FORM ONE KISWAHILI ANNUAL EXAMS

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA

KIDATO CHA KWANZA

KISWAHILI NOVEMBA 2023

Muda: 2:30

MAELEZO 

  1. Mtihani huu una sehemu A, B na C
  2. Jibu maswali yote. Ikiwa na maswali 6
  3. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani

SEHEMU A (Alama 30)

1. Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo;

  1. Ni kiambishi kipi kinachodekeza ukanushi kati ya vifuatavyo
  1. Wa-
  2. Sh-
  3. –a
  4. Si-
  5. Na-
  1. Ni kauli inayotumia maneno ya kawaida lakini hutoa maana tofauti kabisa na iliyopo kwenye maneno yale.
  1. Mafumbo
  2. Nahau
  3. Misemo
  4. Semi
  5. Hadithi
  1. Neno lipi kati ya haya yafuatayo halihusiani na ushairi?
  1. Mshororo
  2. Kipande
  3. Bahari
  4. Dayalojia
  5. Muwala
  1. Nyenzo kuu za lugha ya mazungumzo ni
  1. Usimuliaji
  2. Mdomo
  3. Maandishi
  4. Vitendo
  5. Ishara
  1. Tamadhali inayofanya kitu kisicho na uhai kutenda kama binadamu
  1. Sitiari
  2. Tashihisi
  3. Tashibiha
  4. Mubalaga
  5. Takriri
  1. Silabi zinazotokea katikati au mwishoni mwa kila mstari wa shairi huitwa.
  1. Vina
  2. Mizani
  3. Sitiari
  4. Vituo
  5. Sauti
  1. Juma ameenda Dodoma. Neno Dodoma limetumika kama
  1. Kihisishi
  2. Nomino
  3. Kiwakilishi
  4. Kielezi
  5. Fani
  1. Bosi samahani, kuna barua hapa. Mtindo huu wa mazungumzo unatumika wapi?
  1. Ofisini
  2. Kiwandani
  3. Shambani
  4. Kanisani
  5. Shuleni
  1. Dhana ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana zaidi ya moja?
  1. Kaka amefua nguo
  2. Nipe sahani ya kulia
  3. Eva amenunua kanga
  4. John amempigia mpira
  5. Zote hapo juu
  1. Konsonanti na Irabu ni
  1. Herufi kuu
  2. Fonimu
  3. Tanzu za lugha
  4. Sauti
  5. Vitamkwa

2. Oanisha dhima za nyimbo za fasihi simulizi zilizo katika Orodha A na aina za nyimbo kutoka Orodha B. Kisha andika herufi ya Jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Husimuliwa kama mifano ya kuadiri watu
  2. Husimulia chimbuko la asili ya kitu fulani
  3. Husimulia kwa nia ya kuchekesha na kukejeli
  4. Husimulia kwa lengo la kuwaasa watoto
  5. Husimulia kuhusu matukio ya kihistoria
  1. Soga
  2. Tarihi
  3. Vigano
  4. Visasili
  5. Hadithi
  6. Mizungu
  7. Ngano

3. Tumia mofimu zifuatazo kuonesha thamani ilizopewa katika paradise Mfano Li- Kuonesha wakati uliopita (Aliondoka)

  1. ta - kuonesha wakati ujao   
  2. o - kuonesha mzizi wa neon -  
  3. ni - kuonesha kitenzi kishirikishi-  
  4. ku- kuonesha urejesho kwa mtendwa-  
  5. ki - kuonesha udurushaji -  
  6. me - kuonesha hali timilifu -  
  7. kwa - kuonesha mahali -  
  8. a - kuonesha nafsi -  
  9. ka - kuonesha kauli ya kutendeka -  
  10. ku - kuonesha wakati uliopita -  
  1. (a) Maneno katika lugha yana dhima mbalimbali bainisha aina ya vivumishi katika tungo zifuatazo.
  1. Shamba la bibi limeota nyasi
  2. Gari dogo limepata ajali
  3. Nyumba yetu ni nzuri sana
  4. Kile kiatu ni cha mtoto
  5. Wanafunzi wangapi wanapenda mayai?

