KISWAHILI KIDATO CHA NNE.

I: MADA: UUNDAJI WA MANENO:

Mada ndogo:

  • Dhana ya uundaji wa maneno
  • Mazingira yanayosababisha kuhitajika kwa maneno mapya
  • Njia mbalimbali za uundaji wa maneno
  • Kuunda maneno katika miktadha mbalimbali
  • Umuhimu wa uundaji wa maneno.

Dhana ya uundaji wa maneno.

Uuundaji wa maneno ni hali ya kutengeneza na kuzalisha maneno mapya katika lugha husika.

Kwa kawaida hakuna lugha inayojitosheleza kimatamshi na kimantiki, hivyo hakuna lugha iliyobora kuliko nyingine.

Ili lugha ikidhi haja ya kimawasiliano inahitaji kuwa na msamiati wa kutosha na unaowawezesha wazungumzaji wa lugha kujieleza na kubaini hisia zao kwa wale wanaowasikiliza.

Hivyo basi, katika mchakato wa kukidhi haya ya mawasiliano lulingana na kmaendeleo ya jamii na wakati, lugha inajikita ikilazimika kuongeza msamiati wake na sababu kuu zinazopelekea idadi ya msamiati ni pamoja na:-

Mwingiliano wa tamaduni baina ya jamii moja na nyingine. Kwa mfano:

Mwingiliano baina ya utamaduni wa Waingereza na Waswahili katika Pwani ya Afrika Mashariki na kwingineko, kumesababisha maneno yenye asili ya lugha ya Kiingereza kuingia rasmi katika msamiati wa lugha ya Kiswahili. Mfano, shati, kabati, beseni, basi, foleni na chenji.

Aidha maedeleo ya sayansi na teknolojia yamesababisha uvumbuzii wa dhana mbalimbali mpya. Dhana hizo zimelazimika kutajwa na lugha husika, mathalani, kabla ya uvumbuzi wa simu, televisheni, kiyoyozi, kisimbusi, tarakilishi na kikokotozi haya hayakuwepo katika lugha.

Pia, jamii kutokana na matukio (misimu) mbalimbali kunasababisha kuibuka kwa dhana mbalimbali mpya ambazo lugha hulazikika kuzitafutia msamiati wa kuzitaja. Mathalani, maneno mengi katika lugha ambavyo yanaonesha uhusiano wa kujamii yanaibuka katika jamii. Hii ni ishara inayoonesha tabia ya lugha kuongeza msamiati wake. Mfano, wa maneno hayo ni kasheshe, changamoto n.k.

Njia mbalimbali za uundaji wa maneno:

Zipo njia mbalimbali za uundaji wa maneno, zifuatozo no baadhi ya njia hizo:

Kubadili mpangilio wa vitamkwa: Lugha kwa kutumia vitamkwa ambavyo ni fonimu za lugha husika, hubadilisha mpangilio wake na hivyo kufanya uwezekano wa kuunda maneno mengi, tofauti tofauti.

Mfano: a, e, i, o, u, vitamkwa hivi vinaunda maneno hafuatayo:- au, ua, na oa.

Vilevile, neno tiba lina herufi t, i,b, a. Herufi hizo huweza kujenga maneno mengine kama vile, tabia, bati.

Neno tua lina herufi t, u, a.

Herufi hizo huweza kujenga maneno mengine kama vile tuta, tatu, tatua, uta, utatu, utata.

Unyambulishaji wa maneno: Lugha in kawaida ya kunyumbulisha maneno yake na hivyo kuwa na uwezekano wa kuunda maneno mengi tofauti. Mfano, maneno yanayoweza kunyambulishwa kutokana na neno piga ni pigo, pigana, pigania, pigwa, pigia, pigishwa na pigwa.

