .

  1.  Hewa 
  2. Maji 
  3.  Protini 
  4.  Wanga 
  5.  Vitamini


23, Vipi kati ya virutubisho vifuatavyo vinafaa zaidi kwa mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano?

  1. Wanga, maji na protini
  2. Protini, vitamini na chumvichumvi
  3. Chumvichumvi, protini na Maji
  4. Vitamini, wanga na maji
  5. Kabohaidreti, maji na chumvichumvi


24. Ugonjwa upi kati ya magonjwa yafuatayo unasababishwa na bakteria?..............

  1.  Moyo 
  2.  Kifua kikuu 
  3.  UKIMWI 
  4.  kichocho 
  5.  Kisukari


25. Vitu gani kati ya vifuatavyo hupatikana kwenye gari la zima moto?.............

  1.  Tanki la mafuta, gesi ya kabondayoksaidi na maji.
  2.  Tanki la maji, gesi ya kabondayoksaidi na gesi ya oksijeni.
  3.  Kikosi cha zima moto, map na gesi ya kabondayoksaidi.
  4.  Tanki la maji, tanki la gesi ya mkaa na gesi ya asetilini.
  5.  Tanki la maji, tanki la gesi ya mchanganyiko na makoti makubwa.


26. Ipi kati ya sentensi zifuatazo inatoa maana ya huduma ya kwanza?.............

  1. Msaada wa haraka anaopewa mtu kabla ya kwenda hospitali.
  2. Msaada wa haraka anaopewa mtu baada ya kufika hospitali.
  3. Msaada wa haraka unaotolewa kwa mtu na mtaalamu wa afya.
  4. Msaada unaotolewa kwa mtu aliyezirai.
  5. Msaada unaotolewa kwa mtu aliyeumwa na nyoka.


27. Je nini utakachokifanya ikiwa utaona nguo alizovaa rafiki yako zinaungua kwa moto?..........

  1. Kumpaka mafuta
  2. Kumweka maji kwenye jeraha
  3. Kumfunika kwa blanketi au nguo nzito
  4. Kumpulizia hewa ya oksijeni
  5. Kumvua nguo zilizokwisha ungua


28. Zipi kati ya zifuatazo hazichangii kuenea kwa VVU?.............

  1. Ngono, ulevi, kunyonyesha mtoto
  2. Kuchangia sindano, kuwekewa damu yenye VVU
  3. Kushikana mikono, kucheza, kula pamoja
  4. Elimu duni kuhusu UKIMWI na ngono zembe
  5. Uasherati na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya


29. Ni kwa nini watu wanaoishi na VVU wanahitaji vyakula vyenye virutubisho zaidi?

  1. Ugonjwa wao ni wa mda mrefu.
  2. Maisha yao ni mafupi hivyo wanahitaji chakula cha kutosha.
  3. Wanapata njaa kila wakati.
  4. Wanahitaji kuimarisha kinga ya mwili.
  5. Wanahitaji kunenepa iii kuepuka unyanyapaa.


30. Njia sahihi ya kumtambua mtu mwenye virusi vya UKIMWI ni:

  1. Kupima kifua kikuu.
  2. Kupima mwenendo wa joto la mwili.
  3. Kuangalia kama amekonda kwa mda mfupi.
  4. Kuangalia kama ana vidonda mdomoni na usoni.
  5. Kupima kiwango cha kinga kwenye damn.


31. Ni kitendo kipi kinaonesha kuwa hewa huchukua nafasi?

  1. Kupumua kupitia mdomoni na puani.
  2. Mapovu ya hewa kutokea chupa ya maji inayozamishwa ndani ya maji.
  3. Kupiga chafya na kukohoa kwa mda mrefu.
  4. Mvuke unapopita hewani.
  5. Kutumbukiza jiwe ndani ya kopo chirizi na maji kumwagika.


32. Chunguza Kielelezo Namba 1 kisha jibu swali linalofuata

  1. II
  2. IV
  3. III
  4. I
  5. V


33. Nini kitatokea endapo bilauri iliyojazwa maji na kufunikwa kwa mfuniko wa itageuzwa juu chini?

  1.  Maji yatamwagika 
  2.  Mfuniko utatoka
  3.  Bilauri itapasuka 
  4.  Maji hayatamwagika
  5.  Maji yatachuruzika


34. Ni hatua gani muhimu utachukua baada ya kubaini tatizo katika jamii?

  1. Kuanza uchunguzi wa kina 
  2.  Kubuni dhanio
  3.  Kuandaa dodoso 
  4.  Kuandaa majaribio ya kisayansi
  5.  Kukusanya taarifa na data


35. Upi ni mpangilio sahihi wa kuandika ripoti ya jaribio la kisayansi?

  1. Lengo, njia, vifaa, matokeo, hitimisho
  2. Vifaa, lengo, njia, matokeo, hitimisho
  3. Njia, lengo, vifaa, hitimisho, matokeo
  4. Njia, lengo, hitimisho, matokeo, vifaa
  5. Lengo, vifaa, njia, matokeo, hitimisho


36. Ni kwa namna gani chuma huweza kuzuiwa kisipate kutu?.................

  1.  Kwa kukipaka majivu 
  2.  Kwa kukiosha na maji
  3.  Kwa kukipaka rangi 
  4.  Kwa kukifunika kwa udongo
  5.  Kwa kukifunika kwa masizi


37. Ipi kati ya orodha zifuatazo ni kundi la metali?................

  1.  Klorini, zinki, almasi na dhahabu
  2.  Chuma, kaboni, naitrojeni na oksijeni
  3.  Oksijeni, zinki, salfa na klorini
  4.  Shaba, chuma, kabonmonoksaidi na zinki
  5.  Dhahabu, zinki, aluminium, na silva


38. Mfano mmojawapo wa elementi ni:

  1.  maji 
  2.  chumvi
  3. hydrojeni
  4.  sukari 
  5.  kabondayoksaidi


39. Mawingu yanaposhuka na kukaribia use wa dunia huitwa:.................

  1.  ukungu 
  2.  umande 
  3.  mvuke 
  4.  barafu 
  5.  mvua


40. Chunguza Kielelezo Namba 2, kisha jibu swali linalofuata:

Herufi P inawakilisha.............

  1.  mwale mtuo 
  2.  mwale akisi 
  3.  mwale pindu
  4.  mwale sambamba 
  5.  mwale mkabala


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2017 Try This  |  

SAYANSI 2017 

Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye karatasi ya kujibia.

1. Ipi kati ya tabia zifuatazo humwezesha ndege kuruka hewani?

  1. Mifupa milaini iliyo na manyoya.
  2. Miili iliyochongoka na mifupa iliyo wazi ndani.
  3. Mfupa iliyoungana.
  4. Uwepo wa mifupa mingi.
  5. Mifupa imara ya mabawa iliyo imara.


2. Makundi makuu ya viumbe hai ni:

  1.  Mimea na ndege 
  2.  Mimea na mijusi
  3.  Wanyama na majani 
  4.  Mimea na wanyama
  5.  Wanyama na bakteria


3. Ipi kati ya aina zifuatazo za mbegu hujisambaza zenyewe?.................

  1.  Nazi na pamba 
  2. Kunde na mbaazi
  3.  Kunde na papal 
  4.  Embe na pera
  5.  Chungwa na mbaazi


4. Chunguza Kielelezo Namba 1, kisha chagua jibu lenye mpangilio sahihi wa zilizoonyeshwa kwa alama A - D.

Kielelezo Na. 1

  1. Nyuzi, uboho njano, uboho nyekundu, gegedu.
  2. Uboho nyekundu, gegedu, uboho njano, kano.
  3. Gegedu, kano, uboho njano, uboho nyekundu.
  4. Kano, njano, gegedu, uboho njano, uboho nyekur.: _
  5. Uboho njano, gegedu, kano, uboho nyekundu.


5. Chunguza Kielelezo Namba 2 kisha jibu swali linalofuata

Kielelezo Na. 2

Kifaa katika Kielelezo Namba 2 hutumia tabia ipi ya mwanga?..............

  1.  Kuakisiwa 
  2.  Mpitisho 
  3.  Mwachano
  4.  Mgeuzo 
  5.  Mtawanyiko


6. Magonjwa yapi kati ya yafuatayo huzuiliwa kwa chanjo?................

  1.  Surua na kifaduro 
  2.  Kichocho na malaria
  3.  Kuhara na mkamba 
  4.  Ukimwi na kisukari
  5.  Kifua kikuu na tetekuwanga


7. Kitu gani muhimu mwanamke mjamzito anapaswa kuzingatia?...............

  1. Kula chakula kingi cha wanga anapokaribia muda wa kujifungua
  2. Kufanya kazi ngumu ili awe mkakamavu.
  3. Kuhudhuria kliniki na kula mlo kamili.
  4. Kulala mara kwa mara.
  5. Kutumia sabuni zenye manukato wakati wote.


8. Ugonjwa unaotokana na tatizo la upumuaji ni 

  1.  pumu 
  2.  malaria kali 
  3.  kuzimia
  4.  kifafa 
  5.  kisukari


9. Kitu gani kitatokea endapo mfumo wa fahamu utasimama kufanya kazi?.............

  1. Mtu ataanza kutetemeka.
  2. Mtu ataanza kuhisi udhaifu.
  3. Mtu ataanza kuhisi maumivu makali mwilini.
  4. Kukosekana kwa mawasiliano ndani ya mwili.
  5. Mtu ataanza kupungua uzito.


10. Mojawapo ya dalili za unyafuzi ni.....................

  1. uso kufanana na wa mzee
  2. macho meupe na mafua 
  3. tezi ya shingo kuvimba
  4. kuhisi baridi na kutapika 
  5. tumbo kubwa na kuvimba miguu


11. Njia za uzazi wa mpango ambazo ni salama kwa afya ya mama ni.............

  1. kitanzi na sindano 
  2. njia ya asili
  3. sindano na vidonge 
  4. vidonge na kondomu
  5.  kondomu na sindano


12. Njia bora ya kuepuka utapiamlo ni ..............

  1. kutumia dawa za kinga mara kwa mara.
  2. kuelimisha jamii juu ya matumizi ya mlo kamili.
  3. kula mboga za majani kwa wingi.
  4. kutumia madawa ya kuongeza virutubisho mwilini.
  5. kuongeza idadi ya milo kwa siku.


13. Mtu aliyepigwa na shoti ya umeme anaweza kusaidiwa kwa kutumia ..................

  1.  miguu 
  2.  kipande cha chuma 
  3.  ubao mkavu
  4. mikono 
  5. ubao mbichi


14. Vipande viwili vya ubao safi vilivyofungwa kwenye sehemu mfupa ulipovunjika husaidia

  1. kuzuia kutokwa damu
  2. kukipa joto kidonda. 
  3. kuimarisha sehemu iliyovunjika.
  4. kutibu sehemu iliyovunjika. 
  5. kuunganisha sehemu iliyovunjika


15. Gesi inayotumika kuzima moto ni ................

  1.  haidrogeni 
  2.  kabondayoksaidi 
  3.  naitrojen
  4.  kaboni 
  5.  oksijeni


16. HIV haienezwi kwa ......

  1.  kujamiiana 
  2.  kuchangia sindano 
  3.  kuumwa na mbu
  4.  kuchangia nyembe 
  5.  kuwekewa damu


17. Uhusiano kati ya magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana na UKIMWI ni kwamhz

  1. Ni rahisi kupata maambukizi ya UKIMWI kama umeambukizwa magonjwa yato-,na kujamiiana.
  2. Magonjwa yanayoenezwa kwa kujamiiana ni sawa na UKIMWI.
  3. Dawa za kutibu magonjwa yanayoenezwa kwa kujamiiana zinaweza kutumik,aUKIMWI.
  4. Magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana na UKIMWI yanaenezwa -- kujamiiana pekee.
  5. Majongwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana na UKIMWI yanatibika.


18. Ipi kati ya sentensi zifuatazo ina maana sahihi ya UKIMWI?...............

  1.  Kupoteza kinga ya mwili,
  2.  Kinga kubwa ya mwili.
  3.  Kukosekana kwa kinga mwilini 
  4.  Upungufu wa kinga mwilini.
  5.  Uwezo wa kinga ya mwili.


19. Mbinu mojawapo ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni...............

  1. kutenga eneo la watu wenye virus! vya UKIMWI.
  2. kuepuka kushirikiana vifaa vya chakula na watu wenye virusi vya UKIMWI.
  3. kula chakula bora na kunywa mail safi.
  4. kubadili tabia na kuepuka ngono zembe.
  5. kufanya mazoezi ya mwili.


20. Vitu vilivyorushwa angani hurudi chini.............

  1.  kwa sababu ya uzito 
  2.  kwa sababu ya nguvu ya msuguano
  3.  kwa sababu ya nguvu ya hewa 
  4.  kwa sababu ya nguvu ya sayari
  5.  kwa sababu ya nguvu ya uvutano


21. Uhusiano kati ya sumaku na umeme ni................

  1. Chanzo cha sumaku ni nguvu ya atomiki
  2. Umeme huzuia mvutano wa sumaku.
  3. Popote penye usumaku pana umeme.
  4. Popote penye umeme pana usumaku.
  5. Sumaku huzuia umeme.


22. Kielelezo Namba 3 kinaonyesha mfano wa mashine rahisi. Ipi nafasi ya egemeo mashine inapofanya kazi?

 Kielelezo Na. 3

  1. K
  2. I
  3. J
  4. H
  5. N


23. Kipimo cha nguvu ni...

  1.  Mita 
  2.  Kilogramu 
  3.  Jouli
  4.  Kilomita 
  5.  Nyutoni


24. Kifaa kipi hutumika kupima jotoridi la mwili wa binadamu?

  1.  Kipima joto 
  2.  Galvanometa 
  3.  Ameta
  4.  Mizani 
  5.  Voltimeta


25. Vifuatavyo ni vyanzo vya umeme isipokuwa 

  1.  betri 
  2.  seli kavu 
  3.  glopu
  4.  jenereta 
  5.  sumaku


26. Nini maana ya msuguano?.

  1. Nguvu inayozalisha mwendo.
  2. Nguvu inayosimamisha mwendo.
  3. Nguvu inayosababisha mwendo.
  4. Nguvu inayoongeza kasi ya mwendo.
  5. Nguvu ya kulazimisha.


27. Ipi ni orodha ya vifaa vilivyopo katika kundi la mashine tata?................

  1. Kufuli, nyundo na mkasi
  2. Toroli, wembe na nyundo
  3. Wembe, kufuli na baiskeli
  4. Cherehani, kufuli na baiskeli
  5. Wembe, kufuli na toroli


28. Taarifa ya majaribio ni muhimu kwa sababu hutumika kufanya yafuatayo isipokuwa.............

  1. kulinganisha matokeo ya jaribio moja na jingine.
  2. kutoa taarifa ya jaribio.
  3. kutumika kama rejeo kwa mtaalamu mwingine.
  4. kuwezesha majaribio mengine kufanyika.
  5. kutoa taarifa isiyothibitishwa.


29. Kipi kati ya vifuatavyo ni mambo matano yanayounda ripoti ya kisayansi?...............

  1. Hojaji, vifaa, njia, kusudi na hitimisho.
  2. Nadharia tete, hojaji, vifaa, matokeo na hitimisho.
  3. Hojaji, vifaa, mfano, matokeo na hitimisho,
  4. Kusudi, mfano, seti zana, matokeo na hitimisho.
  5. Kusudi, vifaa, njia, matokeo na hitimisho.


30. Ili kupata nadharia kwa majaribio ya kisayansi lazima kuwepo na ...............

  1.  jaribio 
  2.  data 
  3.  taarifa
  4.  vifaa 
  5.  tatizo


31. Katika wenzo mzigo wa kilo 50 uliwekwa mita 3 kutoka katika egemeo. Nini umbaliunaohitajika kutoka katika egemeo kuweka jitihada ya kilo 20 ili kuleta mizani sawia?

  1.  1.6 m 
  2.  6.7 m 
  3.  7.5 m
  4.  2.5 m 
  5.  3 m


32. Upungufu wa damu husababishwa na...

  1. kupungua kwa sell nyekundu, madini ya chuma na vitamini
  2. kupungua kwa vitamini, protini na plazma
  3. kuongezeka kwa maji mwilini, kupungua kwa madini ya chuma na protini
  4. kuongezeka kwa utegili, madini ya chuma na vitamini
  5. kupungua kwa madini ya chuma, vitamini na protini katika chakula


33. Mwale wa mwanga unaosafiri katika mstari mnyoofu uligonga kitu kisha ukatuakioo bapa. Je nini sifa za taswira itakayotengenezwa katika kioo? ....... ...............

  1. Picha itakuwa imesimama wima.
  2. Picha itakuwa ya rangi.
  3. Picha itakuwa imepinduka.
  4. Picha itakuwa sawa na kifaa.
  5. Picha itakuwa kubwa kuliko kifaa.


34. Mtu ambaye mlo wake unakosa madini joto huenda akapata ugonjwa unaoitwa ......

  1.  beriberi
  2.  kororo
  3.  upungufu wa damu 
  4.  trakoma 
  5.  matege


35. Elementi zinazopatikana katika chumvi ya mezani ni.................

  1.  Potasiamu na klorini 
  2.  sodiamu na klorini
  3.  Potasiamu na sodiamu 
  4.  sodiamu na salfa
  5.  kalisiamu na magnesiamu


36. Zuzu alitumbukiza jiwe kwenye ndoo iliyojaa maji. Kiasi cha 5000 sm3 za majinje. Kanuni gani ni sahihi kuhusu tendo hili la kisayansi?...... ..........

  1. Maji yaliyomwagika nje ni sawa na yale yaliyobaki ndani ya ndoo.
  2. Ujazo wa jiwe ni sawa na ujazo wa maji yaliyomwagika nje.
  3. Maji yaliyomwagika nje ni mazito kuliko jiwe.
  4. Jiwe ni zito kuliko maji yaliyomwagika nje.
  5. Maji yaliyomwagika nje na jiwe yana uzito sawa.


37. Upofu wa usiku ni kasoro inayosababishwa na ukosefu wa ............

  1. vitamini K 
  2.  vitamini A
  3. vitamini E
  4.  vitamini C 
  5.  vitamini B


38. Maada huundwa na chembechembe ndogo zinazojulikana kama

  1.  kizio 
  2.  ambatani
  3.  elementi
  4.  atomu 
  5.  molekuli


39. Kiwango cha mvuke hewani hupimwa kwa..............

  1.  Barometa 
  2.  Haidromita
  3.  anemomita
  4.  Ameta 
  5.  Kipima joto


40. Ili chuma ipate kutu inahitaji unyevu na .............

  1.  haidrojeni 
  2.  kaboni
  3.  neoni
  4.  oksijeni 
  5.  naitrojeni


41. Nini matokeo ya oksidesheni ya glukosi katika damu?................

  1. Maji oksijeni na joto
  2. Maji, joto na monoksaidi ya kaboni
  3. Nishati, maji na kaboni
  4. Umande, joto na kaboni dioksaidi
  5. Oksijeni, nishati na jasho


42. Hi kupata chumvi kutoka kwenye maji lazima maji..............

  1.  yagandishwe 
  2.  yafukishwe
  3.  yapoozwe
  4.  yachemshwe 
  5.  yamiminwe


43. jaribio la kisayansi linalofanyika iii kuhakiki ukweli wa matokeo ya jaribio lingine la kisayansi linaloendelea huitwa

  1.  jaribio maalumu 
  2.  jaribio la kumbukumbu
  3.  jaribio la dhibiti 
  4.  jaribio la mfano
  5.  jaribio la hitimisho


44. Kazi ya nyongo katika mfumo wa mmengenyo wa chakula ni................

  1.  kuua vijidudu 
  2.  kuyeyusha protini
  3.  kuvunjavunja mafuta 
  4.  kuyeyusha wanga
  5.  kunyonya maji


45. Kipi kati ya vyakula vifuatavyo king wanga kwa wingi?.............

  1.  Embe 
  2.  Viazi 
  3.  Maharage ya soya
  4.   Karanga 
  5.  Samaki


46. Viungo vipi huimarishwa kwa madini ya kalisiamu na vitamini D?...................

  1.  Ulimi na pua 
  2.  Ngozi na tumbo 
  3.  Mifupa na meno
  4.   Mapafu na Ini 
  5.  Figo na kibofu


47. Ipi kati ya vifuatavyo siyo sehemu ya damu?...............

  1.  Chumvi 
  2.  Seli nyeupe 
  3.  Chembe sahani
  4.  Seli nyekundu 
  5.  Utegili


48.Endapo kabonidayoksaidi itaunganishwa na maji kikemikali katika mmea pakiweponishati ya mwanga tutapata.......... .............

  1. kabohaidreti na maji
  2. kabohaidreti na oksijeni
  3. kabohaidreti na nishati joto
  4. kabohaidreti na umbijani
  5. kabohaidreti na kabonidayoksaidi


49. Aina ya mnyoo unaosambaza matende unajulikana kama ............

  1.  minyoo mviringo 
  2.  tegu 
  3.  filaria
  4.  jongoo 
  5.  bakteria


50. Sehemu ya mmea inayofyonza maji inaitwa............

  1.  shina 
  2.  tawi 
  3.  mzizi
  4.  ua 
  5.  jani


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2016 Try This  |  

201 6 - SAYANSI

SEHEMU A

Chaguajibu sahihi kisha andika herufiyake kwenye karatariya kujibia.

1. Ili mbegu ichipue inahitaji: 

  1. Maji, udongo na hewa
  2. Mvua, hewa na udongo
  3. Unyevu, udongo na jotoridi
  4. Maji, hewa na jotoridi
  5. Maji, mwanga na upepo


2. Wadudu wanapohama toka ua moja kwenda lingine wanfanya hivyo ili:

  1. kuzalisha mimea  
  2. kuepuka maadui
  3. kutafuta nekta 
  4. kutafuta harufu 
  5. kusambaza mbegu


3. Hali ya mtu kuzimia hutokana na ukosefu wa damu katika .......

  1. Tumbo
  2. Figo
  3. Mapafu
  4. Moyo
  5. Ubongo


4.  Aina kuu mbili za mashine ni:

  1. ngumu na laini
  2.  rahisi na tata
  3. za kumenya na kutwanga 
  4. puli na roda
  5. roda na katapila


5. Mojawapo ya njia za kuondoa takamwili katika mwili ni:

  1.  kutema mate 
  2.  kukojoa
  3. kuoga 
  4. kunawa mikono 
  5. kutoa machozi


6. Mbegu ya kike ambayo haijarutubishwa huitwa:

  1.  kondo 
  2.  yai
  3. uterasi 
  4. ovari    
  5. mrija wa falopio


7.  Angalia kielelezo namba 1 ambapo jotoridi lioneshwa kwa nyuzi za sentigredi kisha jibu maswali yanayofuata.

Mbegu itakayoota ni ya chombo kipi?

