SURA YA PILI

UTENZI

Ufahamu

Soma utenzi ufuatao, kisha jibu maswali yanayofuata

Teknolojia ya kisasa

Zoezi la kwanza: Ufahamu

1Katika ubeti wa kwanza, mwandishi analenga kuwapa soma gani

wasomaji?

  1. Wakati gani teknolojia ya kisasa hutumika?
  2. Teknolojia ya kisasa ina faida gani?
  3. Maendeleo gani yameletwa na teknolojia ya kisasa?
  4. Teknolojia ya kisasa imeleta mabadiliko yapi?
  5. Mtunzi ana maana gani anaposema, "Giza tumeshalipiku"?
  6. Katika ubeti wa 11, kifungu cha maneno "dunia kama kijiji" kina rnaana
    gani?
  7. Teknolojia ya kisasa inasaidiaje katika kukusanya kodi?
  8. Kwa nini "makini yahitajika" katika kutumia teknolojia ya kisasa katikajamii yako?
  9. Umejifunza nini kutokana na utenzi huu?

Zoezi la pili: Msamiati

Tumia maneno uliyopewa kutunga sentensi moja kwa kila neno

Mfano:Ufaulu wa somo la kiswahili katika mitihani wa darasa la saba umeongezeka

  • Somo
  • Geua
  • Aali
  • Epesi
  • Sawia
  • Boresha
  • Masafa
  • Utandawazi
  • Ubunifu
  • Tija

Zoezi la tatu: Vitendawili

Tegua vitendawili vifuatavyo kwa kuandika jibu lake kwenye mabano

Mfano: Nina mdomo lakini sina mikono wala miguu.(nyoka)

Nyumba yangu ni kubwa lakini mlango mdogo.(chupa)

  1. Chumba changu kikubwa lakini nalala peke yangu.
  2. Akamatwapo mkiani, hutii amri.
  3. Nina mwanangu, ukimkata hakatiki.
  4. Tunda langu la ajabu, juu nyama, katikati ngozi na ndani mchanga.
  5. Ukimkata shingo leo, kesho anayo nyingine.
  6. Mama hana miguu lakini mtoto anayo.
  7. Bunduki yangu ikilia, sauti husikika dunia nzima.
  8. Hubeba mishale kila aendako.
  9. Baba akipiga mbizi, huibuka na ndevu nyeupe.
  10. Ukimgusa mwanangu, mimi hucheka.

Zoezi la nne : mazoezi ya lugha

A. Andika umoja au wingi wa maneno yafuatayo:

B. Andika sentensi zifuatazo katika wakati uliopita.

Mfano:Baba amejenga kituo cha kulelea watoto yatima.

Baba alijenga kituo cha kulelea watoto yatima.

  1. Serikali itatoa mikopo ya fedha kwa wajasiriamali wadogo.
  2. Mjomba anatunga utenzi kuhusu maadili ya jamii.
  3. Mwandishi ataikosoa jamii kwa kuendekeza imani potofu.
  4. Mwalimu hatungi mtihani wa muhula wa pill.
  5. Dereva ataendesha gari kwa umakini mkubwa.
  6. Kiranja hasimamii usafi wa mazingira ya shule.
  7. Wanakijui watachagua viongozi wa kijiji chao.
  8. Wanafunzi wanachimba shimo la takataka shuleni.
  9. WanachUo watasafiri kuelekea mbuga ya wanyama.
  10. Kwaya ya shule yetu itatumbuiza kwenye Sherehe za Muungano.

C. Andika kinyume cha maneno yafuatayo:

  1. Dhurika
  2. Nuna
  3. Karibisha
  4. Mkarimu
  5. Taifisha
  6. Werevu
  7. Imara
  8. Afiki
  9. Ghali
  10. Patikana

D. Jaza neno moja sahihi katika sehemuiliyoachwa wazi kutoka kwenye mabano

  1. Mti huumatunda mazuri sana. (amezaa,umezaa, yamezaa, imezaa)
  2. Wajasiriamalini wabunifu wamepewa mtaji wa biashara. (ambaye, ambayo, ambao, ndiye)
  3. Huyu............mwanafunzi bora kitaifa katika mtihani wa
    Darasa la Saba. (ndio, ndiyo, ndiye, ndiwe)
  4. Ukulima wa kisasabudi kutiliwa mkazo iii kuinua
    uchumi wa nchi yetu. (una, ni, si, hauna)
  5. Angalikuwa mwizina wenzake. (angakamatwa,angelikamatwa, angalikamatwa, angekamatwa)
  6. Wachezaji walichelewa kuingia uwanjani walielekezwa wafike mapema. (ama, ingawa, kwa sababu, kwakuwa)
  7. Tabia mbayakatika jamii. (haufai, zinapendwa,zinapaswa,hazifai)
  8. Wanafunzishamba Ia shule sasa hivi. (anapalilia,
    walipalilia, atapalilia, wanapalilia.
  9. Micheya mikahawa imepandwa shambani.
    (wazuri, mzuri, mizuri, kizuri)
  10. Mwaka jana, BahatiDarasa la Sita. (alikuwa,atakuwa, amekuwa, anakuwa)

E. Badili sentensi zifuatazo kuwa katika kauli halisi.Mfano:Dada aliuliza kuwa unapenda mchezo gani."Unapenda mchezo gani?" Dada aliuliza.

Polisi alisema kwamba tunatakiwa kutii sheria bila shuruti."Mnatakiwa kutii sheria bila shuruti," polisi alisema.

  • Mwalimu amesema kwamba twende upesi.
  • Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilisema kwamba tunasajililaini za simu zetu iii kuzuia uhalifu.
  • Bwana Afya aliuliza kuwa kuna umuhimu gani wa kuchemsha maji ya kunywa.
  • Mwanafunzi mwenzangu alisema kwamba kalamu yangu inaandikavizuri sana.
  • Mgeni aliuliza kuwa mimi ni nani.
  • Waziri alisema kwamba ajira huchochea ukuaji wa uchumi.
  • Mwalimu alisema kwamba nidhamu ni msingi wa maendeleo yataaluma shuleni.
  • Mtabiri wa hali ya hewa alisema kwamba mwaka ujao kutakuwana mvua nyingi.
  • Kiranja alisema kwamba kila mwanafunzi atatakiwa kuja na ufagiokwa ajili ya usafi.
  • Daktari alimwambia mgonjwa kuwa anaumwa ugonjwamalaria.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256