SURA YA KWANZA

MASHAIRI

Ufahamu

Soma shairi hill, kisha jibu maswali yanayofuata.

1.Kiswahilinaazimu,sifayo inayokabwa,

Kwa wasiokufahamu, niimbe ilivyo kubwa,

Toka kamachemchemu,furika palipozibwa,

Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.

2.Toka kamamlizamu,juu kwa wingi furika,

Uoneshe umuhimu, kwa wasiokutamka,

Ndipo waingiwe hamu, mapajani kukuweka,

Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.

3.Lugha yangu ya utoto, hadi leo nimekua,

Tangu ulimi mzito, sasa kusema najua,

Pori, bahari na mto, napita nikitumia,

Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.

4.Sababu ya kuipenda, lugha yangu ninatoa,

Natumia toka ganda, nakiinichanelea,

Lugha nyingine nakonda, wakati nikitumia,

Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.

5.Lugha kama Kiarabu, Kirumi na Kingereza,

Kweli mi' nimejaribu, kila hali kuigiza,

Lakini sawa na bubu, nisemapo wanibeza,

Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.

6.Kila mtu lugha yake, ndiye mtumishi mwema,

Kila mkuu na pake, hana hadhi akihama,

Kiswahili univike, joho lako Ia heshima,

Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu.

7.Lugha ngeni ni elimu, hili sana naelewa,

Tena sitishwi ugumu, kujifunza ninajuwa,

Lakini huwa mtamu, ulimi wa kulelewa,

Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.

8.Mtu kwa usemi wake, wanyama milio yao,

Simba kwa ngurumo yake, ni tisho kwa kondoo,

Bali kwa makinda yake, hupendeza masikio,

Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.

9.Kiswahili kikikopa, si ila ndiyo tabia,

Na lugha zilonenepa, jambo hill hutumia

Lugha bila ya kukopa,muhalikujitanua,

Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu.

10.Kiswahili ni tajiri, kwa fasaha na methali,

Na mimi ninafikiri, kimekwishafika mbali,

Kimeweza kufasiri, taaluma mbalimbali,

Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.


  1. Maneno bila hesabu, bado watu kuandika,Nami nadhani karibu, siku njema itafika,Yawe katika vitabu, na vinywa kuyatamka,Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.
  2. Maneno ya uthabiti, yasiyo na ukakasi,Mengi pia tofauti, kwa fasaha na wepesi,Yenye ladha ya sauti, bado kuona kamusi,Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.
  3. Yaandikwe haya yote, kufuata taratibu,Tuweke juhudi zote, kamusi iwe ajibu,Isifike kilapote,katika zotejanibu,Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu.
  4. Kiswahili kina sifa, kwa nahau na maana,Hufanya na mataifa, mengi kusikilizana, Kikitoa taarifa, kwa wengi huwa bayana,Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.
  5. Lugha hii ni ya mbele, ingawa leo i nyuma,Walakini polepole, sifa yake inavuma,Itafikia kilele, cha fahari na heshima,Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu.
  6. Kiswahili ni Naili, kwa kazi ya ushairi,Ambao hutoa mbali, rutuba hadi Misiri,Masika na jua kali, kila siku husafiri,Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu.
  7. Hata tele Iikijaa, titi jingine si zuri,

Mwana aliye na njaa, kunyonya hana hiyari,Lugha ya kigeni pia, ni kaidi kwa amri,

Titi la mama ni tamu, jingine halishi hamu.

  1. Ninashukuru fahari, sikuumbwa kuwa bubu,Titi jingine si zuri, hili nimelijaribu,

Cheo changu hata ari, nikaona laharibu,Titi Ia mama ni tamu, jingine halishi hamu.

19.Kukaa bure siwezi, ndipo nikajinusuru

Kuandika beti hizi, kama zitapata nuru

Ndiyo ya kwangu makuzi, zikikosa haidhuru,

Titi la mama ni tamu, Jingine halishi hamu

Zoezi La kwanza: Ufahamu

  1. Onesha ulna vya kati na vya mwisho katika ubeti wa kwanza.
  2. Kituo katika shairi hill ni kipi?
  3. Kituo hicho kina mizani ngapi?
  4. Kifungu "mapajani kukuweka" kama kilivyotumika katika ubeti wa pillkina maana gani?
  5. Kanuni gani inaelekeza kwamba vina vya mwisho katika shairi Iakimapokeo vifanane?
  6. Eleza maudhui yanayojitokeza katika ubeti wa kwanza, wa pili na watatu.
  7. Nini maana ya mstari wa tatu katika ubeti wa nne na wa tano katikashairi hill?
  8. Mstari "Kila mtu lugha yake, ndiye mtumishi mwema," maana yakenini?
  9. Eleza kwa kifupi ujumbe wa shairi hili.
  10. Pendekeza kichwa cha shairi hili.