  1.  Chombo A    
  2.  Chombo B
  3.  Chombo C    
  4.  Chombo D  
  5.  Chombo A na D


8. Sehemu zinazounda mfumo wa upumuaji katika mwanadamu ni:

  1.  pua, mdomo na tumbo
  2. mapafu, pua na ini
  3. pua, mapafu na masikio 
  4. koromeo, mapafu na kongosho
  5. mapafu, pua na mdomo


9.  Mdudu yupi kati ya wafuatao huleta hasara kwa mkulima akiwa katika hatua ya pili ya ukuaji?

  1. Inzi                                                         
  2. Kipepeo
  3. Panzi                                                    
  4. Mbungo
  5. Mbu


10. Usafirishaji wa chakula mwilini hufanywa na: 

  1. moyo     
  2. damu
  3. misuli                                     
  4. mapafu
  5. maji


11. Tazama kwa makini kielelezo namba 2 kisha jibu maswali yanayofuata:

Alama Y inawakilisha sehemu iitwayo:

  1.  petali
  2.  filamenti
  3.  chavulio
  4.  pistili
  5.  ovari


12.  Mbegu za mimea uhifadhi chakula katika:

  1.  mizizi 
  2. majani      
  3. shina
  4. kotiledoni 
  5. tunda


13. Lipi kati ya magonjwa yafuatayo huambukizwa kwa njia ya kujamiiana?

  1.  Polio  
  2.  Kipindupindu         
  3.  Pepopunda
  4.  Kaswende                            
  5.  Tetekuwanga


14. Nini kitatokea iwapo idadi ya wanyama wanaokula nyama katika eneo ni kubwa kulikc idadi ya wanaokula majani?

  1. Majani yatapungua
  2. Majani yatabakia kama yalivyokuwa awali
  3. Majani yatanyauka
  4. Majani yataongezeka
  5. Majani yataliwa


15. Lipi kati ya mafungu yafuatayo ya vyakula hulinda mwili?

  1.  Samaki na maziwa          
  2.  Ugali na ndizi
  3.  Maharagwe na karanga 
  4.  Mayai na kabichi 
  5.  Matunda na mboga za majani


16. Umuhimu wa asidi ya haidrokloric katika tumbo ni:

  1.  kubadili hali ya besi katika tumbo
  2.  kulainisha mafuta tumboni
  3.  kuongeza uchachu tumboni
  4.  kumengenya vyakula vya sukari tumboni 
  5.  kuua wadudu wanaoingia tumboni na chakula.


17. Nini tofauti kati ya malaria na homa ya matumbo?

  1.  Malaria hushambulia mishipa ya damu, homa ya matumbo hushambulia neva za fahamu.
  2.  Malaria husababishwa na mbu, homa ya matumbo husababishwa na inzi.
  3.  Malaria hutibiwa kwa siku nne, homa ya matumbo hutibiwa kwa siku saba.
  4.  Malaria husababishwa na plasmodiam, homa ya matumbo husababishwa na bakteria.
  5.  Malaria huambatana na maumivu ya kichwa, homa ya matumbo huambatana na maumivu ya uti wa mgongo.


18. Kipi kati ya vifuatavyo vinapaswa kudumishwa? 

  1. Kutumia kikombe kimoja wakati wa kunywa maji. 
  2. Kunawa mikono kabla ya mlo katika karai moja. 
  3. Kupika mboga za majani na nyama kwa muda mrefu.
  4. Kuchemsha na kuchuja maji ya kunywa. 
  5. Kuogelea katika mito na mabwawa.


19. Viungo vinavyohusika katika kutoa takamwili mwilini ni:

  1.  figo, ini na moyo            
  2.  ini, ngozi na figo 
  3.  mapafu, moyo na figo              
  4.  moyo, figo na ngozi 
  5.  Ngozi, Ini na Moyo 


20. Mbungo husababisha ugonjwa uitwao ....

  1.  homa ya matumbo     
  2.  nagana
  3. malale                                           
  4. matende                
  5. homa ya ini


21. Tunaweza kujikinga na magonjwa ya moyo kwa kufanya yafuatayo: .......

  1. Kula chakula na kufanya mazoezi mara kwa mara
  2.  Kufanya mazoezi ya mwili, kuepuka kuvuta sigara na kuepuka kunywa pombe
  3.  Kula chakula chenye chumvi na kunywa pombe 
  4. Kufanya mazoezi ya mwili na kuvuta sigara 
  5. Kula vyakula vyenye mafuta na kunywa pombe


22. Wanawake wajawazito wanashauriwa kula kiwango kikubwa cha vyakula vifuatavyo:

  1.  Wanga, mafuta na hamirojo
  2.  Mafuta, vitamini na protini
  3.  Protini, vitamini na madini ya chumvichumvi
  4.  Madini ya chumvichumvi na vitamini pekee 
  5. Protini, hamirojo na udongo pekee


   23. Ili kujikinga dhidi ya malaria ni muhimu .........

  1.  kumeza mchanganyiko wa madawa
  2.  kutumia dawa za mitishamba
  3.  kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa
  4.  kujifunika na blanketi Zito lililowekwa dawa 
  5.  kufanya mazoezi kila mara


24. Kongosho hutoa homoni inayothibiti kiasi cha:

  1.  damu mwilini    
  2.  sukari mwilini
  3. takamwili                                      
  4. hamu ya chakula                   
  5.  oksijeni


25.  Mojawapo ya kazi za misuli katika mwili ni:

  1.  kuwezesha kujongea
  2.  kuruhusu damu kupita 
  3.  kuruhusu maji kupita
  4. kuruhusu hewa kupita 
  5.  kuimarisha mwili


26.  Lipi kati ya mambo yafuatayo si sahihi kumfanyia mtu aliyebanwa misuli?

  1.  Kuchua eneo lililoathirika kwa kiganja
  2.  Kuchua kwa kukandamiza eneo lililoathirika hadi misuli ilegee
  3.  Kuuchua msuli kwa kitambaa na maji baridi 
  4.  Kuweka kemikali zitakazowezesha misuli kulegea
  5.  Kulala juu chini na kuchua msuli ulioathirika kvva maji moto.


27. Mtu anayetapika na kuharisha anapaswa kupewa:

  1.  asidi, maziwa na maji
  2.  maziwa, besi na sukari 
  3. maji, besi na maziwa
  4. chumvi, sukari na maji 
  5. sukari, asidi na besi


28. Huduma ya kwanza anayopewa mtu aliyezimia ni:

  1.  kumpa hewa ya oksijeni
  2.  kumpa juisi ya nazi mbichi
  3.  kumlaza juu chini na kumbonyeza tumbo
  4.  kumpa maji yaliyochanganywa na glukosi
  5.  kumpa juisi ya malimao, sukari na chumvi


29. Mtandao wa watu wenye virusi vya UKIMWI unatanuka kwa kuwa

  1.  matumizi ya kondom na simu za mkononi yameongezeka
  2.  matangazo kuhusu UKIMWI yameboreshwa
  3.  kuna ongezeko la mahusiano ya kingono yasiyo salama
  4.  elimu ya UKIMWI inatolewa kwa watu wachache
  5.  watu wenye UKIMWI wanazingatia kanuni za kujikinga na UKIMWI


30. UKIMWI husambazwa kwa kupitia:

  1.  kusalimiana kwa kushikana mikono na mgonjwa wa UKIMWI
  2.  kulala chumba kimoja na mgonjwa wa UKIMWI
  3.  kuongea na mwathirika wa UKIMWI 
  4.  kuwekewa damu
  5.  kuosha nguo za mwathirika wa UKIMWI.


31. Ili kuepuka kupata maambukizi mapya ya UKIMWI tunashauriwa:

  1.  kumeza dawa na kufanya mazoezi
  2.  kuwa mwaminifu na kuepuka ngono zembe
  3.  kuepuka kushirikiana na waathirika
  4.  kuepuka kula pamoja na kubadilishana nguo na waathirika 
  5.  kupata chanjo ya UKIMWI na Kifua Kikuu.


32. Nini kati ya vifuatavyo husababisha chupa ya plastiki kusinyaa hewa inapoondoleua ndani?

  1.  Hewa ndani ya chupa kuwa na mgandamizo mkubwa zaidi ya hewa nje ya chupa
  2.  Hewa nje ya chupa kuwa na mgandamizo mkubwa kuliko hewa ndani ya chupa
  3.  Mgandamizo wa nje na ndani ya chupa kulingana
  4.  Mgandamizo wa hewa ndani ya chupa kuwa pungufu ya mngandamizo wa kutoa hewa nje ya chupa
  5.  Mgandamizo nje ya chupa kuwa sawa na ujazo wa hewa mdomoni.


33. Chembe ndogo kabisa za maada zinazounda elementi na zinazohusika katika kutengenezz bondi za kikemikali huitwa:

  1.  molekyuli      
  2.  elektroni      
  3.  protoni
  4.  atomi                                     
  5.  nyutroni


34.     Mwanga hupinda unapopita kutoka

  1.  Ncha ya Kaskazini kwenda Kusini      
  2.  media moja kwenda nyingine
  3.  Ncha ya Kaskazini kwenda Mashariki 
  4.  Magharibi kwenda Mashariki 
  5.  Kaskazini kwenda Magharibi


35. Tazama kielelezo namba 3 kinachoonesha muundo wa atomi.


Je, ni herufi gani inayowakilisha elektroni?

  1.  T
  2.  S
  3.  R
  4.  Q
  5.  P


36. Msuguano baina ya kifaa cha plastiki kama chana na nywele huzalisha:

  1.  oksijeni         
  2.  chaji za umeme
  3.  sumaku 
  4.  mfereji 
  5.  molekyuli za mafuta


37.  Ipi kati ya alama zifuatazo inawakilisha atomi ya klorini?

  1.  K
  2.  P
  3.  Na
  4.  CI
  5.  H


38.     Hewa ya kabonidaiyoksidi hutumika kuzima moto kwasababu:

  1.  haichochei uwakaji
  2.  ni nzito kuliko hewa
  3.  haiwaki
  4.  hunyonya joto
  5.  huungana na oksijeni


39. Ipi kati ya zifuatazo ni kazi za sumaku?

  1.  Kutengeneza uga sumaku na kunyanyua mizigo
  2.  Kuzalisha umeme na kuunda dira
  3.  Hutumika katika vipaza sauti na hutengeneza uga sumaku
  4.  Kuvuta ncha ya kaskazini na kuzalisha umeme 
  5.  Kuonesha mwelekeo na kuundia spika.


40.  Tafuta umbali kati ya mzigo na egemeo katika wenzo iwapo mzigo wa gramu 50, utanyanyuliwa kwa jitihadi ya Nyutoni 100 iliyo katika umbali wa sm 40 kutoka katika egemeo.

  1.  sm75 
  2. 1500 
  3.  sm 140        
  4.  sm 80   
  5.  sm 12.5


41.  Aina kuu mbili za sakiti za umeme ni:

  1. mkondo geu na mnyoofu
  2. sambamba na mfuatano
  3.  mkondo geu na sambamba
  4. mkondo mnyoofu na mkondo geu
  5. mkondo mnyoofu na sambamba


42. Mifupa imeundwa kwa madini ya:

  1. Sodiamu na kalsiamu
  2. Kalsiamu na oksijeni
  3. Fosforasi na kalsiamu 
  4.  Salfa na fosforasi
  5.  Kalsiamu na chuma 


43.  Asidi ikiungana na besi huunda:

  1. chumvi na maji
  2. kaboneti ya sodiamu
  3. chumvi na besi
  4. maji na asidi
  5. chumvi na oksijeni


44. Iwapo mashine yenye mzigo wa kgf 90 huhitaji jitihadi ya kgf 15, ni nini manufaa ya kimakanika?

  1.  15 
  2.  10   
  3.   8
  4.  6
  5.  5


45.    Sumaku inaweza kuvuta vitu vyenye asili ya:

  1.  mpira     
  2.  udongo  
  3.  madini  
  4. karatasi 
  5. chuma


46.Kitendo cha bakteria kuozesha kinyesi cha wanyama kwenye shimo pasipokuwa na hewa ya oksijeni husababisha:

  1.  joto kali 
  2.  gesivunde/biogesi
  3.  asidi kali               
  4.  alkali kali        
  5.  haidrojeni


47.Je ni sehemu ipi ya jicho ambamo taswira hutengenezwa?

  1.  Irisi      
  2.  Lenzi    
  3.  Kano 
  4.  Filim    
  5.  Retina


48.Katika kurunzi, nishati ya umeme inayotoka kwenye betri hubadilishwa na kuwa:

  1.  nishati ya kikemikali  
  2.  nishati ya joto
  3.  nishati ya kimakaniki     
  4.  nishati ya mwanga 
  5.  Nishati ya moto


49.Nini maana ya dhanio katika utafiti wa kisayansi?

  1.  ni wazo tu
  2.  ni utabiri wa matokeo ya kubuni 
  3.  utabiri wa matokeo ya jaribio
  4.  wazo la kina       
  5.  mawazo yaliyojengwa kabla ya utafiti


50.Mojawapo ya hatua za kufuata unapoandaa jaribio la kisayansi ni: 

  1.  uchunguzi    
  2.  udadisi
  3.  utambuzi wa tatizo    
  4.  utatuzi wa tatizo
  5.  kuandaa ripoti


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2015 Try This  |  

2015 -SAYANSI

Chaguajibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye karatariya kujibia.

1. Lipi kati ya makundi yafuatayo linawakilisha sifa za viumbe hai?

  1. Kufa, kula na kuona
  2. Kufa, kuzaa na kubadilika rangi 
  3. Kupumua, kuishi na kusikia 
  4. Kupumua, kuzaa na kutembea.
  5. Kujongea, kupumua na kuzaa.


2. Mbegu chotara kwa wanyama na mimea ni bora kwa sababu gani?

  1. Hurefuka sana na hazihitaji mbolea.
  2. Hutoa mazao mengi na hustahimili magonjwa.
  3. Hukomaa haraka na hutoa mazao yenye uzito mkubwa. 
  4. Hazihitaji virutubisho na hustahimili magonjwa. 
  5. Hukomaa haraka na hazihitaji dawa.


3. Lipi kati ya makundi yafuatayo ni sifa zinazotumika kutambua wanyama wa kundi la reptilia?

  1. Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kuishi majini. 
  2. Kutaga mayai, kuishi majini na kuishi nchi kavu.
  3. Kutaga mayai, kuwa na damu ya joto na kuishi nchi kavu.
  4. Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kupumua kwa kutumia mapezi.
  5. Kutaga mayai, kupumua kwa kutumia ngozi na kuishi majini.


4. Damu huchukua oksijeni na kutoa kabondayoksaidi kupitia:

  1. Viribaehewa 
  2. Kuta za mapafu
  3. Koromeo
  4. Kapilari
  5. Pua


5. Kukosekana kwa chanikiwiti katika mmea huweza kusababisha:

  1. mmea kukosa madini joto
  2. mmea kushindwa kusanisi chakula
  3. majani ya mmea kukauka 
  4. majani ya mmea kuwa njano
  5. maj ani ya mmea kupukutika.


6. Fototropizimu ni kitendo cha mmea kuota kuelekea kwenye:

  1. mwanga 
  2. kani ya mvutano 
  3. maji 
  4. giza
  5. kemikali.


7. Sehemu ya chembe hai inayohusika na kutawala shughuli zote za chembe hai huitwa:

  1. saitoplazimu 
  2. vakuoli
  3. kloroplasti 
  4. kiwambo cha seli
  5. nyukliasi


8. Kielelezo kifuatacho kinaonyesha viumbe hai wenye sumu isipokuwa

  1.    
  2.    
  3.    
  4.    
  5.    


9. Tendo Ia mimea kusafirisha maji kutoka kwenye mizizi hadi kwenye majani huitwa:

  1. osmosis 
  2. difyusheni 
  3. msukumo
  4. mgandamizo 
  5. mjongeo


10. Ni tezi ipi kati ya zifuatazo huratibu utendaji wa tezi zingine zote katika mwili wa binadamu?

  1. Kongosho. 
  2. Pituitari
  3. Thairoidi
  4. Adrenali 
  5. Parathairoidi


11. Sehemu ya kike ya ua inayohusika na uzazi ni:

  1. stameni 
  2. staili 
  3. ovari
  4. Petali
  5. Sepali


12. Tofauti kati ya tunda na mbegu ni: 

  1. Mbegu ina tunda.
  2. Tunda huota.
  3. Tunda lina kotiledoni mbili. 
  4. Mbegu huota. 
  5. Mbegu haziliwi.


13. Mambo muhimu kwa ajili ya afya na uhai ni:

  1. kucheza mpira wa miguu, kuoga, kufua nguo na kula sana.
  2. kula, kuwa msafi, kupumzika na kucheza.
  3. kufanya mazoezi, kula chakula bora, kupumzika na kuwa msafi.
  4. kula mayai, kuburudika, kulala na kusafisha mazingira.
  5. kuoga, kula na kulala.


14. Vyakula vyenye kabohaidreti huwezesha mwili:

  1. kuhimili magonjwa
  2. kuwa na joto
  3. kukua kwa haraka 
  4. kuwa na nguvu 
  5. kuwa mwororo


15. Kati ya yafuatayo ni yapi magonjwa yasiyoambukiza?

  1. Malaria, mafua na kisukari.
  2. Pumu, kisukari na kipindupindu.
  3. Kichocho, safura na matende
  4. Kuhara, homa ya matumbo na pumu
  5. Pumu, kifafa na tetekuwanga.


16. Mapumziko baada ya kazi ni muhimu kwa sababu gani?

  1. Mwili hupoa. 
  2. Mwili hutulia.
  3. Mwili hurejesha nishati. 
  4. Mwili hufanya shughuli nyingine.
  5. Mtu hupata fursa ya kulala.


17. Magonjwa yanayozuilika kwa kutumia chanjo ni :

  1. Pumu, kifaduro, malaria na kipindupindu 
  2. Kifua kikuu, malaria, pumu na surua
  3. Surua, dondakoo, kifua kikuu na kifaduro
  4. Malaria, surua, kifua kikuu na kipindupindu
  5. Dondakoo, kifua kikuu, UKIMWI na surua


18. Wakazi wa Mlalo hula maharage, nyama na wali kwa afya zaidi wanahitaji kuongeza:

  1. samaki 
  2. mboga za majani
  3. kuku
  4. mkate
  5. kunde


19. Kipi kati ya vifuatavyo kinaweza kupungua mwilini kwa kushiriki katika michezo na mazoezi?

  1. Sukari 
  2. Protini 
  3. Sumu
  4. Uchafu 
  5. Fati


20. Kipi kati ya vifuatavyo siyo njia sahihi ya kujikinga na ugonjwa wa malaria?

  1. Kufyeka nyasi 
  2. Kufukia madimbwi
  3. Kutumia chandarua 
  4. Kupuliza dawa
  5. Kuchoma moto taka


21. Mazoezi ni njia mojawapo ya kupunguza:

  1. kutapika 
  2. kuzirai 
  3. kukaza kwa misuli 
  4. kuharisha
  5. kutokwa na damu puani


22. Mtoto mwenye matege amepungukiwa na vitamini:

  1. K
  2. D
  3. A
  4. B
  5. C


23. Ukosefu wa vitamini B husababisha ugonjwa wa:

  1. uti wa mgongo
  2. vidonda vya tumbo
  3. surua 
  4. trakoma 
  5. beriberi


24. Faida mojawapo ya vyakula vya protini katika miili yetu ni:

  1. kukinga dhidi ya magonjwa 
  2. kukua na kukarabati chembe hai
  3. kutia nguvu 
  4. kuongeza uzito 
  5. kutia joto


25. Huduma ya kwanza ni nini?

  1. Msaada wa dharura apewao mgonjwa na daktari.
  2. Msaadawa awali apewao mgonjwa kabla ya kupelekwa hospitali.
  3. Msaada kwa ajili ya mtu aliyeungua moto. 
  4. Msaada kwa ajili ya mtu aliyeumwa na nyoka. 
  5. Msaada kwa ajili ya mtu aliyevunjika mfupa.


26. Mojawapo ya huduma ya huduma muhimu ya kumpa mtu aliye ungua moto ni;-

  1. kummwagia maji
  2. kumfunika nguo
  3. kumwagia asidi
  4. kumfunika blanketi
  5. kumpaka asali


27. Mojawapo ya athari za kupaka mafuta kwenye jeraha la moto ni:

  1. kuongeza joto kwenye jeraha
  2. kuongeza maumivu kwenye jeraha
  3. kuruhusu hewa kupita kwenye jeraha 
  4. kusababisha vijidudu kuingia kwenye jeraha 
  5. kuongeza malengelenge.


28. Ni hoja ipi kati ya zifuatazo iko sahihi kuhusu WU na UKIMWI? 

  1. Kuwa na WU ni sawa na kuwa na UKIMWI
  2. Chanzo cha WU na UKIMWI ni magonjwa ya zinaa. 
  3. Ni rahisi kujikinga na UKIMWI kuliko VVU.
  4. Ukiepuka maambukizi ya VVU pia umeepuka UKIMWI.
  5. Mtu mwenye WU hana chembe nyeupe za damu.


29. Moja ya vimelea vinavyoharibu chembe hai nyeupe za damu ni:

  1. Bakteria 
  2. WU 
  3. Plasmodiamu 
  4. Amiba 
  5. Kuvu


30. Kipi kati ya vifuatavyo ni maarufu kwa kuchangia maambukizi ya WU katika jamii?

  1. Uchangiaji wa sindano, miswaki, damu na ngono zembe. 
  2. Kanda za video, nyimbo, muziki na maigizo. 
  3. Televisheni, magazeti na vipeperushi kuhusu WU.
  4. Kondomu, wataalamu wa afya, semina na taasisi za UKIMWI.
  5. Tohara kwa wanaume na wanawake.


31. Virusi Vya Ukimwi hushambulia aina gani ya chembe hai katika damu?

  1. chembe sahani 
  2. chembe hai nyeupe
  3. Chembe hai nyekundu 
  4. Hemoglobini
  5. Plazima


32. Unaweza kupata sukari kutoka katika majimaji ya miwa kwa:

  1. kuchemsha kisha kuyachuja 
  2. kuchemsha kisha kuyapooza 
  3. kupooza na kugandisha 
  4. kuchemsha hadi kuvukiza
  5. kuyaweka kwenye mwanga wa jua.


33. Mtu anapokata mti kwa mbali unaona shoka likikita kwenye gogo la mti na baada ya muda kishindo hufuata. Hii inaonesha kuwa:

  1. mwanga husafiri katika mstari ulionyooka
  2. sauti husafiri polepole kuliko mwanga
  3. mwanga husafiri polepole kuliko sauti 
  4. sauti husafiri haraka kuliko mwanga
  5. sauti husafiri kwenye mstari ulionyooka.


34. Kuna tofauti gani kati ya barafu na maji? 

  1. Maji ni mazito kuliko barafu.
  2. Maji yana mshikamano mkubwa kuliko barafu.
  3. Maji yana rangi hafifu kuliko barafu.
  4. Maji yanachukua nafasi ilihali barafu haichukui nafasi.
  5. Barafu ni laini kuliko maji.


35. Mabadiliko ya maada yasiyosababisha mabadiliko katika uzito yanajulikana kama :

  1. mabadiliko ya kikemikali 
  2. mabadiliko ya kiumbo 
  3. mabadiliko ya ujazonene
  4. mabadiliko ya hali
  5. mabadiliko ya asili.


36. Myeyuko wa majivu yaliyotokana na majani ya malimao huweza kubadili rangi ya karatasi ya litmasi ya:

  1. bluu kuwa nyeupe
  2. nyekundu kuwa bluu
  3. bluu kuwa nyekundu
  4. bluu kuwa kijani
  5. nyekundu kuwa njano. 


