SURA YA KWANZA

MAJANGA YATOKANAYO NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Msamiati

  • Angahewa- tabaka la gesi mbalimbali, mvuke na hewa zinazozingira sayari
  • Fuel za kisukuku- aina ya fuel zilizotokana na mabaki baada ya kuoza kwa mimea au miili ya viumbe hai mfano bakteria na wanyama
  • Gesijoto- jumla ya gesi zote kwenye angahewa la dunia zenye uwezo wa kutunza joto lake kwa kurudisha kiasi cha joto linalotoka ardhini kwenda anga nje
  • Janga- tukio la hatari linaweza kusababisha maafa
  • Mnururisho wa jua- mrusho wa nuru kutokana na nguvu za miale kama vile ya jua au umeme
  • Unyevuanga- kiwango cha mvuke katika angahewa

Dhana ya mabadiliko ya tabianchi

  • Tabianchi ni wastani wa hali ya hewa ya eneo fulani iliyorekodiwa kwa kipindi cha muda mrefu, kawaida ni miaka 30 au zaidi.
  • Mathalani halijoto na mvua ni vipengele muhimu vya tabianchi. Eneo fulani Iikitajwa kuwa na halijoto ya nyuzi 25 na kiasi cha mvua cha milimita 1000 inamaanisha viwango hivyo ni wastani wa rekodi za miaka 30 au zaidi.
  • Endapo wastani wa viwango hivi utabadilika baada ya kuzingatia rekodi za miaka 30 au zaidi, basi hall hii itaitwa mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi ni mabadiliko makubwa ya wastani ya hall ya hewa inayorekodiwa kwa kipindi cha muda mrefu, kawaida ni miaka 30 au zaidi.
  • Ni muhimu kujua tabianchi ya eneo fulani kwani hubainisha mwenendo wa muda mrefu wa vipengele vya hall ya hewa kama vile mvua, jotoridi, mgandamizo wa hewa, unyevuanga, nuru ya Jua, mawingu na upepo.
  • Vipengele hivi hubadilikabadilika kulingana na majira ya mwaka na eneo husika. Hata hivyo, vipengele hivi hutegemeana hivyo, mabadiliko ya kipengele kimojawapo huweza kuathiri mwenendo wa vipengele vingine.
  • Kwa upande mwingine, tabianchi ina uhusiano mkubwa na aina ya shughulya binadamu zinazoweza kufanyika katika eneo husika. Mfano, kilimo na ufugaji. Pia, tabianchi hubainisha mtawanyiko wa uoto wa asili na aina ya viumbe hai wanaoishi eneo fulani.

Tabianchi ya eneo lolote kwenye use wa dunia huathiriwa na mambo makuu yafuatayo:

  1. Latitudo ya eneo- huu ni umbali kutoka mstari wa ikweta. Maeneo yaliyo karibu na mstari wa ikweta hupokea kiasi kikubwa cha nuru ya Jua kuliko maeneo yaliyo mbali na ikweta. Hivyo basi, maeneo haya huwa na joto jingi na mvua nyingi kuliko maeneo yaliyo mbali na ikweta kama vile ncha ya kaskazini au ya kusini ya dunia;
  2. Mwinuko kutoka usawa wa bahari- maeneo yenye mwinuko mkubwa kutoka usawa wa bahari kama vile Kilimanjaro, Arusha, Iringa na Njombe huila na baridi na mvua nyingi. Kadiri mwinuko kutoka usawa wa bahari unavyoongezeka, jotoridi hupungua. Maeneo ya tambarare na mwinuko kidogo kama Dar es salaam, Tanga na Mtwara huwa na jotoridi kubwa; na
  3. Sura ya NCHI- hii ni umbile la eneo fulani kama vile milima au mabonde.
    Sehemu zenye milima kama vile Usambara huathiri mienendo ya upepo na mvua. Upande wa mashariki wa milima hupata upepo wenye unyevu mwingi kutoka baharini na kutokana na mwinuko, unyevu huu hufanya mawingu na hatimaye mvua. Upande wa magharibi hupata upepo usio na unyevu hivyo kupata mvua kidogo au kukosa kabisa. Vile vile, sehemu zenye milima huwa baridi kwa vile kuongezeka kwa mwinuko husababisha jotoridi kupungua na hewa kuwa ya baridi zaidi.
  • Mabadiliko ya tabianchi hutokea pale ambapo mabadiliko ya mfumo wa kawaida wa tabianchi yanaposababisha mwenendo mpya wa hali ya hewa duniani kwa miongo au karne nyingi.
  • Kwa nyakati zetu, mabadiliko ya tabianchi yanasababishwa zaidi na ongezeko is joto duniani.

