USHAIRI UCHAMBUZI SUBJECT NOTES
CHAPTER : 1  WASAKATONGE

UHAKIKI WA FANI KATIKA USHAIRI

Fani katika Ushairi wa Wasakatonge

MWANDISHI: TAASISI YA KISWAHILI, ZANZIBAR

WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS

MWAKA: 2001

JINA LA KITABU : WASAKATONGE

Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande wa maudhui mambo yanayoelezwa mengi yanaigusa jamii ya sasa. Masuala ya maadili, siasa, uchumi, ukombozi wa kiutamaduni changamoto na suluhisho ya matatizo yanayoikumba jamii yanaendana na wakati wa sasa. Hivyo upya wa malenga wapya ni kweli. Kifani pia Malenga wapya wameweka muundo na mtindo wa kisasa.

MUUNDO

Tunapohakiki muundo katika ushairi tunaangalia idadi ya mistari katika ubeti. Ubeti huweza kuwa na mistari miwili, mitatu, minne na kuendelea. Aina za muundo zimepewa istilahi maalum kuutofautisha aina moja na nyingine mfano mashiri yenye mistari miwili katika ubeti ni Tathnia. Imetumika miundo tofautitofauti katika diwani hii. Mfano:

  • Tathlitha:Haya ni mashairi ambayo yana mistari mitatu kwa kila beti, mengi ya mashairi haya ni ya kisasa. Mfano ni shairi la“Hali halisi”, “Puuzo”, “Ua”, “Kuunge”, “Tunzo”.Shairi la Ua.“Ua limejituliza mtini laning’inia,Mwenyewe laniliwaza, furahani lanitia, Ua sasa limepea, macho walikodolea.”
  • Tarbia:Haya ni mashairi yenye mistari mine. Mfano ni shairi la“Kitendawili”, “Mkulima”, “Majonzi”, “Bahari”, “Samaki mtungoni” “Kifungo”,na mengine mengi.Shairi la“Kifungo.” “Miaka imeshapita, sasa najiamkia,Naanza bila kusita, bahati kujitafutia,Hapo nitapoipata, mola jishukuria,Kifungo kimenichosha, minyororo nafungua.
  • Takhmisa:Haya huwa na muundo wa mistari mitano katika kila ubeti. Mfano ni mashairi ya“Siharakie maisha”, na “Israfu”.Shairi la“Israfu”. “Mali ulojichumia,Ni yako nakubalia,Lakini kiangalia,Vipi unaitumia,Mwenzangu nakuusia israfu haifai.”
  • Sabilia:Haya ni mashairi yenye mistari kuanzia sita na kuendelea. Mfano ni shairi la“Punda”na “Pasua uwape ukweli”.Shairi la“Punda”. “Toka ulipozaliwa, maishayo ni kizogo,Hujapata kuenziwa, waishi tiriigivyogo,Nawe hujajielewa, u kiumbe hu kigogo,Kama ungefadhiliwa, usingebeba mzigo, Hakika ulionewa, hustahili kipigo,Haki umeitambua, idadi japo kidogo.”

MTINDO

Imetumika mitindo ya aina zote mbili. Kwanza wametumia mtindo wa kisasa. Huu ni mtindo ambao haufuati kanuni za urari wa vina na mizani katika beti pia huitwa mashairi huru. Mtindo mwingine ni mtindo wa kimapokeo, huu hufuata kanuni na sheria zote za vina na mizani katika utunzi wake. Mara nyingi huwa na mistari minne katika kila ubeti.

Mfano wa mashairi yaliyotumia mtindo wa kisasa ni mashairi ya“Pasua uwape ukweli”, “Haki” “Payuka

Pia mfano wa mashairi ya kimapokeo ni shairi la“Mkulima”, “Bahari”, “Tuyazingatie haya” “Nipate wapi mwingine”.

MATUMIZI YA LUGHA

Diwani ya malenga wapya imetumia lugha yenye ubunifu bora wa kisanaa.Vilevile ni lugha rahisi na sanifu inayoeleweka kwa hadhira lengwa.

