SURA YA PILI

KUJIVUNIA SHULE NA KUIPENDA NCHI YETU

Msamiati

  • Dola- chombo chenye mamlaka ya kuendesha utawala au siasa ya nchi
  • Dukuduku- machungu, wasiwasi au mfundo unaomsonga mtu moyoni
  • Dumisha- kuendeleza jambo
  • Katika- jumla ya kanuni taratibu au sheria ambazo huwezesha serikali itawale au chama au kampuni iendeshe shughuli zake
  • Maslahi- manufaa au faida aipatayo mtu baada ya kufanya kazi, biashara au kumaliza tendo lolote
  • Mhimili- nguzo, kitu kinachozui kingine kisianguke
  • Minajili- kwa ajili ya
  • Thamini- kukipa kitu hadhi

Katika sura ya kwanza, ulijifunza matendo yenye kuonesha upendo kwa watu wenye mahitaji maalumu, kuheshimu jinsi na kuvaa mavazi yenye staha. Katika sura hii, utajifunza mambo yanayoiletea shule sifa nzuri. Pia, utajifunza umuhimu wa kuenzi tunu za taifa letu ambazo ni tamaduni, mila na desturi zetu. Vilevile, utajifunza alama za utambulisho wa taifa letu pamoja na sikukuu za kitaifa.

Kuipenda na kujivunia shule yetu

  • Hebu jiulize, je, unaipenda shule yako?
  • Je, unajivunia shule yako?
  • Unajivunia vitu gani katika shule yako?
  • Sifa nzuri za shule zinajumuisha tabia njema za wanafunzi na walimu, majengo safi na mazingira yanayovutia.
  • Hivyo, sifa nzuri ya shule inatokana na shule kuwa na mazingira yanayotunzwa kwa kupandwa miti ya vivuli, miti ya matunda pamoja na maua.
  • Vilevile, sifa nzuri ya shule huchangiwa na wanafunzi kuwa nadhifu kwa kutunza sare zao na vifaa wanavyotumia katika mchakato wa kujifunza.
  • Wanashirikiana kutunza rasilimali na samani za shule kama vile majengo, madawati, viti, vitabu na madaftari yao.
  • Hali kadhalika, wanafunzi wanajituma na kuwajibika ipasavyo bila kusukumwa na mtu mwingine.
  • Uwepo wa mambo yote haya husababisha ufaulu mzuri na kujenga sifa nzuri ya shule.
  • Sifa mbaya za shule zinajumuisha tabia zilizopo shuleni ambazo hazikubaliki miongoni mwa jamii inayoizunguka. Sifa mbaya ya shule inachangiwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na uchakavu wa miundombinu na mazingira machafu.
  • Pia, kuna vitendo vya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wanafunzi, kama vile kutovaa sare ya shule kikamilifu, kushindwa kufua sare zao na kuchana madaftari na vitabu. Vilevile, baadhi ya wanafunzi wana tabia ya utoro, uvivu na kuchelewa kufika shuleni.
  • Hali hii huchangia sofa ya shule kuwa mbaya. Aidha, matendo ya baadhi ya walimu kuonesha tabia za uvunjifu wa taratibu na sheria za kazi.
  • Mfano wa vitendo hivyo ni ugomvi baina ya walimu, walimu na wanafunzi, walimu kutotumia lugha yenye staha wawapo mazingira ya shule au katika jamii. Mambo yote haya yanaweza kusababisha shule kuwa na sifa mbaya.

Chunguza picha zifuatazo, kisha jibu maswali yanayofuata.