Ongezeko la joto duniani

  • Ongezeko Ia joto duniani ni hali ya kuongezeka kwa taratibu lakini kwa uhakika cwa wastani wa joto katika uso wa dunia.
  • Ongezeko hill linasababishwa na iwongezeka kwa kiwango cha gesijoto angani.- Gesijoto hizi ni kama vile -lewa ya ukaa au kabonidayoksaidi, mvuke, methani, na ozoni.
  • ljapokuwa umekuwepo na ongezeko la joto kwa maelfu ya miaka iliyopita, ongezeko a joto kwa miaka ya karibuni kuanzia karne ya ishirini limekuwa la kasi zaidi. Hall hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za binadamu.
  • Ongezeko hilo hubainika kwa kulinganisha vipimo vya joto vinavyopatikana katika nyakati tofauti. Kwa mfano, viwango vya joto kati ya majira ya mwaka au muongo mmoja na mwingine.

Uhusiano kati ya shughuli za kibinadamu na ongezeko la joto duniani

  • Tangu karne ya kumi na tisa, kumekuwa na mapinduzi makubwa ya kilimo, viwanda, sambamba na maendeleo ya teknolojia.
  • Shughuli hizi za kibinadamu zimeongeza uzalishaji wa gesijoto mbalimbaii, hususani hewa ya ukaa au kabonidayoksaidi. Pia, nguvu za kiasili kama milipuko ya volkano huzalisha gesijoto mbalimbali.
  • Gesi hizi zinapozalishwa, hupaa angani na kutengeneza utando mfano wa blanket'. Utando huu ndio unaowezesha dunia kuwa na uhai kwa kuzuia baadhi ya miale ya Jua iliyoakisiwa kwenye uso wa dunia kupenya na kusafiri anga la nje.
  • Hivyo basi, utando huu ni muhimu sana kwani hufanya dunia kuwa na joto stahiki kwa maisha ya viumbe hai.
  • Hata hivyo, kuongezeka kwa uzalishaji wa gesijoto hizi kutokana na shughuli za kibinadamu kumesababisha kutengenezwa kwa utando mzito sana wa gesijoto.
  • Hali hii imechangia ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya tabianchi kwa ujumla. Hii inamaanisha kwamba, utando mzito wa gesijoto huzuia kiasi kikubwa zaidi cha miale ya jua aina ya infraredikutoka kwenye uso wa dunia kuliko kawaida.
  • Tafiti zimeonesha kuwa shughuli za kibinadamu zimechangia ongezeko hill kuliko nguvu za kiasili za mfumo wa tabianchi.
  • Baadhi ya shughuli za kibinadamu zinazochangia ongezeko la joto duniani ni kama vile ukataji miti na matumizi ya fueli za kisukuku.

ukataji miti

  • Uoto wa asili, hususani misitu hupunguza kiwango cha mwanga wa Jua kinachoakisiwa na kurudishwa kwenye use wa dunia na hivyo kupunguza joto duniani.
  • Vilevile misitu hupunguza hewa ya kabonidayoksaidi katika angahewa. Kwa hiyo, kuwepo kwa misitu kunapunguza ongezeko Ia joto duniani. Kwa upande mwingine, misitu inapochomwa huongeza gesijoto ya kabonidayoksaidi angani, na hivyo kuchangia ongezeko la joto duniani.
  • Hivyo, kupungua kwa misitu kumechangia kuongezeka kwa gesijoto angani. Kumekuwa na ukataji mkubwa wa misitu kwa ajili ya makazi na kilimo iii kukidhi mahitaji ya watu.
  • Kwa mfano, inakadiriwa kuwa Tanzania hupoteza kiasi cha hekta 372,000 za misitu kwa mwaka kutokana na ukataji miti iii kukidhi mahitaji ya nishati, samani na ardhi kwa ajili ya kilimo. Ni wazi kuwa kama kiwango hiki cha ukataji miti kitaendelea, misitu yetu itapotea na hivyo kuchangia ongezeko Ia joto duniani.