37. Mchanganyiko wa gesi mbalimbali kwa pamoja huitwa

  1. oksijeni 
  2. haidrojeni 
  3. hewa 
  4. naitrojeni 
  5. maada.


38. Lipi kati ya yafuatayo siyo badiliko la kikemikali?

  1. Kuoza kwa takataka 
  2. Kuchacha kwa maziwa 
  3. Kuungua kwa mkaa 
  4. Kuyeyuka kwa sukari 
  5. Chuma kupata kutu.


39. Ipi kati ya jozi zifuatazo ni sahihi kuhusu lenzi? 

  1. Lenzi mbinuko hutawanya miale ya mwanga.
  2. Lenzi mbonyeo hurekebisha kutokuona karibu.
  3. Lenzi mbinuko hurekebisha kutokuona mbali. 
  4. Lenzi mbonyeo kurekebisha kutokuona mbali.
  5. Lenzi mbonyeo hukusanya miale ya mwanga.


40. Matumizi ya roda katika maisha ya kila siku ni:

  1. kunyanyua vitu vizito 
  2. kufungua vizibo vya chupa 
  3. kufunga vitu 
  4. kupunguza mwinuko
  5. kurahisisha kukata kuni.


41. Tazama alama kwenye kielelezo kifuatacho kwa makini, kisha zipe majina kwa kuzingatia zilivyopangwa kutoka upande wa kushoto.

  1. Kapasita, dynamo, seli kavu, swichi, betri
  2. Swichi, glopu, kikinza, kapasita, seli kavu 
  3. Glopu, kapasita, seli kavu, kikinza, betri 
  4. Kikinza, glopu, swichi, seli kavu, kapasita
  5. Swichi, kikinza, glopu, seli kavu, kapasita.


42. Ni kifaa gani hutumika kukuza taswira ya vionwa vidogo sana?

  1. Darubini 
  2. Hadubini 
  3. Periskopu
  4. Prizimu 
  5. Lenzi


44. Kipi kati ya vifuatavyo hakipitishi mkondo wa umeme?

  1. Mpira 
  2. Bati
  3. Shaba
  4. Chuma 
  5. Zebaki


46. Alama zifuatazo zinatumika katika sakiti ya umeme. Je, ni alama ipi inawakilisha kikinza?



47. Kanuni sahihi ya kutafuta kiasi cha kazi kilichofanyika ni: 

  1. Kazi = kani x uzito
  2. Kazi=Umbali / Muda
  3. Kazi=Kani / Muda
  4. Kazi=Kani x Umbali
  5. Kazi=Umbali / Kani


48. Taswira za sura zetu zinaweza kuonekana vizuri tunapotumia:

  1. kioo mbinuko
  2. kioo mbonyeo 
  3.  kioo bapa
  4. lenzi mbinuko 
  5. lenzi mbonyeo


49. Ni muhimu kuweka kumbukumbu za jaribio lililofanyika kwa sababu hutumika:

  1. kama rejea
  2. kutangaza umahiri wa aliyefanya jaribio
  3. kuchora jedwali Ia matokeo
  4. kurekebisha taarifa mbalimbali 
  5. katika kuleta maendeleo


50. Data za uchunguzi zilizochambuliwa huweza kuwasilishwa kwa njia ya:

  1. grafu 
  2. ripoti 
  3. kukokotoa
  4. kutafsiri 
  5. kuchora


31. Utafutaji wa njia ya kwenda India ulifadhiliwa na

  1. Vasco Da Gama 
  2. Bartholomew Diaz 
  3. Cecil Rhodes
  4. King Henry 
  5. Henry Stanley.


32. Soko kuu la watumwa Afrika Mashariki lilikuwa 

  1. Zanzibar 
  2. Mombasa
  3. Kilwa
  4. Bagamoyo
  5. Nairobi


SEHEMU C

JIOGRAFIA

Chaguajibu sahihi kisha andika herufiyake kwenye karatariya kujibia.

33.  Nchi ya Japan ina uwezo wa kufanya biashara kuliko Tanzania kwa sababu ina ...

  1.  watu wengi zaidi 
  2. eneo kubwa la biashara
  3. shule nyingi za biashara
  4. teknolojia ya juu zaidi
  5. wafanyabiashara wengi zaidi.


34.  Mchoro mkato wa ramani huonesha..

  1. mazao na mazingira
  2. sura ya nchi 
  3. mazingira ya eneo husika
  4. hali ya hewa 
  5. makazi ya watu na shughuli za kiuchumi


35.  Mlima mrefu kuliko yote barani Afrika ni .....

  1. Drakensburg 
  2. Everesti 
  3. Atlasi 
  4. Kenya 
  5. Kilimanjaro


36.  Moja kati ya zifuatazo ni sifa za picha: .....

  1. Kimo halisi huonekana.
  2. Sehemu zake zote huonekana.
  3. Umbo linaweza kupunguzwa au kuongezwa. 
  4. Rangi halisi ya kitu haionekani.
  5. Rangi ya picha haiwezi kubadilishwa.


37.  Kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari kutokana na kuyeyuka kwa barafu katika ncha za kaskazini na kusini kunaweza kusababisha....

  1.  wavuvi kuzama baharini 
  2. uharibifu wa maeneo ya pwani
  3. upungufu wa samaki 
  4. mvua za El-nino
  5. kutokea kwa tsunami.


38.  Ikiwa ni saa 12:00 jioni Tanzania ambayo ipo nyuzi 45 Mashariki, itakuwa saa ngapi Rwanda ambayo ipo nyuzi 30 Mashariki?

  1. 1:00 usiku 
  2. 2:00 usiku 
  3. 11:00 jioni 
  4. 12:00 jioni 
  5. 10:00 jioni.


39.  Madhara gani kati ya yafuatayo yanatokana na mlipuko wa volkeno? ...

  1. Kuharibika kwa miundo mbinu
  2. Kupungua kwa eneo la kilimo. 
  3. Ongezeko la maradhi ya ngozi. 
  4. Ongezeko la mvua za El-nino. 
  5. Kuongezeka kwa ukame


40.  Nchi ipi ni maarufu kwa uundaji wa meli duniani? .

  1. Urusi.
  2. Uingereza.
  3. Japani. 
  4. Ufaransa.
  5. Canada.


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2014 Try This  |  

2014 - SAYANSI

Chagua herufi ya jibu lililo sahihi, kisha andika katika karatasi ya majibu/kujibia

1.  Lipi kati ya magonjwa yafuatayo husambazwa na inzi na mende? 

  1. Tetekuwanga   
  2. Kuhara        
  3. Kifaduro
  4. Utapia mlo 
  5. Homa ya matumbo


2. ?pi kati ya yafuatayo sio sehemu ya mfumo wa damu?

  1.  Bronchiole        
  2.  Valvu                
  3.  Auriko 
  4.  Capillari              
  5.  Ateri


3. Lipi kati ya yafuatayo linapaswa kuzingatiwa kabla ya kumhudumia mgonjwa wa UKIMWI?

  1.  Vaa nguo safi 
  2.  Nawa kwa sabuni 
  3.  Vaa glovu 
  4.  Sali 
  5.  Mruhusu apumzike


4.  ?pi kati ya yafuatayo ni ?ifa ya maji safi na salama?

  1.  Yametekwa kwenye kisima.
  2.  Yamehifadhiwa na kupoozwa kwenye mtungi wa maji
  3.  Yamechujwa na kuhifadhiwa kwenye chombo safi
  4.  Yamechemshwa, yamechujwa na kuhifadhiwa kwenye chombo safi
  5.   Yasiwe na magadi mengi


5. Upi kati ya magonjwa yafuatayo hauna chanjo?

  1. Kifua kikuu 
  2.  Pepopunda 
  3. Surua
  4.  Kifaduro        
  5. Trakoma


6. Gesi inayotumiwa na mimea kutengeneza protini ni:

  1. carbondayoksaidi
  2. haidrojen
  3. oksijen
  4.  naitrojen                                         
  5.  gesi asilia


7. Kiwango cha maji kinachopotezwa na mmea huathiriwa na hali za hewa zifuatazo...

  1.  joto na unyevu     
  2.  unyevu na mwanga
  3. upepo na mwanga wa jua               
  4.  mawingu na upepo
  5. unyevu na upepo


8. Tunaweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi kwa kufanya mojawapo ya mambo yafuatayo:

  1. Kukata miti
  2. Kuongeza mbolea kwenye udongo
  3. Kuotesha nyasi 
  4.  Kuweka matuta lavenye maeneo ya mteremko
  5.  Kupanda miti 


9. Shughuli za mwanadamu kama kilimo, ufugaji wa wanyama na uchimbaji madini vyote hutegemea:

  1.  mito 
  2. chemchemi 
  3.  ardhi 
  4.  umwagiliaji 
  5.  upepo


10.  Kinyonga hujibadili rangi yake ili:

  1.  kutafuta chakula         
  2.  kupumua          
  3.  kuzaliana
  4.  kutafuta maadui                          
  5.  kujilinda dhidi ya maadui


11. Mende hupitia hatua kuu ......... katika ukuaji wake?

  1. mbili                                                                     
  2. tatu
  3. nne
  4. tano                                               
  5. sita


12. Yupi kati ya wanyama wafuatao hana uti wa mgongo?

  1.  Buibui
  2.  Popo
  3.  Paka
  4.  Mwanadamu
  5.  Kuku


13. Mojawapo ya kazi ya misuli katika mwili ni:

  1.  kuzuia kutokwa damu 
  2.  kuwezesha mwendo
  3.  kutengeneza selihai nyeupe      
  4.  kushikilia meno mahali pake 
  5.  kuiwezesha kunyooka


14. Viungo katika mifupa huwezesha .........

  1.  kuzuia mifupa kuvunjika        
  2.  mifupa iwe ya sawa
  3.  kurahisisha kujongea 
  4.  kuupa mwili umbo 
  5.  mifupa kunyooka


15. ..... hupinda unapopita kutoka maada ya aina moja kwenda nyingine.

  1.  Upinde wa mvua        
  2.  Mistari sambamba
  3.  Miale ya mwanga                                    
  4.  Lenzi                               
  5.  Mwale na lenzi


16. Mionzi ambayo hupinda zaidi mwanga unapopinda ni ile ya . ....

  1.  rangi nyekundu 
  2.  njano 
  3.  bluu iliyoiva 
  4.  bluu      
  5.  zambarau


17.   Tazama mchoro ufuatao unaoonesha sehemu za ndani za mbegu ya haragwe....

Ni sehemu ipi inayohusika na kuilinda mbegu isiharibiwe na wadudu waharibifu mabadiliko ya jotoridi? 

  1. 2
  2. 3
  3. 5
  4. 4
  5. 1


18. Anga huonekana la rangi ya bluu kwasababu .

  1.   hewa na maji ny vya rangi ya bluu
  2.   rangi nyekundu inatawanywa zaidi kuliko rangi ya bluu
  3.   uwezo wa kuona hupungua
  4.   rangi ya bluu hutawanywa zaidi ya rangi nyingine
  5.   wakati wa mawio jua huonekna kama la manjano


19. Kipi kati ya vifuatavyo hakitumii sumaku?

  1. Kipaza sauti 
  2. Simu ya mezani
  3. Redio
  4.  Simu ya mkono 
  5. Pasi


20. Kipimio cha kazi ni:

  1. kilogramu   
  2. Newton
  3. Tani
  4.  Joule  
  5. Gramu


21. Hatua ya kwanza ya utafiti wa kisayansi ni 

  1.  kuanza jaribio 
  2. kukusanya data
  3.  kutambua tatizo   
  4.  kuchanganua data
  5.  kutafsiri matokeo


22. Hatua ya tatu ya utafiti wa kisayansi ni .........

  1. kuchambua data                           
  2. kutafsiri matokeo
  3. kuandaa na kuanza jaribio             
  4. ukusanyaji wa data
  5. kutambua tatizo


23. Bahati aliweka karatasi nyekundu ya litmus kwenye myeyuko asioutambua. Rangi ya karatasi ya litmas ilibadilika na kuwa bluu.Hii inaonesha kuwa myeyuko ule ulikuwa .........

  1.  asidi 
  2.  besi 
  3.  maji 
  4.  mafuta  
  5.  spiriti


24. Matokeo ya jaribio yanaweza kuwa mojawapo ya yafuatayo:

  1.  Kweli au uongo
  2.  Yaliyochambuliwa au yasiyochambuliwa
  3.  Yenye maswali au yasiyo na maswali
  4.   Ya awali au ya kati
  5.  Ya awali au ya mwisho        


25.Nini kitatokea iwapo ncha mbili za KASKAZINI za sumaku zitaletwa pamoja?

  1.  Zitavutana kwa nguvu
  2.  Zitavutana kuelekea upande mmoja
  3.  Zitasukumana
  4.  Hakuna kitakachotokea
  5.   Zitavunjika


26.PQ ni rula ya urefu wa nusu meta. Mzigo wa gram 20 umewekwa kwenye sehemu P umbali wa meta 0.1 kutoka kwenye egemeo. lwapo mzigo M utawekwa sehemu Q umbali wa meta 0.4 kutoka kwenye egemeo, nini uzito wa M?

  1.  4g
  2.  10g    
  3.  5g
  4.  2.5g 
  5.  25g


27. Dhana ya kuakisiwa kwa mwanga inadhihirika katika moja ya vifaa vifuatavyo: 

  1.  Hadubini 
  2.  Televisheni 
  3.  Saa
  4.  Balbu 
  5.  Miwani


28.Tazama kielelezo namba 2 kinachoonesha sakiti ya umeme yenye balbu zilizounganishwa sambamba na kisha jibu maswali yafuatayo:

Iwapo balbu namba 2 itaungua, balbu namba ......

  1.  3 pekee itabaki ikiwaka 
  2.  1 na 3 zitabaki zikiwaka
  3.  1 pekee itabaki ikiwaka
  4.  1 na 3 zitaungua 
  5. 3 itaungua


29. Uwepo wa viumbehai, maji na hewa ni sifa ya sayari ipi?

  1.  Zebaki 
  2.  Mihiri 
  3.  Utaridi
  4.  Dunia 
  5. Sarateni


30.  Mhimili wa dunia umeinama katika nyuzi ... 

  1.  60 
  2. 18 1/2
  3.  32 1/2
  4.  25 1/2
  5. 23 1/2


31.  Ipi kati ya vifuatavyo huzunguka dunia toka magharibi kwenda mashariki?

  1. Jua    
  2. Nyota 
  3. Mwezi
  4.  Kimondo  
  5. Sayari


32. Mtu mwenye goita ana upungufu wa ... 

  1. madini ya kalsium 
  2. madini joto  
  3. madini ya potasiam 
  4. madini ya fosforas
  5. madini ya chaki


33. Tazama mchoro ufuatao kwa umakini kisha jibu maswali yafuatayo

Herufi gani inaonyesha uterasi?

  1. C
  2. D
  3. E
  4. A
  5. B


34. Mojawapo ya kazi za mifupa ni kutengeneza:

  1.  seli visahani 
  2.  plasma
  3.  selihai nyeupe  
  4. selihai nyekundu
  5.  selihai za kugandisha damu


35. Uhuru ana tatizo la meno yanayovunjika na miguu dhaifu. Ni virutubisho gani utamshaufi atumie ili kutatua tatizo lake hili?

  1.  Madini ya chuma           
  2.  Madini ya fosforasi
  3.  Madini ya kasiamu   
  4. Madini joto
  5. Vitamini K


36. Mwalimu alipomwuliza Ahadi swali juu ya mfumo wa jua alifikiri kwa muda kisha akatoa jibu sahihi kwa mwalimu. Je ahadi alitumia sehemu gani ya ubongo kujibu swali?

  1.  Ubongo wa mbele          
  2.  Ubongo wa nyuma
  3.  Ubongo wa kati      
  4.  Ubongo wa mbele na nyuma
  5.  Ubongo wa kati na wa nyuma


37. Kazi ya uta mgongo katika mfumo wa fahamu wa mwanadamu ni

  1.  Kuongoza matendo ya hiari   
  2.  kuongoza matendo yasiyo ya hiari 
  3.  Kuongoza miondoko ya mwili  
  4.  kudumisha umbo la mwili 
  5.  kupeleka taarifa katika mfumo mkuu wa fahamu.


38. Kupwa na kujaa kwa maji katika bahari na maziwa makubwa husababishwa na ...

  1.  dunia kuzunguka jua 
  2.  dunia kuzunguka katika mhimili wake
  3.  kupatwa kwa mwezi 
  4.  kupatwa kwa jua 
  5.  uvutano kati ya dunia na mwezi


39. Katika hali ya kawaida, kutu ni matokeo ya mjibizo wa athari za kikemikali kati ya:

  1.  shaba, maji na oksijeni  
  2.  sodiamu, maji na oksijeni
  3.  kalsiamu, maji na oksijeni    
  4.  chuma, oksijeni na maji 
  5.  maji, oksijeni na potasiamu


40. Mboga za majani na matunda huwezesha utengenezwaji wa:

  1.  selihai nyekundu 
  2.  selihai nyeupe
  3.  chembe visahani 
  4. plasma 
  5. uboho


41. Njia zifuatazo huweza kutumiwa kuhifadhi vyakula na mazao ili visiharibike ISIPOKUWA:

  1.  kuoka  
  2.  kutumia asali
  3.  kukausha    
  4.  kutumia chumvi 
  5. kutumia maji


42.  Yafuatayo ni makundi ya vyakula isipokuwa:

  1.  madini ya chumvi chumvi  
  2.  vitamini
  3. Maji   
  4. protini 
  5. hamirojo


43.Vipi kati ya vyakula vifuatavyo vinaweza kuhifadhiwa kwa kugandisha kwa baridi?

  1.  Matunda na mbogamboga 
  2.  Mbogamboga na nafaka
  3.  Samaki na matunda 
  4.  Nyama na samaki 
  5.  Nyama na nafaka


44. Ugonjwa utokanao na ukosefu wa madini ya chuma kwenye mlo ni:

  1.  matende    
  2.  kwashakoo
  3.  upungufu wa damu    
  4.  unyafuzi
  5.  beriberi


45. Tazama kielelezo namba 4 kwa uangalifu kisha jibu swali lifuatalo.

Kazi ya vyakula vilivyopo katika kielelezo namba 4 ni:

  1.  kujenga mwili  
  2.  kuupa mwili nguvu na joto
  3.  kukinga mwili dhidi ya maradhi 
  4.  kuupa mwili joto 
  5.  kujenga mifupa


46.  Samaki aliye ndani ya maji anaonekana kuwa juu zaidi ya alivyo kwa sababu .........

  1.  ndani ya maji samaki huwa ametulia
  2.  maji ni matulivu na masafi
  3. kima cha maji hupunguzwa na miale ya maji
  4.  magamba ya samaki humfanya aonekane mkubwa 
  5.  miale ya mwanga hupindishwa na maji


47. Mlishano sahihi ni:

  1. Mwewe Nyasi Chui mbuzi 
  2.  Nyasi Mwewe chui mbuzi
  3.  Chui   Mwewe Nyasi mbuzi
  4. Nyasi mbuzi chui   mwewe
  5. Mwewe chui mbuzi nyasi 


48. Sehemu tatu kuu zinazounda mfumo wa damu ni:

  1.  ateri, vena na kapilari
  2.  damu, moyo na mapafu
  3.  damu, mishipa ya damu na moyo
  4.  mishipa ya damu, moyo na valvu
  5.  moyo, aota na ateri 


49. Tunatumia milango ifuatayo ya fahamu katika kufanya uchunguzi wa kisayansi:

  1.   Ulimi, macho, pua, ngozi, masikio
  2.   Ubongo, pua, macho, neva sa fahamu
  3.   Ubongo, pua, masikio, macho na ngozi
  4.   Ubongo, ulimi, macho, ngozi, masikio
  5.  Macho, ngozi, masikio, neva za fahamu


50.  Matatizo katika mfumo wa uzazi wa wanawake hutokana na upungufu wa hol zifuatazo 

  1. Pituitari na insulin
  2. Estrojen na projesteron
  3. Thyroksin na pituitari
  4. Estrojen na insulin
  5.  Thairoksin na estrojen


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2013 Try This  |  

SAYANSI 2013

Chaguajibu sahihi kisha andika herufiyake kwa kila swali.

1. Ni sehemu zipi za mwili zinahusika na utoaji wa takamwili?

  1. Ngozi na figo 
  2. Tumbo na figo
  3. Bandama na ini 
  4. Ini na tezi 
  5. Mapafu na moyo


2. Kundi lipi limeainisha wanyama wenye uti wa mgongo?

  1. Konokono, mjusi na kenge
  2. Papasi, panzi na mbungo 
  3. Chura, mamba na mchwa
  4. Kuku, popo na bata 
  5. Nyoka, panzi na mbuzi


3. Endapo mito na mabwawa yatakauka, ni viumbe hai Vipi kati ya vifuatavyo vitaathirika zaidi?

  1. Vyura
  2. Samaki 
  3. Mamba
  4. Mbu
  5. Nyoka


5. Ni sehemu ipi ya ua hupokea mbegu za kiume?

  1. Stigma 
  2. Staili 
  3. Testa
  4. Ovyuli
  5. Petali


6.   Uhusiano uliopo kati ya viumbe hai na visivyo hai katika mazingira unaitwa

  1. kutegemeana 
  2. wando chakula 
  3. ikolojia 
  4. mlishano 
  5. mizania asili.


7. Ni Vipi kati ya viumbe hai vifuatavyo hujitengenezea chakula chao kwa kutumia klorofili?

  1. Wadudu
  2. Mimea 
  3. Wanyama 
  4. Virusi 
  5. Ndege


8. Tezi inayodhibiti matendo ya ukuaji wa mwili na kulinda mwili dhidi ya magonjwa huitwa

  1. kongosho 
  2. adrenalini
  3. pituitari 
  4. thairoidi 
  5. gonadi


9. Wanyama wenye uwezo wa kuishi majini na nchi kavu ni wale wa kundi la

  1. Ndege
  2. Amfibia
  3. Reptilia
  4. Samaki
  5. Mamalia


10. Maji safi na salama ni maji ambayo

  1. hayana rangi yoyote 
  2. yamepoozwa kwenye mtungi
  3. yamechotwa bombani 
  4. yamechotwa kisimani
  5. yamechemshwa na kuchujwa


11. Ugonjwa wa kipindupindu ni hatari sana kwa binadamu kwa kuwa

  1. huenezwa kwa njia ya hewa
  2. hujitokeza wakati wa masika tu
  3. husababisha mwili kupoteza maji
  4. hauna tiba wala kinga
  5. chanzo chake halisi bado hakijulikani


12. Mwanafunzi wa Darasa la Sita alipumulia hewa ndani ya neli jaribio yenye myeyuko usiokuwa na rangi, kisha akatikisa neli jaribio hiyo. Baada ya kuitikisa myeyuko ulionekana kuwa na rangi nyeupe. Je, kemikali gani ilikuwa kwenye myeyuko usiokuwa na rangi?

  1. Asidi ya haidrokloriki
  2. Salfa
  3. Asidi ya salfyuriki 
  4. Haidrojeni 
  5. Haidroksaidi ya kalsiamu


13. Homoni inayodhibiti sukari katika mwili wa binadamu huitwa.

  1. amilesi
  2. glukozi 
  3. insulini 
  4. ayodini 
  5. pepsini


14. Himoglobini katika chembe chembe nyekundu za damu inafanya kazi gani?

  1. Kupambana na bakteria 
  2. Kusafirisha oksijeni mwilini 
  3. Kusafirisha takamwili 
  4. Kubeba vimengenyo vya chakula
  5. Kusambaza taarifa mwilini.


