OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOGIA
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA DARASA LA SABA
SAYANSI NA TECHNOLOJIA
MUDA:1:30
JINA_____________________________________SHULE_________________________
Chagua herufi ya jibu sahihi
- Ipi kati ya zifuatazo sio kazi ya mfumo wa upumuaji?
- Usafirishaji wa oksijeni kwenye tishu
- Kutoa joto na maji mwilini
- Mbadilishano wa hewa mwilini
- Kuzungumza, kupiga yowe na kuimba
- Mbadilishano wa gesi hutokea kwenye……….
- Koromeo
- Pua
- Trakea
- Aliveoli
- Vinyweleo na unyevunyevu unaoopatikana katika pua, husaidia……………
- Mbadilishano wa hewa
- Kunasa vijidudu na uchafu
- Kusafirisha hewa kwenda kwenye mapafu
- Kupooza hewa inayoingia mwilini kupitia puani
- Unapotoa hewa nje ya mapafu misuli katika mbavu…………….
- Hulegea
- Hutanuka
- Hukaza
- Hukatika
- Upumuaji umegawanyika katika hatua mbili ambazo ni mbadilishano wa gesi katika mapafu Pamoja na……….
- Kuingiza na kutoa hewa kwenye damu
- Kupitisha hewa kwenye koromeo
- Kuingiza na kutoa hewa kwenye mapafu
- Mapafu na kifua kusinyaa
6. Damu huchukua oksijeni na kutoa kabondayoksaidi kupitia:
- Viribaehewa
- Kuta za mapafu
- Koromeo
- Kapilari
- Pua
- Zifuatazo ni kasoro za milango ya fahamu isipokuwa…………
- Uziwi
- Kutokuona mbali
- Anemia
- Kutokuona karibu
- Mlango wa fahamu unaofanya kazi ya kuhisi baridi au joto ni………..
- Jicho
- Sikio
- Ulimi
- Ngozi
- Kazi ya sikio la nje la binadamu ni………….
- Kukusanya mawimbi ya sauti
- Kutafsiri mawimbi ya sauti
- Kutawanya mawimbi ya sauti
- Kusisimua sikio la ndani
- Mpangilio wa vifupa vitatu katika sikio la kati ni kama ufuatao………….
- Fuawe, nyundo, kikuku
- Kikuku, nyundo, fuawe
- Nyundo, kikuku, fuawe
- Nyundo, fuawe, kikuku
- Ubongo umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni…………
- Serebramu, medula oblongata na ugwemgongo
- Serebelamu, ugwemgongo na medula oblongata
- Serebramu, serebelamu na medulla oblongata
- Medulla oblongata, serebramu na ugwemgongo
- Neva inayopeleka taarifa kutoka kwenye pua kwenda kwenye ubongo inaitwa………..
- Neva ya olifaktori
- Neva ya optiki
- Neva ya akaustika
- Neva ya oditori
- Neva inayotoa taarifa kutoka kwenye retina kwenda kwenye ubongo inaitwa……………
- Neva ya oditori
- Neva ya optiki
- Neva ya akaustika
- Neva ya olifaktori
- Yafuatayo ni aina ya mazoezi ya mwili, isipokuwa……….
- Kutembea
- Kucheza mpira
- Kuruka Kamba
- Kusikiliza muziki
- Mpira wa miguu ni mchezo unaofaa Zaidi kwa kundi la………..
- Wajawazito
- Watoto wachanga
- Wazee wa miaka 70
- Vijana
- Mlo kamili ni chakula chenye………….
- Virutubisho vya mafuta, kabohaidreti na protini, wanga na hamirojo
- Virutubisho vya protini, kabohaidreti, mafuta, vitamini na madini
- Virutubisho vya vitamini, madini na protini, wanga na hamirojo
- Virutubisho vya vitamini, kalisi, potasiamu, chuma na zinki
- Madini yafuatayo ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno………
- Madini ya chuma
- Madini ya magnesiamu
- Kalisi
- Potasiamu
- Bapa ni sehemu ya…………
- Cherehani
- Baiskeli
- Blenda
- Gurudumu la gari
- Mota katika blenda hubadilisha nishati ya umeme kuwa nishati ya………..
- Joto
- Makaniki
- Mwanga
- Joto na mwanga
- Nishati katika mashine ya kusaga nafaka husafirishwa kutoka kwenye mota hadi kwenye kinu kwa kutumia…………
- Mkanda
- Gurudumu na ekseli
- Nyenzo
- Mteremko
- Sehemu ya kutumbukiza ufunguo katika kitasa ina mashine sahili aina ya………….
- Nyenzo
- Springi
- Skrubu
- Gurudumu na ekseli
22. Tazama alama kwenye kielelezo kifuatacho kwa makini, kisha zipe majina kwa kuzingatia zilivyopangwa kutoka upande wa kushoto.
