MTIHANI WA KUJIPIMA WA MADA

MAARIFA YA JAMII DARASA LA NNE

KUTUMIA RAMANI KATIKA MAZINGIRA

Chagua Jibu Sahihi

  1. Ipi kati ya zifuatazo ni sifa ya ramani?
  1. Huonesha pande zote za kitu
  2. Urefu wa kitu huoneshwa
  3. Umbo la asili la kitu hubakia
  4. Rangi ya asili ya kitu huonekana
  5. Huonesha sura ya juu ya kitu.
Choose Answer


  1. Sehemu ya muhimu ya ramani inayoelezea kuhusu alama zilizotumiwa katika ramani ni
  1. ufunguo
  2. fremu
  3. dira
  4. kipimio
  5. kichwa cha ramani
Choose Answer


  1. Katika kuonesha mahali kwa kutumia mistari ya gridi katika ramani huanza kusomwa namba za mstari gani? .
  1. Ulalo halafu wima.
  2. Wima halafu ulalo.
  3. Kushoto halafu kulia.
  4. Kulia halafu juu.
  5. Kulia halafu kushoto.
Choose Answer


  1. Mambo muhimu katika ramani ni
  1. uoto, dira kipimio, mistari na jina la ramani.
  2. rangi, jina la ramani, kipimio, ufunguo na fremu.
  3. mistari, jina la ramani, dira, fremu na kipimio.
  4. jina la ramani, ufunguo, fremu, kipimio na dira.
  5. jina la ramani, ufunguo, kipimio, dira na mistari.
Choose Answer


  1. Kipimo kidogo cha ramani hutumika kuchorea
  1. maeneo madogo
  2. maeneo makubwa
  3. maeneo ya kati tu
  4. maeneo madogo na ya kati
  5. maeneo madogo na makubwa
Choose Answer


  1. kitu kinachotusaidia kutambua uelekea wa mahali tunapokwenda huitwa?
  1. Pande za dunia
  2. Dira ya dunia
  3. Mchoro
  4. Ramani
Choose Answer


  1. alama ya msikiti katika ramani ni
  1. Duara
  2. Msalaba
  3. Nyota
  4. Mwezi.
Choose Answer


  1. Michoro au alama zinazotambulisha kitu huitwa?
  1. Mpaka
  2. Ufunguo
  3. Fremu
  4. Dira
Choose Answer


Andika ndiyo kama sentensi ni sahihi au hapana kama sentensi si sahihi

  1. Kalamu, daftari, kifutio na rula ni vifaa vya kuchorea………………
  2. View Answer


  3. Jua huonekana kuzama upande wa Magharibi…………………..
  4. View Answer


  5. Katika ramani, dira huoneshwa upande wa kushoto mwa ramani…………..
  6. View Answer


  7. Duara ni alama ya msikiti katika ramani………………..
  8. View Answer


  9. Unapochora ramani, ni lazima kuzingatia vipengele vya ramani……………….
View Answer


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256