15. Ili kuimarisha mifupa na meno, mtoto anahitaji

  1. kalsiamu, sodiamu na ayani
  2. wanga, mafuta na protini
  3. vitamin A, wanga na matunda
  4. vitamin A, kalsiamu na fosforasi
  5. mayai, matunda na wanga


16. Ugonjwa unaosababishwa na bakteria aina ya basili ambao hushambulia mapafu huitwa

  1. kifaduro 
  2. surua 
  3. kichocho 
  4. polio 
  5. kifua kikuu


17. Ni magojwa yapi kati ya yafuatayo huitwa magojwa ya kuambukiza? 

  1. Surua, polio na kifaduro 
  2. Kifua kikuu, kisukari na saratani
  3.  Surua, matende na UKIMWI 
  4. Kifaduro, pumu na kikohozi kikali 
  5. Surua, malaria na kisukari.


18. Kemikali inayotumika kubaini uwepo wa chakula aina ya wanga inaitwa.

  1. besi 
  2. asidi 
  3. spiriti 
  4. ayodini 
  5. chumvi


19. Ingawa wanyama huvuta hewa ya oksijeni na kutoa hewa ya kabondayoksaidi, hewa hizi hazipungui wala kuongezeka kwenye mizazi kwa kuwa.

  1. oksijeni ipo kwa wingi kvvenye mizazi
  2. kabondayoksaidi hubadilika kuwa oksijeni
  3. mimea hutumia kabondayoksaidi na kutoa oksijeni
  4. kabondayoksaidi huathiri tabaka la ozoni
  5. oksijeni na kabondayoksaidi hurekebishwa na ozoni


20. Vyakula vyenye mafuta vina umuhimu gani mwilini?

  1. Kujenga mwili 
  2. Kulinda mwili 
  3. Kuzuia maradhi
  4. kuupa mwili nguvu 
  5. kuupa mwili joto


21. Vyakula vinavyosababisha kukua kwa miili ya wanyama huitwa

  1. kabohaidreti 
  2. protini
  3. vitamini 
  4. mafuta 
  5. madini


22. Huduma ya kwanza hutolewa kwa lengo gani?

  1. Kushusha gharama za matibabu
  2. Kuonesha umahiri wa kitabibu
  3. Kuokoa maisha ya wagonjwa 
  4. Kurahisisha matibabu
  5. Kupunguza idadi ya madaktari.


23. Huduma ipi ya kwanza kati ya zifuatazo hutolewa kwa mtu aliyekazwa na misuli?

  1. Kumfanyisha mazoezi ya viungo
  2. Kumpumzisha kitandani
  3. Kufunga misuli kwa bandeji
  4. Kumpa dawa ya kutuliza maumivu
  5.  Kuchua polepole misuli husika


24. Mtu anayeharisha na kutapika anapoteza

  1. Maji na damu
  2. Sukari na chumvi 
  3. maji na chumvi
  4. chumvi na protini 
  5. chumvi na damu


25. Kifaa kifuatacho siyo muhimu kuwemo katika sanduku Ia huduma ya kwanza

  1. Wembe 
  2. Pimajoto 
  3. Mkasi 
  4. Kijiko 
  5. Kibanio


26. Magonjwa yapi kati ya yafuatayo yanazuilika kwa chanjo?

  1. Pepopunda na malaria
  2. Matende na ukoma 
  3. Pepopunda na kichaa cha mbwa
  4. Malaria na kifua kikuu E. Kipindupindu na ukoma


27. Kuvimba miguu, kula sana na kuhisi njaa mara kwa mara ni dalili za ugonjwa wa

  1. homa ya tumbo
  2.  matende
  3. kwashakoo 
  4. Safura 
  5. kisukari


28. Jeki, parafujo, mkasi na patasi ni aina za mashine rahisi ziitwazo

  1. Tata 
  2. Nyenzo 
  3. Ekseli 
  4. Rola 
  5. Roda


29. Chunguza mlinganyo wa kikemikali ufuatao kisha jibu swali linalofuata.

Herufi Y inawakilisha Kemikali ipi?

  1. Nyongo 
  2. Oksijeni 
  3. Kaboneti 
  4. Chumvi 
  5. Haidrojeni


30. Tendo lipi kati ya yafuatayo linasababisha maada mpya kutokea?

  1. Kuyeyusha barafu 
  2. Kuchuja maji machafu
  3. Kuvukiza maji 
  4. Kuyeyusha sukari 
  5. Kuchacha kwa maziwa


31. Madhara gani yatatokea endapo vyanzo vya maji havitalindwa?

  1. Kufa kwa wanyama na mimea
  2. Kupoteza nguvu kazi ya Taifa 
  3. Kutoweka kwa mazalia ya samaki
  4. Mvua za msimu zitapungua 
  5. Mifereji ya kumwagilia mashamba haitatumika.


32. Mchakato wa usafirishaji wa myeyuko wa chumvichumvi katika mimea huitwa.

  1. kusharabu 
  2. kufyonza 
  3. difyusheni
  4. osmosisi 
  5. fotosinthesisi


33. Atomi mbili za haidrojeni zikiungana kikemikali na atomi moja ya oksijeni kampaundi inayotengenezwa huitwa

  1. chumvi 
  2. asidi 
  3. maji 
  4. besi 
  5. gesi


34. Gesi inayosaidia vitu kuwaka ni

  1. oksijeni 
  2. naitrojeni
  3. haidrojeni 
  4. ozoni
  5. kabondayoiksaidi


36. Maji ambayo ukitumia sabuni hubadilika rangi kuwa meupe mithili ya maziwa huitwa

  1. Maji mepesi
  2. Maji machafu
  3. Maji laini
  4. Maji mazito
  5. Maji magumu


36. Mwangwi humaanish sauti...

  1. Iliyopindishwa
  2. iliyosharabiwa
  3. iliyosikika
  4. iliyoakisiwa
  5. Iliyorekodiwa


37. Kwa nini sauti za watangazaji wa radio na televisheni hazisikiki nje ya vyumba vya kutangazia kupitia kuta za vyumba hivyo?

  1. Kuta zimepakwa rangi zinazosharabu sauti
  2. Kuta zimejengwa kwa maada inayosharabu sauti
  3. Kuta zimepakwa rangi inayoakisi sauti 
  4. Kuta huakisi sauti inayosharabiwa
  5. Kuta zinapindisha sauti hizo.


38.Kiasi cha mkondo wa umeme katika sakiti hupimwa kwa kutumia 

  1. rektifaya 
  2. resista 
  3. transfoma 
  4.  voltimita 
  5. amita



39. Kielelezo Na 1 kinawakilisha tendo la kusumakisha.

Iwapo ncha ya sumaku ya kaskazini (N) itatumika kusumakisha ncha X ya kipande cha chuma chenye ncha X — Y, ncha Y ya kipande cha chuma itakuwa sawa na ncha ipi ya sumaku?


  1. Kusini
  2. Mashariki
  3. Kaskazini 
  4. Magharibi
  5.  Kati


40. Ipi kati ya rangi zifuatazo ina uwezo wa kuakisi miale ya mwanga lakini sio kusafirisha miale hiyo?

  1. Nyeusi 
  2. Nyeupe
  3. Njano
  4. Bluu 
  5. Kijani


41. Mshipi na ndoano ya kuvua samaki ni mifano ya nyenzo daraja la ngapi?

  1. Pili 
  2. Kwanza
  3. Tano 
  4. Nne 
  5. Tatu


42. Chunguza sakiti ya umeme iliyooneshwa katika kielelezo Na 2 kisha jibu swali lifuatalo

Sakiti iliyooneshwa katika kielelezo Na 2 huitwa 

  1. sakiti mfuatano
  2. sakiti sambamba
  3. sakiti kinzani 
  4. sakiti pozo
  5. sakiti geu


43.  Mkulima aligundua kuwa jembe lake lililotengenezwa kwa chuma limepata kutu. HaE imesababishwa na jembe kugusana na 

  1. maji na hewa ya okisijeni
  2. maji na hewa ya kabondayoksaidi
  3. mafuta na hewa ya oksijeni
  4. udongo na hewa ya oksijeni
  5. udongo na hewa ya kabondayoksaidi


44. Mtu mwenye WU anaweza kutambulika kutokana na 

  1. anavyoonekana 
  2. mahudhurio ya hospitali
  3. tabia yake 
  4. anavyokohoa
  5. vipimo vya damu yake


45. Mgonjwa wa UKIMWI anastahili kupata mlo maalumu ili

  1. aweze kupona haraka
  2. asiambukize watu WU 
  3. awe na nguvu ya kufanya kazi
  4. mwili upambane na maradhi 
  5. WU viangamie kabisa


46. Unyafuzi ni ugonjwa unaosababishwa na ukosefu wa

  1. mlo kamili 
  2. protini
  3. vitamini 
  4. madini 
  5. mafuta


47. Dalili mojawapo ya ugonjwa wa UKIMWI ni

  1. kupungua uzito kwa haraka
  2. kuwashwa sehemu za siri
  3. kuvimba miguu na tumbo 
  4. kupoteza uwezo wa kuona
  5. kuwa na hasira


48. Katika uchunguzi wa kisayansi hatua ipi hutumika kukubali au kukataa dhanio?

  1. Kukusanya data 
  2. Kufanya jaribio
  3. Kuandika hitimisho 
  4. Kutafsiri data
  5. Kudurusu majarida


49. Kazi ya chembe nyekundu za damu katika mwili wa binadamu ni

  1. kugandisha damu
  2. kupambana na maradhi
  3. kushambulia bakteria 
  4. Kusafirisha virutubisho
  5. Kusafirisha oksijeni


50. Chunguza kielelezo Na. 3 kinachoonesha mzunguko rahisi wa damu katika mwili wa binadamu kisha jibu swali linalofuata.

Herufi zinazowakilisha mishipa ya damu inayosafirisha damu isiyokuwa na oksijeni ni 

  1. M na P
  2. N na P
  3. M na O
  4.  O na P 
  5. M na N


MTIHANI WA SAYANSI DARASA LA IV 2013

SEHEMU A

Jibu sali namba 1 hadi 10 kwa kuchagua jibu sahihi na kisha kuandika herufi yake pembeni ya namva ya swali.

1. Mimea haiwezi kuendelea kukua bila hewa, maji na . . . . .

  1. Mwanga wa jua
  2. Upepo
  3. Baridi
  4. Barafu


2. Jasho hutoka mwilini kwa . . . . . . vilivyoko kwenye ngozi

  1. Mashine
  2. Sehemu za mwili
  3. Vinyweleo
  4. Kupandikiza


3.Chumvi katika maji inaweza kutenganishwa na maji kwa . . . . . . .

  1. kuchuja
  2. kupika
  3. kuvukiza
  4. kugandisha


4. Fagio na sepetu ni mifano ya nyenzo daraja la . . . . . . . . .

  1. Tatu
  2. Nne
  3. Pili
  4. Kwanza


5. Jotoridi la kuganda kwa maji(maji kuwa barafu) ni . . . . . .

  1. 10 oC
  2. 36 oC
  3. 0 oC
  4. 36.9 oC


6. Kutembea, kusimama na kukimbia kwa muda mrefu husababisha . . . . . .  kukaza

  1. mifupa
  2. misuli
  3. viungo
  4. viungo


7. Mzunguko kamili wa . . . . . .  huitwa sakiti

  1. waya
  2. betri
  3. soketi
  4. umeme


8. Vitu vilivyoundwa kwa . . . . . . huweza kuvutwa na sumaku

  1. chuma
  2. vumbi
  3. mbao
  4. kioo


9, Joto husambaa katika kimiminika kwa njia ya . . . . . . 

  1. msafara
  2. mpitisho
  3. mnururusho
  4. mgandamizo


10. Mwanga husafiri katika mstari. . . . . . 

  1. mnyoofu
  2. uliopinda
  3. zigizaga
  4. mwembamba


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2012 Try This  |  

SAYANSI - 2012

Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwa kila swali.

1. Ili kudumisha afya ya mwili, tunapaswa:

  1. kufanya mazoezi, kula chakula bora na kupumzika.
  2. kulala sana, kula chakula bora na kucheza.
  3. kutofanya kazi ngumu, kufanya mazoezi na kulala.
  4. kufanya mazoezi na kushiriki michezo
  5. kula vizuri na kufanya mazoezi muda wote.


2.Ni kipi kati ya virutubisho vifuatavyo ni muhimu kwa mama mjamzito kupata kwa wingi?

  1. Protini.
  2. Kabohaidreti.
  3. Mafuta.
  4. Chumvichumvi.
  5. Vitamini.


3.Kukojoa mara kwa mara, kutoa mkojo mwingi na kupata kiu mara kwa mara ni dalili za ugonjwa upi?

  1. Kansa.
  2. Kisukari.
  3. Kwashakoo.
  4. Kifaduro.
  5. Upungufu wa damu.


4.Ni njia gani kati ya zifuatazo inafaa kumsaidia mtu aliyepata mshtuko uliotokana na kunaswa na waya wenye umeme?

  1. Kumsukuma kwa mikono haraka.
  2. Kuuvuta waya wa umeme uliomshtua. 
  3. Kutumia maji kuuzima umeme.
  4. Kumvuta kwa kutumia kifaa kisichopitisha umeme.
  5. Kumwacha mpaka umeme ukatike wenyewe.


6.  Ipi kati ya zifuatazo siyo dalili ya UKIMWI?

  1. Kuvimba kwa matezi
  2. Kupoteza uzito 
  3. Kuharisha kusikokoma
  4. Kikohozi cha muda mrefu kisicho cha kawaida.
  5. Kutoa jasho kusiko kwa kawaida wakati wa usiku.


7.  Zifuatazo ni njia za kujikinga na majanga mbalimbali katika mazingira isipokuwa:

  1. kuchimba mahandaki
  2. kujenga nyumba mbali na milima ya volcano
  3. kuweka akiba ya chakula
  4. kuishi maisha ya kuhamahama
  5. kudumisha usafi katika mazingira


8.  Ni ipi kati ya zifuatazo ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali?

  1. Mwanga 
  2. Hewa
  3. Mafuta ya taa 
  4. Kabondayoksaidi 
  5. Mvuke


9.  Ni lipi kati ya matendo yafuatayo siyo sababu ya uharibifu wa mazingira?

  1. Uchomaji wa karatasi
  2. Maendeleo ya viwanda
  3. Kuoga ziwani
  4. Kutumia mbolea ya samadi
  5. Kuoshea magari mtoni.


10.  Mfalme wa porini aliamuru wanyama wote walao nyama wauawe. Unafikiri ni nini kitatokea porini baada ya miaka mingi?

  1. Mimea itaota kwa wingi
  2. Idadi ya wadudu haitabadilika 
  3. Mimea itapungua 
  4. Wanyama walao majani watapungua 
  5. Mazingira yatabaki katika hali nzuri ya kuvutia.


11.  Kani za asili husababisha moja kati ya mambo yafuatayo katika mazingira:

  1. Kutoonekana kwa samaki
  2. Tetemeko la ardhi 
  3. Ongezeko la mimea 
  4. Upungufu wa umeme 
  5. Kukauka kwa mito.


12.  Ipi kati ya zifuatazo siyo njia sahihi ya kuhifadhi rutuba ya udongo katika shamba?

  1. Kubadilisha mazao 
  2. Kupanda mimea jamii ya kunde. 
  3. Kupumzisha shamba. 
  4. Kutumia mbolea 
  5. Kupanda zao la aina moja mfululizo.


13.  Chura hupitia hatua kuu ngapi katika kukua kwake?

  1. Moja 
  2. Saba 
  3. Sita 
  4. Tano 
  5. Nane.


14.  Mdudu yupi kati ya hawa wafuatao hupitia metamofosisi isiyokamilika?

  1. Mbu 
  2. Kipepeo 
  3. Inzi 
  4. Nyuki 
  5. Mende


15.     Panya aliyekuwa amefungiwa kwenye kisanduku kilichokuwa na kipande cha nyama alikufa baada ya siku mbili. Ni kitu gani kilisababisha panya huyo kufa?

  1. Alikula nyama iliyooza
  2. Alikosa hewa ya kabondayoksaidi 
  3. Alikosa hewa ya oksijeni.
  4. Alikosa maji ya kutosha baada ya kula nyama.
  5. Alikosa mwanga ambao ni muhimu kwa ukuaji wa wanyama.


16.  Ni kiumbe yupi kati ya hawa wafuatao ni amfibia?

  1. Chura 
  2. Panya 
  3. Mjusi 
  4. Kobe 
  5. Kinyonga.


17.  Wanyama kama mamba, viboko, vyura wanaishi katika maskani gani?

  1. Angani na ardhini
  2. Ardhini na majini. 
  3. Mazingira yoyote ilimradi chakula kiwepo
  4. Ardhini na mapangoni 
  5. Kwenye misitu.


19.  Kuna aina kuu mbili za mbegu za mimea ambazo ni:

  1. ghalambegu kuu na ghalambegu ndogo
  2.  monokotiledoni na daikotiledoni 
  3. daikotiledoni na kikonyo kikuu
  4. mbegu zenye mizizi na zisizo na mizizi.
  5. mbegu za asili na za porini.


20.  Miale ya mwanga wa radi inaonekana kabla ya kusikia mngurumo wa radi kwa kuwa:

  1. miale ya mwanga haizuiwi na chochote 
  2. sauti husharabiwa kwanza na mawingu 
  3. mwanga husafiri haraka kuliko sauti.
  4. sauti husafiri haraka kuliko mwanga
  5. mawingu yanayotoa sauti husafiri polepole.


21. Ukifua vitambaa viwili vya aina moja, kimoja cheupe na kingine cheusi, kile cheusl kitakauka haraka kuliko cheupe kwa sababu:

  1. kinasharabu joto kwa haraka 
  2. kinaakisi mwanga kwa haraka 
  3. kinafyonza unyevu haraka. 
  4. kinahimili upepo unaovuma.
  5. kina uwezo wa kuchuja maji.


22. Ni lipi kati ya makundi yafuatayo linawakilisha vimiminika? 

  1. Hewa, maji na shaba
  2. Petroli, barafu na naitrojoni
  3. Dhahabu, haidrojeni na zebaki 
  4. Petroli, zebaki na maji
  5. Maji, petrol na hewa


23.  Chunguza Kielelezo Na. 1 kisha jibu swali lifuatalo:

Kielelezo 1

Alama hii katika umeme huwakilisha:

  1.  ukizani 
  2. selikavu 
  3. voltimita
  4. swichi 
  5. glopu.


24.  Akyumuleta ni muungano wa seli zilizoungwa pamoja na hutumika kutoa umeme mkondo mnyoofu kwa matumizi ya:

  1. baiskeli, pasi na simu
  2.  magari, matrekta na simu
  3. friji, pasi na feni
  4. baiskeli, friji na jiko la umeme.
  5. Seli kavu, jiko la mkaa na pasi


25. Chunguza Kielelezo Na. 2 kinachoonesha watu wawili, P na Q wakiwa wanavuta mizigo yenye uzito sawa kupeleka juu ya paa, kisha jibu swali linalofuata.

Kielelezo 2 Ni yupi atakayevuta mzigo kiurahisi zaidi?

  1. P kwa sababu yuko chini. 
  2. Q kwa sababu atatumia nguvu kidogo 
  3. Q kwa sababu yuko juu ya paa 
  4. P kwa sababu roda ni moja 
  5. Q kwa sababu nguvu ya mvutano wa dunia ni kidogo.


26. Uwezo wa kusogeza kitu kutoka sehemu moja kwenda nyingine huitwa:

  1.  usawa 
  2. kani 
  3. msuguano 
  4. kazi 
  5. gramu


27. Penseli ikiwekwa kwenye glasi iliyo na maji inaonekana kama imepinda. Hii ni kwa sababu ya:

  1. kupinda kwa mwanga 
  2. kuakisiwa kwa mwanga
  3. kutawanyika kwa mwanga
  4. uwezo wa maji kupitisha mwanga 
  5. ujazonene wa maji


28. Maziwa huweza kusindikwa na kutengenezwa kitu gani kati ya vifuatavyo?

  1. Jibini na sabuni
  2. Matunda na hamira 
  3. Siagi na matunda 
  4. Keki na siagi.
  5. Siagi na jibini.


29. Vyanzo asilia vya nishati katika maisha ya kila siku ni:

  1. kuni, moto na maji 
  2. umeme, sumaku na gesi asili
  3. kuni, jua na upepo 
  4. moto, upepo na sumaku 
  5. umeme, upepo na maji


30. Tazama Kielelezo Na. 3 kisha chagua jibu sahihi kuhusiana na jaribio hilo.

Lengo la jaribio katika Kielelezo Na. 3 ni kuonesha:

  1. Kuchemsha maji ya kunywa
  2. Kupoza maji
  3. Kutanuka na kusinyaa kwa hewa 
  4. Kupoza gesi
  5. Kutengeneza hewa ya oksijeni.


31. Lipi ni badiliko la kiumbo?

  1. Kuchacha kwa maziwa
  2. Kuunguza karatasi
  3. Maji kuwa mvuke
  4. Pambano kati ya tindikali na nyongo 
  5. Mimea kuoza


32. Chunguza Kielelezo Na. 4 kisha jibu swali linalofuata.

Lengo la jaribio katika Kielelezo Namba 4 ni kutafuta:

  1. ujazo wa kopo chirizi
  2. kiasi cha hewa katika kopo chirizi
  3. eneo la jiwe
  4. mzingo wa jiwe
  5. ujazo wa jiwe


33. Ili kuzuia hatari zinazosababishwa na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, kila Taifa linapaswa:

  1. kushirikiana na wanasayansi
  2. kuwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia
  3. kuondokana na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia
  4. kuchukua uvumbuzi wa kiteknolojia toka nchi zilizoendelea
  5. kuweka sera zinazosimamia matumizi ya sayansi na teknolojia.


34. Ipi kati ya yafuatayo hutumika kutabiri kuhusu tatizo katika uchunguzi wa kisayansi?

  1. kukusanya data
  2. dhanio
  3. kuchambua data
  4. hitimisho 
  5. kutoa maoni.


35. Watu wanaopenda kwenda kwenye mwezi wanalazimika:

  1. kubeba kuni za kupikia chakula
  2. kubeba hewa ya oksijeni na chakula
  3. kuwa waangalifu na wanyama wakali
  4. kubeba kabondayoksaidi na chakula
  5. kubeba kabondayoksaidi na maji.


36. Katika utafiti vipimo vya urefu wa mimea sita vimepatikana kama ifuatavyo: sm 12; sm 6; sm 20; sm 14; na sm 10. Wastani wa urefu huo ni:

  1. sm 12 
  2. sm 14
  3. sm 11 
  4. sm 13 
  5. sm 17


37. Ateri kuu imegawanyika katika mishipa midogo midogo iitwayo:

  1.  venekava 
  2. bronchioli 
  3. valvu 
  4. kapilari 
  5. vena.


38. Hemoglobini ni kampaundi inayopatikana ndani ya damu katika:

  1.  seli hai nyeupe 
  2. seli hai nyekundu
  3. ute wa damu 
  4. uroto wa njano katika mifupa
  5. seli zinazogandisha damu.