Matumizi ya fueli za kisukuku

  • Mapinduzi ya viwanda katika nchi za magharibi yameongeza sana matumizi ya fueli ya kisukuku katika sekta ya viwanda na usafirishaji. Mahitaji ya fueli hii bado ni makubwa duniani pote.
  • Nishati hii hutumika kwenye sekta ya viwanda, umeme, usafirishaji na ujenzi, licha ya kuwepo nishati mbadala kama Jua na upepo. Kwa mfano, takribani asilimia 95 ya nishati ya usafirishaji duniani inatokana na fueli za kisukuku.
  • Hata hivyo, matumizi ya aina hii ya fueli huzalisha gesijoto ambazo huchangia kuongezeka kwa kiwango cha joto duniani na hatimaye mabadiliko ya tabianchi.
  • Kwa mfano, takribani asilimia 78 ya gesijoto zilizozalishwa kuanzia 1970-2011 ilitokana na matumizi ya fueli hii. Kielelezo namba 1 kinaonesha shughuli za kibinadamu zinazochangia ongezeko Ia gesijoto-angani.

Picha: Ukataji miti

Uhusiano kati ya ongezeko la joto duniani na majanga

  • Kwa kuharibu mazingira, binadamu amechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa joto na hatimaye mabadiliko ya tabianchi duniani.
  • Mabadiliko ya tabianchi yanaweza kusababisha kutokea au kuongezeka kwa madhara ya majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri shughuli za kila siku za binadamu pamoja na miundombinu. Hebu tujifunze dhana ya majanga katika kisanduku kifuatacho.
  • Majanga ni matukio ya ghafla katika jamii zetu yanayotokea bila taarifa. Majanga yanaweza kusababishwa na nguvu za kiasili au shughuli za kibinadamu.
  • Majanga yanayosababishwa na nguvu za kiasili ni kama vile ukame, tetemeko la ardhi, mafuriko, vimbunga, milipuko ya volkano na maporomoko ya Baadhi ya majanga yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu ni kama vile ajali (za barabarani, majini, angani, viwandani, reli) moto unaotokea nyumbani na msituni.
  • Vilevile, utupaji wa taka hovyo na ujenzi holela'husababisha mikondo na mitaro ya maji kuziba hatimaye mafuriko wakati ‘va mvua. Baadhi ya athari zinazosababishwa na majanga haya ni karria vile ukame unaoweza kusababisha upungufu au kukosekana chakula cha mifugo na binadamu, hali inayosabaisha vifo.
  • Pia husababisha uharibifu wa mali kama miundombinu, mazao na mifugo.

Athari za kuongezeka kwa- Joto duniani

Ongezeko la joto duniani limesababisha mabadiliko ya tabianchi kwa sehemu nyingi duniani. Ongezeko la joto limekuwa na athari zifuatazo:

  • Kutokea mara kwa mara kwa majanga yanayohusiana na hall ya hewa na tabianchi kama vile ukame na mafuriko;
  • Kutokea mara kwa mara matukio ya hali ya vimbunga na upepo mkali;
  • Kuharibiwa na kupungua kwa kiwango cha theluji katika milima mirefu na maeneo yenye barafu. Mfano katika mlima Kilimanjaro, kama inanvyoonekana hapa chini.
  • Kuongezeka kwa mvua kubwa ndani ya kipindi kifupi na kusababisha mafuriko. Kuongezeka kwa joto duniani, huongeza joto la bahari na kusababisha uvukizwaji mkubwa angani unaoleta mawingu na kusababisha mvua kubwa zinazoleta mafuriko
  • Kuyeyuka kwa barafu na theluji kutoka ncha za dunia na hivyo kuongeza ujazo wa maji baharini na kuhatarisha makazi ya watu wanaoishi karibu na bahari na viziwa.

Majanga yasababishwayo na ongezeko la joto duniani

Mojawapo ya athari za ongezeko la joto duniani ni kutokea kwa majanga ya mara kwa mara kama vile ukame na mafuriko. Maelezo kwa undani kuhusu majanga haya na athari zake kwa binadamu ni kama ifuatavyo.