Uambishaji wa maneno: Uambishaji ni upachikaji aur ubandikanji wa viambishi kabla na baada ya mzizi wa neno husika. Maneno hayo mapya huundwa kutokana na mzizi mmoja, huwa na maana tofauti lakini maana hozo huhusiana na kushabihiana. Kwa mfano, Mzizi –chez- unaweza kubandikwa viambishi yakapatikana maneno mbalimbali kama vile cheza, wanacheza, mchezo, mchezaje, walicheza na chezwa.

Kuambatanisha maneno: Kuambatanisha maneno ni njia ya uundaji wa maneno ambayo maneno mawili huambatanishwa pamoja na kuunda neno moja.

Maneno huambatanishwa kwa kutumia aina mbalimbali za maneno.

Mfano:

Kitenzi na nomino

Piga + mbizi = pigambizi

Pima + pembe = piapembe

Nomino na nomino

Mwana + hewa = Mwanahewa

Ofisa + elimu = ofisaelimu.

Nomino na kivumishi

Mtu + kwao = mtukwao

Mtu + mwema = mtumwema.

Kutohoa maneno: Utohoaji ni njia ya kuchukua maneno kutoka lugha moja na kuyaingiza katika lugha nyingine kwa kuzingatia muundo na matamshi ya lugha husika. Kitendo cha kufanya maneno yafuate kamusi za lugha nyingine huitwa kutohoa.

Mfano:-

Lugha ya mwanzo

Kutoholewa kwa lugha ya Kiswahili

1. Kiingereza

1. Kiswahili

  • Shirt
  • Basin
  • Number
  • Shati
  • Beseni
  • Namba

2. Kiarabu

  • Wakil
  • Shukran
  • Salaam
  • Ilim
  • Wakil
  • Shukrani
  • Salamu
  • Elimu

3. Kireno

  • Benjera
  • Mezr
  • Bendera
  • Meza

4. Kihindi

  • Dkan
  • Paisa
  • Dhobi
  • Duka
  • Pesa
  • Dobi

Kuazima maneno kutoka lugha nyingine: kuazima maneno ni njia ya kuunda maneno kuyachukua maneno kama yalivyo kutoka lugha nyingine na kuyaingiza katika msamiati wa lugha ya kiswahili pasipo kuyafanyia marekebisho yoyote.

Jedwali lifuatalo linabainisha baadhi ya maneno ambayo yamechukuliwa kutoka:-

Lugha ya awali

Neno la awali

Neno jipya la Kiswahili

Maana ya neno kwa kiswahili.

Kisukuma/kinyamwezi

Kisambaa/kipare

Kichaga

Kingozi

Ikulu

Kitivo

Kimori

Kipera

Ng’atuka

Ikulu

Kitivo

Kimori

Kipera

Ng’atuka

Makao ya Rais

Idara kuu ya masomo

Vazi linalovaliwa kwa mbele.

Kundi dogo la utanzi

Ondoka madarakani kwa hiari.

Urudufishaji:

Urudufishaji ni njia ya uundaji wa maneno kwa kulirudiarudia neno lile lile.

Mfano:

Neno

Baada ya kulirudia

  • Amsha
  • Amshaamsha
  • Taka
  • Takataka
  • Moto
  • Motomto
  • Funga
  • Fungafunga
  • Foka
  • Fokafoka
  • Mbali
  • mbalimbali

Kufananish sauti, sura, umbo na tabia.

Kufananisha sauti:

Mfano:

Mataputapu – Mwigo wa sauti ya pombe ya kienyeji inapomiminwa.

Malapa – Mwigo wa sauti ya ndala wakati wa kutembea,

Mtutu- Mwigo wa sauti ya mlio wa bunduki.

Kufananisha sura.

Mfano:

Kifaru (silaha ya kivita) – kufananisha na mnyama wa porini.

Umbo:

Mfano:

Mkono wa tembo (aina ya ndizi) – kufananisha na mkonga wa tembo.

Ungo (kifaa cha kutaka matangazo ya setelaiti). Kufananisha na ungo wa kupepetea nfaka.

