FORM SIX KISWAHILI NECTA 2013

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA. NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL
ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION
EXAMINATION

121/1 KISWAHILI 1

(Kwa Watahiniwa Walioko Shuleni na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3     Jumatatu, 11 Februari 2013 asubuhi

Maelekezo

1. Karatasi hii ina maswali kumi (10) katika sehemu A, B, C, D na E.

2. Jibu maswali saba (7) kwa kuzingatia maelekezo kutoka katika kila sehemu.

3. Kila sehemu ina alama ishirini (20).

4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

5. Vikokotozi haviruhusiwi ndani ya chumba cha mtihani.

6. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A

UFAHAMU

1. Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata.

Mimi naitwa muhogo, nani asiyenijua?

Pato hata liwe dogo, ubora nashikilia,

Sijui tega mtego, ni mshindi asilia,

Muhogo ndiye rafiki, nikufaaye kwa dhiki.

Watu walionifuja, kwa nia na pambazuko.

Wakati ulipokuja, walipata hangaiko,

Kwa njaa walinitaja, wakihofu pukutiko,

Muhogo ndiye rafiki, nikufaaye kwa dhiki.

Palipo kame naota, mimi siyo mbamia,

Na sitofanya matata, ukininyima mbolea,

Baridi inayotata, kwangu mbali yapitia,

Muhogo ndiye rafiki, nikufaaye kwa dhiki.

Hebu tafuna muhogo, maji ukigugumia,

Au uchome muhogo, kwa chai ukatumia,

Lau chemsha muhogo, safarini kujilia,

Muhogo ndiye rafiki, nikufaaye kwa dhiki.

Ifikapo Ramadhani, mwezi tunaotubia,

Zaidi chakula gani, kaumu wategemea,

Nimo ndani futarini, wengi wanifuturia,

Muhogo ndiye rafiki, nikufaaye kwa dhiki.

Nikija kwenye ugali, nani asofurahia?

Ni laini kwa asili, kisu hutaulizia,

Wanga wangu kwenye mwili, nguvu utakupatia,

Muhogo ndiye rafiki, nikufaaye kwa dhiki.

Chukua unga ukande, ongeza sukari haba,

Kata biskuti pande, uvioke kwa vibaba,


Ni biskuti vipande, utazila kwa mahaba,

Muhogo ndiye rafiki, nikufaaye kwa dhiki.

Ninayo mboga makini, kisamvu nakutajia,

Kina nyingi vitamini, za muhimu kwa afya,

Chakula utathamini, kisamvu ukitumia,

Muhogo ndiye rafiki, nikufaaye kwa dhiki.

Shina langu ni shani, kuni utajipatia,

Mapishi ya kila fani, vyunguni kujiivia,

Utakuwa gharamani, mafuta ukizoea,

Muhogo ndiye rafiki, nikufaaye kwa dhiki.

MASWALI

(a) Eleza mawazo makuu matatu yanayotokana na shairi hili.

(b) Eleza manufaa matano ya muhogo yaliyoelezwa katika shairi ulilosoma.

(c) Andika kichwa cha shairi hili kwa maneno matatu tu.

(d) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi hili: (i) Pukutiko

(ii)Ukigugumia

(iii)Kaumu

(iv)Hatima

(e) "Atekaye maji mtoni, asimtukane mamba." Unafikiri methali hii inawakilisha wazo la ubeti upi katika shairi hili? Fafanua jibu lako ukihusisha maana na matumizi ya methali hiyo.

View Ans


2. Andika ufupisho wa shairi ulilosoma katika swali la kwanza (1) kwa aya moja tu yenye maneno yasiyozidi mia na hamsini (150) na yasiyopungua mia moja (100).

View Ans


SEHEMU B

MATUM/ZI YA SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

3. Eleza maana tano (5) za neno "Chungu", na kwa kila maana tunga sentensi moja inayofafanua maana hiyo.

View Ans


4. Kwa kutumia mifano, fafanua tofauti tano (5) zilizopo kati ya lugha ya kuzungumza na lugha ya kuandika.

View Ans


5. Kwa kutumia mifano, toa hoja mbili kuonesha ubora na hoja tatu kuonesha udhaifu wa kuainisha ngeli za nomino kwa kigezo cha kimofolojia.

View Ans


6. (a) Elezea umuhimu wa aina tatu wa nomino za Kiswahili.

(b) Onesha miundo mitano ya kiima katika tungo na kwa kila muundo toa mfano dhahiri.

View Ans


SEHEMU C

UTUNGAJI

7. Jifanye wewe ni miongoni mwa wafanyakazi waliopunguzwa kazi katika kiwanda cha Chai kilichopo Mufindi. Kwa bahati nzuri Kampuni ya Usambazaji Sukari imetangaza nafasi ya ajira ya wakala wa usambazaji sukari. Andika wasifu binafsi utakaotuma katika kampuni hiyo. Jina lako liwe Hamsini Uhuru.

View Ans


SEHEMU D

MAENDELEO YA KISWAHILI

8.Kwa kila nchi, eleza njia nne zilizosaidia kuenea kwa Kiswahili katika nchi ya Rwanda na Burundi kabla na baada ya uhuru.

View Ans


9.Taasisi mbalimbali ziliundwa baada ya uhuru ili kukikuza na kukieneza Kiswahili nchini Tanzania. Fafanua kazi nne za Taasisi ya Elimu Tanzania na nne za Chama cha Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

View Ans


SEHEMU E

TAFSIRI

10. Kwa kutumia mifano, fafanua mambo sita yanayosababisha upungufu katika tafsiri.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256