Ukame

  • Ukame ni hali ya ukosefu wa mvua zinzotegemewa katika eneo fulani kwa muda mrefu. Aghalabu wakati wa ukame mvua hunyesha chini ya kiwango cha wastani cha eneo husika.
  • Kwa upande mwingine, kiangazi ni majira ya mwaka yanayosababishwa na ukosefu au uwepo wa mvua kidogo kwa muda mrefu. Kiangazi hutokea kila mwaka na hivyo sio janga kama ukame. Ukame ni janga kubwa katika dunia.
  • Kwa Tanzania, ukame huathiri zaidi mikoa ya kanda ya kati na kaskazini kama vile Dodoma. Arusha, Manyara, Singida, Kilimanjaro, Shinyanga na Simiyu. Ukame unapotokea huambatana na ukosefu wa maji, chakula na malisho kwa ajili ya watu na mifugo.
  • Pia, wakati wa ukame kunakuwa na joto kali wakati wa mchana na baridi wakati wa usiku, vikichagizwa na upepo mkali hasa kwa maeneo yasiyo na uoto wa kutosha.
  • Kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ukame hutokea mara nyingi zaidi na hudumu kwa muda mrefu zaidi. Hivyo, athari za ukame zimekuwa kubwa zaidi.

Athari za ukame

  • UKame unapotokea unaweza kusababisha hasara kubwa kwa watu, mifugo na mazao. Madhara ya ukame yanaongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
  • Kielelezo hapo chini kinaonesha athari za ukame kwa mifugo. Wakulima na wafugaji huathiriwa zaidi na ukame. Baadhi ya madhara ya ukame ni kama yafuatayo:
  • Vifo vya watu, mifugo na mimea kutokana na ukosefu wa chakula na maji;
  • Kukauka kwa mazao shambani na hivyo kusababisha upungufu wa chakula;
  • Kupungua kwa mapato yatokanayo na kilimo na mifugo kwa wakulima na serikali. Hali hii hutokana na kufa kwa mifugo, na kukosekana kwa mavuno;
  • Ukame wa muda mrefu husababisha mmomonyoko wa udongo kutokana na upepo na kuharibika kwa tabaka la juu la udongo;
  • Kukauka kwa vyanzo vya maji kama vile mito, mabwawa, visima, au vijito na kupungua kwa kina cha maji kwenye maziwa na mabwawa makubwa;
  • Ukosefu wa nishati ya umeme utokanao na maji kutokana na kupungua kwa kina cha maji kwenye mabwawa;
  • Kuhama kwa wanyamapori kutoka mbugani hadi makazi ya watu wakitafuta maji ya kutosha na malisho;
  • Kuongezeka kwa migogoro kati ya wakulima na wafugaji kutokana na ukosefu wa maji na malisho ya mifugo; na
  • Kutokea na kuongezeka kwa mato katika misitu na hivyo kutishia maisha ya wanyama na watu.

C:UsersKYAMBODocumentsmaarifa 3536cb943f10d8kenya-drought-effects-of-climate-change-2-.jpgpix.jpg

Picha: Madhara ya ukame

Mbinu za kukabiliana na ukame

Ukame ni janga linalotokea na kujidhihirisha taratibu. Wakulima, wafugaji na wadau wengine wanaweza kujiandaa na kukabiliana na ukame kwa njia mbalimbali kama vile:

  • Kupanda mazao yanayohimili ukame na kukomaa kwa muda mfupi mfano, mtama, uwele na mihogo .
  • Kuhimiza uendeshaji wa kilimo hifadhi iii kupunguza upotevu wa maji na kuhifadhi rutuba ya udongo;
  • Kuhimiza kilimo cha umwagiliaji;
  • Kutoa elimu kwa jamii kuhusu kilimo hifadhi, kilimo cha umwagiliaji,
  • aina nzuri za mbegu za mazao, na matumizi bora ya pembejeo;
  • Kuhimiza ufugaji bora na wa kisasa unaozingatia mifugo michache inayohimili mazingira ya ukame;

Mamlaka ya hali ya hewa kuwa na mfumo imara wa tahadhari ya mapema kwa wadau kuhusu mwenendo wa mvua; na Kuwa na mipango ya kukabiliana na majanga.