2

Kielelezo namba 1: Utunzaji wa mazingira shuleni


Jibu Maswali haya

  1. Unaona nini katika picha namba 1 na 2?
  2. Elezea mazingira ya shule katika picha namba 1.
  3. Linganisha mazingira ya shule iliyopo kwenye picha namba 1 na ya shule yako.
  4. Orodhesha vitendo vya wanafunzi unavyovifahamu vinavyoweza kuifanya shule yenu iwe kwenye hali kama ilivyo kwenye picha namba 1
  5. Je, wanafunzi waliopo kwenye picha namba 2 wameshika nini?
  6. Taja tabia za wanafunzi zinazochangia kuchafua mazingira ya shule yako.
  7. Taja sifa nzuri zinazobainisha shule yako.
  8. Ungepewa nafasi ya kushiriki michezo inayoiletea shule yako sifa nzuri, ungeshiriki mchezo au michezo ipi?
  9. Wewe na wanafunzi wenzako, pamoja na walimu, mnatakiwa kutenda matendo gani ya ziada iii shule yenu iwe na sifa nzuri? (Tofautisha matendo ya wanafunzi na yale ya walimu).

Nembo ya shule yetu

  • Je, unafahamu maana ya neno nembo? Nembo ni alama maalumu inayotambulisha kitu fulani.
  • Nembo ya shule ni alama inayoitambulisha shule inayohusika. Kwa kawaida nembo ya shule hujumuisha kauli mbiu ya shule, shughuli mbalimbali za shule kama vile shughuli za kitaaluma, elimu ya kujitegemea na mazingira ya shule.


  • Je, shule yako ina nembo inayoitambulisha?
  • Je, nini kauli mbiu ya shule yako?
  • Ili kuifahamu vizuri nembo ya shule yako mwalimu atakuonesha na pia atakuongoza kuichora.

Kufanya shughuli mbalimbali za kujitolea shuleni

  • Je, umewahi kufanya kazi za kujitolea shuleni kwako?
  • Ulijisikiaje ulipofanya hivyo? Ilikuwa shughuli gani? Kujitolea ni tabia ya kufanya jambo kwa hiari bila kushurutishwa na pasipo kujali maslahi binafsi.
  • Kwa mfano, unaweza kujitolea kupanda miti na maua katika mazingira ya shule au kuanzisha bustani za mboga. Pia, unaweza kuanzisha na kushiriki katika klabu mbalimbali kwa mfano skauti, klabu ya mazingira, klabu ya UKIMWI, klabu ya kutoa elimu ya kuzuia na kupambana na rushwa na klabu ya elimu kwa mlipa kodi.
  • Aidha, unaweza kushiriki katika shughuli ya kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi, madarasa na vyoo vya shule.
  • Pia, unaweza kushiriki katika shughuli mbalimbali shuleni hasa za elimu ya kujitegemea Ili kuleta maendeleo katika shule na kuongeza kipato_ Baadhi ya shughuli hizo ni kilimo na ufugaji, kuanzisha vitalu vya kuotesha miche ya miti na kujiunga na masomo ya ziada ya ufundi stadi endapo shule yako ina masomo hayo.

Maswali

  1. Eleza umuhimu wa nembo ya shule.
  2. Bainisha mambo ya msingi yaliyomo kwenye nembo ya shule yako.
  3. Je, umewahi kufanya shughuli za kujitolea shuleni kwako au katika jamii? Zitaje.
  4. Baada ya kusoma kipengele cha shughuli za kujitolea shuleni, unafikiri unaweza kuanzisha au kujiunga katika shughuli zipi?

Picha: mfano wa nembo ya shule


Tunu za nchi yetu

  • Tunu ni mambo yote ya thamani ambayo watu hujionea fahari kuwa nayo. Je, tunu za nchi ya Tanzania ni zipi?
  • Tunu za nchi yetu ya Tanzania ni lugha yetu ya Kiswahili, umoja, uzalendo, uwajibikaji, upendo, heshima, utu na kuwajali wazee. Sisi sote yatupasa kuipenda na kujivunia nchi yetu kwa kuzienzi tunu zinazoitambulisha.
  • Vilevile, ni muhimu kuheshimu mila na desturi zetu na kudumisha tamaduni zetu kama sehemu ya tunu za taifa.