Zoezi la pili: Msamiati

Tunga Sentensi mbili kwa kila neno

  1. Azimu
  2. Kabwa
  3. Beza
  4. Muhali
  5. Pote
  6. Chemchem
  7. Janibu
  8. Mlizamu
  9. Kiini
  10. Jikisuru

Zoezi la tatu: Miundo

Tunga sentensi tatu kwa kila muundo.

  1. lakini

Mfano:Mbele yao alikatiza mbwa mkalilakinihakuwadhuru.

  1. Ia

Mfano:Kashalakiberiti limeanguka chini.

  1. za

Mfano:Kelelezachura zilinipotezea usingizi.

Zoezi la nne: Methali

Kamilisha methali zifuatazo kwa kutumia maneno yallyopo kwenyekisanduku.

  1. ....................................huleta heshima
  2. Jambo la ukucha..................................
  3. Daraja lililokuvusha................................
  4. Furaha ya mzazi.......................
  5. Fadhila za punda...........................
  6. ..............................kamwepushia mashunzi
  7. Afadhali jirani mchawi..........................
  8. Usifunue kinywa...................................
  9. Zohali..............................................
  10. Kataa neno..............................................................

Zoezi la tano: Matumizi ya Lugha

A. Pigia mstari vihusishi katika sentensi zifuatazo:
Mfano:Baba amenunua ng'ombe wa maziwa.

Viti vya shangazi vimepotea.

  1. Mpera umeota katikati ya mipapai.
  2. Mtoto ameokota ganda Ia muwa.
  3. Mimi ninapenda dagaa wa kukaanga.
  4. Nyumba yetu imejengwa kando ya bahari.
  5. Mama anapasua mbao za kuuza.
  6. Kiti nilichokalia jana ni cha mtoto.
  7. Nyafuru amesimama ukingoni mwa barabara.
  8. Makoba amebeba viti vya mjomba.
  9. Mbwa wetu anakunywa maji kwa kulapa.
  10. Kulwa ameokota embe chini ya mwembe.

B. Andika umoja au wingi wa maneno yafuatayo

Umoja.

  • Chura
  • Mtu
  • Nyoka
  • Kopo
  • Chuma

Wingi

  • Nyungo
  • Vogoda
  • Simba
  • Soda
  • Milima
  • majengo

C. Bacilli sentensi zifuatazo kuwa katika wakati uliopo hall ya kuendelea.Mfano:Mimi nitacheza mpira kwa uwezo wangu wote.

Mimi ninacheza mpira kwa uwezo wangu wote.

  • Juma hujifunza kutunga shairi.
  • Mwanakwao alikula chakula chote.
  • Shangazi ameenda kumwandikisha mdogo wangu shuleni.
  • Kikundi chetu kitafuga kuku wa nyama.
  • Sisi tulipanda Mlima Meru.
  • Watoto wa baba mdogo walipalilia shamba lao.
  • Ufugaji wa nyuki uliwaneemesha vijana wa Mzee Hango.
  • Mwalimu Kabaka alitufundisha tabia njema.
  • Kabati litakalonunuliwa kesho Iitawekwa hapa.
  • Merama amekunywa uji wa ulezi.

D. Andika KWELI kwa sentensi ya kweli na SI KWELI kwa sentensiisiyo ya kweli katika nafasi uliyopewa.

Mfano:Shairi Ia kimapokeo hufuata kanuni za urari wa vina na mizani.KWELI

  1. Mshororo ni mstari katika ubeti. ..................
  2. Shairi si lazima liwe na mghanaji na waghaniwa. ................
  3. Shairi halibebi ujumbe wowote katika jamii.....................__
  4. Kituo ni mstari wa mwisho katika ubeti wa shairi.___...............
  5. Wakati mwingine shairi lina mizani nane........................__
  6. Aya si ubeti katika shairi. .....................
  7. Katika kuhesabu mizani ya mshororo tunahesabu idadi ya silabi.....
  8. Shairi Ia kimapokeo si lazima vina vya kati na vya mwisho

kufanana katika beti zote. .........................