(b) Badilisha nomino zifuatazo kuwa vitenzi

  1. Wimbo
  2. Umbo
  3. Kilio
  4. Mtoro
  5. Mlo
  1. Toa maana mbili kwa kila neno
  1. Mbuni
  2. Mto
  3. Ota
  4. Pepo
  5. Shuka
  1. (a)Taja alama (5) tano za uakifishaji na kisha utoe dhima moja kwa kila alama.

(b)Kamilisha mchoro ufuatao wa vipera vya ushairi

  1. Mzee kimwaga ni fanani mahiri ambaye kila jioni hukaa na wajukuu zake na kuwatolea vitendawili. Jana amewapa vitendawili vitano lakini hakuna anayoweza kuvitegua. Tumia utaalamu wako uliopata kwenye somo la fasihi kuvitegua.
  1. Yey anatuona , sisi hatumuoni
  2. Popote niendapo ananifuata
  3. Nyumba yangu haina mlango
  4. Kitu kidogo kimemtoa maflame kitini
  5. Mzazi ana miguu bali mzaliwa hanayo
  1. Utata usababishwa na mambo mengi. Toa maana mbili katika maneno yafuatayo na weka mfano mmoja kwa kila maana.
  1. Kanga
  2. Ua
  3. Pamba
  4. Mbuzi
  5. Kata

9. Wewe ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili  ambaye una rafiki wa Kidato cha kwanza. Rafiki yako amekuomba umfafanulie maana ya maneno yafuatayo ili aweze kuelewa zaidi, kwani darasani hakuelewa vizuri. Msaidie rafiki yako kwa kumfafanulia maneno yafuatayo:

(i) Vichekesho

(ii) Mtindo

(iii) Lakabu

(iv)Soga

(v) Dhamira

SEHEMU C (ALAMA 15)

10. Mwandikie baba yako barua ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari Kivukoni SLP 20 Singida kumwomba hela ya safari ya kutembelea mbuga za wanyama. Jina lako liwe Mwaluko likoko SLP 350 Dodoma.

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 156  

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 156  

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA

NOVEMBA 2022

Maelekezo:

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote kwa usahihi.
  3. Soma kwa makini maelekezo ya kila sehemu na kila swali.
  4. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.
  5. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi zilizoachwa wazi

SEHEMU A: (Alama 15)

Jibu maswali yote kwenye sehemu hii

1.Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzunguka kiumbe katika maisha yake. Vitu hivyo vinaweza kuwa vyenye uhai kama vile wanyama, wadudu na mimea au visivyo na uhai kama vile milima, maziwa, mabonde, mito na bahari.

Uharibifu wa mazingira ni uzoroteshaji wa mazingira kwa njia ya kupunguza rasilimali kama vile hewa, maji, mimea, udongo na hata kupotea kwa wanyamapori. Mara nyingi, uharibifu wa mazingira husababishwa na vitendo vya binadamu kuangamiza viumbe vinavyomzunguka. Vitendo hivyo ni kama vile kukata miti hovyo, kulima kandokando ya vyanzo vya maji, kutupa taka hovyo na kutiririsha maji machafu kwenye vyanzo vya maji.

Uharibifu wa mazingira hutokana na shughuli mbalimbali za binadamu kama vile kilimo. Binadamu hupanua mashamba kwa ajili ya shughuli za kilimo kwa kukata miti ovyo na kuchoma misitu. Ukataji wa miti ovyo na uchomaji wa misitu husababisha vifo vya viumbe hai vinavyoishi katika miti hiyo kama vile nyani, tumbili na sokwe.

Utupaji wa taka huweza kuharibu mazingira. Taka hizo hutoa harufu mbaya na kuvutia wadudu kama vile nzi. Wadudu hao husababisha magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu. 