Mila na desturi za Kitanzania

  • Je, umewahi kusikia mtu akikuambia tudumishe mila na desturi zetu?
  • Ulielewa kuwa anamaanisha nini? Mila na desturi ni namna tulivyozoea kufanya mambo katika jamii yetu tangu zamani.
  • Mila na desturi vinaweza kutafsiriwa kama ni mapokeo ambayo jamii hurithishana kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
  • Mila na desturi hujenga au kuunda utamaduni ambao ndio utambulisho wa jamii hiyo. Nchini Tanzania kuna mila na desturi mbalimbali ambazo hubeba utambulisho wa jamii mbalimbali.
  • Kuna mila na desturi zinazofaa na zisizofaa, kama ilivyobainishwa katika Jedwali namba 1.
  • Ili kuimarisha utamaduni wa taifa, inatupasa kudumisha mila na desturi zinazofaa na kutokomeza mila na desturi zisizofaa ambazo ni kikwazo kwa maendeleo ya familia, jamii na hata taifa kwa ujumla.

Tafakari maneno yaliyopo kwenye jedwali hill, kisha jibu maswali yanayofuata.

Mila na desturi zinazofaa

Mila na desturi zisizofaa

Zinahamasisha watu wote kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano.

Zinahamasisha wanawake kubeba majukumu ya kutunza familia, wakati wanaume hawawajibiki ipasavyo.

Vijana kwenda jandoni na kupewa mafunzo na majukumu. Pia, kuwafundisha kuhusu mapokeo mema ya tamaduni zao iii kujenga ari ya uwajibikaji ndani ya jamii.

Baadhi ya makabila, hukeketa wasichana na kuwacheza

ngoma zisizo na maadili mfano kumcheza mwali na vigodoro.

Picha: Tamaduni za watu wa Tanga


Zinahamasisha wanafamilia

Zinahamasisha uvivu na ubaguzi

wa jinsi zote kushirikiana

wa jinsi moja kutoshiriki kufanya

kufanya kazi za nyumbani na za

kazi za nyumbani. Mfano, mtoto

kujiongezea kipato katika familia.

wa kiume kutoshiriki kazi kama kuosha vyombo na kupika.

Mgawanyo wa kazi unaozingatia

Mgawanyo wa kazi usiozingatia

usawa wa kijinsia.

usawa wa kijinsia. Kwa mfano, kumtumikisha mwanamke kufanya kazi nyingi kuliko mwanaume.

Haki za watoto zinaheshimiwa

Watoto hawana haki.



  • Pia, ni mtindo wa jumla wa maisha ya jamii fulani. Hivyo, kudumisha utamaduni wa taifa ni kuzingatia mila na desturi zinazofaa, pamoja na mambo mengine yote yanayojenga umoja katika jamii na taifa.

Umuhimu wa utamaduni

  • Utamaduni ndio unaobeba utambulisho wa taifa letu.
  • Pia, utamaduni unajenga moyo wa kujiamini na kujithamini. Kwa mfano, lugha ya Kiswahili hulitambulisha taifa la Tanzania.
  • Wasanii wanapokwenda nje ya nchi hulitambulisha taifa letu kwa sanaa wanayoipeleka huko.
  • Vilevile, utamaduni hujenga umoja, upendo, ushirikiano, kuthaminiana na kuheshimiana.
  • Utamaduni hudumisha mila na desturi za jamii kwa kupitia mafunzo mbalimbali ya vijana, kwa mfano mafunzo ya jando na unyago katika jamii fulani kulingana na wakati.
  • Mafunzo hayo huwawezesha kuishi maisha yanayokubalika katika jamii husika.
  • Pia, utamaduni huhimiza kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, iii kupanua fursa za ajira.
  • Kazi za sanaa kama vile maigizo, muziki, michezo, ngoma na kuchonga vinyago huimarisha kipato cha mtu binafsi, jamii na taifa.
  • Aidha, kwa kupitia utamaduni tunapata burudani katika miktadha mbalimbali; mfano, nyimbo na ngoma za asili zinapochezwa.
  • Nyimbo na ngoma za asili pia hutumiwa na makabila mbalimbali kama kichocheo cha kuhamasisha kufanya kazi kwa bidii, kujenga tabia nzuri na nidhamu katika maisha.
  • Kwa mfano, kabila la Wasukuma hupiga ngoma wakati wa kulima iii kuhamasisha ari ya kufanya kazi.
  • Tunaweza kudumisha utamaduni wetu kwa njia mbalimbali. Njia mojawapo ni kwa kushiriki katika mambo ya sanaa na ngoma za asili.
  • Njia nyingine ni kutumia lugha zetu za asili, kuitumia na kuienzi lugha ya Kiswahili katika matukio mbalimbali mfano, shughuli za kiserikali na za kijamii.
  • Aidha, tunatakiwa kujivunia, kutumia na kuyaenzi mavazi yetu ya asili, kudumisha mila na desturi zinazofaa, kutumia na kuvitangaza vyakula vyetu vya asili.
  • Pia, tunatakiwa tuzienzi mila na desturi zetu hasa zile zinazoimarisha uhusiano mwema. Vilevile, ni muhimu kuidumisha heshima na uhusiano kwa kuzingatia taratibu za kusalimiana katika jamii.
  • Kwa mfano, kwa kawaida mtu mwenye umri mdogo ndiye anayepaswa kuanza kumsalimia mtu mwenye umri mkubwa.
  • Utamaduni ni kielelezo cha uhai wa jamii yetu.