39. Nini hutokea iwapo mbegu X ya kiume itaungana na mbegu X ya kike?

  1. Mapacha wasiofanana
  2. Mtoto wa kike
  3. Mapacha walioungana 
  4. Mtoto wa kiume 
  5. Mapacha wanaofanana.


40. Ni ubongo wa mnyama yupi kati ya wafuatao umeundwa kiutaalamu zaidi kuliko wengine?

  1. Binadamu
  2. Farasi
  3. Sungura 
  4. Sokwe
  5. Nyani


41. Kutu ni matokeo ya kuwepo kwa pambano Ia kikemikali lifuatalo:

CHUMA + Y +MAJI. Y inasimama badala ya:

  1. oksijeni 
  2. aside 
  3. naitrojeni 
  4. unyevu 
  5. kabondayoksaidi.


42. Ni kipi kati ya vifuatavyo kimeundwa kwa chembe chembe ndogo sana?

  1. Gesi 
  2. Vimiminika
  3. Chembe za damu 
  4. Seli kavu 
  5. Maada


43. Ni kipi kati ya vifuatavyo husababisha upungufu wa damu katika mwili wa binadamu?

  1. Ukosefu wa vitamini B
  2. Ukosefu wa ayani C. 
  3. Ukosefu wa kalsiamu 
  4. Ukosefu wa protini 
  5. Ukosefu wa fosfeti.


44. Tunapopika mboga za majani tunashauriwa:

  1. kuweka magadi kidogo ili ziive vizuri
  2. kupika kwa muda mrefu ili kupunguza maji
  3. kuzifunika na kuzipika kwa muda mfupi
  4. kuzikausha kabla ya kuzipika
  5. kuzikaanga kwa mafuta mengi


45. Ni yapi kati ya yafuatayo husababishwa na mwili kuwa na kabohaidreti nyingi kuliko inavyohitajika? 

  1. Kiribatumbo
  2. Utapiamlo
  3. Kwashakoo
  4. Unyafuzi
  5. Goita


46. Katika jaribio lake, Shida alipitisha mwale wa mwanga katika kioo bapa kama inavyooneshwa kwenye Kielelezo Na. 5.

Kielelezo. 5 Pembe Y itakuwa na ukubwa wa nyuzi:

  1. 180
  2. 35
  3. 70
  4. 90 
  5. 105


47. Msuguano husababisha nini kati ya yafuatayo?

  1. Kupumua
  2.  Kuogelea
  3. Kuwinda
  4. Kuzaliana 
  5. Kujificha


49.Ni viumbehai vipi kati ya vifuatavyo huishi majini?

  1. Bakteria, virusi na kuvu
  2. Dagaa, pweza na bacteria
  3. Bakteria, virusi na pweza 
  4. Dagaa pweza na yungiyungi
  5. Bakteria, virusi na yungiyungi.


50.Mbu aina ya kyuleksi husambaza minyoo inayoitwa filarial ambayo husababisha ugonjwa wa:

  1. pepopunda
  2. matende
  3. surua
  4. homa ya ini
  5. tetekuwanga


MTIHANI WA SAYANSI DARASA LA IV 2012

SEHEMU A

Chagua jibu sahihi na andika herufi yake kwenye nafasi ya kujibia

1. Baadhi ya ajali na maafa yatokanayo na nguvu za asili ni . . . . . . . .

  1. mvua kubwa, umeme, kimbunga
  2. radi, kimbunga, mvua kubwa
  3. umeme, madaraja, kimbunga
  4. mitambo, mafuriko, miti


2. Wanyama wanaokula nyama wana . . . . . . . . 

  1. pembe ndefu na kali
  2. mikia mipana na mifupi
  3. meno makali na kucha kali
  4. pembe kali na kucha kali


3. Mbu wanaosambaza vimelea vya malari huuma. . . . . . . . 

  1. usiku tu
  2. mchana tu
  3. usiku na mchana
  4. usiku wa manane


4. Zifuatazo ni njia za kumsaidia mtu aliyezirai isipokuwa. . . . . . . . 

  1. Mweke mgonjwa katika sehemu salama yenye hewa ya kutosha
  2. Inua miguu ya mgonjwa kuruhusu damu iende kichwani
  3. Mvue viatu na kulegeza mkanda wake
  4. Kama hapumui umwagie maji ya baridi mwili mzima


5. Maji huganda katika nyuzijoto

  1. 100 oC
  2. 36 oC
  3. 0 oC
  4. 36.9 oC


6. Milango ya fahamu in . . . . . . . .  katika uchunguzi

  1. udhaifu
  2. uhakika
  3. ubunifu
  4. tofauti


7.  Mikono (mishikio) ya pasi na vikaangio hutengenezwa kwa mbao kwa sababu . . . . . . . 

  1. mbao hupendezesha pasi na vikaangio
  2. mbao ni kipitisho hafifu cha joto
  3. mbao huharibika haraka
  4. mbao ni kipitisho kizuri cha joto


8. Kipi kati ya vifuatavyo ni chanzo kisicho cha asili cha mwanga? . . . . . . . . 

  1. Jua
  2. Radi
  3. Nyota
  4. Moto


9. Ni aina gani ya nguo haitokani na viumbe hai? Ni nguo za . . . . . . . . 

  1. nailoni
  2. silki
  3. pamba
  4. sufu


10. Rangi ya kijani katika mmea huitwa . . . . . . . . 

  1. usanisi
  2. umbijani
  3. usanisi nuru
  4. majani


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2011 Try This  |  

SAYANSI 2011

Chagua jibu sahihi na andika herufi inayohusika mbele ya namba ya kila swali katika karatasi ya kujibia.

1. Kifaa kinachotumika katika kuangalia sell za viumbehai huitwa:

  1. Darubini 
  2. Periskopu 
  3. Hadubini
  4. Kamera 
  5. Horoskopu


2. Mlango wa fahamu unaotumika kutambua hali ya joto au baridi ni: 

  1. ulimi 
  2. sikio 
  3. jicho 
  4. pua 
  5. ngozi


3. Ni yupi kati ya wafuatao ni mamalia?

  1. Njiwa 
  2. Kuku 
  3. Bata 
  4. Popo 
  5. Nyoka.


4. Kielelezo Na. 1 kinaonesha mbegu yenye ghala mbili.

Kielelezo Na. 1

Katika Kielelezo Na. 1 sehemu inayoota na kuwa mzizi imeoneshwa kwa herufi ipi?
  1. H
  2. J
  3. K
  4. L
  5. M


5. Kitu gani kitatokea endapo maua ya mmea wa mhindi yatanyofolewa?

  1. Mmea utastawi
  2. Mmea utakufa
  3. Mizizi ya mmea haitakua
  4. Majani yake yatageuka rangi
  5. Mmea hautazaa


6. Muungano ufuatao ni muhimu kwenye utengenezaji wa kabohaidreti katika mimea:

  1. Oksijeni, klorofili na maji
  2. Kabondayoksaidi na maji
  3. Kabondayoksaidi, maji na mwanga wa jua
  4. Klorofili, maji na mwanga wa jua
  5. Klorofili, wanga na mwanga wa jua.


7. Ni taka mwili zipi zitolewazo na mapafu?

  1. Oksijeni na maji
  2. Oksijeni na kabondayoksaidi
  3. Kabondayoksaidi na maji
  4. Kabondayoksaidi na chumvi
  5. Oksijeni na chumvi


8. Kipi kati ya vifuatavyo husafirisha chavua kutoka katika stameni kwenda kwenye stigma? 

  1. Watu 
  2. Wadudu 
  3. Maji 
  4. Umande 
  5. Staili


9. Mtu asiyekula matunda na mboga za majani huweza kupata matatizo ya:

  1. kuugua mara kwa mara
  2. kupunguza uzito wa mwili
  3. kuongezeka kwa hamu ya kula nyama
  4. rangi ya ngozi huwa njano
  5. kuongezeka uzito wa mwili.


10. Mtoto mwenye kwashakoo ni yule aliyekosa chakula chenye: 

  1. vitamini 
  2. mafuta 
  3. madini 
  4. wanga
  5. Protini


11.Konokono waishio majini hueneza ugonjwa uitwao:

  1. kichocho 
  2. Pepopunda
  3. kipindupindu 
  4. surua
  5. matende


12. Mshipa mkuu unaotoa damu kwenye moyo unaitwa: 

  1. veini 
  2. aota 
  3. vena kavu 
  4. palmonari 
  5. hepatik.


13. Homoni inayorekebisha uingiaji wa hewa ya oksijeni katika mfumo wa upumuaji katika mwili wa binadamu inaitwa.

  1. adrenalini 
  2. insulin 
  3. thairoksini 
  4. estrojeni 
  5. amilesi.


14. Katika hali ya kawaida, tofauti kati ya hewa inayoingia na hewa inayotoka katika mwili binadamu ni kuwa hewa inayotoka ina wingi wa:

  1. Oksijeni 
  2. haidrojeni 
  3. maji
  4. naitrojeni 
  5. kabondayoksaidi.


15. Ugonjwa wa rovu (goita) husababishwa na upungufu wa: 

  1. ayani 
  2. ayodini 
  3. kalsiamu 
  4. potasiamu 
  5. fosfeti


16. Ugonjwa wa beriberi unasababishwa na upungufu wa vitamini: 

  1. B1 
  2. B2 
  3. A


17. Samaki huvuta hewa kwa kutumia: 

  1. pua 
  2. mdomo 
  3. mapezi 
  4. matamvua 
  5. magamba


18. Chakula kilichoyeyushwa katika utumbo mwembamba husambazwa mwilini kwa msaaaz wa:

  1. maji B.
  2. oksijeni 
  3. damu 
  4. difyusheni 
  5. kusharabu


19. Chakula cha aina ipi kati ya vifuatavyo kinaweza kukarabati chembe hai za binadamu?

  1. Mafuta 
  2. Wanga 
  3. matunda 
  4. Protini 
  5. Madin_


20. Uzazi wa mpango una umuhimu gani kwa familia?

  1. Huwezesha familia kumiliki nyumba
  2. Huongeza idadi ya watoto
  3. Huwezesha familia kumudu safari za pamoja
  4. Huwafanya wanafamilia kuwa na furaha
  5. Huwezesha familia kupata chakula cha kutosha.


21. Huduma ya kwanza ni tiba inayotolewa kwa:

  1. mtu anayeugua ugonjwa unaojulikana.
  2. mtu baada ya kutoka hospital'
  3. lengo la kuonesha umahiri wa madaktari
  4. mgonjwa kabla hajapelekwa hospital'
  5. lengo la kutangaza kazi za Msalaba Mwekundu.


22. Lengo la kupaka asali kwenye jeraha linalotokana na kuungua moto ni:

  1. kupunguza maumivu
  2. kuupa mwili nishati
  3. kutoa matibabu ya awali
  4. kuzuia uchafu usiguse kidonda
  5. kukinga na uambukizo wa tetanus.


23. Mtu anayetapika hupatiwa nini kati ya yafuatayo kama huduma ya kwanza?

  1. Maziwa yaliyochemshwa
  2. Juisi iliyotokana na limao
  3. Myeyuko wa sukari na limao
  4. Myeyuko wa sukari na chumvi
  5. Kumpumzisha sehemu yenye baridi na ukimya.


24. Ni vipi kati ya vifuatavyo ni muhimu kwa huduma ya kwanza kwa mtu aliyevunjika mfupa bila kupata jeraha?

  1. Mkasi, bandeji, vibanzi, uzi na shazia
  2. Taulo, sabuni, machela, pamba na spirits
  3. Taulo, maji, mafuta, vibanzi na sabuni
  4. Blanketi, kiti, sabuni, kamba na mkasi
  5. Blanket', bandeji, vibanzi, mkasi na kamba


25. Nini kinatakiwa kifanyike baada ya kumhudumia mtu aliyeumia?

  1. Kupewa maji ya kunywa ya kutosha
  2. Kupelekwa hospital kwa matibabu zaidi
  3. Kulazwa chins na kupuliziwa pumzi mdomoni
  4. Kupumzishwa kwenye kivuli cha mti
  5. Kupewa mapumziko ya kulala wote.


26. Protini huanza kumeng'enywa kikemikali kwenye:

  1. mdomo 
  2. tumbo 
  3. puru
  4. utumbo mpana 
  5. utumbo mwembamba.


27. Huduma ya kwanza inayomfaa mtu aliyekunywa sumu ni:

  1. kumtapisha 
  2. kumpatia maziwa ya kunywa
  3. kumpatia dawa 
  4. kumpatia maji ya kunywa
  5. kumpatia glukozi.


28. Maada inapatikana katika hail zifuatazo:

  1. Vimiminika, maji na gesi 
  2. Yabisi, vimiminika na hewa
  3. Yabisi, vimiminika na gesi 
  4. Mawe, yabisi na gesi
  5. Yabisi, hewa na gesi.


29. Chumvi iliyomwagika kwenye ndoo ya maji inaweza kutenganishwa na maji hayo kwa kutumia njia ipi?

  1. Kuchuja mchanganyiko huo
  2. Kuchuja myeyuko huo
  3. Kuvukiza myeyuko huo
  4. kuchemsha mchangayiko huo
  5. Kuvukiza mchanganyiko huo.


30. Katika utengenezaji wa sabuni, haidroksaidi ya sodiamu huchanganywa na mafuta yanayochemka. Endapo kemikali hiyo haipatikani maada ipi hutumka kama mbadala?

  1. Majivu ya majani
  2. Myeyuko wa limao
  3. Unga wa mhogo
  4. Mafuta ya nazi
  5. Maji ya majani ya mpapai


31. Kuyeyuka kwa barafu ni badiliko la aina ipi?

  1. kikemikali 
  2. kiumbo
  3. Kimazingira
  4. kibayolojia 
  5. kifiziolojia


32. Njia ya asili ya kurutubisha udongo ni:

  1. kuchanganya samadi na mbolea ya chumvichumvi
  2. kuchoma miti inayokausha vyanzo vya maji
  3. kuchoma majani na mabua ya mahindi
  4. kunguza idadi ya ng'ombe wanaochungwa
  5. kulima mazao ya jamii ya kunde kwa mbadilishano.


33. Njia rahisi ya kugeuza maji magumu kuwa laini ni:

  1. kuyasafisha kwa dawa 
  2. kuyazimua
  3. kuyachemsha 
  4. kuyeyusha sehemu ngumu
  5. kuchuja maada ngumu.


34. Ni vitu vipi kati ya vifuatavyo huweza kutenganishwa na sumaku?

  1. Unga wa ayani na mchanga
  2. Unga na vipande vya karatasi
  3. Pini za plastiki na mchanga
  4. Unga wa kioo na mchanga
  5. Mchanga na mchele


35. Mabadiliko ya hali ya hewa na maji ni viambato vinavyosaidia:

  1. kufanya use wa ardhi uwe mzuri
  2. wanyama kumudu mazingira yao
  3. wanyama na mimea kuishi
  4. kuharakisha mmomonyoko wa udongo
  5. kusawazisha uhusiano wa mlishano.


36. Gesi inayosaidia moto kuwaka ni:

  1. haidrojeni 
  2. naitrojeni
  3. ozoni
  4. gesi asilia 
  5. oksijeni.


37. Chunguza kwa makini Kielelezo Na. 2 kisha jibu swali linalofuata.

Kielelezo Na. 2

Tafuta thamani ya X katika Kielelezo Na. 2.

  1. gm 250 
  2. gm 280 
  3. gm 437.5 
  4. gm 240 
  5. gm 175


38. Kuta za ndani za flaski ya themosi zinapakwa rangi ya fedha ili kuzuia kupotea kwa joto kwa njia ya:

  1. mpitisho 
  2. kuakisi 
  3. msafara
  4. kupinda 
  5. mnururisho.


39. Retina katika jicho ni sawa na kifaa gani kwenye kamera?

  1. Hama
  2. Lenzi
  3. Glopu
  4. Swichi 
  5. Fokasi.


40. joto husafiri katika maada yabisi kwa njia ya:

  1. mpitisho 
  2. msafara
  3. mnururisho  
  4. mitetemo 
  5. kusharabu.


41. Katika mashine manufaa ya kimekanika ni uwiano kati ya:

  1. kani egemeo na kani mzigo
  2. umbali lilipo egemeo na umbali ulipo mzigo
  3. kani mzigo na kani egemeo
  4. umbali ulipo mzigo na umbali lilipo egemeo
  5. kani iliyopo sehemu moja na kani iliyo sehemu nyingine.


42. Bainisha kioo kinachotoa taswira wima inayofanana na kitu halisi na ambayo umbali kati ya kioo ni sawa na umbali kati ya kioo na kitu halisi:

  1. Kioo cha konkevu
  2. Kioo cha bikonkevu
  3. Kioo cha konveksi
  4. Kioo cha prismu
  5. Kioo bapa.


43. Mkondo wa umeme katika sakiti ni ampia 2. Kama nguvu ya umeme ni volti 4, ukinzani katika sakiti hiyo ni:

  1. omu 3.5
  2. omu 4
  3. omu 2 
  4. omu 5
  5. omu 0.5.


44. Chunguza sakiti ya umeme iliyooneshwa katika Kielelezo Na. 3 kisha jibu swali linalofuata.

Kielelezo Na. 3

Sakiti iliyooneshwa katika Kielelezo Na. 3 inalt­waje?

  1. Sakiti mfuatano
  2. Sakiti sambamba
  3. Sakiti kinzani
  4. Sakiti geu
  5. Sakiti pozo


45. Magonjwa ya zinaa huambukizwa kwa njia ya:

  1. kugusana 
  2. kupeana damu
  3. kucheza pamoja 
  4. kuchangia vikombe
  5. kujamiiana


46. Ni chembe chembe zipi za damu katika mwili wa binadamu hushambuliwa na VVU?

  1. Chembe nyekundu
  2. Chembe sahani
  3. Chembe nyeupe
  4. Chembe selimundu
  5. Chembe za plasma.


47. Njia sahihi ya kujikinga na maambukizi ya VVU ni:

  1. kuacha kunywa pombe
  2. kuepuka kushiriki ngono zembe
  3. kushiriki mihadhara ya dini
  4. kusambaza dawa kwa waathirika
  5. kutangaza hadharani majina ya waathirika.


48. Sentensi ipi kati ya zifuatazo ni sahihi kuhusu VVU na UKIMWI?

  1. VVU vinaenezwa na watu waliopevuka tu.
  2. Watu wanaoonekana kuwa na afya hawana VVU.
  3. VVU na UKIMWI huathiri watu wa rika zote.
  4. Wagonjwa wote wanaougua kansa wana VVU.
  5. Chanjo huzuia maambukizo dhidi ya VVU.


49. Huduma inayotakiwa kwa watu wanaoishi na VVU ni:

  1. kuwapa nyumba za kuishi 
  2. kuwapa misaada ya fedha 
  3. kuwapa ushauri nasaha
  4. kuwapa elimu bure
  5. kuwafungulia akaunti benki.


50. Katika uchunguzi wa kisayansi data hukusanywa kwa kutumia mbinu ya:

  1. kusafiri sehemu mbalimbali
  2. kusoma taarifa mbalimbali
  3. kubaini tatizo
  4. kuunda mabunio
  5. kufanya majaribio anuwai


STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2010 Try This  |  

SAYANSI 2010

 SEHEMU A

Chagua jibu sahihi na kuandika herufi inayohusika mbele ya namba ya kilo swali katika karatasi ya kujibia.

1. Ipi kati ya zifuatazo si faida ya michezo kwa afya zetu?

  1. Husaidia kujenga misuli
  2. Huzuia mwili kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara
  3. Husababisha shinikizo la damu
  4. Huleta burudani
  5. Hudumisha afya ya mwili


2. Maji yaliyochanganywa na sukari na chumvi ni huduma ya kwanza kwa mtu. anayesumbuliwa na

  1. Malaria na kuumwa kichwa
  2. Kuhara na kutapika 
  3. Uti wa mgongo na homa ya matumbo
  4. Kifua kikuu na mafua 
  5. Kuvunjika mguu au mkono


3. Moja ya magonjwa yafuatayo si ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya zinaa

  1. UKIMWI 
  2. Trikomona
  3. Kaswende 
  4. Klamedia
  5. Trakoma


4. Ni vitamin ipi kati ya zifuatazo hutengenezwa mwilini kwa kuwepo mwanga wa jua? 

  1. Vitamini A            
  2. Vitamini B
  3. Vitamini C 
  4. Vitamini D
  5. Vitamini E


5. Chanjo ina manufaa gani kwa binadamu?

  1. Hupunguza maumivu 
  2. Huponyesha maradhi
  3. Huzuia magonjwa 
  4. Hurudisha vitamin na madini mwilini
  5. Hurudisha seli chakavu mwilini


6. Ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na bacteria gani?