Viwanda kutiririsha maji machafu kwenye vyanzo vya maji ni sababu nyingine ya uharibifu wa mazingira. Maji yanayotiririshwa huchafua maji yanayotumiwa na binadamu kutoka kwenye mito na maziwa hivyo husababisha magonjwa kwa binadamu kama vile kansa. Viwanda pia hutoa moshi ambao huchafua hewa inayovutwa na watu hivyo watu hupata madhara kama vile ugonjwa wa mapafu.

Maswali

i.        Kichwa kinachofaa kwa habari hii ni:

A.    Hali ya hewa

B.     Kutunza mazingira

C.     Sababu za uharibifu wa mazingira

D.    Ukataji miti ovyo

E.     Athari za mazingira

ii.      Kwa nini ni muhimu kutunza mazingira yetu?

A.    Ili kuepukana na magonjwa, vita na njaa

B.     Ili kupata mazao mengi, wanyama wengi na miti.

C.     Ili kupendezesha mazingira, kupata majalala na maziwa

D.    Ili kuepuka magonjwa, kupata mvua za kutosha na afya bora

E.     Ili kuondoa mmomonyoko wa udongo, kupata miti mingi na kuondoa unyevuunyevu

iii.    Shughuli zingine zinazofanywa na binadamu na hupelekea uharibifu wa mazingira ni:

A.    Kufuga wanyama wengi katika eneo dogo

B.     Kujenga nyumba nzuri

C.     Kusafisha maziwa yetu

D.    Kuuza madini

E.     Kufua nguo

iv.    Ugonjwa wa mapafu unaoweza kusababishwa na kuvuta hewa kutoka kwa mtu mwingine hujulikana kama vile_______

A.    Athma

B.     Kifua kikuu

C.     Pumu

D.    Kipindupindu

E.     Kansa 

v.      Magonjwa mengine yanayoweza kutupata baada ya kutupa taka ovyo ni pamoja na __

A.    Upele

B.     Amiba

C.     Pumu

D.    Kuhara

E.     Homa 

vi.    Ni ugonjwa gani wa mlipuko unaozungumziwa na mwandishi katika habari hii?

A.    Korona

B.     Kipindupindu

C.     Kansa

D.    Homa ya mapafu

E.     Maji machafu

vii.  Waziri wa tanzania mwenye dhamana ya kusimamia mazingira anaitwa _______

A.    Umi Mwalimu

B.     Tundu Antipasi Lisu

C.     Godbless Lema

D.    Majaliwa kasimu majaliwa

E.     Seleman Jafo

 viii. Kutokana na habari uliyoisoma, Rasilimali ni nini?

A.    Ni jumla ya mali aliyonayo mtu au nchi

B.     Vyanzo vya maji

C.     Upepo

D.    Barabara

E.     Mali inayopatikana kutokana na njia isiyo sahihi

ix.    Zifuatazo ni njia za kutunza mazingira

A.    Kulipua mabomu, kupanda miti na kuchimba vyoo.

B.     Kupanda miti, kutupa taka ovyo na kutiririsha maji machafu

C.     Kupanda miti, kutoa elimu dhidi ya mazingira na kuchimba mashimo ya kuhifadhi taka. D. Kuendesha magari makubwa, kujenga nyumba nzuri na kunawa mikono kabla ya kula

E. Kuwafundisha wanafunzi, kuchoma taka na kupanda maua.

x.      Ni uharibifu gani wa mazingira kati ya yafuatayo husababisha mmomonyoko wa ardhi?

A.    Kutupa vinyesi vya watoto ovyo

B.     Kupanda ukoka

C.     Kuchoma misitu

D.    Kufuga wanyama wengi

E.     Mikusanyiko ya watu

2. Oanisha safu ya maneno A na B. 

SEHEMU B: (Alama 70)

Jibu maswali yote kwenye sehemu hii

3.      Fafanua maana ya istilahi zifuatazo kama zinavyotumika kwenye lugha ya Kiswahili

(a)   Shina la neno 

…………………………………………………………………………………………………

 (b)   Sarufi 

…………………………………………………………………………………………………

 (c)   Vielezi 

…………………………………………………………………………………………………

 (d)   Sintaksia 

…………………………………………………………………………………………………

 (e)   Viambishi 

…………………………………………………………………………………………………

4.Bainisha dhima tano (5) za viambishi awali katika lugha ya Kiswahili. Kwa kila dhima toa mfano mmoja.