Tamathali za Semi

  • Tashibiha:“Nizikwe kama wezangu, nisitupwe kama paka” -Shairi la“Nini wanangu”.“Hata pamoja muweko, ubaguzi umezama,kama nguzo” -Shairi la“Tunzo ubeti wa nne”.“Mfanowe kama radi, chini inapoanguka”.-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Nikabaki kama ng’onda” -Shairi la“Nipatieni dawa”.“Maisha ni kama njia”-Shairi la“Maisha ni kama njia”.“Yameotewa na kombe, mithili gome la mti”-Shairi la“Bahari ubeti wa pili”.
  • Tashihisi:“Ewe ulimi sikia” -Shairi la“Ulimi”.“Haki wa tutisha,tusikuandame,kwa matendo yetu” –Shairi la“Haki ubeti wa kwanza”.“Njiwa ameishanitoka, nipate wapi mwingine”-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Samaki wasikitika, kudai walikotoka, Wote wamekasirika, uhuru wanachotaka,”-Shairi la“samaki mtungoni”.
  • Sitiari:“wamejipa uwezo wa Rabuka” – “Mpaka lini”“Paka shume jigeuza” – “Kwanini?”“mshumaa ” – “Hali halisi”

Mbinu nyingine za kisanaa

  • Onomatopea/ tanakali sauti:“kokoriko”- “Mkulima”“Parakacha” – “kwanini”.
  • Takriri:“Charuka” – “charuka”
  • Tashititi:“Nasikia mnatunga mwatungani washairi?” “mwabwaja mwasema nini”

Matumizi ya semi

  • Methali:“Simwamshe asilani aliyelala usingizini” – “Payuka”“Fahali wapiganapo, nyasi ndio huumia”- “Sokomoko baharini”“Subira yavuta heri”- “Siharakie maisha”

Matumizi ya taswira

  • “Samaki” – wanyonge – “samaki mtungoni”
  • “Ua” – mpenzi – “Ua”
  • “Punda”-wanyonge – “Punda”
  • “Mvuvi” – wanyonyaji – “Samaki mtungoni”
  • “Njiwa” – mpenzi – “Nipate wapi mwingine”
  • “Baharini” – nchi – “Sokomoko”
  • “Abiria”- wananchi –“Sokomoko”

UHAKIKI WA MAUDHUI KATIKA USHAIRI

Maudhui katika Ushairi wa Wasakatonge

DHAMIRA

Kupinga unyonyaji na ukandamizwaji.

Mashairi ya“Wasakatonge”, “Mvuja jasho”, “Sikuliwa sikuzama”, “Madikteta”ni mashairi yanayopinga na kukemea sula la unyonyaji na ukandamizwaji wa watu wanyonge wa tabaka la chini. Mwandishi amesema haya makusudi ili kukomesha mambo haya kwani huendelea kukuza utaaka katika jamii. Anaishauri serikali kuweka mikakati ya kuwakomboa wanyonge. Mfano katika shairi la“wasakatonge”anasema:

Pia katika shairi la“Mvuja jasho”mwandishi anawashauri wanyonge kushirikiana ili kujikomboa.

Kupigania haki na ukweli

Mwandishi pia anaona upo umuhimu wa jamii kutafuta na kuisimamia haki ya kweli. Anaona kuwa suala la haki likizingatiwa katika jamii itaepusha matatizo kama vile ya migogoro nk. Mfano wa mashairi ni shairi la“Kosa”, “Marufuku”.Mfano katika shairi la“Kosa”anasema:

Mwandishi ameonesha hali halisi ya baadhi ya wananchi walio wengi ambao kipato chao bado ni duni. Anaona sababu ya hali hii ni mifumo mibovu ya kiuchumi inayoendelea kukuza utabaka katika jamii kati ya walio nacho na wasio nacho mfano katika shairi la “Walalahoi”anasema:

Mashairi mengine ni“Waasakatonge”na“Mvuja jasho”

Kupiga vita matabaka katika jamii

Matabaka ni suala lisilo zuri katika jamii kwani husababisha walio chini kuendelea kukandamizwa na walio juu kiuchumi, kisiasa nk. Mfano wa mashairi yanayopinga ni “Miamba” na “Wasakatonge”. Mfano akatika shairi la “Miamba”

