SAYANSI 2011
SEHEMU A
Chagua jibu sahihi na andika herufi yake kwenye karatasiya kujibia
1.Tunapaswa kuoga kila siku ili . . . . . . . . .
- kuchangamsha mwili na kuondoa magonjwa
- kuondoa harufu mbaya na kuzuia magonjwa ya ngozi
- kupendeza na kuonekana nadhifu
- kunukia vizuri na kupendeza sana
Chagua Jibu
2 Inatupasa kuepuka kula vyakula vinavyosababisha meno kuoza: Mfano wa vyakula hivyo ni . . . . . . . . .
- peremende, machungwa na ndizi
- peremende, biskuti na mananasi
- peremende, keki na biskuti
- peremende, keki, biskuti na maziwa
Chagua Jibu
3. Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula vyenye protini . . . . . . . . .
- Nyama, maharage, samaki na mayai
- Maharage, ndizi samaki na wali
- Samaki, nyama, kunde na mhogo
- Ndizi, maharage, mayai na nyama
Chagua Jibu
4. Vifuatavyo ni vyanzo vya umeme isipokuwa . . . . . . . . .
- jenereta
- jua
- sufuria
- betri
Chagua Jibu
5. Kifaa kinachotumika kupimia vimiminika kama vile maji na mafuta ya taa huitwa . . . . . . . . .
- Themometa
- Silinda kipimo
- Barometa
- Pima maji
Chagua Jibu
6. Vishikio vya pasi, vikaangio na masufuria hutengenezwa kwa mbao ili kuvifanya . . . . . . . . .
- vipendeze
- viwe vyepesi
- visiunguze mikono
- visiharibike upesi
Chagua Jibu
7 Mtu anayeota moto hupata joto kwa njia . . . . . . . . .
- mnunurisho na msafara
- mpitisho na mnunurisho
- myuko na mpitisho
- mgandamizo wa hewa
Chagua Jibu
8. Ni kundi lipi la vitu vifuatavyo vinaelea kwenye maji? . . . . . . . . .
- Meli, mpira na kijiko
- Meli, boti na msumari
- Mpira, boti na sindano ya kushonea
- Boti, mpira na kipande cha ubao
Chagua Jibu
9. Zifuatazo ni sifa zinazomwezesha mnyama kuruka . . . . . . . . .
- Mifupa yenye hewa, mabawa na mwili uliochongoka
- Mabawa, mwili uliochongoka na mwili nwororo
- Mwili mwororo, mifupa yenye hewa na mwili uliochongoka
- Mabawa, mwili mwororo na mwili uliochongoka
Chagua Jibu
10. Mojawapo kati ya makundi yafuatayo ya wanyama hutaga mayai . . . . . . . . .
- Kuku, popo na mamba
- Bata, chura na mbwa
- Kuku, bata na mbu
- Popo, kinyonga na kuku
Chagua Jibu
SEHEMU B
Jaza nafasi zilizoachwa wazi
11. Joto husafiri kwa njia zipi? . . . . . . . . . . . . . . . na . . . . . . . . . . . . . . .
Fungua Jibu
12. Taja milango ya fahamu . . . . . . . . . . . . . . .
Fungua Jibu
13. . . . . . . . . . . . . . . . katika ramani huelezea kwa kifupi kile kilichokusudiwa kuoneshwa katika ramani.
Fungua Jibu
14. Ni njia gani ambayo joto husafiri na kufikia maji yaliyoko kwenye birika katika mchoro hapo chini?
Fungua Jibu
15. Virusi vya UKIMWI (VVU) daima hushambulia chembe chembe . . . . . . . . . . . . . . za damu.
Fungua Jibu
16. Jua ni chanzo kikuu cha . . . . . . . . . . . . . . duniani.
Fungua Jibu
17. Mwanga husafirishwa katika mstari . . . . . . . . . . . . . .
Fungua Jibu
SEHEMU C
Andika Kweli au Si Kweli
18. Maji siyo sehemu ya mlo kamili . . . . . . . . . .
Fungua Jibu
19. Sumaku huvuta vitu vilivyotengenezwa kwa chuma au shaba . . . . . . . . .
Fungua Jibu
20. Katika nyenzo daraja la pili, mzigo upo kati ya jitihada na egemeo . . . . . . .
SEHEMU D
Fungua Jibu
Oanisha maneno ya Fungu A na Fungu B ili kupata jibu sahihi
FUNGU A | FUNGU B |
. 21. Taswira 22. Nguo za hariri 23. Husababisha upofu kwa watoto wachanga 24. Ogani inayotusaidia kutambua harufu 25. Hutumika katika kitendo cha usanisi wa chakula | - Kaswende
- Hutokana na manyoya ya kondoo
- Husharabu sauti
- Oksijeni
- Matokeo ya kupinda kwa mwanga
- Kabonidayoksaidi
- Hutokana na buu wa nondo
- Kisonono
- Huakisi sauti
- Matokeo ya kuakisi mwanga
- Pua
- Ngozi
|
Fungua Jibu