Alama za taifa

Ulipokuwa darasa la nne ulijifunza matendo ya kuipenda nchi yetu kama vile kuonesha heshima kwa wimbo wa taifa na bendera ya taifa, pamoja na kuthamini fedha ya Tanzania. Katika sura hii, utajifunza kwa undani zaidi matumizi ya alama hizi za taifa. Aidha, utajifunza matumizi ya bendera ya taifa, wimbo wa taifa, mnyama wa taifa (twiga), nembo ya taifa, fedha ya taifa, bendera ya rais, mwenge wa uhuru, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ramani ya Tanzania.

Nembo ya Taifa

Matumizi ya alama za taifa

Je, ulishajiuliza umuhimu wa alama za taifa? Alama hizi hutumika wakati fulani, kwenye mazingira fulani na kwa lengo fulani. Hebu tuyabaini matumizi ya alama za taifa Ia Tanzania.

Bendera ya taifa

  • Bendera ya taifa inaitambulisha nchi ya Tanzania miongoni mwa mataifa
    mengine. Bendera yetu ya taifa hupepea katika nchi zote ambako Tanzania imefungua ofisi za ubalozi.
  • Pia, viongozi na baadhi ya Watanzania wanaposafiri nje ya nchi kwa lengo la kuiwakilisha Tanzania, hubeba bendera yetu ya taifa.
  • Bendera ya taifa hutambulisha pia vyombo vya usafiri vinavyosajiliwa Tanzania.
  • Vyombo hivyo ni meli, ndege, magari na pikipiki. Vilevile, bendera ya taifa hutambulisha ofisi au taasisi za serikali kama vile shule, ofisi ya serikali ya kijiji, kata, wilaya na mkoa, majengo ya mahakama na ofisi za wizara mbalimbali.

Bendera ya Taifa

  • Pia, bendera ya taifa hutumika kuonesha majonzi pale inapotokea msiba au janga Ia kitaifa. Mifano ya majonzi hayo ni kama vile kifo cha baba wa taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ajali ya MV Bukoba iliyotokea tarehe 21 mwezi wa 5 mwaka 1996 na Kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 mwezi wa 9 mwaka 2018 katika Ziwa Viktoria ambapo meli na kivuko hicho vilizama na kusababisha vifo vya watu wengi. Katika maombolezo ya matukio kama hayo bendera ya taifa hupepea nusu mlingoti.

Wimbo wa taifa

  • Kwa kiasi kikubwa matumizi ya wimbo wa taifa yanafanana na yale ya bendera ya taifa. Wimbo wa taifa huimbwa wakati viongozi wa nchi wanapotembelea nchi nyingine.
  • Pia, huimbwa wakati vikundi vya utamaduni na michezo wanapocheza michezo ya kimataifa ndani na nje ya nchi.
  • Pia, wimbo wa taifa huimbwa kabla ya tangazo Ia msiba wa kiongozi mkuu wa nchi, kama vile rais, makamu wa rais na waziri mkuu. Hali kadhalika, kabla ya rais kufanya uzinduzi wa jambo muhimu linalogusa maslahi mapana ya taifa, huimbwa wimbo wa taifa.
  • Mfano wa matukio hayo ni uzinduzi wa meli mpya au ndege mpya. Aidha, wimbo wa taifa huimbwa katika taasisi mbalimbali kama vile, shuleni na katika vikosi vya majeshi yetu ili kukuza uzalendo.
  • Vilevile, wimbo wa taifa huimbwa katika matukio muhimu ya kitaifa, kama vile sikukuu za kitaifa na hafla zinazohusisha viongozi wakuu wa serikali.