- Kapasita, dynamo, seli kavu, swichi, betri
- Swichi, glopu, kikinza, kapasita, seli kavu
- Glopu, kapasita, seli kavu, kikinza, betri
- Kikinza, glopu, swichi, seli kavu, kapasita
- Swichi, kikinza, glopu, seli kavu, kapasita.
23. Kipi kati ya vifuatavyo hakipitishi mkondo wa umeme?
- Mpira
- Bati
- Shaba
- Chuma
- Zebaki
24. Alama zifuatazo zinatumika katika sakiti ya umeme. Je, ni alama ipi inawakilisha kikinza?
-
-
-
-
-
25. Mzunguko kamili wa . . . . . . huitwa sakiti
- waya
- betri
- soketi
- umeme
- Makundi ya alama za usalama ni………..
- Alama za kuzuia, alama za onyo, alama za lazima na alama za dharura
- Alama za dharura, alama za binafsi na alama hatarishi
- Alama za amri, alama za kuzuia na alama za kukubali
- Alama za hospitali, alama za onyo, alama za barabarani na alama za angani
- Alama za lazima au amri huoneshwa kwa rangi gani?
- Njano
- Nyekundu
- Bluu
- Kijani
- Alama hii inawakilisha nini?
- Sumu
- Inashika moto
- Inamomonyoa na kuunguza
- Inadhuru
- Mojawapo kati ya maneno yafuatayo, hayawekwi kwenye viuatilifu vya kuua wadudu.
- Inashika moto
- Sumu au hatari
- Maji yasiyo salama
- Inakereketa
- Unapotumia vitu vinavyohatarisha macho, unapaswa kuchukua tahadhari gani?
- Kuvaa barakoa
- Kufunga kitambaa usoni
- Kuvaa kofia
- Kuvaa miwani
- Nini kinachosababisha kitu kuelea au kuzama kwenye maji?
- Urefu wa kitu
- Upana wa kitu
- Densiti ya kitu
- Kimo cha kitu
- Kama densiti ya kitu ni ndogo kuliko ya maji, nini kitatokea ukidondosha kitu hicho kwenye maji?
- Kitazama
- Kitaelea
- Kitazama na kuelea
- Kitazama au kuelea
- Densiti ya kitu ni tungamo ya kizio kimoja cha…………..
- Uzito
- Urefu
- Kina
- Ujazo
- Nyambizi inazama baharini ikiwa densiti yake ni…….
- Ndogo kuliko densiti ya maji
- Kubwa kuliko densiti ya maji
- Sawasawa na densiti ya maji
- Kubwa au ndogo kuliko densiti ya maji
- Moto wa daraja gani hutokana na kuungua kwa vitu yabisi kama nguo na karatasi?
- Daraja D
- Daraja C
- Daraja A
- Daraja F
- Tindikali ni dutu lenye kemikali ambayo hutumika kubadili karatasi ya litimasi………
- Nyekundu kuwa njano
- Bluu kuwa nyekunu
- Kijani kuwa bluu
- Nyekundu kuwa bluu
- Ni kwa namna gani unaweza kuzuia vitu vya chuma visioate kutu?
- Kuviweka kwenye maji
- Kuvipaka majivu
- Kuviongeza oksijeni
- Kuvipaka rangi
- Nyongo ina tabia mbili muhimu, ambazo ni…………
- Kubadili karatasi ya litimasi ya bluu kuwa nyekundu na kuua vijidudu
- Kubadili karatasi ya litimasi bluu kuwa nyekundu na kuvunja mafuta mwilini
- Kubadili karatasi ya litimasi nyekundu kuwa bluu na kuvunja mafuta ya wanyama mwilini
- Kubadili karatasi ya litimasi ya bluu kuwa nyekundu na kukinga magonjwa
- Ni gesi gani hutumika wakati wa kuzima moto?
- Kabonidayoksaidi
- Oksijeni
- Haidrojeni
- Naitrojeni
40. Chembe ndogo kabisa za maada zinazounda elementi na zinazohusika katika kutengenezz bondi za kikemikali huitwa:
- molekyuli
- elektroni
- protoni
- atomi
- nyutroni
41. Mwanga hupinda unapopita kutoka
- Ncha ya Kaskazini kwenda Kusini
- media moja kwenda nyingine
- Ncha ya Kaskazini kwenda Mashariki
- Magharibi kwenda Mashariki
- Kaskazini kwenda Magharibi
SHEMU YA B. CHUNGUZA PICHA IFUATAYO KISHA JIBU MASWALI
Andika majina ya sehemu zifuatazo:
- A
- B
- C
- D
- E
- F
- G
- H