Tabia

Mfano:

Beberu – Tabia ya mbuzi kuwa na uonevu.

Popo – Limetokana na mnyama popo kutokuwa na sifa madhubuti.

Kinyonga – Limetokana na mnyama kinyonga kubadilikabadilika rangi.

Kuangalia hali na kazi ya kitu.

Hali ya kitu:

Mchemsho – Kitu kilicho katika hali ya kuchemka

Mgando - Kitu kilicho katika hali ya mgando

Mbonyeo – Kitu kilicho katika hali ya kubonyea.

Kazi ya kitu –

Kifuniko – Hufanya kazi ya kufunika kitu

Kipimapembe – Hufanya kazi ya kupima pempe.

Kipima joto – Hufanya kazi ya kupima jotoridi.

Kufupisha maneno: Kufupisha maneno ni njia ya kuunda maneno kwa kutumia vufupisho vya maneno marefu. Ufupishaji unaweza kuhushisha silabi pekee au herufi pekee.

Mfano:

Herufi pekee:

Chama cha Walim Tanzania – C.W.T

Umoja wa Wanawake Tanzania

Chama cha Mapunduzi

Silabi pekee.

Mfano:

Baraza la sanaa la Taifa – Basata.

Usanifu wa Kiswahili na ushairi Tanzania UKUTA.

Baraza la Kiswahii la Taifa – BAKITA.

Kuhulutisha maneno:

Kuhulutisha maneno ni njia ya uundaji wa maneno kwa kutena maneno kadhaa kutoka katika maneno mengine na kuunda neno moja.

Mifano:

Chakula cha mchana – CHAMCHA

Chakula cah jioni – CHAJIO

Bunge la Muungano – BUMUU.

Kuhamisha maana ya maneno: Kuhamisha maana ya maneno ni njia ambayo maana halisi za maneno hubadilishwa na kupewa maana tofauti kwa kusudi la kuonyesha dhana fulani.

Mfano:

Neno

Maana halisi

Maana mpya

Nyoka

Mnyama mwenya sumu anayetembea

Mtu hatari sana

Sungura

Mnyama

Mtu mjanja na mlaghai

Chai

Aina ya kinywaji

Rushwa

Changudoa

Aina ya samaki

Mwanamke mhuni

UUNDAJI WA MANENO KATIKA MIKTADHA MBALIMBALI:

Maneno ya lugha ya kiswahili yameingia rasmi katika msamiati wa lugha ya kiswahili kutokana na mabadiliko na maendeleo ya binadamu kiuchumi, kielimu, kisiasa, kiteknolojia na kiutamaduni. Tuangalie mifano ya maneno yaliyopatikana kutokana na nyanja mbalimbali:-

Maendeleo ya uchumi: Maneno yaliyoingia kutokana na maendeleo ya uchumi ni kama vile pesa, hela, benki, kodi, tozo, ushuru na fedha.

Maendeleo ya sayansi na teknolojia: Maneno yaliyoingia kutokana na uwanja huu ni mgombea mwenza, demokrasia, kampeni, kura, wapigadebe, walala hoi na makabwela.

Maendeleo ya mfumo wa dawa na tiba: Maneno yaliyoingia kutokana na uwanja huu ni asprini, dozi, plasta, wodi, hospitali, bendeji, bomba, nesi, tabibu na daktari.

Maendeleo ya kiutamaduni: Manenno yaliyoingia katika msamiati rasmi wa kiswahili ni kama vile kanzu, baibui, posa, mkamwana, suti, biriani, dansi, rumba, disko, bendi, timu, refarii, goli, dimba na mechi.

UMUHIMU WA KUONGEZA MSAMIATI:

Dhana ya uongezaji wa msamiati katika lugha ina umuhimu mkubwa. Hoja zifuatazo ni hoja zinabainisha umuhimu wa uongezaji wa msamiati katika lugha.