Umuhimu wa kutunza amani

Mwandishi analizungumzia suala la amani katika shairi la“Afrika”.Bado anaona jamii bila amani haiwezi kuendelea. Watu huhitaji amani ya kuishi pamoja na sio kwa vigezo vya ukabila au utaifa. Mfano anasema katika moja ya beti zake:

Suala la uongozi

Hapa uongozi umejadiliwa katika pande zote yaani uongozi mzuri na mbaya. Lakini mwandishi ana lengo moja la kuwafanya viongozi wasio waadilifu kubadilika na walio waadilifu kuacha. Anazungumzia kiongozi bora anatakiwa aweje anamfananisha na nahodha katika shairi la“Nahodha”anasema;

Mwandishi anafananisha nahodha wa ngalawa na nahodha wa nchi. Anaona kiongozi bora ni Yule anayeongoza kwa matakwa ya wananchi na sio matakwa yake binafsi. Anawataka viongozi walioshindwa kutawala waachie madraka kwa wenye uwezo huo. Pia yapo mashairi mengine kama vile“Madikteta”, “Saddam Hussein” ‘Unyama”ambayo yanakemea uongozi wa mabavu na unyonyaji. Haoni umuhimu wote kwaviongozi kutawala kwa mabavu bali watumie sheria na demokrasia ya kweli.

Vilevile anazungumzia viongozi walio wasaliti. Anaona kuwa viongozi wa aina hii ndio wanaokwamisha mendeleo. Walipewa madaraka lakini wanayatumia vibaya na kushindwa kutekeleza waliyoahidi. Mfano wa mashairi ni“asali lipotoja” na “waramba nyayo

Ukombozi wa wanawake

Wanawake wakiwa ni watu muhimu sana katika jamii mwandishi anaona kuna umuhimu wa wao kuheshimiwa na kupewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za kimaendeleo. Anayasema haya katika mashairi ya “Wanawake wa Afrika”, “tohara”, “Mwanamke”, na “Mama ntliye”.Mfano katika shairi la“wanawake wa Afrika” anasema.

Pia mwandishi anapinga mila mila potofu kama vile tohara kwa wanawake katika shairi la“Tohara”.Kwani ina madhara makubwa kwa mwanamke kama vile kifo.

Suala la mapenzi na ndoa

Mwandishi amejadili kwa kiasi kikubwa kuhusu mapenzi ya kweli na ya dhati. Mfano katika mashairi ya “Nakusabiliya”, “Tutabakia wawili” “Nilinde” “Mahaba”.Mfano katika shairi la“mahaba”anasema;

Anakemea mapenzi yasiyo ya kweli ya usaliti. Mfano katika shairi la“Sili nikashiba” ”Si wewe?Mfano katika shairi la“Sili nikashiba”anasema juu ya usaliti;

Kupinga ukoloni mamboleo

Huu ni ukoloni ambao pamoja na nchi kupata uhuru wa kujitawala lakini bado huendelea kupitia njia zingine kuwakandamiza watu. Mwandishi anakemea hili na kuitaka serikali kuaangalia kwa makini suala hili.mfano katika shairi la“Wafadhiliwa” “Bundi”,na“Fahali la dunia”.Mfano katika shairi la “Wafadhiliwa”anasema;

Ukombozi wa kiuchumi

Suala la jamii nkukomboka katika masuala ya uchumi ni jambo la msingi sana. Mwandishi ankisemea hili katika shairi la“Klabu

Maadili mema na maonyo

Maadili mema ndio msingi jkatika jamii. Mtu anapoenda kinyume na makubaliano ya jamii huyo huhesabiwa kuwa amepotoka kimaadili. Mwandishi amejadili mambo mbalimbali kuhimiza maadili mema na maonyo. Mfano ni;