C:UsersKYAMBODocumentsmaarifa 3download (7).jpg

Picha: Zao linalohimili Ukame

  • Mafuriko yanaweza kutokea kutokana na sababu mbalimbali. Mojawapo ni kunyesha kwa mvua nyingi katika kipindi kifupi au kipindi kirefu. Sababu nyingine ya mafuriko ni mito, vijito, mabwawa, maziwa au bahari kuzidiwa na maji mengi, hivyo kulazimisha maji kutofuata uelekeo wake.
  • Hali hii husababisha maji kuelekea kwenye sehemu zisizotakiwa kama kwenye makazi, shambani, viwandani au sehemu za kufanyia biashara.
  • Pia, mafuriko yanaweza kusababishwa na kupasuka kwa mabwawa makubwa yanayotumika kuhifadhia maji kwa ajili ya kuzalisha umeme au umwagiliaji.
  • Mara nyingi mabwawa haya hupasuka kutokana na hitilafu za kiufundi au kuzidiwa na maji mengi. Mafuriko pia yanaweza kusababishwa na kuyeyuka kwa barafu au theluji katika ncha za kaskazini na kusini mwa dunia.
  • Hii ni kutokana na kuongezeka kwa joto duniani kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Vilevile, ongezeko la joto duniani husababisha kuongezeka kwa joto la bahari. Joto hill huongeza uvukizwaji mkubwa angani. Kuongezeka kwa uvukizi husababisha vimbunga vinavyoleta mvua nyingi na hatimaye mafuriko maeneo ya pwani na tambarare.
  • Aidha, mafuriko yanaweza kusababishwa na kuziba kwa mifereji ya maji kwenye makazi yetu kunakosababishwa na uchafuzi wa mazingira, hususan utupaji hovyo wa taka ngumu.
  • Wakati wa mvua nyingi, maji hushindwa kupita kwa urahisi na hivyo kusababisha mafuriko.
  • Kielelezo namba 5 kinaonesha mifereji ya maji machafu iliyoziba kutokana na mrundikano wa taka ngumu Hivyo, baada ya maji kukosa mahali pa kutiririkia hutuama na kusababisha
    athari kwa watu, wanyama na viumbe wengine. Pia huharibu makaC:UsersKYAMBODocumentsmaarifa 3download (8).jpgzina mazao.

Picha: Madhara ya mafuriko

C:UsersKYAMBODocumentsmaarifa 33605536d-812a-4170-aafe-72d04b4cc1e2-2060x1236.jpeg

Picha: Wanyama na binadamu wakisombwa na maji

Maeneo hatarishi kwa mafuriko ni pamoja na maeneo ya tambarare chini ya miinuko mikubwa, maeneo ya pwani, makazi ya watu yasiyofuata kanuni za mipango miji kwa mfano, eneo la bonde la Msimbazi lililopo katika mkoa Na Dar es Salaam. Maeneo mengine ni yale yaliyo karibu na kingo za mito, iaziwa au mabwawa makubwa ya kuhifadhia maji, na maeneo yasiyo na uoto kama misitu, nyasi au vichaka.

Athari za mafuriko

.Tanga la mafuriko linaweza kusababisha maafa makubwa kwa jamii na mazingira kama vile:

  • Vifo vya watu na mifugo;
  • Kuharibiwa kwa miundombinu kama vile barabara, reli, njia za mawasiliano, mifumo ya maji safi na maji taka;
  • Kuharibiwa kwa makazi na mali
  • Kupotea kwa mall, watu na mifugo kutokana na kusombwa na mafuriko;
  • Kuharibiwa kwa mazao na mimea katika ardhi, na hivyo kuiweka nchi katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa na magonjwa;
  • Uchafuzi wa mazingira kwa mfano, kemikali za sumu zinaweza kuingia kwenye maji kutoka migodini au makazi ya watu; na
  • Kukosekana kwa nguvu za umeme, mawasiliano na maji salama kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu.

Mbinu za kukabiliana na athari za mafuriko

Hatua mbalimbali zinaweza kuchukuliwa ill kujikinga au kupunguza athari za mafuriko pindi yakitokea. Hatua hizo ni pamoja na:

  • Kuepuka kuishi maeneo hatarishi kwa mafuriko kama vile bondeni, kandokando ya mito na mabwawa, na kwenye makazi yasiyo rasmi;
  • Kuhakikisha mazingira ni masafi muda wote, ikiwemo kusafisha mifereji ya maji taka kwenye makazi yetu;
  • Kuwa na mipango mqi endelevu inayosimamiwa ipasavyo iii kuepusha ujenzi wa makazi maeneo hatarishi kwa mafuriko;
  • Kuotesha nyasi na mitt iii kuilinda ardhi dhtdi ya mmomonyoko wa udongo kutokana na mafuriko; na
  • Kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kujikinga na mafuriko. Kudhibiti uharibifu wa mazingira
  • Serikali ya Tanzania inachukua hatua za kukabiliana na uharibifu wa mazingira na majanga mbalimbali.
  • Hatua hizo ni kama vile kuweka sheria za kudhibiti uharibifu wa mazingira, kuhamasisha shughuli za utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati mbadala.