  1. Unaweza kutumia methali katika utunzi wa shairi................____
  2. Hatutumii kiulizo katika shairi Ia kimapokeo..................___

E. Pigia mstari vitenzi vikuu, kisha weka herufi T chini ya neno linalohusika.Mfano:Bibi yanguanafuganyuki.

T

  1. Leo tumecheza mpira kwa furaha kubwa.
  2. Mimi ninawapenda sana baba na mama.
  3. Otaigo ameandika insha kwa mwandiko mzuri sana.
  4. Kisima kimebomoka mara to baada ya mvua.
  5. Wiki ijayo tutakuwa tunafanya mtihani.
  6. Mtendaji waalikuwa anagawa pembejeo.
  7. Wanafunzi wa shule yetu walishinda mechi kwa kishirdc
  8. Baba yao atakuwa anapalilia mikorosho.
  9. Nyumbani kwetu tunauza mafuta ya alizeti.
  10. Mtoto alianguka vibaya sana.

Zoezi la sita: Utungaji

Soma shairi hili kisha jibu Maswali yafuatayo

  1. Nitakapojua kutunga vizuri,

Siku moja nitaandika shairi

Kuwashukuru wazazi

2.Nitamshukuru mama,

Alenibeba turnboni

Kwa muda wa miezi tisa,

Akiniengaenga kwa upendo

  1. Nitamweleza nilivyohisi
    Furaha yake

Kila alipokuwa nami,

Akisemezana nami,

Au akinielekeza.

  1. Mamangu

Alinibeba mgongoni,

Akiniimbia nyimbo,

Kunituliza.

5.Nitamshukuru babangu

Alesaidiana na mama

Kunibeba na kuniengaenga,

Alenipakata kwa huba

Akihakikisha

Sihangaishwi

Na maradhi ya utotoni.

6.Nitamweleza nilivyoihisi

Furaha yake

Kila akiniona

Na kuongea nami.

7.nitaandika shairi

Kuelezea raha niliyoipata

Kwa kuguswa na upendo wao

Ulonifanya niote ndoto tamutamu

8.Nitakapojua kutunga vizuri,

Nitaandika shairi,

Kuwashukuru wazazi.

9.Wazazi wamenifunza

Ukuu wa upendo,

Ukuu wa tumaini;Wamenifunza

Kuwa mnyenyekevu;Wamenifunza

Kuwa mwenye bidii;Wamenifunza

Kuwa muungwana;Wamenifunza

Kuwa mcheshi;Wamenifunza

Kuwa mwenye furaha.

10. Nitaandika shairiKuwashukuru wazazi

Kwa kunizaa,

Kunilea,

Kunitunza,Kunipenda,Kunifunza.

11.Nitaandika shairi

Kuwashukuru wazazi.

Nitakapojua kutunga vizuri.

Zoezi la saba

  1. Mshairi anasema kuwa ni lini atatunga shairi?
  2. Kwa nini mshairi atamshukuru baba yake?
  3. Upendo wa wazazi ulimfanya mtunzi aote ndoto gani?
  4. Mshairi amesema wazazi wake wamemfunza nini?
  5. Kwa mujibu wa shairi hili, majukumu ya baba na mama au mieziyanatofautiana?
  6. Mshairi anasema furaha yake ilitokana na nini?
  7. Kwa nini tunatakiwa kuwapenda wazazi?
  8. Ubeti wa nane una mishororo mingapi?
  9. Pendekeza kichwa cha shairi hill.
  10. Je, shairi hilo lina urari wa vina na mizani?

Zoezi la nane: Msamiati

Tunga Sentensi mbili kwa kila neno

Mfano:Niliguswa sana na shairi alilotunga mwalimu.

Wanafunzi waliguswa na matokeo mazuri ya Darasa Ia Saba.

  • Engaenga
  • Hisi
  • Semezana
  • Elekeza
  • Tuliza
  • Huba
  • Hakikisha
  • Hangaisha
  • Guswa
  • Muungwana

Zoezi la tisa: Miundo

Tunga sentensi mbili kwa kila muundo.

  1. .........Hata hivyo............

Mfano: Hata hivyo,shangazi amechoka kula wali.

  1. kwetu.......................

Mfano:Shulenikwetutumestawisha mahindi.

  1. pahala pa_.............

Mfano:Mwaki amesimamapahalapazuri.

  1. Badala ya............

Mfano: Badala yakununua gari, anunue bajaji.

Zoezi la kumi: Mazoezi ya Lugha

A. Pigia mstari vielezi katika sentensi zifuatazo:Mfano:Mama atafikakesho jioni.

Wanafunzi waliimba wimbovizuri.

