MAARIFA YA JAMII

SURA YA PILI

Utunzaji wa kumbukumbu za matukio ya kihistoria

Ulipokuwa darasa la nne, ulijifunza matukio yaliyotokea katika familia yako na shuleni, njia za kupata taarifa za matukio ya kihistoria, vifaa vinavyotumika kuchukua taarifa za matukio na njia za kutunza taarifa za matukio hayo. Katika sura hii utachambua matukio ya kihistoria yaliyowahi kutokea Tanzania, vyanzo vya taarifa za matukio ya kihistoria na namna ya kukusanya na kuandika taarifa za matukio katika mazingira yanayokuzunguka. Pia, utajifunza maeneo ambayo kumbukumbu za kihistoria zinatunzwa.

Matukio ya kihistoria Tanzania

Yapo matukio mbalimbali ya kihistoria yaliyowahi kutokea nchini Tanzania. Baadhi ya matukio hayo yameorodheshwa katika jedwali lifuatalo.

Mwaka

Matukio ya kihistoria

1961

Tanzania ilipata uhuru

1964

Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

1967

Azimio la Arusha

1972

Kifo cha raisi wa kwanza wa Zanzibar hayati Sheikh Abeid Amani Karume

1974

Azimio la Musoma

1978-1979

Vita vya kagera

1984

Kisho cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine

1996

Ajali ya meli ya M.V Bukoba

1997-1998

Mvua ya Einino

1999

Kifo cha rais wa kwanza wa Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye pia alikua raisi wa kwanza wa Tanganyika.

2002

Ajali ya Gari- Moshi Dodoma

Vyanzo vya taarifa za matukio ya kihistoria

Katika ukusanyaji na utunzaji wa kumbukumbu, wanahistoria hutumia vyanzo mbalimbali kama ifuatavyo:

  1. Akiolojia ni njia ambayo mwanaakiolojia hufukua ardhini kutafuta mabaki ya kale ya binadamu, majengo, na zana zilizotumika enzi za kale. Mwanahistoria hutumia mambo hayo yaliyogunduliwa na wanaakiolojia katika kuandika historia ya maisha ya watu, matukio na muda.
  2. Anthropolojia ni njia anayotumia mwanahistoria kupata taarifa zinazohusu historia na utamaduni wa maisha na maendeleo ya binadamu. Vitu vinavyochunguzwa ni pamoja na mila, desturi na lugha.
  3. Lugha ni njia mojawapo inayotumika kukusanya taarifa mbalimbali za kihistoria kutoka katika jamii. Lugha inabeba taarifa za kihistoria na husaidia kufuatilia asili ya watu husika. Mfano baadhi ya maneno katika lugha ya Kingoni yanafanana na maneno ya lugha ya Kizulu. Hii inaonesha uhusiano wa karibu kati ya Wangoni wa Tanzania na Wazulu wa Afrika ya Kusini.

(d) Masimulizi ya mdomo ni njia ya kurithisha taarifa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kupitia masimulizi tunapata taarifa za kihistoria zilizohifadhiwa vichwani mwa watu kwa njia ya sanaa, muziki, michezo au kusimulia hadithi au Habari za matukio Mbalimbali.

  1. Machapisho ni maandiko yanayotunza taarifa mbalimbali za kihistoria mfano, majarida, vitabu na magazeti.
  2. Makumbusho ya Taifa ni mahali ambako kumbukumbu za matukio ya kihistoria zimehifadhiwa au zinapatikana, mfano jengo Ia Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam na jengo Ia kumbukumbu ya hayati Mwalimu Nyerere Butiama. Jengo hili hutumika kuhifadhi kumbukumbu za kihistoria za Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Njia za kukusanya taarifa za matukio ya kihistoria katika mazingira

Taarifa za matukio ya kihistoria katika mazingira huweza kukusanywa kwa kutumia njia mbalimbali. Njia hizo ni pamoja na:

  • Mahojiano
  • Kutumia dodoso
  • Kusoma maandiko mbalimbali
  • Kufanya uchunguzi kwenye maeneo ya kihistoria

Taarifa za matukio ya kihistoria zinaweza kupatikana katika maktaba, Makumbusho ya Taifa na kwa watu mbalimbali katika jamii waiioshuhudia matukio husika.

Baadhi ya vifaa vinavyoweza kutumika katika kukusanya taarifa za kihistoria ni:

  • Kinasa sauti
  • Daftari
  • Kamera

Vyanzo na maeneo yenye kumbukumbu za matukio ya kihistoria Tanzania

  • Wanahistoria hupata taarifa za kumbukumbu za matukio ya kihistoria kwa kutumia vyanzo na maeneo mbalimbali. Vyanzo na maeneo hayo ni Makumbusho ya Taifa, Nyaraka za Taifa, Maktaba mbalimbali, Kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam, Kijiji cha Kaole kilichoko Bagamoyo na maeneo ya Ujiji huko Kigoma. Jumba kuu Ia makumbusho ya Taifa lipo Dar es Salaam, na mengine madogo yapo Kalenga - Iringa, Bujora - Mwanza, Halwego Handebezyo Ukerewe - Mwanza na Butiama - Mara kunakotunzwa kumbukumbu za hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Vyanzo na maeneo mengine ni Mji Mkongwe Zanzibar, Kilwa, Isimila, Bonde la Olduvai, Kondoa Irangi, Engaruka, Makumbusho ya Mashujaa wa vita vya Maji Maji eneo la Mahenge mjini Songea na makumbusho ya kumbukumbu za Azimio Ia Arusha. Katika Makumbusho na nyaraka za Taifa tunapata taarifa za kihistoria zinazohusu masuala ya kiutamaduni, kijamii, kiuchumi, kisiasa na maendeleo ya teknolojia kuanzia zama za kale hadi sasa.
  • Taarifa za kihistoria zinazohusu shughuli mbalimbali za binadamu wa kale hadi sasa huhifadhiwa katika maktaba mbalimbali. Taarifa hizo ziko kwenye vitabu, majarida yaliyoandikwa na wamisionari na wapelelezi wa kwanza, barua za kibiashara na machapisho mengine. Pia, katika maktaba kunahifadhiwa taarifa mbalimbali za kiserikali, taasisi na vyama. Taarifa hizi zinatusaidia kujua vipindi mbalimbali vya maisha ya binadamu na jinsi alivyoishi.

www.learninghubtz.co.tz

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256