Mnyama wa taifa

  • Je, unamfahamu mnyama wa taifa? Anaitwa nani ? Na ulimwona wapi? Mnyama wa taifa Ia Tanzania anaitwa twiga.
  • Mnyama huyu hutumika kama alama kificho katika fedha ya noti ya Tanzania. Pia, hutumika pamoja na alama ya bendera ya taifa kutambulisha ndege inayomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile, alama ya twiga hutumika kama kielelezo cha utajiri wa maliasili iliyopo Tanzania.

Twiga mnyama wa Taifa

Nembo ya taifa to Tanzania

  • Je, umewahi kuiona nembo ya taifa? Ina vitu gani? Uliiona wapi? Nembo ya taifa ina jumla ya alama 13 ambazo ni: mwanamke na mwanaume, mwenge wa uhuru, pembe za ndovu, mlima Kilimanjaro, mawimbi ya bahari, bendera ya taifa, mkuki, mazao ya pamba na karafuu, jembe na shoka, ukanda wenye maneno uhuru na umoja, rangi ya njano na nyekundu.
  • Nembo ya taifa inatumika kuonesha umiliki wa mali na nyaraka za Serikali ya Tanzania. Alama hiyo huonekana katika vitabu na machapisho mbalimbali ya serikali, Kati za kusafiria nje ya nchi na mavazi ya viongozi wa juu wa kijeshi.
  • Pia, hutumika katika mawasiliano rasmi ya kiserikali kama vile barua za kiserikali na matamko ya kiserikali. Nembo ya taifa la Tanzania hutumika pia kama muhuri wa rais.

Fedha ya Tanzania

Alama nyingine ya kitaifa ni fedha ya Tanzania. Fedha ya Tanzania inaitwa shilingi. Fedha hutumika kwa namna mbili. Hutumika kuitambulisha Tanzania kama nchi huru. Pia, hutumika kuthamanisha vitu na mali. Fedha ya Tanzania iko katika sura mbili: noti na sarafu.

Noti za Tanzania

Bendera ya Rais

  • Alama hii hutumika kutambulisha mamlaka rasmi ya rais katika shughuli rasmi ambazo rais anahudhuria ndani au nje ya nchi.
  • Vilevile, hutumika katika chombo cha usafiri anachokitumia rais.

Bendera ya Rais

Mwenge wa uhuru

  • Mwenge wa uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro siku ambayo Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9 mwezi wa 12 mwaka 1961.
  • Mwenge huu wa uhuru hutumika kukumbuka na kuitambulisha Tanzania kama nchi huru.
  • Hutumika pia kuonesha mshikamano wa kitaifa. Mwenge wa uhuru hutumika katika matukio ya kuzindua baadhi ya miradi ya maendeleo nchini pindi unapokimbizwa kwenye maeneo husika.
  • Vilevile, mwenge wa uhuru hutumika kuhamasisha na kudumisha uzalendo kwa Watanzania.
  • Wakati wa kukimbiza mwenge wa uhuru, kuna wimbo maalumu unaoimbwa iii kuwakumbusha Watanzania jukumu lao la kuulinda uhuru wao.
  • Mbio za mwenge hufanyika mara moja kila mwaka kuzunguka nchi nzima.

Rais Samia Akiwasha Mwenge wa Taifa

Hebu imba, kisha tafakari maudhui ya wimbo huu wa "Kuwasha mwenge."

K inuz ih rrnus e

"Sisi tumekwisha kuwasha Mwenge,

Tumekwisha kuwasha Mwenge, Na kuuweka juu ya mlima, Mlima Kilimanjaro.