Sheria ya usimamizi wa mazingira

  • Tanzania ilitunga sheria ya usimamizi wa mazingira namba 20 ya mwaka 2004.
  • Sheria hii pamoja na mambo mengine inakataza shughuli zinazoweza kusababisha uharibifu wa mazingira. Hit ni sheria mama katika kutunza mazingira.
  • Sheria hii inasema ni makosa kujenga jengo kwenye fukwe za baharii ziwa au kingo za mto na bwawa.
  • Pia, inakataza kuchoma misitu, kutupa taka na kemikali katika vyanzo vya maji. Vilevile, inakataza kuchimba mchanga katika maeneo ya fukwe, kuchepusha na kuzuia maji yasipite katika mkondo wake.
  • Kuwepo kwa sheria hii kumesaidia kupunguza vitendo vya uharibifu wa mazingira kwa sababu wananchi wanaojihusisha na shughuli zinazochangia uharibifu wa mazingira huchukuliwa hatua za kisheria.
  • Baadhi ya hatua zinazochukuliwa ni pamoja na kulipa faini, kubomoa makazi yaliyojengwa kwenye vyanzo vya maji na maeneo ya milima na kushitakiwa mahakamani.

Sheria ya misitu

  • Vilevile, katika kudhibiti uzalishaji wa gesijoto, sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002 inalenga kudhibiti matumizi ya mazao ya misitu na kuzuia uharibifu wa misitu.
  • Sheria hii ikitekelezwa ipasavyo itahakikisha uwepo wa misitu na hivyo kupunguza ongezeko la joto duniani.

Sheria ya ushuru wa asilimia 30 ya bei ya magari yaliyotumika

  • Ili kudhibiti uzalishaji wa gesijoto kwa upande wa vyombo vya usafiri na mitambo, serikali imeweka kodi ya `uchakavui kwa magari yasiyokuwa ya uzalishaji yenye umri wa miaka 10 na zaidi.
  • Kwa sasa, ushuru huu ni kiwango cha asilimia 30 kwa gari iliyotumika zaidi ya miaka 10.
  • Lengo la sheria hii ni kushawishi ununuzi wa magari yale yasiyokuwa na athari kubwa kwa mazingira. Hii itapunguza uchafuzi wa mazingira yetu.

Matumizi ya nishati mbadala

  • Nishati mbadala ni chanzo chochote cha nishati kinachotumika badala ya chanzo cha awali.
  • Kwa sasa matumizi makubwa ya nishati ya kupikia hutokana na mkaa na kuni. Matumizi ya nishati mbadala yanapunguza uharibifu wa mazingira.
  • Nishati mbadala inaweza kuwa ni matumizi ya makaa ya mawe, mkaa unaotengenezwa kwa kutumia maranda ya mbao au mabaki ya mazao.
  • Mkaa huo hutumika badala ya mkaa unaotengezwa kwa magogo ya miti
  • Mkaa utokanao na maranda ya mbao husaidia usafi wa mazingira. Maranda yatokanayo na mbao kama hayatakuwa na matumizi, husababisha uchafuzi wa mazingira.
  • Hivyo, matumizi ya mkaa huu husaidia kupata vyanzo vya nishati mbadala wakati huohuo husaidia kuweka mazingira katika hali ya usafi.
  • Matumizi ya gesi nyumbani kwa ajili ya kupikia pia inaweza kuwa matumizi ya nishati mbadala wa mkaa wa magogo ya miti na kuni. Ni wajibu wetu kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kuepuka na kuacha kutumia nishati zinazosababisha uharibifu wa mazingira.

Nishati mbadala za umeme maji

Nishati mbadala za umeme maji ni pamoja na umeme wa Ala na gesi.

Umeme wa gesi asilia

Gesi asilia ni gesi inayopatikana katika ardhi na inayotumiwa na binadamu kama fueli. Umeme wa gesi ni umeme unaotengenezwa kwa kutumia gesi asilia. Matumizi ya umeme wa gesi asilia unaweza kusaidia kupunguza matumizi ya maji ambayo yangetumika kufua umeme. Matumizi ya umeme wa gesi asilia yamechangia kuongeza umeme katika gridi ya taifa. Kielelezo namba 8 kinaonesha mitambo ya kufua umeme wa gesi asilia.

Umeme wa Jua

Umeme wa Jua ni umeme unaotengenezwa kwa mionzi ya Jua. Umeme wa jua ni nishati mbadala kwa matumizi mbalimbali kama vile kuwasha vifaa vya kielektroniki mfano, taa, jokofu, televisheni, kuchaji simu na hata kupika.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256