  1. Wote walioko hewani 
  2. Basili
  3. Plasimodiamu 
  4. Fungi 
  5. Amiha


7. Viwanda havipaswi kujengwa karibu na makazi ya watu kwasababu

  1. ujenzi wake huchukua eneo kubwa
  2. sehemu kubwa ya taka za viwandani huwa na kemikali ambazo ni sumu
  3. mitambo ya viwandani hutoa sauti kubwa hivyo kuathiri ngoma za masikio
  4. viwanda husababisha watu kuhamahama makazi
  5. wenye viwanda hawaweki mazingira yao katika hall ya usafi


8. Vitendo vifuatavyo huharibu vyanzo vya maji isipokuwa

  1. kukata miti
  2. kuchoma misitu
  3. kulisha wanyama wengi kupita kiasi kwenye vyanzo vya maji
  4. kutupa taka za kemikali katika vyanzo vya maji
  5. kuchota maji ya kupikia toka kwenye vyanzo vya maji



9. Asilimia kubwa ya uso wa dunia imefunikwa kwa maji. Sehemu kubwa ya maji haya hupatikana kwenye

  1. bahari 
  2. Mito 
  3. maziwa 
  4. mabwawa 
  5. madimbwi


10. Mahali palipoinuka panafaa zaidi kujenga choo cha shimo kwasababu

  1. ni rahisi kujenga ukuta
  2. harufu itakuwa mbali na usawa wa ardhi
  3. si rahisi kuharibika upesi
  4. maji yatakuwa mbali na usawa wa choo chenyewe
  5. choo hakitafurika kwa muda mfupi


11. Maji yanayobubujika kutoka ardhini hujulikana kwa jina gani?

  1. Bahari 
  2. Ziwa 
  3. Chemichemi 
  4. Bwawa 
  5. Mto


12. Vitu muhimu katika uotaji wa mbegu ni

  1. udongo, mwanga wa jua na maji
  2. udongo, hewa na maji
  3. joto la kiasi, maji na hewa ya oksijeni
  4. joto la kiasi, udongo na mwanga wa jua
  5. maji, udongo na hewa ya kabonidayoksaidi


13. Kundi la viumbe hai waishio majini na nchi kavu hujulikana kama

  1. Amfibia 
  2. Athropoda 
  3. Samaki 
  4. Ndege 
  5. Mamalia


14. Kati ya viumbe wafuatao ni yupi si mamalia?

  1. Popo 
  2. Nyangumi 
  3. Simba 
  4. Sungura 
  5. Mamba


15. Chunguza Kielelezo Namba 1 kwa makini kisha jibu swali lifuatalo

Kielelezo Na.1

Kiumbe aliyeoneshwa katika kielelezo Namba 1 huishi kwa kutegemea

  1. asali
  2. Nyama
  3. nafaka
  4. vyakula vya majini
  5. maada zilizooza


16. Mmea uliochorwa katika kielelezo Namba 2 una sifa ya kuishi wapi?

Kielelezo Na. 2

  1. Kwenye misitu minene
  2. Majini
  3. Kwenye majani marefu
  4. Jangwani
  5. Milimani


17. Kwanini baadhi ya mimea haipukutishi majani yake wakati wa masika?

  1. kuhifadhi maji yake 
  2. kuruhusu transipiresheni
  3. kuhifadhi chakula chake 
  4. kuhifadhi udongo
  5. kuufanya udongo uwe na rutuba



18, Mchoro katika kielelezo Namba 3 unaonesha picha ya ua

Kielelezo 3

Ni sehemu gani  ya ua huvutia wadudu kuja kulichavua

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5


 19. Umeme unaotolewa katika seli kavu, chanzo chake ni nishati gani?

  1. Jua
  2. Kimakanika
  3. Sauti
  4. Sumaku
  5. Kikemikali


20. Kibata alitumia nyutoni 50 kusukuma ukuta kutwa nzima bila mafanikio. Je, lipi sahih: kutokana na tukio hilo?

  1. alitengeneza kazi 
  2. alitumia kani kubwa sana
  3. hakufanya kazi yoyote 
  4. alifanya kazi nzuri
  5. alitumia kani ndogo


21. Endapo pembe mtuo itasomeka nyuzi 60, je pembe akisi itasomeka nyuzi ngapi kioo bapa?

  1.  90° 
  2.  40° 
  3.  30° 
  4.  60° 
  5.  45°


22. Chunguza kielelezo Namba 4 kisha jibu swab linalofuata

Kielelezo 4

Ikiwa umeme unaopita katika sakiti hiyo ampi 5, kiasi cha ukinzani (R) wa waya katika sakiti hiyo ni omu              

  1. 100
  2. 50
  3. 10
  4. 4
  5. 0.4



23. Mzee Juakali mche wa sumaku hewani, Je, ncha ya kaskazini ya sumaku itaelekea upande gani wa dunia?

  1. Kusini 
  2. Kaskazini 
  3. Mashariki
  4. Magharibi 
  5. Kaskazini-mashariki


24. Musa alitumia nyutoni 10 kusukuma mkokoteni umbali wa mita 5. Musa alifanya kazi - cha jouli ngapi?

  1. 15 
  2. 50 
  3. 0.5
  4. 5


25. Katika uchunguzi wa kisayansi kitu gani kinachomfanya mtu kutabiri matokeo?

  1. Kufahamu tatizo 
  2. Kuchunguza kwa muda mrefu
  3. Kuona kwa macho 
  4. Kufanya jaribio
  5. Kugusa kitu


26. Jaribio la kuotesha mbegu limeoneshwa katika Kielelezo Namba 5. Ni kitu gani muhimu kinakosekana kwa mbegu hiyo kuota?

  1. Maji 
  2. Hewa 
  3. Udongo 
  4. Mbolea 
  5. Upepo


27. Milango ya fahamu inayotumika kutambua vitu katika majaribio ya kisayansi ni

  1. pua, macho, ngozi, ulimi na masikio
  2. pua, masikio, ngozi, miguu na ulimi
  3. masikio, ngozi, pua, miguu na mikono
  4. masikio, pua, ngozi, macho na mikono
  5. macho, miguu, ulimi, masikio na pua


28. Data zifuatazo zimepatikana kwa kupima urefu kwa sm wa mimea mitano; 10, 12, 15, 28 na 40. Wastani wa urefu wa mimea yote kwa sm ni

  1. 22 
  2. 50
  3. 27
  4. 38 
  5. 21


29. Kusudi kuu la kuzalisha mbegu mbalimbali ni lipi?

  1. Kupunguza urefu wa mimea 
  2. Kuongeza mazao ya mimea
  3. Kufanya mimea Hale haraka 
  4. Kupata mimea inayostahimili ukame
  5. Kuongeza urefu wa mimea


30. Kati ya vifuatavyo nikipimo kipi kinapima urefu?

  1. Kilogramu 
  2. Sentimita 
  3. Rula 
  4. Volti 
  5. Ampia


31. Umuhimu wa utando wa ozone ni

  1. kuongeza joto kwenye use wa dunia
  2. kupunguza mionzi hatarishi ya jua kutufikia
  3. kupunguza gesi ya kabonidayoksaidi angani
  4. kuongeza mvua duniani
  5. kupunguza baridi


32. Sayari inayongfraa kuliko zote huitwa

  1. Zebaki 
  2. Dunia 
  3. Jupita 
  4. Pluto 
  5. Venasi


33. Dunia hutumia siku ngapi kulizunguka jua?

  1. 3651 
  2. 28 
  3. 24 
  4. 12 
  5. 7


34. Vitu vinavyofanya mfumo wa damu ni pamoja na

  1. moyo, seli hai nyeupe na damu
  2. seli hai nyeupe, self hai nyekundu na mishipa ya damu
  3. moyo, mapafu na damu
  4. seli hai za damu, maji na moyo
  5.  moyo, mishipa ya damu na damu


35. Taka mwili zilizochujwa na figo husafirishwa kwenda kwenye kibofu kupitia mirija iitwayo 

  1. bronchioli
  2. Urethra  
  3. umio
  4. Ureta   
  5. falopia



36. Chunguza Kielelezo Namba 5 cha jino kisha jibu swab lifuatalo

Kielelezo Na. 5

Herufi Z kwenye kielelezo inawakilisha .............

  1. utando
  2. kichwa cha jino
  3. uvungu
  4. mshipa wa jino
  5. ufizi


37. Sehemu gani ya moyo husukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili?

  1. Auriko ya kushoto 
  2. Ventriko ya kushoto
  3. Auriko ya kulia 
  4. Ventriko ya kulia
  5. Vena kava


38. hunguza kielelezo Namba 6 kisha jibu swali linalofuata

Sukari iliyowekwa katika bika iko katika hal. gani ya maada?

  1. Kimiminika
  2. Gesi
  3. Yabisi
  4. Elementi
  5. Kompaundi


39. Chuma kupata kutu ni mfano wa badiliko gani?

  1. Kikemikali 
  2. Kiumbo
  3. Rangi
  4. Kimiminika 
  5. Tungamo


40. Ni kundi lipi la vyakula linawakilisha vyakula vyenye vitamini A?

  1. Chungwa, ndimu, limau
  2. Karoti, maziwa, maini
  3. Chungwa, hamira, maharage
  4. Ndimu, Chungwa, maini


  5. 42. Badiliko la maada lisilokuwa na tofauti katika uzito linaitwaje?

    1. Kikemikali 
    2. Kiugumu
    3. Kiumbo 
    4. Kiurefu
    5. Kiupana


    43. Unyafuzi ni utapiamlo unaosababishwa na

    1. upungufu wa madini ya kalsiamu na fosforasi
    2. kula kupita kiasi
    3. ukosefu wa ayadini mwilini
    4. ukosefu wa protini
    5. ukosefu wa vyakula vinavyotia mwili nishati na joto


    44. Ni viini lishe gani vinavyopatikana katika vyakula vya kujenga mwili?

    1. Protini 
    2. Kabohaidreti
    3. Vitamini 
    4. Madini
    5. Fati


     45. Chunguza mlishano ufuatao kisha jibu swali linalofuata

    Katika mlishano huo nini kitatokea ikiwa duma watahama katika mazingira haya?

    1. Mimea itakauka 
    2. Nyati watapungua
    3. Mimea itaongezeka 
    4. Mimea itapungua
    5. Nyati nao watahama


    STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2009 Try This  |  

    SAYANSI 2009

    SEHEMU A

    Chagua jibu sahihi na andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasi ya kujibia.

    1. Unaweza kumhudumia mtu aliyezirai kwa:

    1. kumpa hewa safi 
    2. kumtingisha kwa nguvu
    3. kumlaza kifudifudi 
    4. kumbonyeza tumboni polepole
    5. kumwekea kitambaa cha maji baridi usoni


    2. . . . . . . . .. husababishwa na upungufu wa virutubisho vya vitamin A.

    1. Utapiamlo 
    2. Ukavu macho 
    3. Matege
    4. Kiribatumbo 
    5. Unyafuzi


    3. Umuhimu wa kadi ya kliniki kwa watoto ni kuwezesha wahusika

    1. kujua tarehe ambayo mtoto alizaliwa
    2. kuhakikisha kuwa mtoto alizaliwa
    3. kufahamu maendeleo ya ukuaji wa mtoto
    4. kupata huduma za kiafya kiurahisi 
    5. kwenda na wakati


    4. Mgonjwa anayeharisha anatakiwa kupatiwa huduma gani ya kwanza?

    1. kumpeleka kwa daktari mapema
    2. kumpa vidonge kupunguza maumivu
    3. kumpa maji yaliyochanganywa limau, sukari na chumvi
    4. kumpeleka kwa mganga wa kienyeji 
    5. kumpa chakula cha kutosha


    5. Njia kuu inayoongoza kueneza virusi vya UKIMWI kwa watu ni:

    1. kutoboa masikio na pua 
    2. kuwekewa damu
    3. kujamiiana 
    4. ajali
    5. kudunga sindano


    6. Panda alikatazwa na mama yake kuchezea konokono. Unafikiria mama yake alikuwa anamwepusha na ugonjwa upi?

    1. kichocho 
    2. kuhara
    3. malaria
    4. malale 
    5. UKIMWI


    7. Todi alifungulia gesi toka kwenye mtungi na kuielekeza kwenye moto. Moto uliwaka zaidi. Je, mtungi ulikuwa na gesi gani?

    1. oksijeni 
    2. kabondayoksaidi 
    3. monoksaidi 
    4. Haidroksaidi
    5. gesi ya upepo


    8. Baadhi ya majanga ya asili ambayo huweza kuhatarisha mimea na misitu ni:

    1. mvua zinazoambatana na tufani, ukame na volcano
    2. moto, ukame na volcano
    3. mvua zilizoambatana na tufani, moto na volcano
    4. moto, ukame na mvua zilizoambatana na tufani
    5. moto, kemikali za mimea na mifugo mingi kupita kiasi


    9. Wakati wa mchana mimea ya kijani hupunguza gesi gani kwenye anga?

    1. kabonidayoksaidi 
    2. naitrojeni 
    3. haidrojeni 
    4. oksijeni 
    5. naitret


    10. Inashauriwa mahali pa kujenga Choo cha shimo pawe:

    1. bondeni karibu na mto
    2. ndani ya nyumba ya kuishi 
    3. mbali kidogo na nyumba ya kuishi
    4. tambarare sana 
    5. karibu sana na nyumba ya kuishi


    11. Iwapo swala katika mlishano ufuatao wataongezeka, lipi litajitokeza kwa haraka? MAJANI → SWALA → SIMBA

    1. majani yatapungua 
    2. simba watakufa
    3. idadi ya simba haitabadilika
    4.  kiasi cha majani hakitabadilika
    5. majani yataongezeka


    12. Baada ya utungisho, kitoto chura huitwa:

    1. lava 
    2. buu 
    3. tunutu 
    4. tedipoli
    5. yai


    13. Sehemu mbili za ua zinazoungana na kuwa stameni ni:

    1. mbegu na pistili 
    2. staili na kikonyo
    3. ovari na sepali 
    4. petali na sepali
    5. filamenti na kichavua


    14. Hatua ya pili katika ukuaji wa mende ni:

    1. lava 
    2. tunutu
    3. buu 
    4. mende kamili
    5. yai


    15. Kwa kawaida mimea hukua kuelekea wapi?

    1. kwenye maji
    2. kwenye mwanga
    3. mwelekeo wa upepo
    4. kwenye rutuba
    5. gizani


    16. Sehemu ya ua ambayo hupokea chavua au poleni huitwa:

    1. staili 
    2. stigma 
    3. ovari 
    4. stameni
    5. ovuli


    17. Mchoro ufuatao unaonesha kiumbe anayeishi majini.

    Kielelezo 1

    Ni sehemu ipi ya mwili wake humsaidia kuogelea?

    1. U
    2. R
    3. T
    4. V
    5. S


    18. Ni ogani ipi inayohusika kubadili seli hai nyekundu za damu kuwa chembechembe za nyongo katika mwili wa binadamu?

    1. ini 
    2. figo 
    3. moyo 
    4. mapafu 
    5. wengu


    19. Vifuatavyo ni vyanzo vya kuzalisha nishati ya umeme isipokuwa:

    1. maporomoko ya maji 
    2. nishati ya jua
    3. ngurumo ya mvua 
    4. fueli 
    5. upepo


    20. Eleza mabadiliko ya nishati yanayotokea katika Kielelezo kifuatacho wakati mvuke unapotumika kuzungusha kata upepo:

    Kielelezo 2
    1. umeme kuwa sauti
    2. sauti kuwa joto
    3. joto kuwa kimakanika
    4. sauti kuwa umeme
    5. umeme kuwa sumaku


    21. Joto husafiri njia ya mpitisho katika maada zipi kati ya zifuatazo?

    1. maji na chuma 
    2. chuma na aluminiamu
    3. aluminiamu na mvuke
    4. hewa na maji 
    5. hewa na chuma


    22. Katika kielelelezo Namba 3, ni mchoro upi unaonesha sakiti sambamba?

    Kielelezo 3


    23. Kati ya mashine zifuatazo ipi ni mashine rahisi?

    1. baiskeli 
    2. pikipiki 
    3. winchi
    4. wenzo
    5. gari


    24. Sehemu kubwa ya nishati ya bayogesi ni:

    1. kabondayoksaidi 
    2. oksijeni 
    3. naitrojeni
    4. gesi asilia 
    5. mvuke


    25. Uchunguzi wa kisayansi unaanza na:

    1. maswali 
    2. uchunguzi 
    3. dhanio
    4. udadisi 
    5. data


    26. Katika jaribio Ia kisayansi data humaanisha:

    1. taarifa ya mambo yanayojitokeza unapofanya jaribio
    2. orodha ya vifaa utakavyotumia kwenye jaribio
    3. taarifa ya jaribio thibiti
    4. mpangilio wa hatua kwa hatua jinsi ya kufanya jaribio
    5. mapendekezo ya hatua za kutatua tatizo


    27. Nyuzi 212 za Fahrenhaiti ni sawasawa na nyuzi za Sentigredi

    1. 100 
    2. 108 
    3. 176
    4. 40
    5. 75


    28. Katika majaribio ya kisayansi ni katika hatua ipi wanasayansi hutumia data kukubalia au kukataa dhanio?

    1. hatua ya kwanza
    2. hatua ya pili
    3. hatua ya tatu 
    4. hatua ya nne
    5. hatua ya tano


    29. Taarifa ya jaribio Ia kisayansi inatakiwa kuzingatia mfululizo wa vipengele vifuatavyo:

    1. lengo, gharama, maoni na mapendekezo 
    2. lengo, vifaa, mbinu, matokeo na hitimisho
    3. lengo, mbinu, matokeo na hitimisho
    4. lengo, vifaa, maoni na mapendekezo
    5. lengo, jaribio lenyewe na mapendekezo


    30. Mpemba alitumbukiza jiwe kwenye kopo chirizi lililojaa maji. Maji yaliyotoka yalikuwa na sentimeta za ujazo 200. Sentensi ipi ni sahihi kuhusu tendo hilo?

    1. maji ni mazito kuliko jiwe
    2. jiwe ni zito kuliko maji
    3. maji yaliyobaki ni machache kuliko yaliyotoka
    4. ujazo wa jiwe ni sawa na wa maji yaliyotoka
    5. uzito wa maji yaliyotoka ni sawa na maji yaliyobaki


    31. Chunguza mchoro ufuatao wa kupwa na kujaa kwa maji, kisha jibu swali lifuatalo:

    Ikiwa maji yatajaa Kaskazini basi yatakupwa pande zipi za dunia?

    1. kusini na mashariki 
    2. kusini na magharibi
    3. mashariki na Magharibi
    4. kaskazini na Maghahribi
    5. kaskazini na mashariki


    32. "Nyota ya asubuhi" ni jina maarufu Ia sayari

    1. Satani 
    2. Pluto 
    3. Mekyuri 
    4. Venasi 
    5. Jupita


    33. Vifuatavyo ni vitu vya asili vianavyopatikana angani isipokuwa kimoja tu ambacho ni:

    1. mwezi
    2. jua 
    3. setilaiti 
    4. vimondo 
    5. sayari


    34. Samaki huishi majini tu na hawezi kuishi nchi kavu. Hii ni kwa sababu kwenye nchi kavu hawezi:

    1. kutembea 
    2. kuruka 
    3. kusikia 
    4. kupumua 
    5. kuona


    35. Ipi kati ya sentensi zifuatazo ni sahihi kuhusu neva mota?

    1. huchukua taarifa kutoka sehemu za mwili kwenda mfumo wa fahamu wa kati 
    2. huchukua taarifa kutoka mfumo wa fahamu wa kati kwenda sehemu za mwili
    3. hupeleka taarifa kwenye mfumo wa fahamu wa kati kwenda sehemu za mwili
    4. huunganisha fahamu katika sehemu za kichwa tu 
    5. hupeleka na kurudisha taarifa katika sehemu za ungwe mgongo


    36. Chunguza mchoro ufuatao kisha jibu swali linalofuata.

    Kielelezo kinaonesha jicho lenye kasoro gani?

    1. kutokuona karibu 
    2. kutokuona vizuri
    3. kutokuona mbali 
    4. makengeza 
    5. lensi ndogo


    37. Wakati wa ujauzito kijuzi hupokea chakula na hewa toka kwa mama kupitia:

    1. uterasi 
    2. plasenta
    3. mirija ya falopiana 
    4. ovari 
    5. mdomoni


    38. Mambo ambayo yanasababisha kutokea kwa kutu kwenye misumari ni pamoja na hewa oksijeni, kingine ni kipi kati ya vifuatavyo?

    1. kabondayoksaidi 
    2. maji 
    3. pamba
    4. aluminiamu 
    5. oksaidi ya zinki


    39. Kitu kikiwa katika hali ya joto kubwa, kikipoa hubadilika hali. Ni katika mtitiriko upi mabadiliko hutokea?

    1. gesi→ kimiminika →yabisi 
    2. yabisi →kimiminika →gesi
    3. gesi→ yabisi →kimiminika 
    4. kimiminika →gesi→ yabisi 
    5. kimiminika →yabisi →gesi


    40. Upungufu wa virutubisho vya madini ya chuma mwilini husababisha:

    1. upungufu wa uzito 
    2. kuwa na uso unaofanana na wa mzee
    3. udhaifu katika mifupa 
    4. damu kukosa wekundu
    5. kupoteza hamu ya kula


    41. Vijijidudu vinavyoweza kusababisha vyakula kuoza ni:

    1. virusi 
    2. plasimodiamu 
    3. bakteria 
    4. mende 
    5. kunguni


    42. Mgonjwa wa homanyongo hushauriwa kula vyakula vyenye:

    1. mboga za majani
    2. protini
    3. sukari kwa wingi 
    4. kiasi kidogo cha sukari
    5. protini na maji kwa wingi


    43. Ni aina ipi kati ya vitamini zifuatazo ambayo hufanya kazi ya kugandisha damu kwenye jeraha?

    1. K
    2. E
    3. D
    4. C
    5. B


    44. Sehemu ya damu inayohitaji chuma kwa wingi wakati wa kutengenezwa ni:

    1. chembe kisahani 
    2. plazma
    3. chembechembe nyeupe 
    4. chembechembe nyekundu 
    5. limfu


    45. Kwa nini majani ya baadhi ya mimea hujikunja wakati wa jua kali?

    1. yanafanya uchavushaji 
    2. yanatengeneza chakula
    3. yasipoteze uelekeo 
    4. yasipoteze maji mengi
    5. yasiharibike na kupoteza rangi


    STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2008 Try This  |  
    SAYANSI 2008

    SEHEMU A

    Chagua jibu sahihi kisha andika herufi inayohusika mbeleya kila swali katika karatasi yakoya kujibia.

    1.  Licha ya kusaidia kujenga misuli michezo huimarisha nini?

    1. Miguu 
    2. Viungo vya mwili
    3. Viungo vya kichwa 
    4. Mikono 
    5. Viungo vya sehemu ya juu ya mwili


    2.  Faida kubwa ya uzazi wa mpango kwa familia ni .........

    1. kuwapa watoto elimu
    2. kufanya idadi ya watoto kuwa kubwa
    3.  kuweza kujenga nyumba imara kwa ajili ya familia
    4.  kuepuka matatizo
    5. kuwa na uwezo wa kutoa huduma zote muhimu kwa familia


    3. Ni kundi lipi kati ya makundi yafuatayo hutoa mafunzo ya Huduma ya kwanza pamoja na huduma yenyewe?

    1.  Msalaba mwekundu
    2. Angaza 
    3. Askari wa zimamoto 
    4. Wasamaria wema 
    5. Askari wa usalama barabarani


    4. Chakula kinachoupatia mwili virutubisho vyote katika uwiano sahihi ni:

    1.  mlo wenye protini 
    2. mlo wenye protini na kabohaidreti
    3. mlo kamili 
    4. chakula kilichopikwa vizuri
    5. chakula kinachonukia vizuri


    5. Namanji anaonekana kupinda miguu. Unafikiri anakosa madini gani?

    1. Kalsiamu
    2. Sodiamu
    3. Magnesiamu 
    4. Chuma 
    5. Aluminiamu


    6.  Yafuatayo ni magonjwa yanayoweza kuzuiwa kwa njia ya chanjo kwa watoto:

    1. Kifaduro, polio, pepopunda na surua
    2. Kuhara, tetekuwanga, surua na homa ya matumbo
    3. Polio, unyafuzi, pepopunda na kifaduro
    4. Tetekuwanga, utapia mlo, surua na polio
    5. UKIMWI, kifua kikuu, pepopunda na kuhara damu


    7.  Degedege husababishwa na:

    1.  ugonjwa wa mafua ya ndege
    2. kikohozi kikali
    3. homa kali 
    4. kipindupindu
    5. UKIMVVI


    8.  Mama Katu ameingia chumbani na kumkuta mumewe ameanguka chini baada ya kushituliwa na umeme. Mama Katu atamsaidia mumewe kwa:

    1.  kumpa maji safi ya kunywa 
    2. kumpa maziwa
    3. kumtikisa kwa nguvu 
    4. kumpulizia hewa
    5. kumwogesha


    9.  Hewa ni mchanganyiko wa:

    1.  Oksijeni 
    2. kabondayoksaidi
    3. gesi 
    4. mvuke 
    5. maji na oksijeni


    10.  Maji katika hali ya mvuke ni:

    1.  Mawingu 
    2. mvua 
    3. barafu 
    4. umande 
    5. unyevu


    11.  Moja kati ya hatua ziifuatazo huzuia mmomonyoko wa udongo:

    1.  Kupunguza wingi wa miti 
    2. Kuchoma misitu
    3. Kupanda miti 
    4. Kukwatua nyasi
    5. Kuongeza idadi ya mifugo


    12 Kiwavi ni lava wa

    1. panzi 
    2. mende 
    3. chura 
    4. kipepeo 
    5. mbu


    13.Jambo lipi linaweza kusababisha kutokea kwa "badiliko chanya" katika maliasili ya mazingira?