  1. ................................................................................................................................
  2. ................................................................................................................................
  3. ...........................................................................................................................
  4. ...........................................................................................................................
  5. ................................................................................................................................

5.a) Sentensi zifuatazo ni tata. Tunga sesntensi mbili kila sentensi ondoa utata huo.

i. Mama amenunua mbuzi

....................................................................................................................................................

ii. Baba Amina ameondoka

…………………………………………………………………………………………………

iii. Mwajuma ametumwa na Rama

…………………………………………………………………………………………………

iv. Kaka amevunja kijiko chake

…………………………………………………………………………………………………

v. Ali amempigia Asha ngoma

…………………………………………………………………………………………………

 b) Taja mifano ya kauli zinazoonyesha muktadha wa rejesta zifuatazo:

 i. Hotelini

…………………………………………………………………………………………………

ii. Sokoni

…………………………………………………………………………………………………

iii. Bandarini

…………………………………………………………………………………………………

iv. Darasani

…………………………………………………………………………………………………

v. Ndani ya basi

…………………………………………………………………………………………………

6.   (a) Panga maneno yafuatayo kama yanavyokuwa katika kamusi

     Kafeli, Tosha, Zaituni, Buriani, Roho, Paroko, Kaheshimu, Amina, Amani

       …………………………………………………………………………………………………………………………………….

(b) Fafanua dhima tano za kamusi 

  1. ...............................................................................................................
  2. ...............................................................................................................
  3. ....................................................................................................
  4. .....................................................................................................
  5. ............................................................................................................

7.         Taja methali moja ambayo ungeweza kuitumia kuonya au kuadilisha kulingana na tukio lililoelezwa hapo chini

Mfano: Mtoto alilelewa vibaya hatimaye ajawa jambazi

Methali: Samaki mkunje ingali mbichi

i.        Ndege alijenga kiota kwa kuchukua jani moja moja na hatimaye baada ya siku tatu kiota kikakamilika kujengwa.

Methali: ………………………………………………………………………………..…….

ii.      Wastara alikuwa masikini, akajibidisha sana kufanyakazi usiku kucha, hatimaye akafanikiwa kupata utajiri na kuishi maisha yenye hadhi.

Methali: ……………………………………………………………………………………….

iii.    Simba alivamia zizi la Mzee Mahende na kukamata ng’ombe mmoja, alipotoka na mkuki kumkabili, alishindwa akarudi nyuma kwa hofu kisha yowe wanakijiji wakakusanyika wakiwa na mikuki na mapanga na marungu wakampiga na kumuua.

Methali: ……………………………………………………………………………………….

iv.    Dereva aliendesha gari kwa kasi na kusababisha ajari mbaya

Methali: ……………………………………………………………………………………….

v.      Baba alipofiwa na mtoto wake alilia sana hadi akazimia

Methali: ………………………………………………………………………………………..

8.   Amina ni mwanafunzi wa darasa la saba anayesoma shule ya msingi Majimengi, tatizo la Amina alikuwa anaamini kuwa lugha haina umuhimu wowote katika jamii. Wewe kama mwanafunzi wa kidato cha pili unamshawishi vipi Amina aweze kubadili imani yake? Kwa hoja tano (05)

  1. .................................................................................................
  2. .................................................................................................
  3. ............................................................................................
  4. ............................................................................................
  5. .................................................................................................

9. Wahusika ni kipengele muhimu sana katika kazi yoyote ile ya fasihi. Onyesha aina ya wahusika katika fasihi simulizi (05).

  1. ............................................................................................
  2. ............................................................................................
  3. .......................................................................................
  4. .........................................................................................
  5. ..............................................................................................

SEHEMU C: (Alama 15)

10.  Andika insha yenye maneno 150 na yasiyozidi 200 inayohusu madhara ya mimba za utotoni 

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 111  

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 111  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256