SAYANSI 2012
SEHEMU A
Chagua jibu sahihi na andika herufi yake kwenye nafasiya kujibia
1. Baadhi ya ajali na maafa yatokanayo na nguvu za asili ni . . . . . . . . .
- mvua kubwa, umeme, kimbunga
- radi, kimbunga, mvua kubwa
- umeme, madaraja, kimbunga
- mitambo, mafuriko, miti
Chagua Jibu
2. Wanyama wanaokula nyama wana . . . . . . . . .
- pembe ndefu na kali
- mikia mipana na mifupi
- meno makali na kucha kali
- pembe kali na kucha kali
Chagua Jibu
3. Mbu wanaosambaza vimelea vya malaria huuma ... ... ...
- usiku tu
- mchana tu
- usiku na mchana
- usiku wa manane
Chagua Jibu
4. Zifuatazo ni njia za kumsaidia mtu aliyezirai isipokuwa ... ... ...
- Mweke mgonjwa katika sehemu salama yenye hewa ya kutosha.
- Inua miguu ya mgonjwa kuruhusu damu iende kichwani.
- Mvue viatu na kulegeza mkanda wake
- Kama hapumui umwagie maji ya baridi mwili mzima.
Chagua Jibu
5. Maji huganda katika nyuzijoto . . . . . . . . .
- 1000 C
- 360C
- 0 0 C
- 36.90 C
Chagua Jibu
6. Milango ya fahamu ina . . . . . . . . . katika uchunguzi.
- udhaifu
- uhakika
- ubunifu
- tofauti
Chagua Jibu
7. Mikono (mishikio) ya pasi na vikaangio hutengenezwa kwa mbao kwa sababu
- mbao hupendezesha pasi na vikaango
- mbao ni kipitisho hafifu cha joto
- mbao huharibika haraka
- mbao ni kipitisho kizuri cha joto
Chagua Jibu
8. Kipi kati ya vifuatavyo ni chanzo kisicho cha asili cha mwanga? . . . . . . . . .
- Jua
- Radi
- Nyota
- Moto
Chagua Jibu
9. Ni aina gani ya nguo haitokani na viumbe hai? Ni nguo za .... .....
- nailoni
- silki
- pamba
- sufu
Chagua Jibu
10. Rangi ya kijani katika mmea huitwa
- usanisi
- umbijani
- usanisi nuru
- majani
Chagua Jibu
SEHEMU B
Jaza nafasi zilizoachwa wazi
11. Hewa iliyo katika mwendo huitwa . . . . . . . . .
Fungua Jibu
12. Joto kutoka kwenye moto hufikia ngozi zetu kwa njiaya . . . . . . . . .
Fungua Jibu
13. Taswira ni matokeo ya kioo
>. . . . . . . . . kinasambazwa na konokono kutokana na kukojoa na kujisaidia haja kubwa kwenye vyanzo vya maji.
Fungua Jibu
15. Maji katika hali ya yabisi huitwa . . . . . . . . .
Fungua Jibu
16. N cha za sumaku zinazotofautiana zikikaribiana . . . . . . . . .
Fungua Jibu
17. Mwanga unapotoka media moja kwendz nyingine nini hutokea? . . . . . . . . .
Fungua Jibu
SEHEMU C
Andika Ndiyo au Hapana
18. Hewa ya kaboni dayoksaidi inasaidia moto kuwaka . . . . . . . . .
Fungua Jibu
19. Chuma kinapopashwa moto hutanuka . . . . . . . . .
Fungua Jibu
20. Chembe chembe hai nyeupe husaidia kulinda mwili dhidi ya magonjwa . . . . . . . . .
Fungua Jibu
SEHEMU D
Oanisha fungu 'A' na fungu B kwa kuweka herufiyajibu sahihi
FUNGU A | FUNGU B |
21. Sepali 22. Fagio 23. Minyoo 24. Mwangwi 25. Kapani | - Kitu kinachoruhusu kiasi kidogo cha mwanga kupenya
- Sehemu ya ua yenye rangi, huvutia wadudu na ndege
- Mashine rahisi daraja la tatu
- Sauti iliyosharabiwa
- Sehemu ya ua yenye rangi ya kijani, hulinda ua
- Mashine rahisi daraja la pili
- Kula mboga na matunda yasiyooshwa.
- Sauti iliyoakisiwa
- Kitu kinachoruhusu mwanga kupenya
- Hupima uzito
- Kipima pembe
|
Fungua Jibu