Kukidhi haja ya mawasiliano: Mawasiliano katika nyanja mbalimbali hufanikiwa pindi msamiati wa lugah unapoongezeka.

Kukuza lugha: Msamiati unapoongezeka katika lugha husika, lugha hiyo hukua na kupanuka katika jamii husika. Lugha ya kiswahili imepokea maneno mbalimbali kutoka katika nyanja mbalimbali. Mfano, msamiati wa shule, kalamu, darasa, dawati, unifomu, paredi, bweni na mtaala upo katika miktadha wa elimu.

Hurahisisha utoaji wa elimu: Uongezaji wa msamiati husaidia katika utoaji wa elimu, aghalabu kwenye taasis mbalimbali za elimu kama vile shule.

Husaidia kila taaluma kujitosheleza kimsamiati: Mfano, Elimu; - azimio la kazi, muhtasari, ikama, vipindi, mwalimu, andalio la somo yametoka katika taaluma ya elimu.

Tiba na dawa;- - dozi, dripu, mahututi, kozi, upasuaji, wodi na maabara.

Sheria na mahakama;- Jalada, shahidi, kesi, korti, hukumu, kizimbani, jaji, rufaa na wakili.

Hutoa mvuto katika lugha: Uongezaji wa msamiati hujenga na kudumisha mvuto wa lugha.

Mfano, Msamiati ufuatao unaonesha mvuto katika lugha ya kiswahili;- Changudoa, chakachua, king’amuzi, kisamaki, mapochopocho, mahanjumati na kisimbusi.

www.learninghubtz.co.tz

MASWALI YA MADA. MADA YA KWANZA.

MADA: UONGEZAJI WA MSAMIATI:

KIDATO CHA NNE.

A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI.

  1. Neno “Kizibo” limeundwa kutokana na njia ya uundaji wa maneno iittwayo:-
  1. Kuambatanisha maneno
  2. Kubadili mpangilio wa maneno
  3. Kuangalia kazi ya kitu.
  4. Kubadili mpangilio wa neno.
  1. Ipi orodha ya maneno ambayo yameundwa kwa njia ya utohoaji wa maneno?
  1. Bendera, meza, beseni na pesa.
  2. Shuka, saa, doti na kigoda.
  3. Bajia, leso, waya na ikulu.
  4. Namba, elimu, papaya na ng’atuka.
  1. Ipi kati ya njia zifuatazo za uundaji wa maneno si njia sahihi ya uundaji wa maneno.:-
  1. Uambishaji.
  2. Kutohoa.
  3. Kuambatanisha maneno.
  4. Kutafsiri.
  1. Lipi kati ya maneno yafuatayo limeundwa kwa njia ya kufananisha sauti?
  1. Malapa.
  2. Redio
  3. Kikunio.
  4. Shati.

B: JAZA NAFASI ZILIZO WAZI:

  1. Neno “Kikunio” limeundwa kutokana na njia ya uundaji wa maneno iitwayo__________
  2. Mfano wa neno lililoundwa kwa njia ya uambishaji ni ________________
  3. Maneno motomot, mbalimbali, sawasawa, yameundwa kwa njia ya______________
  4. Neno “Kipanya” limeundwa kutokana na njia ipi?_________________
  5. Njia mbili za uundaji wa maneno ni __________________ na ________________
  6. Mfano wa neno lililoundwa kwa kufupisha maneno ni ________________

C: MAJIBU YA MAELEZO MAREFU:

  1. Eleza namna maneno yaliyoundwa katika miktadha ya:

(i) Maendeleo ya kiuchumi

(ii) Maendeleo ya sayansi na teknolojia

(iii) Mabadiliko yo mfumo wa siasa

(iv) Maendeleo ya mfumo wa tiba

(v) Maendeleo ya kiutamaduni.

  1. Eleza umuhimu wa kuongeza msamiati katika lugha. Toa oja tano.

LEARNINGHUBTZ.CO.TZ Page 1

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256