Kuwasha Mwenge, Kuwasha Mwenge, Na kuuweka Kilimanjaro.

Umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini,

Pale ambapo hakuna matumaini, Upendo mahali ambapo pang chuki,

Na heshima ambapo pamejaa dharau."

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

  • Katiba ni sheria, kanuni na taratibu zinazotumika kuendesha shughuli za nchi, chama au kikundi cha watu wenye malengo yanayofanana.
  • Tanzania tunatumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonesha muundo, madaraka na majukumu ya serikali.
  • Katiba huonesha pia haki na wajibu wa raia wa Tanzania.
  • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni alama mojawapo miongoni mwa alama zinazolitambulisha taifa letu.
  • Katiba hutumika kuhifadhi na kulinda sheria zote zinazotungwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Inaeleza bayana mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili mikuu mitatu ya dola ambayo ni serikali, bunge na mahakama.
  • Katiba hutumika wakati viongozi wanapoapishwa baada ya kuteuliwa na kuchaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi.
  • Wanaapishwa na katiba ili kuitetea na kuilinda katiba hiyo. Vilevile, katiba hueleza bayana madaraka na mipaka ya viongozi iii kuepusha migogoro na matumizi mabaya ya madaraka.
  • Aidha, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huhifadhi sheria zinazotetea maslahi na haki za binadamu.

Katiba ya Tanzania

Ramani ya Tanzania

  • Alama hii hutumika kutambulisha na kuonesha mipaka ya nchi yetu na nchi nyingine zilizo jirani yetu. Upande wa mashariki,Tanzania inapakana na Bahari ya Hindi, upande wa magharibi inapakana na nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Rwanda. Upande wa kaskazini Tanzania imepakana na nchi za Kenya na Uganda. Upande wa kusini inapakana na nchi za Malawi, Msumbiji na Zambia.

Sikukuu za kitaifa

Je, unazifahamu sikukuu gani za kitaifa? Kama mwanafunzi umewahi
kushiriki sikukuu gani za kitaifa? Sikukuu za kitaifa ni zile siku ambazo
zinaadhimishwa kitaifa kila mwaka, iii kukumbuka matukio muhimu ya

kitaifa. Ifuatayo ni orodha ya sikukuu zinazoadhimishwa kitaifa nchini Tanzania:

Jedwali namba 2: Sikukuu za Kitaifa

Pia, kuna sikukuu nyingine za dini ya Wakristo kama vile Krismas, Ijumaa Kuu, Pasaka na Jumatatu ya Pasaka. Vilevile, kuna sikukuu za Waislamu, mfano Eid - El Fitri, Eid - El Haji na Maulid.

Umuhimu wa sikukuu za kitaifa

  • Sikukuu za kitaifa hutumika kuenzi matukio ya kitaifa na kudumisha ujumbe ulio katika matukio hayo.
  • Sikukuu za kitaifa, hutoa fursa kwa viongozi kueleza mafanikio na changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi.
  • Wakati wa maadhimisho ya sikukuu hizo, viongozi hutumia nafasi hizo kuchanganua na kufafanua mambo ya kitaifa na kutafakari mwelekeo wa nchi. Pia, hutoa elimu mbalimbali kwa wananchi kuhusu mambo yanayohusu maendeleo ya nchi yao.
  • Kwa mfano, wakati wa sherehe za wakulima ambazo huadhimishwa tarehe 8 mwezi wa 8 kila mwaka, viongozi wetu wa kitaifa huwahamasisha wakulima kutembelea maonesho mbalimbali yatakayo wasaidia wakulima kupata mbinu na njia za kisasa za kuboresha kilimo na ufugaji.
  • Vilevile, sikukuu hizi huwasaidia wananchi kupata fursa ya kuwasiliana na viongozi wao. Aidha, kwa kupitia sikukuu hizi wananchi hupata fursa ya kusherehekea mafanikio na kutafakari changamoto mbalimbali.
  • Mfano, katika sikukuu ya Mei Mosi wafanyakazi hutoa dukuduku zao kuhusu changamoto zinazowakabili.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256