    1.  Kuvua samaki kwa kutumia sumu
    2.  Kulima holela kwenye miinuko
    3.  Kukata miti ovyo karibu na vyanzo vya maji
    4. Kuvua samaki kwa kutumia baruti E. Kupanda miti na nyasi


    14.Zifuatazo ni sifa muhimu zinazotambulisha viumbe hai. Unafikiri ni sifa ipi haihusiki?

    1.  Kupumua 
    2. Kukua
    3. Kujitengenezea chakula
    4. Kujongea 
    5. Kuzaliana


    15.Sehemu ya mbegu inayotunza chakula cha mbegu inayoota ni:

    1. ghala
    2. ganda 
    3. embryo
    4. kijusi 
    5. kikonyo


    16. Chunguza jani la mmea lililooneshwa kwenye kielelezo kisha jibu swali linalofuata.

    Jani hilo unaweza kulifananisha na jani la mmea upi kati ya ifuatayo?

    1.  Mpunga
    2.  Mtama
    3.  Kunde
    4.  Mahindi
    5. Mnazi


    17. Nta hutengenezwa kutoka katika ......... ya nyuki.

    1. Matezi 
    2. Mabawa 
    3. Macho
    4. Miguu
    5. Mafumbatio


    18.Sehemu ya ua inayovutia wadudu wanaokuja katika mmea na kusaidia uchavushaji na uchukuaji wa poleni inaitwaje?

    1. Petali 
    2. Sepali 
    3. Stigma 
    4. Kikonyo
    5. Pistili


    19. Mgongo wa chura ni mfupi ili kumwezesha .........

    1. kukimbia 
    2. kulala 
    3. kupaa
    4. kuruka na kutua 
    5. kugeuka


    20.Kipi kati a Vitu vifuata  husafirisha •oto kwa haraka zaidi?

    1. A
    2. B
    3. C
    4. D
    5. E


    21.Mwanafunzi mmoja wa darasa la saba aliweka penseli kwenye glasi yenye maji. Chagua mchoro unaoonesha jinsi penseli itakavyoonekana kati ya ifuatayo:



    22. Ukimwangalia mtu anayekata mti ukiwa mbali utaona kitendo cha kuka?a mti kabla ya sauti ya kuka?a kusikika kwa sababu:

    1. shoka ni butu
    2. sauti husafiri polepole kuliko mwanga
    3. mwanga husafiri polepole kuliko sauti
    4. kazi ya kuka?a mti ni ngumu 
    5. mkataji hatumii nguvu


    23.Chunguza mchoro ufuatao. Kiasi cha mkondo wa umeme ni ampia ngapi?

    1. 0.2 
    2. 2.0 
    3. 12 
    4. 20 
    5. 1.2


    24. Katika vifaa vifuatavyo kipi hutumia umeme mkondo mnyoofu?

    1. Jokofu 
    2. Pasi ya umeme 
    3. Feni 
    4. Jiko la umeme 
    5. Tochi


    25. Eneo lote lililoathiriwa na kani ya sumaku hujulikana kama:

    1. ncha za sumaku 
    2. ncha ya kaskazini
    3. ncha ya kusini 
    4. unga wa chuma 
    5. uga wa sumaku


    26.Ndugu Chapakazi alitumia kani ya nyutoni 10 kunyanyua mzigo kwa umbali wa mi?a 5. Je, ndugu Chapakazi alifanya kazi kiasi gani?

    1. joule 100 
    2. nyutoni 20 
    3. joule 20 
    4. joule 50 
    5. kilo 10


    27.Moja kati ya zifuatazo ni mashine tata:

    1. Mkasi
    2. Ngazi 
    3. Kisu 
    4. Tochi 
    5. Baiskeli


    28. Mwanasayansi alipitisha gesi katika kimiminiko Fulani ambapo kiligeuka rangi na kuwa rangi ya maziwa. Je kimiminiko hicho ni kipi na gesi hiyo ni ipi?

    1. Maji ya chokaa - oksijeni 
    2. Maji ya chungwa — kabondayoksaidi
    3. Maji ya chokaa - naitroni 
    4. Maji ya chokaa - kabonidayoksaidi
    5. Maziwa - oksijeni


    29.Hali ya kuchunguza mambo au matukio kwa kujiuliza ni:

    1. unajimu
    2. udadisi 
    3. usomi 
    4. uelewa 
    5. uwajibikaji


    31. Diana alichukua kiazi na kukichonga ili kutengeneza shimo katikati, na ndani yake akaweka myeyuko wa chumvi, kisha akakiweka katika bakuli lenye maji kidogo. Baada ya saa nne maji yaliongezeka katika lile shimo lenye chumvi. Je, Diana aligundua nini?

    1. Maji hutoka kwenye myeyuko hafifu kwenda kwenye myeyuko mzito
    2. Mimea hupata maji kwa njia hiyo
    3. Chumvi ni nyepesi kuliko maji
    4. Viazi havipatikani na chumvi E. Hitimisho


    31.  Katika uandishi wa ripoti ya jaribio la kisayansi jambo la nne kuandikwa ni:

    1. njia 
    2. vifaa 
    3. matokeo 
    4. kusudi 
    5.  hitimisho


    32.  Kielelezo kifuatacho kinaonyesha urefu wa wanafunzi katika sentimeta walipopimwa mwishoni mwa mwaka jana katika Shule ya Msingi Pangani. Je, Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi wangapi?

    1. 200 
    2. 00 
    3. 100 
    4. 1000 
    5. 50


    33.  Matunda hudondoka kutoka juu ya miti. Hii inadhihirisha kuwepo kwa kani:

    1. mnyanyuo
    2. mburuto
    3. mvutano
    4. msukumo
    5. mkabala


    34. Mkojo huchujwa katika:

    1. ini 
    2. mapafu
    3. figo 
    4. kibofu
    5. bandama


    35. Vipimo vya msingi vya umeme ni:

    1. waya, betri, omu
    2. joule, betri, balbu
    3. joule, ampia, betri 
    4. omu, volti, ampia
    5. meta, kilogramu, sekunde


    36. Chakula kilichomeng'enywa husharabiwa na zilizopo kwenye utumbo mdogo.

    1. puru 
    2. kongosho 
    3. vilasi 
    4. umio 
    5. virusi


    37. Mama Mambosasa ana watoto mapacha wasiofanana. Je, nini kilitokea ndani ya tumbo la uzazi Ia mama huyo?

    1.  Mayai mawili yalirutubishwa na gametiume tofauti
    2.  Mayai manne yaligawanyika mara mbili
    3.  Yai lililorutubishwa lilijigawa mara mbili
    4.  Mayai mawili yalirutubishwa na gametiume moja
    5. Mayai matatu yalirutubishwa na gametiume tofauti


    38. Chunguza kielelezo kifuatacho na kisha jibu swali linalofuata.

    Sehemu inayooneshwa kwa herufi M huitwa:

    1.  dendraiti 
    2. aksoni 
    3. saitoplazimu
    4. nyukliasi 
    5. kisahani cha neva


    39. Oksihaimoglobini inapofika kwenye seli zinazohitaji oksijeni hutengeka kutoa oksijem ambayo hutumika kwa ajili ya:

    1. kuondoa maradhi 
    2. kuzalisha joto la mwili
    3. transpiresheni 
    4. respiresheni 
    5. kurekebisha damu


    40. Kiumbe hai kifuatacho kinasemekana kinachangia kuharibu mazingira kwa kiasi kikubwa.

    1. Miti 
    2. Ng'ombe 
    3. Binadamu 
    4. Kunguru 
    5. Tembo


    41. Lipi kati ya haya yafuatayo ni badiliko la kikemikali?

    1. Kugandisha maji kuwa barafu
    2. Kuyeyusha mafuta ya mgando
    3. Kufanyika kwa mawingu na mvua
    4. Mshumaa kuyeyuka
    5. Chuma kupata kutu


    42. Katika ukuaji wa binadamu ni kati ya umri wa miaka mingapi ambao ushauri nasaha unahitajika zaidi?

    1. 0 -5 
    2. 6- 10
    3. 11 - 18 
    4. 19-25 
    5. 26-30


    43. ?li kuzuia kutokwa na damu kwenye fizi tunashauriwa kula vyakula gani?

    1. Ndimu, machungwa, mapapai na mboga za majani
    2. Wali, maharage, nyama na samaki
    3. Viazi, ndizi, mihogo na mtama
    4. Nyama, samaki, maziwa na mayai
    5. Karanga, maharage, korosho na nazi


    44. Shule ya Songanane ilibainika kuwa na wanafunzi wenye nyongea. Je, tatizo hilo linatokana na kukosekana kwa virutubisho gani?

    1. Protini 
    2. Mafuta
    3. Wanga
    4. Vitamini 
    5. Chumvi


    45. Zifuatazo ni aina za utapiamlo isipokuwa:

    1. ukavumacho 
    2. kwashakoo 
    3. unyafuzi
    4. kiribatumbo 
    5. surua


    STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2007 Try This  |  

    SAYANSI 2007

    SEHEMU A

    Chagua jibu sahihi kisha andika herufi inayohusika mbele ya namba ya kila swali katika karatasi ya kujibia.

    1. Umuhimu wa vyakula vya kabohaidreti mwili ni

    1. Kujenga mwili
    2. Kulinda mwili 
    3. Kutia nguvu 
    4. Kuweza kufikiri 
    5. Kuongeza joto


    2. Ukiwa katika chumba chenye giza na ghafla taa ikawashwa kitatokea nini kuhusu jicho?

    1. Mboni ya jicho itaongezeka ukubwa
    2. Mbona ya jicho itabaki vilevile
    3. Lenzi ya jicho itabinuka
    4. Mboni ya jicho itapungua ukubwa
    5. Kelele za nguvu zitasikika


    3. Kikohozi kikavu, homa, kutoka jasho usiku na kukohoa damu ni dalili za . . . . . .

    1. Kifua kikuu 
    2. Tetekuwanga 
    3. Pepopunda
    4. Homa ya matumbo 
    5. Kifaduro


    4. Michoro katika kielelezo namba 1 inawakilisha seli katika mwili wa binadamu ambazo kazi zake ni:

     Kielelezo Na. 1
    1. Kuzuia na kukinda mwili
    2. Kusafirisha oksijeni
    3. Kugandisha damu 
    4. Kurekebisha joto 
    5. Kusafirirsha taka mwilini


    5. Mtu mwenye kiribatumboni ni rahisi zaidi kupata ugonjwa gani?

    1. Moyo na msukumo mkubwa wa damu
    2. Kansa 
    3. Unyafuzi
    4. Kuvia kwa ukuaji wa akili 
    5. Kwashakoo


    6. Vinyesi na vitu vya wanyama na mimea vilivyooza

    1. Huufanya udongo usifae kwa kilimo
    2. Vinakaribisha wadudu wengine wanaoharibu mazao
    3. Vinaongeza mbolea ya mboji kwenye udongo 
    4. Havina umuhimu katika udongo
    5. Vinatumika kama chombo kwa wavuvi.


    7. Mwanga na sauti vina tabia moja tu. Je tabia hiyo ni ipi?

    1. Kupinda
    2. Kuakisi 
    3. Kusharabiwa
    4. Kupita kwenye vakyumu 
    5. Kusambaa


    8. Kuhifadhi vyakula katika jokofu ni njia ambayo ..

    1. Hufanya vyakula vikae muda mrefu bila kuharibika
    2. Inapunguza kazi ya kupika mara kwa mara
    3. Inapoteza ladha na kuvifanya vioze iwapo vitakaa siku nyingi 
    4. kugeuza chakula kuwa barafu
    5. inapunguza gharama ya kwenda sokoni.


    9. Ukiweka sarafu ya shilingi 20 katika beseni lenye maji, sarafu hiyo inaonekana mepansa juu. Hali hiyo hutokea kwa sababu .........

    1. Sarafu hiyo ni nyepesi
    2. Macho yanamatatizo
    3. Mwanga umenyooka 
    4. Maji ni kidogo
    5. Mwali wa mwanga hupinda unapoingia katika maji


    10. Kwa nini chupa za soda na bia hazijazwi hadi pomoni?

    1. Kwa ajili ya nafasi ya gesi
    2. Husaidia kufungwa chupa kwa urahisi
    3. Kuruhusu kutanuka wakati ya joto
    4. Kupunguza gharama
    5. Ikijazwa huweza kumwagikia mnywaji


    11. Volkano hai hutoa kimiminika kizito katika uso wa dunia kiitwacho:

    1. Lava 
    2. Kreta 
    3. Gesi 
    4. Volcano 
    5. Maji


    12. Kwa nini kwa kawaida mwanga unaonekana kwanza kabla ya muungurumo wa radi ingawa vyote vinatokea pamoja?

    1. Mwanga unamawimbi makubwa kuliko sauti
    2. Mishipa ya fahamu ya macho inafanya kazi haraka kuliko mishipa ya fahamu ya kusikia
    3. Mwendokasi wa mwanga ni wa haraka kuliko sauti
    4. Mwanga na sauti kwa kawaida husafiri wima 
    5. Mawimbi ya sauti hayasafiri katika hewa


    13. Vipi kati ya Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha uchafuzi wa hewa?

    1. Maji machafu ya viwandani, spiriti na ujenzi wa biashara
    2. Moshi, Majivu na mbolea
    3. Moshi wa viwandani na matokeo ya kuungua kwa petrol
    4. Misitu asili, viwanda na mbolea
    5. Mbolea, mboji na maji machafu ya viwandani



    14. Ni kiumbe kipi kati ya vifuatavyo huishi kwenye maji?

    1. Inzi 
    2. Buibui 
    3. kaa 
    4. Panzi 
    5. Mende


    15. Ukuaji wa mbu hupitia katika hatua/kuu nne. Mtiririko sahihi wa ukuaji huo ni  . . . . . . . . .

    1. Yai, pupa, lava, mbu 
    2. Pupa, yai, lava, mbu
    3. Yai, lava, pupa, mbu 
    4. Lava, yai, pupa, mbu
    5.  Pupa, lava, yai mbu


    16. Kitendo cha mmea kufuata mwanga katika kielelezo na 2 huitwa .........

    Kielelezo Na. 2
    1. Kutembelea
    2. Kukua
    3. Kujongea
    4. Kuitikia kichocheo
    5. Kuhisi


    17, Chanzo cha chakula kwa wanyama ni .........

    1. Mmea
    2. Mimea na nyama
    3. Mimea kwa hebivora na nyama kwa canivora
    4. Maziwa 
    5. Maharage


    18. Vyombo vya kupikia Vina mikono iliyotengenezwa kwa mbao na plastiki kwa sababu ...m

    1. Haipitishi joto haraka
    2. Haipitishi joto
    3. Husharabu joto
    4. Huakisi joto 
    5. Hutunza joto kwa muda mrefu


    19. Kuta, sarafu na dari ya nymba ya utangazaji vimewekewa Vitu Iaini ili.

    1. Kupunguza sauti 
    2. kuakisi
    3. Kuongeza sauti na nguvu
    4. kufanya sauti kuwa Iaini na safi
    5. Kupunguza mwamgwi


    20. Kuna uhusiano gani kati ya sumaku na umeme.

    1. Zote ni nishati za kemikali
    2. Zote ni sakiti za umeme
    3. Kuliko na sumaku lazima kuwe na umeme
    4. Kuliko na umeme lazima kuwe na sumaku
    5. Zote zinatoa nishati ya mwanga


    21. Katika mchoro wa sakiti ya umeme inawakilisha:

    1. Seli kavu 
    2. Seli 
    3. Fyuzi 
    4. Transfoma
    5. Adapta


    22. Ni kundi lipi linalowakilisha mashine rahisi?

    1. Nyundo, shoka, kisu, mkasi 
    2. Mkasi, gari, toroli na msumari
    3. Shoka, skrubu, mkasi na cherehani 
    4. Kitasa, toroli, baiskeli na msumeno
    5. Baiskeli, gari, cherehani na nyundo


    23. Wakati mtu anasukuma toroli, mikono yake na mishikio ya toroli inafanya .

    1. Egemeo 
    2. Mzigo 
    3. Jitihada 
    4. Nyenzo
    5. Nihati


    24. Dira huelekea upande wa kaskazini wa dunia kwa sababu .........

    1. Kuna nguvu ya sumaku ndani ya dunia inayoingiliana
    2. Watu wamezoea zaidi ncha ya kaskazini
    3. Sio rahisi kupotea kama upo cha ya kaskazini
    4. Wavumbuzi wa mwanzo waligundua zaidi
    5. Nchi ya kaskazini iko juu kuliko nchi ya kusini


    25. Ni mabadiliko gani yatatokea kama mtu akipumulia kwenye uso wa kioo?

    1. Kuganda 
    2. Kuyeyuka 
    3. Kuvukishwa
    4. Matonesho 
    5. Kutanuka


    26. Vitundu vilivyoko kwenye mimea jamii ya kunde Vina bacteria ambao husharabu na kubadili . kuwa naitrojeni.

    1. Naitrojeni 
    2. Yurea 
    3. Fosforasi
    4. Haidrojeni
    5. Salfeti ya ammonia


    27. Chunguza kwa makini kielelezo namba 3 na kisha jibu swali linalofuata

    Kielelezo Na. 3

    Nini ujazo wa jiwe baada ya kutumbukiza katika maji

    1. srn3 15 
    2. sm3 45
    3. sm3 30
    4. sm3 5
    5. sm3 20


    28. Myeyuko wa majivu yaliyotokana na majani ya mgomba huweza kubadili karatasi ya litmasi .........

    1. Bluu kuwa nyekundu 
    2. Nyekundu kuwa bluu
    3. Bluu kuwa njano 
    4. Nyekundu 
    5. Bluu


    29. Ripoti ya jaribio la kisayansi huandikwa kwa mpangilio ufuatao

    1. Njia, vifaa kusudi, matokeo, hitimisho
    2. Njia, vifaa, kusudi, hitimisho, matokeo
    3. Njia, vifaa, matokeo, kusudi, hitimisho
    4. Kusudi, njia, vifaa, matokeo, hitimisho
    5. Kusudi, vifaa, njia, matokeo, hitimisho


    30. Tezi iliyo katika ubongo inayofanya kazi ya kuchochea tezi zingine kufanya kazi huitwa

    1. Kongosho
    2. Gonadi
    3. Tezi ya adrenali
    4. Tezi ya thairoidi
    5. Tezi ya pituitari


    31. Ni kipi kati ya mishipa ya damu ifuatayo hupeleka damu kwenye mapafu?

    1. Vena kava
    2. Ateri ya pulmonari 
    3. Aota
    4. Vena ya pulmonari 
    5. Vena ya renali


    32. Chembe nyekundu za damu hutengenezwa katika sehemu gani ya mwili?

    1. Uroto mwekundu 
    2. Moyo 
    3. Tumbo 
    4. Ini 
    5. Mapafu


    33. Ipi ni njia bora ya asili ya uzazi wa mpango?

    1. Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana
    2. Kutumia njia ya kitanzi
    3. Kutumia sindano
    4. Kutumia vidonge vya uzazi wa majira
    5. Kutojamiiana katika kipindi cha hatari


    34. Sehemu ya mbegu ambayo huhifadhi chakula cha mmea kwenye udongo ni ..

    1. Embryo 
    2. Testa
    3. Kotiledoni 
    4. Epikapi 
    5. Kianza mche


    35. Mayai ya kike hutengenezwa kwenye

    1. Korodani 
    2. Mirija ya falopia
    3. Uterasi
    4. Ovari 
    5. Mlango wa uzazi


    36. Matokeo ya mwisho ya myeyusho wa protini ni .........

    1. Asidi za fati na gliseini 
    2. Asidi za amino
    3. Glukosi
    4. Asidi ya haidrokloriki E. Sukari laini


    37. Sehemu ya ua ambayo ni sawa na ogani ya uzazi ya kike katika mwili wa binadamu ni ... ......

    1. Stigma 
    2. Stameni 
    3. Ovyuli
    4. Ovari 
    5. Nihati


    38. Tunashauriwa kupanda miti kwa wingi sehemu zilizo kame ili

    1. Kuzuia mmomonyoko wa udongo
    2. Kuleta kivuli 
    3. Kupata kuni
    4. Kupata mbao na matunda
    5. kusaidia kuleta mvua


    39. Watu waishio katika sehemu ya baridi hupaswa kula zaidi vyakula aina ya mafuta kwa sababu vyakula hivyo . .. . . . . . .

    1. Hulinda mwili 
    2. Hujenga mwili
    3. Huleta joto 
    4. hutuliza njaa 
    5. Huleta nguvu


    40. Tunapopiga picha kutumia kamera tunatumia moja ya sifa mwanga sifa hiyo ni . 

    1. Kuakisiwa kwa mwanga 
    2. Mwanga kusafiri katika mstari mnyoofu
    3. Kupinda kwa mwanga
    4. Kusambaa kwa mwanga
    5. Kusharabu kwa mwanga


    41. Ua (Ethi) la radi hutengenezwa kwa shaba kwa sababu shaba

    1. Haipati kutu
    2. Haipitishi umeme
    3. Haiathiriwi na maji
    4. Hupambana kirahisi na kemikali
    5. Hupitisha umeme kirahisi


    42. Ni ugonjwa upi kati ya mangojwa yafutayo unaweza kumpata mtu kwa kula nyama ambayo haikuiva ?

    1. Punye 
    2. Kwashakoo
    3. Tegu 
    4. Malaria 
    5. Unyafuzi


    43. Kipi kati ya vifuatavyo husababisha kansa ya mapafu?

    1. Kuvuta tumbaku
    2. Kunywa bia
    3. Chanjo dhidi ya kipindupindu
    4. Kunywa Chai 
    5. Kunywa soda


    44. Iwapo mtu akitengemea sana pombe na hawezi kuiacha, ana tatizo la hali ijulikanayo kama .........

    1. Utapiamlo
    2. Ulevi wa kupindukia
    3.  Kuzimia
    4. Ungonjwa unaoua seli za ini
    5. Unyong'onyefu


    45. Nini kati ya vifuatavyo ni chanzo kikuu cha vitamin C?

    1. Jibini 
    2. Machungwa
    3. Maharage 
    4. Nyama
    5. Mayai


    STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2006 Try This  |  
    SAYANSI 2006

    SEHEMU A

    Chaguajibu sahihi kisha andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasi yakoya kujibia.

    1. Katika mambo yafuatayo, lipi linawakilisha badiliko la kiumbo?

    1. Maji kuwa mvuke
    2. Kuchoma karatasi
    3. Asali kubadilika kuwa pombe
    4. Chuma kupata kutu 
    5. Kuni kuwa mkaa


    2. Mojawapo ya yaliyoorodheshwa hapa chini husaidia kuhifadhi mazingira nayo ni:

    1. kukata miti kwa ajili ya kuni na kujenga;
    2. kubadilibadili mazao ya kupanda shambani;
    3. kutumia mbolea ya chumvi chumvi; 
    4. kusafisha mashamba kwa kukatua;
    5. kufuga ng'ombe kwa wingi.


    3. Madini iliyo ngumu kuliko nyingine zote ni ipi?

    1. Almasi
    2. Makaa ya mawe 
    3. Shaba 
    4. Ulanga 
    5. Dhahabu


    4. Nyama, samaki, maziwa na mayai ni vyakula vya:

    1. kutia nguvu 
    2. kulinda mwili 
    3. kujenga mwili 
    4. kutia joto mwili 
    5. kuhitaji mbinu bora za kuhifadhi.