  • Kupinga uovu:Katika shairi la “Kansa”, “Mtemea mate mbingu” anapinga suala la uovu nahimiza kutenda wema. Mfano katika shairi la“Mtemea mate mbingu”.
  • Kupinga mapenzi ya jinsia moja:Hili ni tatizo kubwa kwa jamii ya sasa. Kwani tamaduni ambazo si zetu zinavamia kwa kasi jamii ya leo. Mwandishi ameliona hili na kulisema katika jamii. Anaeleza matatizo ya kuwa na mapenzi ya jinsia moja katika shairi la“Jiwe si mchi.”
  • Tamaa sio nzuri:Mwandishi anakemea suala la tamaa. Anawashauri watu kuridhika na walivyojaliwa kwani tamaa mbele mauti nyuma. Anayasema haya katika shairi la “Si wewe?”
  • Umuhimu wa kujibidisha katika kazi:Ili upate mafanikio si budi kujibidisha tena kwa moyo wote. Mwandishi anasema kuwa vitu vizuri havipatikani bure tu. Bali mtu anapaswa kushughulika haswa. Mfano katika shairi la“Mcheza hawi kiwete”anafananisha bidii katika kazi na uchezaji wa ngoma.
  • Umuhimu wa kusoma na kuitumia vizuri elimu:Mwandishi pia anaona kuna umuhimu wa wanajamii kuwa na elimu kwani elimu ndio dira ya maisha. Si hivo tu anawaasa wanajamii kuitumia vizuri elimu pindi wanapoipata. Watoemchango chaya katika maendelo na maadili ya jamii badala ya kuchochea mmomonyoko wa maadili na kukwamisha uchumi. Amebainisha haya katika shairi la “Wasomi”;
  • FALSAFA: Mwandishi wa kitabu hiki anaamini kuwa matatizo katika jamii yanasababishwana watu wachache wanaonyonya watu wengine mfano katika masuala ya uchumi. Tabaka la wasakatonge linaendelea kukandamizwa na kuwa chini zaidi kwa sababu ya wachache tu. Anaamini ili jamii iweze kuwa na haki na usawa upo ulazima wa kufuta matabaka na kuboresha vipato vya watu wa chini. Aidha anaamini pia jamii ili iwe na amaendeleo na amani watu wanapaswa kuenenda katika maadili yaliyo mema.
  • MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi katika diwani hii ni wa kiyakinifu. Kwa sababu matatizo kama vile, hali ngumu ya kimaisha na kuwepo tabaka la walalahoi ni mifumo mibovu ya kiuchumi ikienda sambamba na matumizi mabaya ya pesa za umma, uzembe katika kazi, unyonyaji na unyanyasaji. Anatoa suluhisho linalowezekana katika jamii kwa kukemea yote yale yanayoenda kinyume na maadili sambamba na kuwawajibisha viongozi wasiotimiza wajibu wao. Anaona wanyonge wanaweza kukomboka kwa kuwa na ushirikiano nakusimamia ukweli popote pale.
  • MSIMAMO: Msimamo wa S. Khatib ni wa kimapinduzi. Analenga kupindua maovu, kupindua viongozi wasio waadilifu, anapindua mambo ambyo ni kinyume na maadili ya jamii zetu lakini pia anapinga suala la utabaka kataika jamii. Mambo hayo yanatufanya tuone kuwa kweli mwandishi analenga kuibadilisha jamii. Hajayafumbii macho maovu na dhuluma zinazoendelea katika jamii bali ameyaweka bayana ili watu wayafahamu na kujirekebisha.

UJUMBE

  • Kufanya kazi kwa bidii ndio msingi wa maendeleo.
  • Suala la utabaka katika jamii si zuri, hivyo si budi kulipiga vita.
  • Unyonyaji, ukandamizwaji na unynyasaji haufai kwani unadidimiza walio chini na kuwatweza wachache.Elimu ni ufunguo wa maisha.
  • Wasomi wanapaswa kutumia vizuri elimu walizopata.Haki na amani ni vitu muhimu hivyo si budi kuvidumisha.
  • Viongozi wasiowajibika wanapaswa kuachia madaraka na sio kung’ang’ania.
  • Mwanamke anatakiwa kukombolewa kutoka katika mila na desturi potofu.
  • Mataifa ya Afrika ili yaendelee yanapaswa kupiga vita ukabila.
  • Wanajamii wanapaswa kuwa waaminifu katika mapenzi na kuwa na mapenziya dhati.
  • Usaliti ni pigo katika mapenzi.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256