  1. Binamu yangu analima kwa bidii.
  2. Mtoto wa mjomba anacheza polepole.
  3. Wanafunzi wameingia darasani.
  4. Baba mkubwa anaishiTarime.
  5. Mwalimu atafika saa tatu kamili.
  6. Hapa pameinuka sana.
  7. Mama atafika kesho jioni.
  8. Ndama wataingia zizini.
  1. Kinyonga anatembea kwa maringo.
  2. Maji ya kunywa yalimwagika mwaaa!

B. Andika visawe vya maneno yafuatayo:

Mfano:

wali -ubwabwa

mlingoti-nguzo

  • Kenda
  • Makamo
  • binadamu
  • nidhamu
  • kitendo
  • bao
  • ng'atuka
  • kiasi
  • ning'iniza
  • nchi

C. Badili sentensi hizi kuwa katika hall ya mazoea.

Mfano:Wazazi wanakarabati shule ya

Wazazi hukarabati shule ya !Nip.

  1. Watanzania wanapenda mpira wa miguu.
  2. Doto alisafiri umbali mrefu kwenda shuleni.
  3. Mtoto amelia kwa sauti kubwa.
  4. Nchama alifika ofisini saa mbili asubuhi.
  5. Watoto wanacheza mpira kwa bidii.
  6. Ng'ombe wetu alitoa maziwa mengi.
  7. Wanafunzi waligawiwa vitabu kwa ajili ya kujisomea.
  8. Jogoo aliwika saa kumi alfajiri.
  9. Mwajuma ataogelea bwawani.
  10. Kitigwa alikwenda bandarini kuchukua mizigo.

D. Badili sentensi zifuatazo kuwa katika wakati ujao.Mfano:Utukutu wangu uliniponza.

Utukutu wangu utaniponza.

  1. Musa anaimba vizuri nyimbo za kwao.
  2. Baba anaendesha gari mpaka nje ya nchi.
  3. Sisi tunaishicha Nyarero.
  4. Mievi ameanguka kwenye mtaro.
  5. Wao walikula wall jana.
  6. Dagaa wamepungua sokoni.
  7. Mvua za masika zimeanza kunyesha.
  8. Kilimo cha matunda kimemsomeshea watoto.
  9. Mwanariadha ametunukiwa medali ya dhahabu.
  10. Kidado anajua kupika ugali.
  1. Tunga sentensi mbili kwa kila neno. Kila sentensi iwe na maanatofauti.

taa, paa, kaa, koo, kioo, mbuzi, paka, tembo, laki, kata

Mfano:Robinaalikatamti uliopo uani.

Didani anaishiKataya Manzese.

  1. Jibu maswali yafuatayo kwa kupigia mstari jibu sahihi.Mfano:Anakula ugalikwakijiko. Neno kwa katika sentensi hii ni:kitenzi, kielezi,kihusishi,kihisishi
  1. Kaka anacheza mpiravizuri.Neno vizuri katika sentensi hii ni:(kitenzi, kivumishi, kiwakilishi, kielezi)
  2. Mtotomzurianafua nguo zake. Neno mzuri katika sentensi hii ni:(kivumishi, kitenzi, kielezi,
  3. Damarianapika pilau. Neno Damari katika sentensi hii ni:(kiunganishi, kitenzi, nomino, kiwakilishi)
  4. Mihogo__________tayari kwa kusagwa unga.
    (imenyauka, imekauka, imeungua, imechanua)
  5. Kaka ameuza viatu___________vya ngozi.
    (chao, chake, vyake, yake)
  1. Mimi ni mtoto wa________kuzaliwa nyumbani kwetu.
    (moja, mbili, pill, chanzoni)
  2. Maneno ya yule kijana___________sana.

(yaliniusi, yaliniudhi, yaliniuzi, yaliniuthi)

  1. Baba amenunua nguo zilizotengenezwa kwa_______ya kondoo.
    (safi, supu, sufu, sufi)
  2. Neno ambalo ni tofauti na mengine ni:

(panzi, mende, kinyonga, mbu)

  1. Moja kati ya yafuatayo ni jina lililo tofauti na mengine:(batamzinga, kanga, batamaji, batabukini)

G. Kamilisha methali zifuatazo:

Mfano:Mimi nyumba ya udongo,sihimili kishindo.

Inafaa kusemea mgomba,ungali wima.

  1. Maneno ni daraja,
  2. Mfukuzwa kwao,................
  3. Jiwe Ia kutupa ngomani
  4. Raha haiji ila.......
  5. Riziki kama ajali,
  6. ...........................................................ukienda haurudi.
  7. ..........................................., huonana kwa nyaraka.
  8. Mpanda farasi wawili..............
  9. Kimya kitanguliapo,...................
  10. , mtii.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256