    5. Mimea hujipatia maji na madini ya chumvi chumvi kwa njia inayowakilishwa na herufi L katika mchoro ufuatao. Njia hiyo ni ipi?

    1. mjongeo wa maji na madini
    2. translokesheni
    3. fototropizimu
    4. Osmosis
    5. fotosinthesis


    6. Gurudumu kapi ni mashine ... ... ...

    1. tata itumikayo kupandisha vitu juu
    2. imara iliyoshikishwa na gurudumu dogo
    3. yenye meno yanayoingiliana na ya gurudumu jingine
    4. rahisi itumikayo kupandisha vitu juu 
    5. nayotumika kufungia maunzi pamoja.


    7. Namba gani katika mchoro ufuatao inawakilisha tezi itoayo homoni ambayo humfanya mtu asipate ugonjwa wa kisukari?

    1. 1
    2. 2
    3. 3
    4. 4
    5. 5


    8. Meli inaelea katika maji (baharini au ziwani) kwa sababu ina:

    1. nafasi kubwa tupu iliyojaa hewa ndani
    2. nafasi yenye hewa kidogo
    3. uzito mdogo kuliko maji
    4. mstari wa plimsoli unaozuia maji
    5. ujazo nene mdogo kuliko maji


    9. Jaribio hili (chunguza kwa makini mchoro ufuatao) hudhihirisha kvvamba mwanga

    1. husafiri na kugawa vitu sehemu mbili
    2. husafiri katika mstari mnyoofu
    3. husafiri na kupinda upitapo katika media tofauti
    4. husafiri ndani ya maji kwa kujikunja
    5. husafiri na kusababisha vitu kupinda


    10. Mnyororo wa baiskeli hupitia gia mbili (tazama mchoro ufuatao). Gia iliyozungushwa na tairi la nyumba ina meno 20 na ile iliyounganishwa na pedali ina meno 50. Iwapo pedali zitafanya mizunguko miwili, tairi la nyuma litazunguka mara .........

    1. Tano 
    2. Nne 
    3. Tatu
    4. Moja 
    5. Nyingi


    11. Sehemu zinazofanya mfumo wa mzunguko wa damu ni damu yenyewe,

    1. ubongo na mishipa ya damu 
    2. mapafu na mishipa ya damu
    3. moyo na mishipa ya damu 
    4. moyo na mishipa ya fahamu
    5. moyo na ubongo


    12. Uzito wa mzigo x katika mchoro ufuatao ni:

    1. kilo 200
    2. kilo 2.5
    3. kilo 25
    4. kilo 250
    5. kilo 36.2


    13. Tendo Ia kuvunjavunja na kubadili chakula ili kiweze kunyonywa au kufyonzwa na mwili hujulikana kama

    1. kumeng'enya 
    2. kurutubisha 
    3. kusharabu 
    4. eksrisheni 
    5. respiresheni


    14. Chunguza mchoro ufuatao kwa makini. Je, ni kitu kipi chembe zake zimeachana sana?



    15. Ugonjwa upi kati ya magonjwa yafuatayo husababishwa na ukosefu wa vitamini?

    1. Kifua kikuu 
    2. Kiseyeye
    3. Tetekuwanga 
    4. Malaria
    5. Kuhara


    16. Usumaku unaweza kuondolewa kwa kufanya yafuatayo:

    1. kugongagonga na kupasha joto ikiwa imening'inizwa Mashariki-Magharibi
    2. Kuining'iniza Mashariki-Magharibi na kuiosha
    3. Kuizungusha koili na kupitisha umeme
    4. Kuizungushia koili na kuichoma
    5. Kuigongagonga na kuzungushia koili


    17. Uvuvi wa samaki kwa kutumia baruti ni njia mojawapo ya:

    1. kukuza sayansi
    2. kuua magugu maji yanayochafua mazingira
    3. kuharibu mazalio ya samaki na kuchafua mazingira
    4. kuondoa aina ya samaki wakubwa
    5. kuwafukuza papa wakali wasiwale samaki wadogo wadogo


    18. Sehemu inayooneshwa kwa herufi Z katika mchoro ufuatao huitwa

    1. nyukliasi
    2. vakyuli
    3. saitoplazimu
    4. ukuta wa seli
    5. epithiliamu


    19. Ni ugonjwa upi kati ya magonjwa yafuatayo huweza kuzuiwa kwa chanjo?

    1. Kifaduro
    2. Kisonono 
    3. Malaria 
    4. Homa ya matumbo 
    5. Kipindupindu


    20. Kati ya matendo yafuatayo, ni yapi huongeza kasi ya mmomonyoko wa ardhi?

    1. Kufuga mifugo mingi na kukata miti
    2. Kilimo cha sesa na kutandaza nyasi
    3. Kilimo cha matuta na umwagiliaji
    4. Kufuga mifugo mingi na kupanda miti 
    5. Kupanda miti na kuchoma mbuga


    21. Mbegu zinazotawanywa na wanyama Zina sifa ya kuwa:

    1. na miiba 
    2. nyepesi
    3. na gamba gumu
    4. nzito
    5. zinabebeka kwa urahisi


    22. Chunguza vizuri mchoro ufuatao. Je, matokeo yake nini?

    1. Glopu itawaka
    2. Glopu haitawaka
    3. Seli haifanyi kazi
    4. Glopu itapasuka
    5. Glopu iaungua


    23.Ipi katika sehemu zifuatazo, damu hupambana na viini vya magonjwa?

    1. Chembe hai nyekundu 
    2. Chembe kisahani
    3. Chembe hai nyeupe 
    4. Maji maji ya damu 
    5. Protini za damu


    24. Mlishano sahihi katika mfululizo ufuatao ni upi?

    1. Majani ya miti → mchwa → binadamu → kuku 
    2. Majani ya miti → mchwa → kuku → binadamu
    3. Mchwa → majani ya miti →  kuku → binadamu
    4. Kuku→  binadamu → majani ya miti→  mchwa
    5. Binadamu→  majani ya miti→  kuku → mchwa


    25. Alama ifuatayo inawakilisha

    1. ukinzani 
    2. taa ya umeme
    3. galvanomita
    4. amita 
    5. seli


    26. Ukimwi unaweza kuenezwa kwa njia ipi kati ya zifuatazo?

    1. Kushikana mkono na mtu aliyeathirika
    2. Kuchangia vyoo na bafu na mtu aliyeathirika
    3. kujamiiana
    4. Kuogelea pamoja na mtu aliyeathirika
    5. Kuumwa na wadudu kama vile mbu na mbung'o


    27. Chunguza kwa makini mchoro ufuatao. Kazi ya sehemu iliyooneshwa na herufi M ni:

    1. kulinda mbegu isiharibiwe na wadudu
    2. kuota na kuwa shina
    3. kutunza chakula kwa ajili ya mche unaochipua
    4. kutunza maji
    5. kufyonza chakula ardhini


    28. Katika magonjwa yafuatayo yapi yanatokana na urithi

    1. Surua na pumu
    2. Uzeruzeri na sickle cell anemia (selimundu)
    3. Kisukari na matende
    4. tetekuwanga na sickle cell anemia (selimundu)
    5. Uzeruzeru na matege


    29. Hatua muhimu katika kufanya utafiti wa kisayansi ni: (i) kukusanya data; (ii) kufanya jaribio; (iii) kutafsiri data; (iv) kutambua tatizo; (v) kuchambua data. Je mfululizo upi ni sahihi?

    1. (i) → (iv)→ (v)→ (iii)→ (ii) 
    2. (iii) →(iv)→ (i)→ (v)→ (ii)
    3. (iv) →(ii)→ (i)→  (v)→ (iii)
    4. (iii)→ (iv)→ (ii)→ (i)→  (v)
    5. (ii)→ (iii)→ (iv)→ (i)→ (v)


    30. Bahati aliandaa jaribio kama inavyoonekana katika mchoro ufuatao. Aliipasha joto chupa kwa kuimwagia maji ya moto. Je, nini kitatokea kwa maji yaliyomo kwenye mrija?

    1. Yatashuka chini
    2. Yatapanda juu
    3. Yatabaki palepale
    4. Yataanza kuchemka
    5. Yataanza kuvukishwa


    31. Mwali wa mwanga hupinda upitapo katika:

    1. media ya aina moja 
    2. media tofauti
    3. maji 
    4. glasi 
    5. hewa


    32. Athari mojawapo ya kuongezeka viwanda kwa mazingira ya dunia ni:

    1. kuongezeka kwa ajira
    2. kuongezeka kwa bidhaa za kuuza
    3. kuongezeka kwa utaalamu wa uzalishaji
    4. kuongezeka kwa joto
    5. kuongezeka kwa manufaa ya kiuchumi


    33. Mojawapo ya sehemu za mwili zifuatazo hutumika kutoa taka mwilini nayo ni:

    1. pua 
    2. utumbo
    3. ngozi 
    4. kucha 
    5. vinyweleo


    34. Chanzo cha nishati yote iliyoko duniani ni:

    1. jua 
    2. mwezi 
    3. mimea 
    4. wanyama 
    5. maji


    35. Mimea iotayo jangwani huwa na majani membamba kama sindano. Hii husaidia:

    1. mmea kukua haraka
    2. mmea usiliwe na wanyama
    3. kuhifadhi maji
    4. fotosinthesis ifanyike kwa urahisi
    5. kupata mwanga wa jua kiurahisi


    36. Mpangilio wa ripoti ya jaribio huwa na sehemu kuu tano ambazo ni 1. kusudi, 2. matokeo 3. vifaa 4. hitimisho 5. Njia. Mfululizo upi ni sahihi kwa ripoti iliyo nzuri?

    1. 1→ 3→ 5→ 2→ 4
    2. 3→ 2→ 4→ 1→ 5
    3. 4→ 3→ 1→ 5→ 2
    4. 2→ 1→ 5→ 4→ 3
    5. 5→ 1→ 3→ 2→ 4


    37. Sayari iliyo kubwa kuliko zote ni .........

    1. Satani 
    2. Yuranus 
    3. Jupita
    4. Neptuni 
    5. Dunia


    38. Sehemu kuu tatu za pistili ni 

    1. ovari, staili na filamenti
    2. stigma, staili na kichavua
    3. stigma, staili na ovary
    4. ovari, stigma na filamenti 
    5. staili, kichavua na stigma


    39. Tunashauriwa kupeleka watoto kliniki ili kupata chanjo za kuzuia magonjwa yafuatayo:

    1. Surua, malaria, upungufu wa damu na ukimwi
    2. Kifaduro, dondakoo, ukimwi na malaria
    3. Surua, dondakoo, pepopunda na kifaduro
    4. Dondakoo, upungufu wa damu, kipindupindu na homa ya uti wa mgongo
    5. Kipindupindu, malaria, surua na ukimwi


    40. Ili mmea uweze kusanisi chakula chake wakati wa mchana unahitaji hewa ya:

    1. oksijeni
    2. naitrojeni 
    3. ozone 
    4. haidrojeni 
    5. kabondayoksaidi


    41. Njia pekee ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa trakoma ni:

    1. kula vyakula vyenye vitamini A
    2. kula vyakula vya aina ya wanga
    3. kuosha macho kwa maji safi
    4. kuvaa miwani ya kuzuia mwanga
    5. kupima macho mara kwa mara


    42. Katika kufanya majaribio ya kisayansi, hatua tunapoweka kanuni ni ipi?

    1. Hitimisho 
    2. Matokeo 
    3. Bunio 
    4. Vifaa 
    5. Lengo


    43. Mchoro ufuatao unaonesha

    1. kupatwa kwa jua 
    2. majira ya mwaka
    3. mfumo wa jua 
    4. kupatwa kwa mwezi 
    5. kusikia na kuona


    44. Mojawapo ya sifa za viumbe hai ni pamoja na kuzaliana. Sifa zingine ni:

    1. kuhisi na kusikia
    2. kujongea na kusikia
    3. kupumua na kujongea
    4. kuona na kukua
    5. kusikia na kuona


    45. Sehemu iliyooneshwa kwa herufi B katika mfumo wa uyeyushaji chakula katika mchoro ufuatao ina asidi ya:

    image

    1. naitriki
    2. sitriki
    3. asetiki
    4. haidrokloriki
    5. salifyuriki


    STD VII SAYANSI NECTA EXAM OF YEAR 2005 Try This  |  

    SAYANSI 2005

    Chaguajibu sahihi na andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasiya kujibia.

    1. Zilizoorodheshwa hapa chini ni sehemu za jicho la binadamu isipokuwa

    1. siliari
    2. retina 
    3. mboni 
    4. shata 
    5. irisi


    2. Usambazaji wa chakula mwilini hufanywa na:

    1. damu 
    2. maji 
    3. hewa
    4. misuli
    5. neva


    3. Kemikali inayotumika kutambua iwapo chakula Fulani ni cha aina ya wanga ni:

    1. besi 
    2. alkoholi 
    3. aside 
    4. alkali
    5. ayodini


    4. Ombwe katika chupa ya chai (kielelezo namba 1) huzuia upotevu wa joto kwa njia ya:

    Kielelezo Na. 1
    1. kuakisi
    2. mpitisho
    3. msafara na mpitisho
    4. mnururisho
    5. msafara na mnururisho


    5. Taswira halisi hufanywa na vitu vyenye tabia ya:

    1. kutupa mwanga kwenye kiwambo
    2. kukusanya mwanga 
    3. kutawanya mwanga
    4. kuruhusu mwanga kupenya
    5. kuzuia kupinda kwa mwanga


    6. Mbung'o husababisha ugonjwa uitwao

    1. matende
    2. surua
    3. kipindupindu 
    4. malale
    5. malaria


    8. Kiini cha ugonjwa kinachooneshwa katika kielelezo namba 2 kinaitwa

    Kielelezo Na. 2
    1. bacteria
    2. plasmodiamu
    3. kirusi
    4. amiba
    5. fungi


    9. Uga wa sumaku ni eneo

    1. lililoko kwenye sumaku
    2. ambalo unga wa chuma huonekana
    3. ambalo nguvu ya sumaku hupatikana
    4. linaloonesha sehemu za kaskazini na kusini za sumaku


    10. Wakati wa kiangazi mimea hupukutisha majani kwa sababu ya:

    1. kuruhusu majani mapya yaote
    2. kukomaa sana
    3. kuongeza rutuba ardhini
    4. kuruhusu maua yaote 
    5. kupunguza upotevu wa maji


    11. Shinikizo la damu hutokana na:

    1. mafuta 
    2. ateri kuwa kubwa
    3. kupasu a kwa vena 
    4. mgandamizo wa mishipa
    5. vena ku kubwa


    12. Ni muhimu kuchukua tahadhari zifuatazo wakati wa vita isipokuwa:

    1. kusafisha mazingira kwa kukata miti
    2. kujenga nyumba imara 
    3. kuhifadhi chakula
    4. kuchimba mahandaki 
    5. kuhamia mahali pengine


    13. Mlo kamili ni ule wenye mchanganyiko ufuatao:

    1. muhogo, maharage, mayai, maziwa na tunda
    2. tunda, mayai, wali, karanga na nyama
    3. mkate, mchicha, kunde, karanga na tunda 
    4. ugali, mayai, samaki, wali na tunda
    5. mchicha, karanga, mayai, maharage na tunda.


    14. Sayari hutofautiana na nyota kwasababu sayari:

    1. ni kubwa kuliko nyota 
    2. zina mwanga wa asili
    3. zipo katika hali ya gesi 
    4. hazizunguki jua
    5. huzungukwa na mwezi au miezi


    15. Ulinganifu wa rula inayooneshwa katika kelelezo namba 3 utapatikana tu iwapo uzito wa P utakuwa gm .

    Kielelezo 3
    1. 46
    2. 16
    3. 10 
    4. 40 
    5. 24


    16. Watu wanaofanya mazoezi ya viungo wanapaswa kula chakula chenye wingi wa:

    1. protini
    2. kabohaidreti
    3. vitamin D 
    4. vitamini C 
    5. madini


    17. Herufi J katika kielelezo namba 4 inawakilisha mshipa unaotoa damu kutoka kwenye moyo unaoitwa:

    Kielelezo Na. 4
    1. venakava
    2. auriko
    3. ventriko
    4. vena
    5. aorta


    19. Nyakati za joto kali, si vema kuvaa nguo nyeusi kwasababu nguo hizo:

    1. huakisi mwanga 
    2. hukinga joto
    3. huakisi joto
    4. husharabu joto 
    5. hupindisha nuru.


    20. Kitumi cha umeme kinachobadili mkondogeu wa umeme kuwa mkondo mnyofu huitwa:

    1. rektifaya 
    2. transista
    3. amplifaya
    4. resista. 
    5. transfoma


    21 . . . . . . . . . ni ugonjwa utokanao na ukosefu wa chakula bora:

    1. Kuhara damu 
    2. Unyafuzi 
    3. Ukimwi
    4. Kipindupindu 
    5. Ukoma


    22. Ili kujikinga na upungufu wa damu, mama mjamzito anashauriwa kula vyakula vyenye:

    1. wanga 
    2. mafuta
    3. chumvi za madini 
    4. protini
    5. sukari


    23. Ndege inayoonekana katika kielelezo namba 5 itaweza kupaa iwapo kani ya mwimn (mnyanyuko) itakuwa kubwa kuliko kani ya uvutano na kani ya msukumo itakuwa kubwz kuliko.

    Kielelezo Na. 5
    1. kani zuizi
    2. kani mwondoko
    3. kani mburuto
    4. uzito wa eropleni
    5. mchapuko


    24- Viungo vifuatavyo hutumika kuongeza ladha na harufu nzuri katika chakula:

    1. pilipili, bilinganya na bizari
    2. bizari, pilipili na bamia 
    3. karafuu, bizari na bamia
    4. bilinganya, karafuu na pilipili 
    5. bizari, pilipili na karafuu


    25. Damu safi huzunguka kutoka kwenye ... .... ..... kwenda sehemu zote za mwili:

    1. figo 
    2. moyo 
    3. mishipa 
    4. maini 
    5. mapafu


    26. Katika kielelezo namba 6, herufi S inawakilisha

    Kielelezo Na. 6
    1. ovari 
    2. kibofu
    3. figo
    4. ureta
    5. korodani


    27. Kauri ni aina gani ya madini yenye sifa ya:

    1. kung'ara 
    2. ugumu kuliko madini mengine
    3. kunyumbuka 
    4. kunatanata
    5. kuwa na rangi ya manjano


    28. Hatua muhimu za kupitia ili kutengeneza sumaku kutumia msumari na sumaku moja ni:

    1. kukwaruza msumari kuelekea pande mbili
    2. kuambukiza msumari usumaku
    3. kuzipangilia atomi za msumari
    4. kuviringisha waya wa umeme kwenye msumari 
    5. kukwaruza msumari kuelekea upande mmoja


    29. Nyota inayong'ara zaidi katika anga ya kusini inaitwa:

    1. Alpha centauri 
    2. Cassiopeia 
    3. Little dipper 
    4. Big dipper 
    5. Gemini


    30. Bayogesi ni gesi maalumu itokanayo na mchanganyiko wa:

    1. kaboni dayoksaidi, metheni na oksijeni
    2. metheni, mvuke wa maji na kaboni dayoksaidi
    3. mvuke wa maji haidrojeni na oksijeni
    4. metheni, oksijeni na naitrojeni
    5. oksijeni, kaboni dayoksaidi na naitrojeni


    31. Kazi mojawapo ya paneli za nishati ya jua ni:

    1. kuunguza takataka za karatasi
    2. kukokotoa mahesabu 
    3. kuchemsha maji
    4. kuzalisha umeme 
    5. kugandisha maji


    32. Mbinu rahisi ya kujua ukubwa wa vitu visivyo na maumbo halisi ni kutumia kitu chenyewe, kopo la eureka:

    1. flaski ya mviringo na maji 
    2. maji na chupa
    3. glasi na maji 
    4. silinda ya kupimia maji
    5. mizani na maji


    33. Ovyule katika kielelezo namba 7 inawakilishwa na herufi:

    Kielelezo Na. 7
    1. P
    2. Q
    3. R
    4. S
    5. T


    34. Mtoto anapozaliwa huweza kufanya yafuatayo:

    1. kulia, kunyonya maziwa ya mama na kuvuta hewa
    2. kunyonya maziwa ya mama, kucheka na kulia
    3. kuvuta hewa, kuona na kucheka
    4. kusikia, kuvuta hewa na kunusa
    5. kutabasamu, kusikia na kulia


    35. Faida mojawapo ya wadudu wanaoruka kutoka ua moja kwenda jingine ni

    1. kutoa taarifa ya mvua
    2. kutoa harufu nzuri
    3. kuchavusha maua 
    4. kupendezesha mazingira 
    5. kutengeneza asali


    36. Binadamu anapotembea hatelezi na kuanguka kwa urahisi kwasababu ya kani:

    1. mvutano 
    2. umeme 
    3. joto 
    4. msuguano
    5. kemikali


    37. Mpangilio wa kani za sumaku unaooneshwa katika kielelezo namba 8 hutokea wakati:

    Kielelezo Na. 8
    1. ncha za kusini na kaskazini zimetazamana
    2. ncha za kusini na kusini zimetazamana
    3. Sumaku ya umbo la duara inapotazamana na sumaku yenye umbo la U
    4. Sumaku yenye umbo U inapokabiliana na yenye Kielelezo 8 umbo la chungu.
    5. ncha za kaskazini na kaskazini zimetazama.


    38. Sehemu zifuatazo hufanya kazi sawa ya kuhifadhi gamete za uzazi kwa binadamu:

    1. mirija ya falopio na mirija ya manii
    2. uume na uke
    3. korodani na uterasi
    4. ovari na uume
    5. ovari na korodani


    39. Sauti haiwezi kusafiri katika:

    1. maji 
    2. vakyumu
    3. maada yabisi
    4. hewa
    5. kioo


    40. Katika kielelezo namba 9 kiasi cha ukinzani katika R2 baada ya kufungwa ni omu .........

    Kielelezo Na. 9
    1. 6.4
    2. 4.5
    3. 6.0
    4. 2.0
    5. 8.0


    41. Udhaifu wa sayansi upo katika kushindwa kuthibitisha:

    1. uwepo wa jua
    2. dunia kulizunguka jua
    3. baadhi ya imani potofu
    4. matatizo yatokanayo na ushirikina
    5. teknoIojia za kisasa


    42. Mbolea ya NPK ni mchanganyiko wa viasili vya:

    1. naitrojeni, fosforasi na kalsiam
    2. naitrojeni, salfa na fosforasi
    3. fosforasi, salfa na naitreti
    4. naitrojeni, potasiam na fosforasi
    5. naitreti, potasiam na kalsiam


    43. Ugonjwa wa surua huenezwa kwa njia ya:

    1. inzi 
    2. sindano 
    3. kugusana
    4. mbu
    5. hewa


    44. Aina ya udongo unaopitisha maji kwa urahisi na haraka zaidi ni

    1. tifutifu 
    2. mboji
    3. mchanga
    4. mfinyanzi 
    5. udongo mchanganyiko.


    45. Kemikali inayotumika kuua wadudu kwenye maji ya kunywa huitwa

    1. klorini 
    2. kalsiam 
    3. florin
    4. kabonidayoksaidi
    5. ayodini


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

   Click Here To Access You Scheme(ONLY IF YOU A HAVE CODE)